Zitto Kabwe: Nini kifanyike Tanzania?

Zitto Kabwe: Nini kifanyike Tanzania?

Ndugu Zitto Kabwe, juzi tu umetuacha kwenye taharuki mpaka sasa tunashindwa kujua wa kumuamini ni nani kati yako na polisi kuhusiana na tuhuma ulizotoa za kuuwawa kwa watu zaidi ya 100 ndani ya kijiji kimoja, tuthibitishie basi hilo kwanza hata kwa kuonesha makaburi tu maana watu 100 ndani ya kijiji kimoja sio mchezo, angalau tuthibitishie hilo kwanza basi ili tujenge imani na wewe lasivyo tuamini kuwa huna source reliable za habari zako ila unaokoteleza vijiweni!!!
 
Anzisha vuguvugu nasi tutakufuata
Nalog off
Kweli nchi hii iko ICU Hata zamani nilitaka kuangalia taarifa ya habari ya ITV siku hizi nasubiri ya BBC ya saa tatu make nchi hii imekosa dira. Hakuna tofauti kati ya habari ya TBC na ITV kwasababu hata wamiliki wa vituo vya habari hawajiamini kuanika ukweli, badala ya kuripoti matukio wanatunga ngonjera kusifu jiwe
 
Huyu mtu au dogo anaitwa Zitto sijui yukoje???!!! Kuna hofu gani TZ?? Kama iko hofu basi ni miongoni mwa wachache sana tena sana ambaosidhani wanafika hata watano ambao wao hawataki kutii mamlaka na wanadhani wanajua kila kitu kwa niaba ya Watanzania...hakuna democracy without restrictions...ikiwemo democracy ya aina hiyo basi hiyo ni chaos....Mimi naona yaliyomo kwenye hoja iliyowekwa hapa ni ya kuchochea vurugu....Kuandika eti "tunaweza tukiamua, haya twenzetu tukaunda vuguvugu hili kuanzia mitaani tunamoishi, vijijini na mijini" ni maneno ya uchochezi ili kuleta vurugu katika nchi...kama maneno haya kweli ni ya zitto basi huyu dogo ana matatizo na ni sahihi kwa dola kumshughulikia....halafu kuandika kuwa eti "watanzania wapo tayari wanapaswa kuongozwa tu" kwa maana ya kuasi mamlaka ni uchochezi wa kiwango cha hali ya juu kabisa...huyu dogo kama kweli ameandika yeye ni vema afunzwe adabu..watanzania wa wapi hao ambao wapo tayari kuleta vurugu!!!???
We hujitambui
 
Sina haja ya kujua alitengenezaje kwani ni FIX iliyokubuhu . Eti dunia yote ilijaa maji na safina kuelea !!!
 
Mkuu, unaweza kuelezea hizo mila na tamaduni za Kitanzania ambazo demokrasia (a western construct) lazima iziakisi?
Usitakeujitoa akili wewe. Unaona utamaduni wa Kiafrika na kizungu upo sawa?
 
Usitakeujitoa akili wewe. Unaona utamaduni wa Kiafrika na kizungu upo sawa?

Dah! Mbona lugha mbaya tena mkuu? Nimeuliza kwa nia ya kupenda kujadili hoja yako.

Pili, utamaduni wa Kiafrika ndiyo utamaduni wa Kitanzania? Afrika ni kubwa mno! Hata kusema utamaduni wa Kitanzania, inaweza kuwa ni simplistic assertion tu!

Tatu, ukitaka “utamaduni wa Kitanzania” uakisi kwenye vitu vinavyotoka Magharibi/Kaskazini basi usi-cherrypick. Demokrasia ni moja ya matrilioni ya vitu na masuala yaliyoletwa.

Nne, tujadili kwa lugha ya staha.
 
Watanzania tumeshaamuka usingizini huu siyo wakati wa kudanganya tena we zito,ulituibia ilitutosha hapa kila mtu yuko macho

Kama bado una sababu imani kwamba yupo mtanzania atafuata uongo wenu Hayupo tena ,we malizia ubunge uende ujerumani kutafuta Maisha mengine haya huyawezi
 
Mkuu Z
Tatizo lilipo siku tukigundua tutalitatua.
Sitaki kukanusha lakini kuwasemea wanachi kwamba wanaishi kwa hofu, bora ungesema wewe unaishi kwa hofu maana mimi hapa nilipo sina hofu yoyote.
Wananchi huwa tunaweka imani kwa viongozi, hivyo inatakiwa viongozi wawe ndiyo dira yetu. Tumeshuhudia mengi upande tuliouamini ukitusaliti hivyo tukakosa dira na ndo maana sasa kila mmoja anapambana na hali yake. Tukianza wewe na CDM, bado hatujui nani alikuwa sahihi na sasa tunawaona meza moja je tuendelee kuwamini kuwa mlifikia suluhu? ni suluhu ipi mbon hatukuona hata kikao cha maridhiano? Au mnakaa pamoja pale ambapo masilahi yenu yanapoguswa?
Tumeshuhudia CDM na Lower sir, bado tuendelee kuwaamini?
Tumeshuhudia wabunge wakiunga mkono juhudi, bado tuendelee kuwaamini?
Wananchi waliokuwa na Imani kubwa kwa kwenu, sasa wamekosa dira, ndo sasa wanaona bora hawa maadui tuliowazoea kuliko mtu mwenye rangi mbili kama kiganja cha mkono.
Mtaani tunamoishi ni kugumu kuanzisha vuguvugu maana tumeshuhudia ninyi mkiwa na wanasheria huku waliokuwa bega kwa bega nanyi wakiozea lupango.

Nawatakia siasa safi na uongozi bora

Fisiemi tamboni
 
Huyu mtu au dogo anaitwa Zitto sijui yukoje???!!! Kuna hofu gani TZ?? Kama iko hofu basi ni miongoni mwa wachache sana tena sana ambaosidhani wanafika hata watano ambao wao hawataki kutii mamlaka na wanadhani wanajua kila kitu kwa niaba ya Watanzania...hakuna democracy without restrictions...ikiwemo democracy ya aina hiyo basi hiyo ni chaos....Mimi naona yaliyomo kwenye hoja iliyowekwa hapa ni ya kuchochea vurugu....Kuandika eti "tunaweza tukiamua, haya twenzetu tukaunda vuguvugu hili kuanzia mitaani tunamoishi, vijijini na mijini" ni maneno ya uchochezi ili kuleta vurugu katika nchi...kama maneno haya kweli ni ya zitto basi huyu dogo ana matatizo na ni sahihi kwa dola kumshughulikia....halafu kuandika kuwa eti "watanzania wapo tayari wanapaswa kuongozwa tu" kwa maana ya kuasi mamlaka ni uchochezi wa kiwango cha hali ya juu kabisa...huyu dogo kama kweli ameandika yeye ni vema afunzwe adabu..watanzania wa wapi hao ambao wapo tayari kuleta vurugu!!!???

Watanzania wengi kama siyo wote au ukitoa wanafiki kama wew na wanaolipwa tu labda ndiyo hawana hofu, hivi hata kama kusoma hujui hata picha huoni au ndiyo itifaki zenu za kinafiki
 
Mwalimu nyerere alihubiri falsafa zifuatazo:

Uhuru na umoja,
Uhuru na kazi,
Uhuru na ujamaa,
Uhuru na maendeleo.

Jiwe amevuruga vyote, anakimbia kwa kasi kurudi nyuma.
Jiwe anapaswa ashinikizwe aelewe kuwa tanzania ya sasa inahitaji Uhuru na Katiba mpya zaidi kuliko kutazama SGR.

Wachache sana ndiyo watakuelewa, ila kijani wa lumumba kuelewa kwao mpaka damu itoke masikioni, kama moja linasema eti wananchi wenye hofu hawafiki watano, unabaki unashangaa kama mtu huyo anaishi tz hii au yuko nje ya nchi
 
Acheni hoja zisizo na msingi bwana...Je, ni katika awamu hii tu ndiyo baadhi ya watu hawana uhakika wa hata mlo mmoja?? Mimi nilikuwapo wakati wa kiongozi wetu mpendwa Nyerere na tulikuwa tunapanga foleni kununua unga wa yanga, sukari, kiberiti, mche wa mbuni na mchele, lakini hatukupiga kelele eti tuiasi nchi yetu, tulimpenda Nyerere kwa kuwa alikuwa na nia njema na nchi hii na wala hakujilimbikizia mali...Akaja Mwinyi watu wakawa wanafanya watakavyo chakula kilikuwapo lakini wengine wengi walikuwa hawana uwezo,akaja Mkapa tukaona mashirika yanauzwa watu wakataka kuzuia wale makaburu wasichukue Tanesco lakini wakavurumishwa na polisi na kutandikwa kisawasawa lakini kuna positives zilikuwepo akaja JK hapo ndipo tukaona wenye fedha wakitamba na vyombo vya dola vikidharauliwa na wenye pesa na hata hapo wako ambao kupata mlo ilikuwa ni shida amekuja JPM ameanza kujenga misingi ya utawala bora na misingi imara ya uchumihuku mafisadi na vibaraka wao wakitikiswa na ndipo tunaanza kusikia kelele za eti wako ambao hawapati mlo mmoja na kwamba TZ kuna hofu...Yaani hofu gani hiyo mnaizungumzia???!! Mwacheni JPM achape kazi, acheni fujo, acheni uchochezi...

Ufisadi mnao mtoa jiwe huwa ni ufisadi gani huo? Mnatia aibu kwakweli, jiwe anaweza kuwa fisadi kuliko wote waliotangulia, pamoja na kuwajaza watu hofu lakini ukweli utasemwa tu hata kama wengi watapotezwa
 
Huyu Zito ni mpenda rushwa na hii tabia imejengeka miaka mingi akilini mwake anawatia jambajamba mkiwa dhaifu awavute fedha na amekuwa hivi hata alivyokuwa kwenye ile kamati ya PAC amewasumbua sana mifuko ya jamii akiwatetemesha anahongwa sasa kwenye serikali hii ameona hakuna anayemjali au kusikiliza na sasa anajidai kutaka kuwafarakanisha serikali na wananchi ili aitwe mezani apewe chochote lakini dili lake limekwama . Zito watanzania hawawaamini tena nyie wanasiasa uchwara na ukigeugeu wenu , achana na sisi fata yako sie sio wajinga waliwao pambana na hali yako tumekuchoka.

Semea nafsi yako mkuu, watz wengi wamemchoka jiwe wako unayemlamba viatu.
 
Naunga mkono hoja. Twasubiri tamko tu. Tumechoka. Ndugu yangu engineer wa umeme ni miaka miwili sasa yuko mtaani hata ukimuuliza what is power factor hakumbuki tena.

Inauma sana sana, Kama na umri wangu huu nshaanza kuwa na majukumu mengi hivi kuliko baba wa familia ya watoto 8 sidhani Kama Kuna kutoboa.

Toeni tamko potelea pote mbele kwa mbele tutajua huko. Kipindi hiki hata kununua boksa ya pili unaona Kama ni anasa, maisha haya tutafika kweli?
 
Tufanyeje? It’s so simple, ukianza wewe kuacha ubinafsi, tamaa ya pesa, tamaa ya vyeo na usaliti the rest can easily be done. Mimi CCM but I like to have a strong opposition as a watchdog for checks and balance ila wewe ulishiriki sana kuidhoofisha chadema na pia ulimsaliti mama Annah Mgwira kipindi cha Kampeni na ukataka aache kampeni eti chama hakina pesa. Mama akawa strong akasonga mbele. Ndio maana sikushangaa alipohamia CCM maana ulimuumiza sana. Sasa leo unakuja na hizi ngonjera who do you think will trust you? Bora tubaki na rais wetu kulikoni kukufuata wewe usiye na msimamo.

Baki na jiwe pekeyako au na familia yako
 
ZZK,
Ukiwa tukiwa wakweli na ukiwa mkweli, hakuna uhusiano wa moja kwa moja kati ya mengi uliyoandika na maendeleo. Rwanda wanapiga hatua ya maendeleo kuliko sisi na uhuru walio nao kujieleza umebinywa sana, yet ukipima maendeleo kiuchumi wanafanya vizuri sana kuliko sisi. Uhuru tulio nao ni mkubwa mnoo. Hiyo hofu sijui iko wapi maana wanaokosoa watawala ni wengi na wapo.

Dr.Kitima wa TEC alikosoa kwa uwazi pale UDSM kwenye kongamano la miaka 3 ya JPM, kuwa uwekezaji wa miradi ambayo haikisi uwezo wa Watanzania kumudu bidhaa na huduma toka viwandani kuna haja ukangaliwa kwa jicho la pili na yupo.

Humu JF mara kibao tunakosoa mambo ambayo tunadhani hayaendi sawa na tuko tunaishi bila hofu yoyote.

Mimi ntakuelewa sana kama ukija na hoja ambayo itaongeza ajira kwa vijana na kwa kuwa serikali ilikuwa na uwezo wa kuzinunua korosho zote in 2days kama waunuzi wangegoma kununua kwa 3,000; basi kumbe tuihimize serikali kutumia fedha hizo kuwakopesha Watanzania kuja na miradi (Project Financing) ya kuongeza thamani ya mazao ya kilimo ikiwemo Pamba, Kahawa, Korosho na kuuza zikiwa zimeongezewa thamani, athari yake kiuchumi itazalisha ajira zaidi, atarejesha ndani fedha za kigeni nyingi zaidi kuliko mauzo ya korosho ghafi au pamba ghafi. Matokeo yake fedha zingerejeshwa na tax base ingepanuka.

Binafsi nakuona umekuwa too much subjective kuliko kuwa objective kwa kutoa mifano relevant na mifano mbadala kuliko kuwa na hisia hasi.

Tanzania iko salama na hofu unayoisema kuna wengine hatuioni

Mtu kama wew ulidhani unaweza kuona hofu iliyopo kwa watz? Acha kujipa uwezo usiokuwa nao
 
Mkuu unatamani tuishi maisha ya zamani,watu waendelee kutekwa kwa kuwa zamani watu walikuwa wanatekwa nadhani uzee umekushika vibaya,style up!bwana

Unapoteza mda wako na zee zima bado linategemea buku 7, kwa kuwa watu zamani walitekwa na kuuwawa basi yeye anaona ina justify watu pia kuuwawa hata kipindi hiki, kumbe hata baadhi ya wazee ni bure kabisa
 
Back
Top Bottom