Zitto Kabwe: Nini kifanyike Tanzania?

Zitto Kabwe: Nini kifanyike Tanzania?

Huyu mtu au dogo anaitwa Zitto sijui yukoje???!!! Kuna hofu gani TZ?? Kama iko hofu basi ni miongoni mwa wachache sana tena sana ambaosidhani wanafika hata watano ambao wao hawataki kutii mamlaka na wanadhani wanajua kila kitu kwa niaba ya Watanzania...hakuna democracy without restrictions...ikiwemo democracy ya aina hiyo basi hiyo ni chaos....Mimi naona yaliyomo kwenye hoja iliyowekwa hapa ni ya kuchochea vurugu....Kuandika eti "tunaweza tukiamua, haya twenzetu tukaunda vuguvugu hili kuanzia mitaani tunamoishi, vijijini na mijini" ni maneno ya uchochezi ili kuleta vurugu katika nchi...kama maneno haya kweli ni ya zitto basi huyu dogo ana matatizo na ni sahihi kwa dola kumshughulikia....halafu kuandika kuwa eti "watanzania wapo tayari wanapaswa kuongozwa tu" kwa maana ya kuasi mamlaka ni uchochezi wa kiwango cha hali ya juu kabisa...huyu dogo kama kweli ameandika yeye ni vema afunzwe adabu..watanzania wa wapi hao ambao wapo tayari kuleta vurugu!!!???
Mkuu upepo unavuma vzr kwa upande wenu,siku ikikubadilikia ndo utajuta kumfahamu,akimaliza wapinzani atahamia upande wenu
 
Nadhani wewe umri wako ni mdogo sana na huijui vizuri historia ya nchi hii...Hivi unadhani wakati wa Mwalimu Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete watu walikuwa hawauwawi? Miaka ya Mwalimu watu walikuwa 'wanashughulikiwa' kisawasawa na hasa wale wakorofi...Upo wakati watu waliuawa gerezani mpaka Mwinyi akiwa Waziri wa mambo ya ndani akajiuzulu nafasi yake...mapambano ya wakulima na wafugaji yalikuwa ni balaa...karibu na kijijini kwangu miaka ya 80 yalitokea mapambano makali kati ya wafugaji na wakulima watu kadhaa walikufa lakini habari hazikutangazwa kwa kuwa vyombo vya habari vilikuwa vichache na hivyo vichache wakati mwingine vilikuwa controlled...kulikuwa na vifo kadhaa kwenye migodi na kadhalika wakati wa Mwinyi, Mkapa na hata wakati wa Kikwete...sijui kama unayo historia ya namna Mkuu wa mkoa wa iringa alipouawa kwa risasi na muuaji akabeba maiti na kuipeleka polisi...je, unafahamu kilichowapata wafanyabiashara kadhaa waliojaribu kuchangisha fedha 'kumsaidia' muuaji wa mkuu wa mkoa?? Je, unafahamu namna baadhi ya wanywa gongo na wengine wakorofi walivyokuwa wakishughulikiwa? ... Ni matajiri gani wametekwa unaowazunbumzia wewe? Kutekwa ni jambo la jinai na huyo aliyetekwa siyo jambo la jabu katika dunia hii...matajiri kadhaa hutekwa katika nchi nyingi ...it is a crime...na kutekwa kwa tajiri mmoja huwezi ukasema kuwa hali ya Tanzania ni mbaya...huko Russia baadhi ya matajiri huuawa, na ni kosa la jinai...hujui kuwa kuna mwanasiasa aliuawa karibu na Kremlin yaani makao makuu ya Russia...huko Marekani ndiyo usiseme, yanayoendelea kule huwezi kulinganisha na Tanzania...Ours is a peaceful country...kule mwanafunzi anaweza kuamua kuwaua wenzake kadhaa...

Masikini gani amenyang'anywa kidogo alicho nacho hapa Tanzania??!! Ni masikini gani huyo...hapa sheria zipo na mahakama zipo..kama amenyang'anywa anashughulikiwa na vyombo husika...ofcourse vyombo husika vinaweza kuwa na kasoro za hapa na pale lakini hiyo ni hulka ya binadamu na ni tatizo duniani kote...Waandishi gani hawako huru kuandika na wanapotezwa...kama yuko aliyepotea hilo ni suala la jinai na huwezi ukaanza kuandika kulalamika eti waaandishi wanapotezwa...Waandishi wa habari hapa Tanzania wako huru mno kuandika na wala hawafuatiliwi kihivyo...kwenye mitandano ya kijamii ndiyo usiseme..wewe kwa mfano uko huru na ndiyo maana umeweka uzi wako humu na hutafuatiliwa, ila ukiendelea na kuuchezea uhuru huu kwa kuwatukana viongozi na kuhamasisha fujo na maasi nchini utashughulikiwa tu kwa mujibu wa taratibu na 'hutapotezwa'...

Hivi unafikiri huko Marekani kuna uhuru wa vyombo vya habari unavyofikiri? Kule vyombo vya habari ni vya makampuni makubwa na elites wachache wenye madaraka...Trump mwenyewe analia na baadhi ya vyombo vya habari kwa kuandika 'habari za upendeleo'...

Unafahamu kilichowapata walalahoi walioandamana katika jiji la London miaka michache tu iliyopita na kuanza kuchoma maduka na vituo vyakibiashara? Unafikiri huko Uingereza, Marekani na kadhalika kuna demokrasia au uhuru wa kuandamana 'kwa shari'???
Kumuunga Ba jesca kwa ulazima haiwezekani,maana mnataka kutuaminisha vitu visivyoaminika,huo ndo udikteta
 
Zitto umeongea kizalendo sana,kila mtu kaguswa kwa namna yake.

Muhimu ni kuunganisha nguvu ili kuhakikisha demokrasia ,
Mtaji wa wanasiasa wengi ni kumbukumbu fupi za wafuasi wao. Jamaa walianzisha ACT na wakaweka mgombea wao wa Urais ili UKAWA wavune mabua. Na wakavuna mabua kweli. Leo memory zimefuta sasa wanapigiwa vigelegele na mauno kibao!
 
Nadhani wewe umri wako ni mdogo sana na huijui vizuri historia ya nchi hii...Hivi unadhani wakati wa Mwalimu Nyerere, Mwinyi, Mkapa na Kikwete watu walikuwa hawauwawi? Miaka ya Mwalimu watu walikuwa 'wanashughulikiwa' kisawasawa na hasa wale wakorofi...Upo wakati watu waliuawa gerezani mpaka Mwinyi akiwa Waziri wa mambo ya ndani akajiuzulu nafasi yake...mapambano ya wakulima na wafugaji yalikuwa ni balaa...karibu na kijijini kwangu miaka ya 80 yalitokea mapambano makali kati ya wafugaji na wakulima watu kadhaa walikufa lakini habari hazikutangazwa kwa kuwa vyombo vya habari vilikuwa vichache na hivyo vichache wakati mwingine vilikuwa controlled...kulikuwa na vifo kadhaa kwenye migodi na kadhalika wakati wa Mwinyi, Mkapa na hata wakati wa Kikwete...sijui kama unayo historia ya namna Mkuu wa mkoa wa iringa alipouawa kwa risasi na muuaji akabeba maiti na kuipeleka polisi...je, unafahamu kilichowapata wafanyabiashara kadhaa waliojaribu kuchangisha fedha 'kumsaidia' muuaji wa mkuu wa mkoa?? Je, unafahamu namna baadhi ya wanywa gongo na wengine wakorofi walivyokuwa wakishughulikiwa? ... Ni matajiri gani wametekwa unaowazunbumzia wewe? Kutekwa ni jambo la jinai na huyo aliyetekwa siyo jambo la jabu katika dunia hii...matajiri kadhaa hutekwa katika nchi nyingi ...it is a crime...na kutekwa kwa tajiri mmoja huwezi ukasema kuwa hali ya Tanzania ni mbaya...huko Russia baadhi ya matajiri huuawa, na ni kosa la jinai...hujui kuwa kuna mwanasiasa aliuawa karibu na Kremlin yaani makao makuu ya Russia...huko Marekani ndiyo usiseme, yanayoendelea kule huwezi kulinganisha na Tanzania...Ours is a peaceful country...kule mwanafunzi anaweza kuamua kuwaua wenzake kadhaa...

Masikini gani amenyang'anywa kidogo alicho nacho hapa Tanzania??!! Ni masikini gani huyo...hapa sheria zipo na mahakama zipo..kama amenyang'anywa anashughulikiwa na vyombo husika...ofcourse vyombo husika vinaweza kuwa na kasoro za hapa na pale lakini hiyo ni hulka ya binadamu na ni tatizo duniani kote...Waandishi gani hawako huru kuandika na wanapotezwa...kama yuko aliyepotea hilo ni suala la jinai na huwezi ukaanza kuandika kulalamika eti waaandishi wanapotezwa...Waandishi wa habari hapa Tanzania wako huru mno kuandika na wala hawafuatiliwi kihivyo...kwenye mitandano ya kijamii ndiyo usiseme..wewe kwa mfano uko huru na ndiyo maana umeweka uzi wako humu na hutafuatiliwa, ila ukiendelea na kuuchezea uhuru huu kwa kuwatukana viongozi na kuhamasisha fujo na maasi nchini utashughulikiwa tu kwa mujibu wa taratibu na 'hutapotezwa'...

Hivi unafikiri huko Marekani kuna uhuru wa vyombo vya habari unavyofikiri? Kule vyombo vya habari ni vya makampuni makubwa na elites wachache wenye madaraka...Trump mwenyewe analia na baadhi ya vyombo vya habari kwa kuandika 'habari za upendeleo'...

Unafahamu kilichowapata walalahoi walioandamana katika jiji la London miaka michache tu iliyopita na kuanza kuchoma maduka na vituo vyakibiashara? Unafikiri huko Uingereza, Marekani na kadhalika kuna demokrasia au uhuru wa kuandamana 'kwa shari'???
Mkuu unatamani tuishi maisha ya zamani,watu waendelee kutekwa kwa kuwa zamani watu walikuwa wanatekwa nadhani uzee umekushika vibaya,style up!bwana
 
Umetoka lini selo? Watu zaidi ya 100 kufariki ndani ya kijiji kimoja siyo jambo dogo, yafaa ukaoneshe makaburi.

Hongera kwa kutoka mikononi boss
Kesi iko mahakamani tayari, jadili mada au potezea tu!
 
Sio wa kuamini kama walivyosema wao usiamini mwanasiasa yoyote kwa 100%
Kweli kabisa wanasiasa siyo wa kuamini kwa asilimia 100. Hata hivyo, mwanasiasa asiyeaminika anaweza kutoa maoni mazuri ambayo yakifanyiwa kazi yanaweza kuwa na tija. Je, kuna jambo lolote chanya katika hoja ya Zitto? Hebu hilo lililo chanya tuungane kuliunga mkono for a better tomorrow!
 
Tanzania inayotakiwa ni ile Hakuna kufufua ATC, Ufisadi na mafisadi ruksa yaani unaagiza gari 10 unalipia ushuru gari moja tu, Hakuna kuhamia Dodoma, Vyeti vya kughushi ruksa, Hairuhusiwi kuanzisha mradi wa kutengeneza umeme utakaolifanya taifa liuze umeme nje ya nchi, Hakuna kutengeneza reli ya SGR wala kufufua shirika la reli la umma kwa sababu ukifanya hivyo mafisadi watakosa biashara ya kusafirisha mizigo kwa malori makubwa waliyonunua kutoka nje na kuyapitisha bandarini kwa kulipia lori moja kati ya 10 yaliyoagizwa. Hawa wanaotaka Tanzania ya namna hii wanaitaka kwa maslahi ya nani?
Hiyo ndo Tanzania unayoitaka wewe? Kweli umefilisika.
 
Huna lolote....
Nini kifanyike Tanzania?

Na Zitto Kabwe

Hali yetu ya sasa

Ni dhahiri kuwa hofu imetanda miongoni mwa Watanzania. Ingawa watawala na mashabiki wao hukanusha jambo hili, ukweli ni kuwa nina amini wao wenyewe ndani ya mioyo yao wanakiri kuwa nchi sasa inaendeshwa kwa hofu na wananchi wamejaa hofu kubwa.

Hivi sasa mwananchi akifanya jambo lolote linaloonekana kuwa kinyume na fikra za watawala, wenzake wanamtazama kwa jicho kuwa atakuwa mhanga wa vitisho, mateso, kutekwa, kupotea ama kubambikiwa kesi.

Hakika jamii iliyojaa hofu haiwezi kuwa jamii huru na kamwe haiwezi kupata maendeleo.

Hofu hii iliyotamalaki imekomazwa na matendo ya utawala kukandamiza uhuru wa watu kujieleza, kupata/kupasha habari, kukusanyika na kuhoji/kukosoa Serikali yao. Hizi ni haki za kikatiba ambazo wajibu wa Serikali ni kuzilinda.

Tumeshuhudia wananchi na haswa vijana wakishtakiwa mahakamani kwa makosa yatokanayo na haki yao ya kujieleza kwenye mitandao ya kijamii. Baadhi ya vijana wamehukumiwa vifungo ama kulipa faini.

Mmiliki wa mtandao wa JamiiForums, mtandao wenye kutoa mawazo huru kwa wananchi na kwa muda uliochangia kwa kiasi kikubwa vita dhidi ya ufisadi nchini, Maxence Melo bado anaendelea na kesi zilizofunguliwa dhidi yake ikiwa sehemu ya vitisho vya dola ambavyo pamoja na shauri hilo amekuwa akilazimishwa kutoa majina ya wachangiaji wa mtandao huo.

Licha ya kwamba katiba yetu inaruhusu vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara na kujitangaza, kuandikisha wanachama, kukosoa sera za Serikali na hata kueneza sera mbadala, Serikali kupitia amri isiyo ya kikatiba wala kisheria ya Rais imezuia vyama kufanya shughuli zake hizo halali.

Matamko halali kabisa ya kisiasa ya wanasiasa sasa yanachukuliwa kama ni uchochezi na watoa matamko kushtakiwa kwa makosa ya jinai ikiwemo kwa kutumia sheria mpya kandamizi ya huduma za habari (The Media Services Act 2016 ).

Tumeshuhudia wabunge wakifungwa jela kwa makosa ya matamko ya kisiasa ambayo yangepaswa kujibiwa kisiasa tu kutoka upande wa pili ( watawala ).

Hivi sasa viongozi wakuu wa vyama vya upinzani wanakwenda mahakamani kila wiki kujibu tuhuma za kisiasa, lengo likiwa ni kuwapotezea muda na kuwajaza hofu washindwe kufanya shughuli zao ipasavyo.

Utawala umeweza kusambaza hofu kwa kugusa kila kundi katika jamii. Wanasiasa wanatishiwa na kesi za uchochezi, kutekwa au majaribio ya kuuawa kwa kupigwa risasi mchana kweupe ndani ya eneo lenye ulinzi mkubwa.

Waandishi wa Habari wanatishwa kwa ama vyombo vya habari kama magazeti kufungiwa au kutekwa na kutoonekana kabisa; Wakulima bei za mazao yao zimeporomoshwa makusudi kutokana na maamuzi ya hovyo ya kisera ya Serikali; Wavuvi wanachomewa nyavu zao na mitumbu yao kuchomwa moto; Wafugaji wanaondolewa kwenye maeneo yao ya malisho ili kuanzisha ranchi binafsi na wengine kuuwawa; Wafanyabiashara wanabambikiwa kesi ama kodi kubwa ili kuwakomesha na kuweka utii kwa dola; Wanawake wanatukanwa na kudhalilishwa ikiwemo kuwanyima fursa ya kujiendeleza kimasomo watoto wa kike wanaopata uja uzito mashuleni.

Viongozi wa dini wanaojaribu kuhoji watawala wanachunguzwa uraia wao; Wanaharakati wa asasi za kijamii wanaotoa mawazo yasiyopendeza watawala wanatangazwa sio raia wa Tanzania na asasi zao kutishiwa kufutwa kwa kutungiwa kanuni kandamizi za uendeshaji wa asasi hizo.

Wananchi kwa ujumla wanaumizwa na hali mbaya ya uchumi inayotokana na maamuzi ya hovyo ya kisera ya Serikali katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo. Wananchi wa Zanzibar wamenyimwa haki ya kuongozwa na Serikali waliyoichagua katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Hakuna kundi katika jamii ambalo limebakizwa, kila kundi limeguswa.

Tunataka nini?
Kwa maoni yangu Watanzania wengi wanapenda kuwa huru; Uhuru wa Mawazo, kujieleza, kukusanyika nk. Nadhani tunataka Tanzania yenye raia wenye uhuru kwa mujibu wa Katiba. Vyama vya siasa viwe huru kufanya shughuli zao bila bugudha na kwa mujibu wa sheria, Bunge la Wananchi liwe huru kuisimamia Serikali bila kuzongwazongwa na Watendaji, vyombo vya habari viwe huru kuandika/kutangaza habari bila woga wala upendeleo; Wananchi wawe huru kuikosoa serikali dhidi ya sera zake kandamizi zinazowasokomeza kwenye umasikini, Wazanzibari wapate haki yao ya uchaguzi (electoral justice) waliyoporwa Oktoba 2015 na viongozi wa dini na asasi za kiraia wawe huru kufanya kazi zao bila vitisho. Kiufupi tunataka nchi ya kidemokrasia ambayo asasi za kidemokrasia zinatimiza wajibu wao kwa uhuru.

Tufanye nini?

Sasa wakati umefika wa kujenga mshikamano kurejesha demokrasia tuliyokuwa nayo nchini na kujenga demokrasia madhubuti ambayo haitachezewa tena na yeyote. Haitoshi kila mtu kusema lake kwa wakati wake anapoguswa na matendo ya kidikteta, tunapaswa kuwa na sauti nyingi lakini zinazoratibiwa ili kuhakikisha kuwa tunalinda haki za watu na kuhami uchumi wa nchi wetu usiendelee kuporomoka. Tunapaswa kuwa na harakati za kutetea haki za kijamii (social justice), haki za kujieleza (freedom of speech) na Demokrasia. Tunapaswa kujenga vuguvugu pana la watu a broad based popular movement) ili kuleta mabadiliko ya kijamii, kiuchumi na kisiasa.

Ili kujenga vuguvugu hili ni lazima kuweka mbele maslahi mapana ya Taifa letu na kuachana na maslahi binafsi ambayo yamekuwa yakitawala siasa za Tanzania kwa miongo miwili sasa bila mafanikio ya maana. Ni lazima kukubali ukweli kuwa, kwa hali ya nchi ilivyo sasa hakuna chama kimoja pekee ama kundi la jamii moja pekee linaweza kukabili utawala dhalimu wa kidikteta uliopo nchini na kushinda. Wasioweza kuukabili ubinafsi wao kwenye mambo haya tuwaombe basi wauweke kama akiba kisha tukimaliza kazi hii ya mabadiliko waendelee nao. Kila jambo tufanyalo lazima lijibu swali ‘ hili linatusaidia kutufikisha kwenye lengo la kuondoa utawala wa kidikteta nchini?’

Ni lazima tuwe na mshikamano katika kukabili dubwana tunalokabiliana nalo. Hatupaswi kuruhusu hata siku moja ya ziada baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 tukiwa na ‘regime’ hii tuliyonayo sasa.

Hili ni jambo linalowezekana iwapo tutakuwa na mshikamano madhubuti bila kujali vyama vyetu vya siasa.

Watanzania wapo tayari, wanapaswa kuongozwa tu. Uongozi huu ni lazima uwe na watu wasiopenda yanayoendelea nchini ndani ya watawala, walio nje ya watawala, Wafanyakazi, Wakulima, Wavuvi, Wafugaji, Vjana, Wanawake, Wafanyabiashara, wana harakati na kila mtu anayetaka Tanzania na Zanzibar zilizo njema zenye Uhuru na Demokrasia.

Tunaweza tukiamua. Haya #twenzetu tukaunde vuguvugu hili kuanzia mitaani tunamoishi, vijijini na mijini.

Dar Es Salaam
5/11/2018
.....
 
Mwandishi mmoja yeye aliwahi kutoa ushauri wa kiteolojia, akifananisha hali ya sasa na gari bovu lililokatika break na kuanza kugonga kila kitu kilicho mbele yake, akashauri dawa ni mtu mmoja ambaye kwa maoni yake alisema awe Pengo, atakayejitolea kwenda kuliwekea kigingi cha jiwe lile gari liliokatika break, kulizuia au kulikimbia hakusaidii kitu, maana litatugonga wote tu bila kujali una makosa au la.
 
lianzisheni viongozi wetu. wananchi wenu tupo stand by kukiwasha!
Mafisi nyinyi waoga sana, nyuma ya keyboard mnajifanya watata.
Walianzishe mara ngapi muwaache kwenye mataa.
 
kuna watu humu watakuja kugundua umuhimu wa maandiko haya ya zitto too late
na hamtaona aibu kuja kulia humu,we have seen it before
teteeni udikteta lakini siku inakuja ndugu yako au rafiki yako ataguswa na mikono ya kidikteta na utatuelewa
Kuna watu humu wapo kutetea udikteta wa dikteta tu. Iko siku watayakumbuka maneno ya Zitto!
 
Tatizo wa Tanzania ni waoga na wanafiki ukijitoa kwa ajiri yao wanaona kama hakuna unachokifanya
Nikiangalia akina Lisu, Saanane, na wote wanaotetea haki za wanyonge huishia matatani wanainchi wakishangilia tu

TUMEJENGWA KATIKA MISINGI YA HOFU ITACHUKUA MUDA MREFU KUISHINDA HOFU
 
kuna mtu atakuja hapa kutuambua tukasome mtandaoni uwezo wa risasi ya 50 cal kumsambaratisha binadam
 
UPO SAHIHI.
Lakini ...
Tatizo nyie wapinzani mmekuwa wasaliti wa wananchi, bado hatujasahau wewe mh zitto na wenzako mlivyofanya harakati za kudhoofisha chadema .. na sasa unakuja na swali ati tufanyeje? acheni unafiki na ubinafsi , vinginevyo mtaendelea kukosa imani ya wananchi.. waacheni wananchi wapambane na hali zao sio kuwahadaa ...
LAKINI SI AMEANDIKA UKWELI NA HIYO NDIYO HALI HALISI KWA MAMA TANZANIA?
 
Back
Top Bottom