ACT Wazalendo
JF-Expert Member
- May 5, 2014
- 610
- 1,540
Chama chetu kiliona dhamira ya Rais Samia Suluhu ya kuboresha mazingira ya Siasa nchini na kuamua kumwunga mkono; na hii ni kufuatia hotuba yake aliyoitoa siku ya kula Kiapo cha Urais, hotuba zake zingine za Bungeni, Mkutano wa Wadau (Dodoma I), kuundwa kwa Kikosi Kazi, Mkutano wa TCD (Dodoma II), Mazungumzo na Vyama na makala yake ya maarufu ya 4R; yaani Reconciliation, Resilience, Reforms na Rebuilding of the nation.
Hayo yalidhihirisha uungwana na nia yake thabiti kama Kiongozi; kwa sababu hiyo tulimuunga mkono. Tuliamua kumpa moyo (INCENTIVISE) kwani tunajua yupo katikati ya mfumo ambao hautaki mabadiliko yeyote.Tulikataa kuwa upande wa kumkatisha tamaa (DISCOURAGE.) Hivyo tulishiriki Kikosi Kazi KIKAMILIFU.
Tulitukanwa. Tulibezwa. Tulikashifiwa. Hatukujali. Sasa Kikosi Kazi kimekamilisha Taarifa na hivi karibuni itawasilishwa kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ushauri wangu kwa wanasiasa wenzangu: Jivueni MINYORORO ya 2020. Hairudi tena. Mageuzi yanahitaji MSHIKAMANO kwa kila mmoja anayetaka Mageuzi Nchini ni muhimu kufanikisha Nchi yetu kuwa kwenye njia ya Demokrasia.
Tujenge mshikamano na Rais Samia Suluhu na kumpa moyo ili kufanikisha Hatua inayofuata ya utekelezaji wa Mageuzi makubwa ya kisheria na kikatiba. #INCENTIVISE
#WeAreTheFuture
#TheFutureIsPurple