Bujibuji Simba Nyamaume
Platinum Member
- Feb 4, 2009
- 78,483
- 167,056
Zitto, nimesoma ujumbe wako wenye maneno matamu mno juu ya Tanzania tuitakayo. Maneno mengi tumeyasikia, yalikuwa ni matamu mno, yakutujenga imani, tukasahau methali ya wahenga Kuwa maneno matupu hayavunji mfupa.
Maneno pasi na vitendo yafaa nini? Ni sawa na chumvi iliyoharibika, Je uiweke nini hadi ikolee?
Ninachokuasa ni Kuwa Huo mfumo uliotufikisha hapa hauwezi kuvunjwa kwa chama kipya!, Ukweli huo mfumo ungetoka kwa katiba mpya! Na wanyonge kuungana kwa kuistopisha hii inayopigiwa debe na waliotufikisha hapa.

Zitto Kabwe:-
Adui wa Watanzania ni Mfumo wa Uchumi wa Kinyonyaji na Kifisadi unaofukarisha Watanzania.ACT Wazalendo kazi yao ni hiyo kumpiga adui huyu na waliojenga mfumo huo na wanaofaidika na mfumo huo. Adui yetu sio chama chochote cha siasa kilichoko kwenye upinzani.
Adui yetu ni Chama kilichojenga na kurutubisha mfumo huu.Nkrumah alisema " One struggle, Many fronts".ACT Wazalendo kamwe haitasumbuka kujibizana na wanachama wengine wa vyama vya Upinzani.
Tumeshapiga mstari " Forward ever, Backward never". Kazi yetu ni moja tu, kuirudisha Tanzania kwenye misingi iliyoasisi Taifa letu.