Zitto Kabwe: Tangu lini Rais anaheshimu Bunge? Kosa la Lugola ni kufanya dili kwa kumzunguka Rais, hoja ya Bunge ni kisingizio tu

JPM anaweza akamuonea mtu lakini siamini na sidhani kama Ikulu ya Tanzania wanaweza kumuonea mtu. Labda tu kwa sababu kuaminiana kumepungua sana kwenye siasa za Tanzania ndio maana baadhi ya watu wanadhani waliotenguliwa wameonewa.
 
Taasisi za serikari aziwezi kukopa au kuingia mkataba wowote wenye marejesho bila ya idhini ya wizara ya fedha.

Unapokopa au kuingia mkataba wowote wa marejesho hizo hela ulizochukua au investment costs zinakuwa accumulated kwenye deni la taifa.

Ndio maana waziri huwa anatoa takwimu za deni la serikari na madeni ya taasisi kwenye total debt.

Ata kama taasisi zinalipa madeni yenyewe lazima DMO (debt management office) ndio ina facilitate hizo process.

Hayo ni matakwa ya frameworks za international lenders kama WB/IMF kwenye kufanya stress test ya nchi kama inakopesheka.

Kwa ivyo ni upuuzi kwenda kuingia makubaliano ya kifedha bila ya waziri husika kutoa baraka zake, hizi ndio sababu NHC majengo yao yameishia kati hawana hela ya kuyaendeleza na serikari imekataa kuwapa guarantee lenders.

Sasa iwapo taasisi kama NHC yenye income stream inayoeleweka na imekuwa ikilipa madeni yake miaka yote, inaelewa umuhimu wa kupata kibali cha waziri kwanza; kwanini zimamoto wasijue utaratibu wakati uki default deni linageuzwa la walipa kodi.

Vitu vingine ni uchokozi tu, hao akina Lugola walijitakia.
 
Preliminary Memorandum of Understanding, ndiyo gani kwayo! sasa huo mradi umesha sainiwa, na wahusika wamejiuzulu, je mradi utaendelea? au ndiyo utaishia hapo kwenye P.M/Andastandingi?

Huyu Waziri kaingizwa chaka makusudi, either na Rais mwenyewe kwa sababu hamtaki, au na official subordinates wake, but hakustuka mapema, na hata sasa hajui! anaenda kikondoo tu!

Inawezekana pia alijua kinachoendelea, akaona sawa tu, na iwe ivo, amechoka kazi, za kupumuliwa shingoni, kama jinga fulani hivi, Musoma type wana viburi hao, hawajali matokeo!!!!!!!!

Ukiwa mkubwa kicheo, kiutawala, kifedha km Mengi, lazima uwe na personal guardian inner circle agency! watakao ku feed, nyeti zote! na namna ya kujinasua na mitego, Lugola maskini hayajui haya, alikimbia Jeshi.

But Rais ameyawezea sana haya kwa kutumia TISS. hata mimi hapa sijui wananijua hawa jamaa manake hawatabiriki! utashangaa siku uko kitaani ''wewe Nyarusare simama juu songa mbere?...''
 
Siasa ndo ivo unaweza kuwa huyu anaandaliwa kuwa Mrithi wake!

Sijui Waalimu wangu wako wapi ni mamburula mbona hakuna hata mbunge huko juu? angalieni wenzenu mtu na Mwalimu wake wana Madaraka, Nyerere na Mkapa, kikwete na nani yule dogo!

Kama una miaka 30+ huna katibu kata wala Diwani mliesoma wote au Mwalimu, basi hiyo ilikuwa st Kayumba!
 
Hivi
1. UWanja wa ndege wa chato ulipitishwa na bunge lipi?
2. Ununuzi wa ndege Je? mi nataja tu hayo mawili, najua yako mengine mengi. Si yeye awe wa kwanza kujiuzulu?
Mkuu Rais anajinyima budget yake ya kula Bata na Trump anatuletea maendeleo, hebu uliza miradi iliyofadhiliwa na kasma 22
 
Back
Top Bottom