Zitto, Kitila na Mwigamba wajisalimisha CHADEMA

Status
Not open for further replies.

yegella

JF-Expert Member
Nov 18, 2010
3,114
1,250
Ule usemi samaki ana ujanja akiwa ndani ya maji umetimia.

Baada ya kushindwa kukihujumu chama kwa mbinu mbalimbali ikiwemo ya kushambulia mikutano ya Dr Slaa na kutoa matamko ya kipuuzi wakiqatumia viongozi mbalimbali wale wasaliti waliokwapuliwa vyeo vyao ndani chadema na kinachosubiliwa ni kupokonywa uanachama wao Zitto, Kitila na Samson Mwigamba wamejisalimisha jana baada ya kujibu barua waliyotumiwa na kuomba wasamehewe na wasinyang'anywe uanachama kuwa wana mapenzi na chama.
 

Honolulu

JF-Expert Member
Jan 20, 2012
5,648
1,225
Kama kweli wanataka msamaha ni vizuri wakasema ukweli wote jinsi CCM ilivyowatumia! Wawe wazi bila kuficha neno!!! Kusema tu wana mapenzi na CDM haitoshi!! Hayo ni mazingaombwe ya mchana kweupe! Wajieleze kwanza kwa umma! Baada ya hapo nguvu ya umma ndiyo itakayowahukumu!!
 

Domhome

JF-Expert Member
Jun 28, 2010
2,790
2,000
"Mtoto akinyea mkono haukatwi bali unaoshwa" huu ni usemi maarufu sana unaopendwa kutumiwa na wazee wetu. Maana yake ni kuwa anayekosa basi asamehewe, lakini wakati mwingine mikono huwa haiwezi takata hasa kama "mtoto" huyo anajinyea mara kwa mara na dawa hapo ni Kuikata mikono hiyo.
Hawa jamaa hawastahili kusamehewa kwani ni wasaliti. Let them go.....
 

lane

JF-Expert Member
Jan 17, 2013
894
500
kwa ufupi hizi spinning za akina zitto na wenzake imekula kwao.

chadema imeshakuwa kubwa mno, ni taasisi ambayo ina taratibu, kanuni, miongozo na katiba. Walishindwa kutambua hilo hawa ndugu, wamelikoroga, hawana budi ila kulinywa

sioni option yeyote iliyobaki kwa cc ya chadema zaidi ya kupigilia msumari wa moto wa hawa jamaa kufukuzwa chama completely

they betrayed watanzania, they betrayed harakati za ukombozi, they betrayed taifa letu la tanzania.

vitani askari akigeuka nyuma anapigwa risasi na vita inaendelea. sioni matumizi tofauti ya falasafa hii kwa cc ya chadema. ni fukuza kabisa.

nyoka akiingia chumbani kwako ni shurti untafute katika kona zote na umgonge kichwa afilie mbali la sivyo atakufanyia timing na kukukwiba kwa simu kali na unaweza kufa.

kwaherini wasaliti wote. chadema iliwapenda lakini naona ccm imewapenda zaidi
 

Kennedy

JF-Expert Member
Dec 28, 2011
26,001
2,000
Tutawaona wale wenye siasa nyepesi
kama wanamapenzi na CDM kwanini
wanahusika kukihujumu chama ?

Kwa walioangalia Bunge trh 06.12
Mbunge Kafulila alipopewa nafasi ya
kusema neno kuhusu kifo cha Mandela

Baada ya maongezi yake yote akasema
kwaniaba ya Chama chake Nccr Mageuzi
anatoa pole sana. Ukumbi wa Bunge ulicheka
sana hasa wakimwambia wewe sio Mwanachama
wa Nccr Mageuzi bali Mbunge wa Mahakama

Nao hao wanasema wabakipenda je hujuma
zao zingefanikiwa.
 

Uchaguzi

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
915
170
Unafiki wa chadema kwa hiyo kila kitu mnakiweka hadharani?
Hivi akina Zitto wakiamua kuweka kila jambo uchi mtabaki salama?
 

sixgates

JF-Expert Member
Mar 19, 2011
3,979
2,000
Mods ondoa huu uchafu. Naona tusubiri taarifa kamili. Hii tetesi source yake sio reliable.
 

Uchaguzi

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
915
170
Unafiki wa chadema kwa hiyo kila kitu mnakiweka hadharani?
Hivi akina Zitto wakiamua kuweka kila jambo uchi mtabaki salama?
 

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,491
2,000
Aisee..!!

Hii kweli ni Breaking News.Sasa kutapatapa kote huko na kuitisha mikutano inayofadhiliwa na CCM mwisho wake ni kuomba Radhi?

Chezeya Chadema weye?
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom