Mwaka 2024 ni wa matokeo zaidi: Haya ni baadhi ya mambo yatakayotiliwa mkazo

Rashda Zunde

Senior Member
May 28, 2022
199
231
Akitoa salamu za kuaga mwaka 2023 na kuukaribisha mwaka 2024, Mheshimiwa Rais Samia Suluhu alisema maneno yafuatayo, "mwaka 2023 ulikuwa ni mwaka wa mageuzi na mwaka ujao 2024 utakuwa ni mwaka wa utekelezaji na matokeo zaidi."

Katika hotuba hiyo alianisha masuala mbalimbali ambayo Serikali yake itatilia mkazo mwaka 2024 ili kuhakikisha ustawi wa wananchi na maendeleo ya Taifa kwa ujumla, ikiwa ni pamoja na kuadhimisha miaka 60 ya Muungano na miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, matukio ambayo ni muhimu na chachu ya kuendelea kudumisha umoja wa kitaifa.

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ni eneo jingine la kipaumbele katika mwaka huu ambapo amewasihi Watanzania kushiriki ili kuchagua viongozi wanaowafaa. Katika muktadha huohuo, Serikali itaboresha daftari la kudumu wa wapigakura kwa ajili ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Serikali imeahidi kuendelea kuongeza tija na kupunguza gharama za uzalishaji kwa wakulima na kuhakikisha usalama wa chakula, ambapo miongoni mwa mikakati itakayoendelezwa ni programu ya Jenga Kesho iliyo Bora (BBT), kuanza kwa miradi ya kuuza na kukodisha, kwa bei ya ruzuku, zana za kilimo kwa wakulima ikiwamo matrekta.

"Vilevile tutaendelea na mageuzi (reforms) katika sekta mbalimbali, ikiwemo uendeshaji wa mashirika ya umma na taasisi, lengo likiwa kuongeza ufanisi na tija katika uendeshaji wake. Tutaimarisha pia utekelezaji wa Sera ya Elimu ili kuhakikisha kuwa tunaanda watoto wetu kwa mazingira ya sasa na kuendelea na mchakato wa kuandika Dira Mpya ya Maendeleo," ameeleza Mheshimiwa Rais.

Eneo jingine ni kuziwezesha kampuni changa (startups) kukua kwa kuziwekea mazingira wezeshi, kuandaa mikutano ya kimataifa ukiwemo kilele cha nchi 25 za Afrika zinazolisha kahawa. Aidha, kutokana na kuendelea kutokea kwa majanga nchini na duniani, Serikali itaimarisha uwezo wa kukabiliana na majanga, na katika michezo Tanzania itakuwa wenyeji wenza wa michuano ya kombe la Afrika kwa wachezaji wa ndani yani (CHAN).

Ili kufanikisha hayo yote, Mheshimiwa Rais Samia alisema "natoa rai kwa wananchi wenzangu, kuazimia kubadilika, kila shughuli halali tunayoifanya tuifanye kwa bidii, maarifa na uadilifu na InshaAllah, Mwenyezi Mungu atabariki kazi za mikono yetu."
 
Namuamini huyu mama, anayosema anatekeleza japo anafeli kukomesha majizi ndo yanamkeamisha.
 
Back
Top Bottom