GE2025 Zitto Kabwe: Polisi atakayebeba Kura Bandia ni halali yetu

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Waufukweni

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2024
Posts
4,393
Reaction score
14,500
Kiongozi mstaafu wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, ametoa onyo kali kwa maafisa wa polisi na watendaji wengine wa serikali wanaoshiriki katika kile alichokiita uingizaji wa kura bandia kwenye uchaguzi, akisema chama hicho hakitasita kuchukua hatua hata kama mhusika ni askari wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Akihutubia iku ya Alhamisi Julai 10, 2025 katika Jimbo la Tunduru Kaskazini, wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma katika mwendelezo wa Operesheni Majimaji ya chama hicho, Zitto ameeleza kuwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024, ACT Wazalendo ilimkamata afisa wa polisi akiwa amepakia kura bandia kwa lengo la kuzisambaza kwenye kituo cha kupigia kura.

"Tunajua CCM wanatumia kura bandia, kura bandia zinapigwa halafu zinaletwa kwenye kituo cha kupigia kura. Isivyo bahati, kule Kigoma tulimkamata Afisa wa Polisi akiwa amepakia kura bandia. Afisa yule alichokipata sidhani kama atarudia jambo lile," amesema Zitto.

Katika kauli hiyo, Zitto amesema chama hicho hakitavumilia tena majaribio yoyote ya kuvuruga uchaguzi kwa mbinu chafu kama hizo.

"Ninataka nitangaze rasmi hapa, na maafisa wa polisi watusikie: hatutajali magwanda yao, hatutajali nyota zao, hatutajali mitutu yao. Polisi atakayebeba kura bandia ni halali yetu," ameongeza kwa msisitizo.

Suala la maafisa wa usalama kuhusishwa na uingizaji wa kura bandia ni mojawapo ya hoja kubwa zilizowasilishwa na ACT Wazalendo katika mashauri kadhaa waliyoyafungua kupinga matokeo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024, hasa katika baadhi ya maeneo ya Kigoma.

Zitto amesisitiza kuwa Operesheni Majimaji inalenga kulinda demokrasia na kuhakikisha kuwa uchaguzi wa mwaka 2025 unakuwa huru na wa haki.

Epuka matapeli
 
😆😆😆😆😆😆😆
Mbona mapema sana, utapambana na CCM wakiwa na bunduki na wakala wako akiwa hana hata kirungu?
Mnaacha kukomalia mabadiliko ya mfumo wa uchaguzi ili kuepuka kuvunja watu miguu na kutolewa roho, mnapatuka payuka Tu kwamba mtazuia wizi WA Kura,alichokiasisi marehemu, CCM hawawezi kukiacha kwa vimaneno vyenu!
 
Zito hana sifa hizo, wakati akiwa cdm alikuwa anasema dola inachukuliwa kwa hoja na sio vurugu. Sasa hivi anaongea lugha alizokuwa anazikataa akiwa cdm. Hakuna mjinga wa kusikiliza utapeli wa Zito labda wasiomjua. Cdm ndio wapinzani walio serious.
 
Zitto kabwe kawa mpumbavu sana. Sio kwamba hajui anachokifanya ila ameamua kuwa mbinafsi
 
Ile albair ya ngamia ilileta matunda Gani?

Vijana wa mwandiga, buzebazeba, ujiji na mlole mtagongeshwa virungu mpaka mchakae.

CCM Haina urafiki kwenye kushika Dola.

Waulizeni wazenji walichezea kibano Cha Mzee nkapa, Dr jakaya hakuwa na utani mpaka akawashugulikia ipasavyo 2015 na anko Magu hakutaka kucheka na kima 2020 mpaka mkazisha kuwa kaleta wakuda Toka Burundi.

Siku ya uchaguzi kama unapiga kura katimize haki yake urudi kufanya kazi zako. Hata ukilinda kura utaambulia ulemavu, kifo au gereza.

CCM haitakubali kuachia madaraka kifara kama anavuowaza Mwami Kabwe
 
Kiongozi mstaafu wa chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe, ametoa onyo kali kwa maafisa wa polisi na watendaji wengine wa serikali wanaoshiriki katika kile alichokiita uingizaji wa kura bandia kwenye uchaguzi, akisema chama hicho hakitasita kuchukua hatua hata kama mhusika ni askari wa vyombo vya ulinzi na usalama.

Akihutubia iku ya Alhamisi Julai 10, 2025 katika Jimbo la Tunduru Kaskazini, wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma katika mwendelezo wa Operesheni Majimaji ya chama hicho, Zitto ameeleza kuwa katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024, ACT Wazalendo ilimkamata afisa wa polisi akiwa amepakia kura bandia kwa lengo la kuzisambaza kwenye kituo cha kupigia kura.

"Tunajua CCM wanatumia kura bandia, kura bandia zinapigwa halafu zinaletwa kwenye kituo cha kupigia kura. Isivyo bahati, kule Kigoma tulimkamata Afisa wa Polisi akiwa amepakia kura bandia. Afisa yule alichokipata sidhani kama atarudia jambo lile," amesema Zitto.

Katika kauli hiyo, Zitto amesema chama hicho hakitavumilia tena majaribio yoyote ya kuvuruga uchaguzi kwa mbinu chafu kama hizo.

"Ninataka nitangaze rasmi hapa, na maafisa wa polisi watusikie: hatutajali magwanda yao, hatutajali nyota zao, hatutajali mitutu yao. Polisi atakayebeba kura bandia ni halali yetu," ameongeza kwa msisitizo.

Suala la maafisa wa usalama kuhusishwa na uingizaji wa kura bandia ni mojawapo ya hoja kubwa zilizowasilishwa na ACT Wazalendo katika mashauri kadhaa waliyoyafungua kupinga matokeo ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2024, hasa katika baadhi ya maeneo ya Kigoma.

Zitto amesisitiza kuwa Operesheni Majimaji inalenga kulinda demokrasia na kuhakikisha kuwa uchaguzi wa mwaka 2025 unakuwa huru na wa haki.

Sioni uhalisia
 
Inahitajika moyo wa bandia kumwamini tapeli z kabwe.kura haibiwi kwnye vituo tu pia mshndi anapatikana kwa yule mwenye mamlaka anaxemtangaza.arejee kauli ya nape.ZITO NI CCM PURE AMETUMIKA AWAMU YA JK MAGU AKAMTOSA AKAANZA KULALAMA.LEO YUKO NA SAMIA KTK ULAGAI WA SIASA.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom