Zitto Kabwe: Nini kifanyike Tanzania?

Zitto Kabwe: Nini kifanyike Tanzania?

kuna watu humu watakuja kugundua umuhimu wa maandiko haya ya zitto too late
na hamtaona aibu kuja kulia humu,we have seen it before
teteeni udikteta lakini siku inakuja ndugu yako au rafiki yako ataguswa na mikono ya kidikteta na utatuelewa
 
Mbona musiba bado ana dunda uraini pamoja na kutishia kumroga? ni kweli umekula mke wa marehemu na kufuja mali za rafiki yako?
 
Tukianza kuangalia nyuma badala ya mbele tunaokoenda tutakuwa tunakosea. Sema wewe ni lisisiemu tu unaogopa umoja wa wanasiasa wa upinzani sasa hivi. Wewe una uchungu kuliko Lema, Heche na Mbowe ambao wameamua kuungana na kina Zitto kuhakikisha hali iliyopo sasa inaondoka. Furaha yako ni kuona hawapatani na kupatana kwako kunakutia chuki.
Labda wameungana kwa sababu zao binafsi!
 
Tukianza kuangalia nyuma badala ya mbele tunaokoenda tutakuwa tunakosea. Sema wewe ni lisisiemu tu unaogopa umoja wa wanasiasa wa upinzani sasa hivi. Wewe una uchungu kuliko Lema, Heche na Mbowe ambao wameamua kuungana na kina Zitto kuhakikisha hali iliyopo sasa inaondoka. Furaha yako ni kuona hawapatani na kupatana kwako kunakutia chuki. Pole sana

Misiba hukutanisha maadui
inawezekana kwa ndani ccm wana malalamiko kuliko wapinzani na wengine wote
 
nilibahatika kuishi kwenye kamji kamoja huko pembezoni mwa nchi hali ni mbaya sana kwakweli ! kamji kale kana wanajeshi na mapolisi wengi ambao kimsingi hawana walifanyalo zaidi ya kujaza hofu
Ni kweli baadhi ya maeneo nchini Congo hali sio shwari!
 
Mwalimu nyerere alihubiri falsafa zifuatazo:

Uhuru na umoja,
Uhuru na kazi,
Uhuru na ujamaa,
Uhuru na maendeleo.

Jiwe amevuruga vyote, anakimbia kwa kasi kurudi nyuma.
Jiwe anapaswa ashinikizwe aelewe kuwa tanzania ya sasa inahitaji Uhuru na Katiba mpya zaidi kuliko kutazama SGR.
Tatizo lenu mkipata upenyo kidogo mnafanya ya Amber Rutty!
 
Kweli kabisa siku hizi hata tunavyojadili siasa kwenye vilinge vyetu tunaangaliana kwanza sura kama tunajuana....mkiona sura ngeni kati yenu....mnaanza stori za kuiponda Manchester United....

Kwa hili la kutujaza hofu watawala wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa, japo haimaanishi watu hatuongei.

Sasa mlikuwa mnataka Mtu wa kuturudisha enzi Za Mwl Nyerere bila ya kujua Kwa Nyerere tuliishi je?

Enzi zile tulikuwa Hata tukiona Kichaa kuokota Makopo tunasema 'Usalama yule'


Enzi hizo Hata ukiwa Na Mkeo Chumbani ukitaka kumsoma Nyerere unajikuta automatically umepunguza sauti Na kunong'ona

Magufuli kanyaga twende mPaka Maji yaitwe 'Mma'
 
Tutafika tu. Ngoja angalau vilio viwe vingi ndo tutaona kweli kuna haja ya kudai tunachonyang'anywa.
 
Ninachojua mimi takriban wanasiasa wote ni wanafiki tu wapo kwa maslahi yao na pale tu maslahi yao yanapoguswa ndio huanza kelele kutafuta huruma ya wananchi, kabla nini la kufanya anzeni nyinyi wanasiasa kusafisha nyoyo zenu na kupunguza undumilakuwili.
 
Kweli kabisa siku hizi hata tunavyojadili siasa kwenye vilinge vyetu tunaangaliana kwanza sura kama tunajuana....mkiona sura ngeni kati yenu....mnaanza stori za kuiponda Manchester United....

Kwa hili la kutujaza hofu watawala wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa, japo haimaanishi watu hatuongei.
Policing each other is a bad thing. Muda si mrefu tutaanza kupigana beto. Uhuru ukiminywa kwa kiasi hicho ni rahisi kupata watu wenye mawazo hasi.
 
Huyu mtu au dogo anaitwa Zitto sijui yukoje???!!! Kuna hofu gani TZ?? Kama iko hofu basi ni miongoni mwa wachache sana tena sana ambaosidhani wanafika hata watano ambao wao hawataki kutii mamlaka na wanadhani wanajua kila kitu kwa niaba ya Watanzania...hakuna democracy without restrictions...ikiwemo democracy ya aina hiyo basi hiyo ni chaos....Mimi naona yaliyomo kwenye hoja iliyowekwa hapa ni ya kuchochea vurugu....Kuandika eti "tunaweza tukiamua, haya twenzetu tukaunda vuguvugu hili kuanzia mitaani tunamoishi, vijijini na mijini" ni maneno ya uchochezi ili kuleta vurugu katika nchi...kama maneno haya kweli ni ya zitto basi huyu dogo ana matatizo na ni sahihi kwa dola kumshughulikia....halafu kuandika kuwa eti "watanzania wapo tayari wanapaswa kuongozwa tu" kwa maana ya kuasi mamlaka ni uchochezi wa kiwango cha hali ya juu kabisa...huyu dogo kama kweli ameandika yeye ni vema afunzwe adabu..watanzania wa wapi hao ambao wapo tayari kuleta vurugu!!!???
Duh! Hii imenikumbushia zile posting za watu wasiojulikana kwenye ile thread ya Ben Saanane. Haukupita muda akatekwa na hadi sasa haujulikani alipo wala ni ni kimempata huko alipo. So mh Zitto ni lazima uwe makini all the time kuna watu hawalali wana kazi ya kuwatizama mkiteleza mkiingia anga zao mmekwishaa!
 
Nini kifanyike Tanzania?

Na Zitto Kabwe

Hali yetu ya sasa

Ni dhahiri kuwa hofu imetanda miongoni mwa Watanzania. Ingawa watawala na mashabiki wao hukanusha jambo hili, ukweli ni kuwa nina amini wao wenyewe ndani ya mioyo yao wanakiri kuwa nchi sasa inaendeshwa kwa hofu na wananchi wamejaa hofu kubwa.

Hivi sasa mwananchi akifanya jambo lolote linaloonekana kuwa kinyume na fikra za watawala, wenzake wanamtazama kwa jicho kuwa atakuwa mhanga wa vitisho, mateso, kutekwa, kupotea ama kubambikiwa kesi.

Hakika jamii iliyojaa hofu haiwezi kuwa jamii huru na kamwe haiwezi kupata maendeleo.

Hofu hii iliyotamalaki imekomazwa na matendo ya utawala kukandamiza uhuru wa watu kujieleza, kupata/kupasha habari, kukusanyika na kuhoji/kukosoa Serikali yao. Hizi ni haki za kikatiba ambazo wajibu wa Serikali ni kuzilinda.

Tumeshuhudia wananchi na haswa vijana wakishtakiwa mahakamani kwa makosa yatokanayo na haki yao ya kujieleza kwenye mitandao ya kijamii. Baadhi ya vijana wamehukumiwa vifungo ama kulipa faini.

Mmiliki wa mtandao wa JamiiForums, mtandao wenye kutoa mawazo huru kwa wananchi na kwa muda uliochangia kwa kiasi kikubwa vita dhidi ya ufisadi nchini, Maxence Melo bado anaendelea na kesi zilizofunguliwa dhidi yake ikiwa sehemu ya vitisho vya dola ambavyo pamoja na shauri hilo amekuwa akilazimishwa kutoa majina ya wachangiaji wa mtandao huo.

Licha ya kwamba katiba yetu inaruhusu vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara na kujitangaza, kuandikisha wanachama, kukosoa sera za Serikali na hata kueneza sera mbadala, Serikali kupitia amri isiyo ya kikatiba wala kisheria ya Rais imezuia vyama kufanya shughuli zake hizo halali.

Matamko halali kabisa ya kisiasa ya wanasiasa sasa yanachukuliwa kama ni uchochezi na watoa matamko kushtakiwa kwa makosa ya jinai ikiwemo kwa kutumia sheria mpya kandamizi ya huduma za habari (The Media Services Act 2016 ).

Tumeshuhudia wabunge wakifungwa jela kwa makosa ya matamko ya kisiasa ambayo yangepaswa kujibiwa kisiasa tu kutoka upande wa pili ( watawala ).

Hivi sasa viongozi wakuu wa vyama vya upinzani wanakwenda mahakamani kila wiki kujibu tuhuma za kisiasa, lengo likiwa ni kuwapotezea muda na kuwajaza hofu washindwe kufanya shughuli zao ipasavyo.

Utawala umeweza kusambaza hofu kwa kugusa kila kundi katika jamii. Wanasiasa wanatishiwa na kesi za uchochezi, kutekwa au majaribio ya kuuawa kwa kupigwa risasi mchana kweupe ndani ya eneo lenye ulinzi mkubwa.

Waandishi wa Habari wanatishwa kwa ama vyombo vya habari kama magazeti kufungiwa au kutekwa na kutoonekana kabisa; Wakulima bei za mazao yao zimeporomoshwa makusudi kutokana na maamuzi ya hovyo ya kisera ya Serikali; Wavuvi wanachomewa nyavu zao na mitumbu yao kuchomwa moto; Wafugaji wanaondolewa kwenye maeneo yao ya malisho ili kuanzisha ranchi binafsi na wengine kuuwawa; Wafanyabiashara wanabambikiwa kesi ama kodi kubwa ili kuwakomesha na kuweka utii kwa dola; Wanawake wanatukanwa na kudhalilishwa ikiwemo kuwanyima fursa ya kujiendeleza kimasomo watoto wa kike wanaopata uja uzito mashuleni.

Viongozi wa dini wanaojaribu kuhoji watawala wanachunguzwa uraia wao; Wanaharakati wa asasi za kijamii wanaotoa mawazo yasiyopendeza watawala wanatangazwa sio raia wa Tanzania na asasi zao kutishiwa kufutwa kwa kutungiwa kanuni kandamizi za uendeshaji wa asasi hizo.

Wananchi kwa ujumla wanaumizwa na hali mbaya ya uchumi inayotokana na maamuzi ya hovyo ya kisera ya Serikali katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo. Wananchi wa Zanzibar wamenyimwa haki ya kuongozwa na Serikali waliyoichagua katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Hakuna kundi katika jamii ambalo limebakizwa, kila kundi limeguswa.

Tunataka nini?
Kwa maoni yangu Watanzania wengi wanapenda kuwa huru; Uhuru wa Mawazo, kujieleza, kukusanyika nk. Nadhani tunataka Tanzania yenye raia wenye uhuru kwa mujibu wa Katiba. Vyama vya siasa viwe huru kufanya shughuli zao bila bugudha na kwa mujibu wa sheria, Bunge la Wananchi liwe huru kuisimamia Serikali bila kuzongwazongwa na Watendaji, vyombo vya habari viwe huru kuandika/kutangaza habari bila woga wala upendeleo; Wananchi wawe huru kuikosoa serikali dhidi ya sera zake kandamizi zinazowasokomeza kwenye umasikini, Wazanzibari wapate haki yao ya uchaguzi (electoral justice) waliyoporwa Oktoba 2015 na viongozi wa dini na asasi za kiraia wawe huru kufanya kazi zao bila vitisho. Kiufupi tunataka nchi ya kidemokrasia ambayo asasi za kidemokrasia zinatimiza wajibu wao kwa uhuru.

Tufanye nini?

Sasa wakati umefika wa kujenga mshikamano kurejesha demokrasia tuliyokuwa nayo nchini na kujenga demokrasia madhubuti ambayo haitachezewa tena na yeyote. Haitoshi kila mtu kusema lake kwa wakati wake anapoguswa na matendo ya kidikteta, tunapaswa kuwa na sauti nyingi lakini zinazoratibiwa ili kuhakikisha kuwa tunalinda haki za watu na kuhami uchumi wa nchi wetu usiendelee kuporomoka. Tunapaswa kuwa na harakati za kutetea haki za kijamii (social justice), haki za kujieleza (freedom of speech) na Demokrasia. Tunapaswa kujenga vuguvugu pana la watu a broad based popular movement) ili kuleta mabadiliko ya kijamii, kiuchumi na kisiasa.

Ili kujenga vuguvugu hili ni lazima kuweka mbele maslahi mapana ya Taifa letu na kuachana na maslahi binafsi ambayo yamekuwa yakitawala siasa za Tanzania kwa miongo miwili sasa bila mafanikio ya maana. Ni lazima kukubali ukweli kuwa, kwa hali ya nchi ilivyo sasa hakuna chama kimoja pekee ama kundi la jamii moja pekee linaweza kukabili utawala dhalimu wa kidikteta uliopo nchini na kushinda. Wasioweza kuukabili ubinafsi wao kwenye mambo haya tuwaombe basi wauweke kama akiba kisha tukimaliza kazi hii ya mabadiliko waendelee nao. Kila jambo tufanyalo lazima lijibu swali ‘ hili linatusaidia kutufikisha kwenye lengo la kuondoa utawala wa kidikteta nchini?’

Ni lazima tuwe na mshikamano katika kukabili dubwana tunalokabiliana nalo. Hatupaswi kuruhusu hata siku moja ya ziada baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 tukiwa na ‘regime’ hii tuliyonayo sasa.

Hili ni jambo linalowezekana iwapo tutakuwa na mshikamano madhubuti bila kujali vyama vyetu vya siasa.

Watanzania wapo tayari, wanapaswa kuongozwa tu. Uongozi huu ni lazima uwe na watu wasiopenda yanayoendelea nchini ndani ya watawala, walio nje ya watawala, Wafanyakazi, Wakulima, Wavuvi, Wafugaji, Vjana, Wanawake, Wafanyabiashara, wana harakati na kila mtu anayetaka Tanzania na Zanzibar zilizo njema zenye Uhuru na Demokrasia.

Tunaweza tukiamua. Haya #twenzetu tukaunde vuguvugu hili kuanzia mitaani tunamoishi, vijijini na mijini.

Dar Es Salaam
5/11/2018
Tufanyeje? It’s so simple, ukianza wewe kuacha ubinafsi, tamaa ya pesa, tamaa ya vyeo na usaliti the rest can easily be done. Mimi CCM but I like to have a strong opposition as a watchdog for checks and balance ila wewe ulishiriki sana kuidhoofisha chadema na pia ulimsaliti mama Annah Mgwira kipindi cha Kampeni na ukataka aache kampeni eti chama hakina pesa. Mama akawa strong akasonga mbele. Ndio maana sikushangaa alipohamia CCM maana ulimuumiza sana. Sasa leo unakuja na hizi ngonjera who do you think will trust you? Bora tubaki na rais wetu kulikoni kukufuata wewe usiye na msimamo.
 
Umetoka lini selo? Watu zaidi ya 100 kufariki ndani ya kijiji kimoja siyo jambo dogo, yafaa ukaoneshe makaburi.

Hongera kwa kutoka mikononi boss
Ad hominem is a fallacious argumentative strategy whereby genuine discussion of the topic at hand is avoided by instead attacking the character, motive, or other attribute of the person making the argument, or persons associated with the argument, rather than attacking the substance of the argument itself.
 
Back
Top Bottom