Jamani wandugu acheni kutumia vibaya elimu kiasi hicho...Mnaposema Zitto hana elimu ya madini mna maana gani hapa?..
Hivi nyie nyote mloona kasoro ktk mikataba hii mmesomea madini? ama nyote ni wanasheria?.
Duh! mimi naona karibu hata bunge letu litahitaji watu wenye shahada ya sheria ili kutunga sheria nikifuata mtazamo wenu kwani yaonyesha wazi mnaamini kuwa huwezi kufahamu uzito na athari ya kitu bila kuwa na elimu yake. Yaani hata njaa inahitaji elimu ya upishi wa chakula uweze ku solve tatizo la njaa bila kujua kwamba njaa kinachotakiwa ni mahesabu ya kiwango cha shibe sio degree ya upishi.
Jamani haya si ndio maswala tunayosema huhitaji kuwa mwana sayansi! - ama.
Damn!
Mkandara,
Hilo ndio tatizo la sisi Waafrika, tunathamini mno certificates badala ya kuthamini elimu.
Watu wanaona ili uwe na elimu lazima uwe na Ph.D kwenye jambo husika, that is nosense.
Kuna mwalimu mmoja alikuwa anatufundisha kazini, akasema wanapotuma mtu Afrika, wanambandika cheo cha Dr. hata kama ana degree moja, maana waafrika hawawezi kuamini kama jamaa anajua anachokifundisha kama sio Dr.
Ndio maana hata bungeni kila mtu anakimbilia kujiita Dr au prof. wakati kazi wanazofanya bungeni haziendani na hizo Ph.D.
Mara ngapi umesikia huku nje wanaita Dr. Condorize au Dr. Brown kwa UK? Hawa wote wana Ph.D lakini unaweza kukaa miaka kumi usisikie hata mtu anaongelea hizo Ph.D
Wangelikuwa wanafundisha au kwenye research basi hizo Ph.D zao zingetajwa lakini wanapofanya kazi tofauti, hizo Ph.D zao zinakuwa na faida ndogo sana.
Nina MD wangu, imenichukua miaka miwli kuja kujua ni Dr. Hata hiyo nilijua through ku serach kwenye internet na wala sio kupitia kazini. Lakini ingelikuwa Tanzania, hata kusahau kumwita Dr. ingelikuwa nongwa na balaa kubwa.
Zitto kwa kufuatilia madini, tayari ana elimu kubwa ya madini labda hata kuliko hao waliosomea madini miaka 20 iliyopita na sasa ni wanasiasa. Elimu ya madarasa sawa inasaidia lakini elimu bora zaidi ni ile unayojifunza kila siku na ile unayotumia kutatua matatizo yanayokuzunguka. Elimu ya kutundika ukutani ni upuzi mtupu wa kutudanganya na kututambia watanzania, wakati madini yanaibiwa wanashindwa hata kutetea.