Maneno ya Nchimbi hayana maana yoyote ile!

Maneno ya Nchimbi hayana maana yoyote ile!

Nyani Ngabu

Platinum Member
Joined
May 15, 2006
Posts
98,350
Reaction score
144,919
Nadhani zimeshapita siku mbili sasa tokea Emmanuel Nchimbi [mimi simuiti makamu wa Rais kwa sababu hakuchaguliwa kushika hiyo nafasi] azungumzie mambo ya katiba mpya, uanaharakati, na mengineyo.

Soma Dkt. Nchimbi: Hakuna sheria inayotengua Katiba. Watanzania pambaneni kupata Katiba mpya

Katika huu muda wa siku hizi mbili nimeyafikiria kwa kina, upana, na urefu wa hayo aliyoyazungumza.

Kwa juu juu, aliyoyazungumza, ni maneno flani matamu matamu maana kazungumza yale ambayo wengi wetu tunataka kuyasikia.

Kwa sisi ambao huishi maisha kwa kutumia kanuni, maneno aliyoyazungumza Nchimbi hayana maana yoyote ile kwa sababu hayalingani na matendo yake na yale ya wenzake.

Baadhi yetu huwa tunaishi kwa kanuni ya ‘nionyeshe matendo yako kuliko vile ambavyo unaweza kunielezea kwa maneno pekee [show me better than you can tell me].

Huyu Nchimbi ni haramu. Hakuna mtu aliyemchagua awe makamu wa Rais.

Baada ya kuua maelfu ya Watanzania, yeye na mwenzake Samia wakakimbilia kujiapisha kwenye kambi ya jeshi huku wakijua kabisa kuwa hakuna aliyewapigia kura.

Hapo maana yake ni kwamba walipora madaraka.

Huyo Nchimbi mpaka leo hii hajawahi kusema chochote kuhusu maelfu ya Watanzania waliouwawa na serikali ya chama chao ili tu waendelee kukaa madarakani.

Kwa maneno hatujui anasimama wapi ila tukiangalia matendo yake tunajua pasipo na shaka kuwa anaunga mkono mauaji yaliyofanyika.

Mtu yeyote mwenye dhamiri iliyo safi hawezi kukaa kimya halafu kwa wakati huo huo akawa sehemu ya hao waliopora madaraka kwa kumwaga damu mpaka za watoto wadogo kabisa.

Nchimbi hajaonyesha kusikitishwa na hayo mauaji.

Hajaenda hata kwenye msiba mmoja wa hao watu waliouliwa.

Hajakemea mauaji ya watoto yaliyofanyika.

Hajatoa hata pole kwa yeyote yule aliyeondokewa na mpendwa wake hiyo siku ya Oktoba 29.

Kwa ufupi ni kajikausha kana kwamba hakuna kilichotokea siku hiyo.

Mtu mwenye akili timamu na mwenye nia ya dhati kabisa ya kutaka kuibadilisha Tanzania, utarukaje hayo mauaji na kuanza kuongelea mambo ya katiba mpya?

Watanzania tunawezaje kwenda kwenye mambo ya katiba mpya bila kuujua ukweli wa Oktoba 29, kuhakikisha kunakuwepo na uwajibikaji wa waliohusika akiwemo Samia, na kuazimia kuwa hayo hayatatokea tena?

Mimi siwezi kumpongeza Nchimbi kwa maneno matupu yasiyoendana na matendo ya kundi lake.

Show me better than you can tell me and we may talk.

Other than that, you can either go kick rocks or go pound sand somewhere…..
 
Naungana na wewe Mkuu na nakuheshimu sana ila mimi maoni yangu ni kwamba hata kama kweli anachosema anamaanisha bado suala la katiba daima litabaki kuwa ni mchakato yaani hakuna namna utasema fulani aonyeshe kwa vitendo ni process inahitaji muda maelewano na pesa…so mimi sitegemei nchimbi kufanya kitendo chochote kudhihirisha wapo tayari kwa katiba imagine tu NEMC wanataka kuwa mamlaka kamili miaka na miaka na kila mtu anaunga mkono mpaka nchimbi yuko nao ila haiwi sijui hizi nchi zetu zina shida gani
 
Yaani hata kusema tu kuwa kilichotokea Oktoba 29, 2025, hakikuwa sawa, mpaka sasa hajatoa kauli yoyote ile.

Hivi kuna ugumu gani kusema kwamba kilichotokea siku hiyo si sawa?

Ukimya wake kuhusu hayo mauaji ni sawa na kukubaliana nayo.
 
Haya unayoyataka yameshasemwa na bosi wake. Sioni logic ya kutaka kila mmoja atoe kauli kivyake vyake wakati issue ni ile ile na wote wapo kwenye mfumo ule ule.
 
Hata kichaa huwa anaongea Ukweli mkuu.
Akisema
1+2= 3
Anakuwa amejibu sahihi kabisa.

Kuna Muda saa mbovu huwa inaongea ukweli

Ema anasukuma kete vizuri sana kuelekea 2030
USIWAAMINI CCM.
USIWAAMINI CCM.
 
Kule Kwenye mtandao wa X zamani Tweeter Kuna mtu anatumia jina linalofanana na lako je ni wewe au majina tu yamefanana?
 
Wakati Mwangosi anauawa Nchimbi alikuwa waziri wa mambo ya ndani alifanya nini, fatilia historia ya Nchimbi akiwa mwenyekiti wa umoja wa vijana nini kilitokea kwa watu waliotaka kushindana naye. Watanzania wengi ni watu wa kusahau haraka kwa kifupi jafai kama kweli haridhiki ajiuzulu.
 
Back
Top Bottom