Zitto Kabwe: Nini kifanyike Tanzania?

Zitto Kabwe: Nini kifanyike Tanzania?

Tutakapo kuwa na demokrasia kwenye kaya zetu na vyama vyetu. hakika wananchi tutaona wakati wa kuiondoa CCM umefika. otherwise, unataka kuact kama Mange...tunataka Bunge live!-Kiss my rear End.
 
Zitto umeongea kizalendo sana,kila mtu kaguswa kwa namna yake.

Muhimu ni kuunganisha nguvu ili kuhakikisha demokrasia ,
 
Nini kifanyike Tanzania?

Na Zitto Kabwe

Hali yetu ya sasa

Ni dhahiri kuwa hofu imetanda miongoni mwa Watanzania. Ingawa watawala na mashabiki wao hukanusha jambo hili, ukweli ni kuwa nina amini wao wenyewe ndani ya mioyo yao wanakiri kuwa nchi sasa inaendeshwa kwa hofu na wananchi wamejaa hofu kubwa.

Hivi sasa mwananchi akifanya jambo lolote linaloonekana kuwa kinyume na fikra za watawala, wenzake wanamtazama kwa jicho kuwa atakuwa mhanga wa vitisho, mateso, kutekwa, kupotea ama kubambikiwa kesi.

Hakika jamii iliyojaa hofu haiwezi kuwa jamii huru na kamwe haiwezi kupata maendeleo.

Hofu hii iliyotamalaki imekomazwa na matendo ya utawala kukandamiza uhuru wa watu kujieleza, kupata/kupasha habari, kukusanyika na kuhoji/kukosoa Serikali yao. Hizi ni haki za kikatiba ambazo wajibu wa Serikali ni kuzilinda.

Tumeshuhudia wananchi na haswa vijana wakishtakiwa mahakamani kwa makosa yatokanayo na haki yao ya kujieleza kwenye mitandao ya kijamii. Baadhi ya vijana wamehukumiwa vifungo ama kulipa faini.

Mmiliki wa mtandao wa JamiiForums, mtandao wenye kutoa mawazo huru kwa wananchi na kwa muda uliochangia kwa kiasi kikubwa vita dhidi ya ufisadi nchini, Maxence Melo bado anaendelea na kesi zilizofunguliwa dhidi yake ikiwa sehemu ya vitisho vya dola ambavyo pamoja na shauri hilo amekuwa akilazimishwa kutoa majina ya wachangiaji wa mtandao huo.

Licha ya kwamba katiba yetu inaruhusu vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara na kujitangaza, kuandikisha wanachama, kukosoa sera za Serikali na hata kueneza sera mbadala, Serikali kupitia amri isiyo ya kikatiba wala kisheria ya Rais imezuia vyama kufanya shughuli zake hizo halali.

Matamko halali kabisa ya kisiasa ya wanasiasa sasa yanachukuliwa kama ni uchochezi na watoa matamko kushtakiwa kwa makosa ya jinai ikiwemo kwa kutumia sheria mpya kandamizi ya huduma za habari (The Media Services Act 2016 ).

Tumeshuhudia wabunge wakifungwa jela kwa makosa ya matamko ya kisiasa ambayo yangepaswa kujibiwa kisiasa tu kutoka upande wa pili ( watawala ).

Hivi sasa viongozi wakuu wa vyama vya upinzani wanakwenda mahakamani kila wiki kujibu tuhuma za kisiasa, lengo likiwa ni kuwapotezea muda na kuwajaza hofu washindwe kufanya shughuli zao ipasavyo.

Utawala umeweza kusambaza hofu kwa kugusa kila kundi katika jamii. Wanasiasa wanatishiwa na kesi za uchochezi, kutekwa au majaribio ya kuuawa kwa kupigwa risasi mchana kweupe ndani ya eneo lenye ulinzi mkubwa.

Waandishi wa Habari wanatishwa kwa ama vyombo vya habari kama magazeti kufungiwa au kutekwa na kutoonekana kabisa; Wakulima bei za mazao yao zimeporomoshwa makusudi kutokana na maamuzi ya hovyo ya kisera ya Serikali; Wavuvi wanachomewa nyavu zao na mitumbu yao kuchomwa moto; Wafugaji wanaondolewa kwenye maeneo yao ya malisho ili kuanzisha ranchi binafsi na wengine kuuwawa; Wafanyabiashara wanabambikiwa kesi ama kodi kubwa ili kuwakomesha na kuweka utii kwa dola; Wanawake wanatukanwa na kudhalilishwa ikiwemo kuwanyima fursa ya kujiendeleza kimasomo watoto wa kike wanaopata uja uzito mashuleni.

Viongozi wa dini wanaojaribu kuhoji watawala wanachunguzwa uraia wao; Wanaharakati wa asasi za kijamii wanaotoa mawazo yasiyopendeza watawala wanatangazwa sio raia wa Tanzania na asasi zao kutishiwa kufutwa kwa kutungiwa kanuni kandamizi za uendeshaji wa asasi hizo.

Wananchi kwa ujumla wanaumizwa na hali mbaya ya uchumi inayotokana na maamuzi ya hovyo ya kisera ya Serikali katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo. Wananchi wa Zanzibar wamenyimwa haki ya kuongozwa na Serikali waliyoichagua katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Hakuna kundi katika jamii ambalo limebakizwa, kila kundi limeguswa.

Tunataka nini?
Kwa maoni yangu Watanzania wengi wanapenda kuwa huru; Uhuru wa Mawazo, kujieleza, kukusanyika nk. Nadhani tunataka Tanzania yenye raia wenye uhuru kwa mujibu wa Katiba. Vyama vya siasa viwe huru kufanya shughuli zao bila bugudha na kwa mujibu wa sheria, Bunge la Wananchi liwe huru kuisimamia Serikali bila kuzongwazongwa na Watendaji, vyombo vya habari viwe huru kuandika/kutangaza habari bila woga wala upendeleo; Wananchi wawe huru kuikosoa serikali dhidi ya sera zake kandamizi zinazowasokomeza kwenye umasikini, Wazanzibari wapate haki yao ya uchaguzi (electoral justice) waliyoporwa Oktoba 2015 na viongozi wa dini na asasi za kiraia wawe huru kufanya kazi zao bila vitisho. Kiufupi tunataka nchi ya kidemokrasia ambayo asasi za kidemokrasia zinatimiza wajibu wao kwa uhuru.

Tufanye nini?

Sasa wakati umefika wa kujenga mshikamano kurejesha demokrasia tuliyokuwa nayo nchini na kujenga demokrasia madhubuti ambayo haitachezewa tena na yeyote. Haitoshi kila mtu kusema lake kwa wakati wake anapoguswa na matendo ya kidikteta, tunapaswa kuwa na sauti nyingi lakini zinazoratibiwa ili kuhakikisha kuwa tunalinda haki za watu na kuhami uchumi wa nchi wetu usiendelee kuporomoka. Tunapaswa kuwa na harakati za kutetea haki za kijamii (social justice), haki za kujieleza (freedom of speech) na Demokrasia. Tunapaswa kujenga vuguvugu pana la watu a broad based popular movement) ili kuleta mabadiliko ya kijamii, kiuchumi na kisiasa.

Ili kujenga vuguvugu hili ni lazima kuweka mbele maslahi mapana ya Taifa letu na kuachana na maslahi binafsi ambayo yamekuwa yakitawala siasa za Tanzania kwa miongo miwili sasa bila mafanikio ya maana. Ni lazima kukubali ukweli kuwa, kwa hali ya nchi ilivyo sasa hakuna chama kimoja pekee ama kundi la jamii moja pekee linaweza kukabili utawala dhalimu wa kidikteta uliopo nchini na kushinda. Wasioweza kuukabili ubinafsi wao kwenye mambo haya tuwaombe basi wauweke kama akiba kisha tukimaliza kazi hii ya mabadiliko waendelee nao. Kila jambo tufanyalo lazima lijibu swali ‘ hili linatusaidia kutufikisha kwenye lengo la kuondoa utawala wa kidikteta nchini?’

Ni lazima tuwe na mshikamano katika kukabili dubwana tunalokabiliana nalo. Hatupaswi kuruhusu hata siku moja ya ziada baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 tukiwa na ‘regime’ hii tuliyonayo sasa.

Hili ni jambo linalowezekana iwapo tutakuwa na mshikamano madhubuti bila kujali vyama vyetu vya siasa.

Watanzania wapo tayari, wanapaswa kuongozwa tu. Uongozi huu ni lazima uwe na watu wasiopenda yanayoendelea nchini ndani ya watawala, walio nje ya watawala, Wafanyakazi, Wakulima, Wavuvi, Wafugaji, Vjana, Wanawake, Wafanyabiashara, wana harakati na kila mtu anayetaka Tanzania na Zanzibar zilizo njema zenye Uhuru na Demokrasia.

Tunaweza tukiamua. Haya #twenzetu tukaunde vuguvugu hili kuanzia mitaani tunamoishi, vijijini na mijini.

Dar Es Salaam
5/11/2018
Ndugu yangu Tanzania bado ni taifa lenye wajinga zaidi ya 90% kwa utafiti wangu ...

Haya yanasababishwa na haya yafuatayo

1) ukosefu wa elimu ya uraia , elimu ya kujitambua na ujinga ulio kithiri mfano hata sasa unaona waliokuwa wanakosoa wanaunga mkono ujinga

2) unafiki na ubinafsi

3) Tabia za kiswahili na umasikini wa akili na roho yaani watu wanaishi kama.misukule bora liende roho mbaya , chuki bila sababu uchawi na vijicho

Yaani bongo ni k...nina

Solution ni kukomalia ninyi vyama vya upinzani mpiganie katiba mpya ile ya yule mzee warioba
 
Neno "democracy " linapendwa na kila mtu... Lakn masharti yake hakuna ayapendaye... Unalala, ukiamka unatoa tamko la kisera bila kupitisha vikao. Kuna democracy hapo?

Je, hili n tamko "binafsi" la Zitto au n msimamo wa ACT-Wazanyeti?

Tuchoree picha ya Tanzania utajayotuletea baada ya kuondoa hii iliyopo... Je, unataka kusema kuwa Tanzania yako:
(1) kila MTu atasema lolote na atatukana yeyote
(2) hakuna kulipa kodi
(3) uvuvi Haram ruksa
(4) Hakuna hifadhi za wanyama wala mapori yatakayohifadhiwa...tutachunga mifugo popote
(5) bunge Hakuna kutunga sheria
(6) nk... Au unamaanisha nini?

Populism inawasumbua sana...
Zitto ni hatari kuliko hao anaotuaminisha ni hatari. Huyu jamaa ni mnafiki na mbinafsi mkubwa.
 
Wanasiasa msituburuze. Tutafanya maamuzi wenyewe tukiwa tayari.
Mshatutia nyege mara nyingi tu kisha mkatuacha njiani. Hatutaki tena!
 
Umetoka lini selo? Watu zaidi ya 100 kufariki ndani ya kijiji kimoja siyo jambo dogo, yafaa ukaoneshe makaburi.

Hongera kwa kutoka mikononi boss
Walizikwa kwenye kaburi la pamoja mafichoni kama congo wanavyofanya
 
Ndugu Zitto, mnasubiri lini kudai Katiba Mpya ama Tume Huru ya Uchaguzi? Mambo yakiendelea katika hali hii hii, kamwe msitarajie mabadiliko. Ni ndoto za mchana.
 
Tunaweza tukiamua. Haya #twenzetu tukaunde vuguvugu hili kuanzia mitaani tunamoishi, vijijini na mijini.
Tatizo huaminiki
Toa kwanza ile laana na dhana ya usaliti uliopewa na chadema
Unahangaika sana kuwavuta chadema lakini wanakuchunia,na hawawezi kukukubali labda Lema afe
Hiyo pesa uliokula utaitema tu kwa kua unaelekea kushindwa vita vibaya sana
 
Hili nalo elimu yake kiduchu ndio maana linashindwa kuelewa kilichozungumuziwa hapo.
Neno "democracy " linapendwa na kila mtu... Lakn masharti yake hakuna ayapendaye... Unalala, ukiamka unatoa tamko la kisera bila kupitisha vikao. Kuna democracy hapo?

Je, hili n tamko "binafsi" la Zitto au n msimamo wa ACT-Wazanyeti?

Tuchoree picha ya Tanzania utajayotuletea baada ya kuondoa hii iliyopo... Je, unataka kusema kuwa Tanzania yako:
(1) kila MTu atasema lolote na atatukana yeyote
(2) hakuna kulipa kodi
(3) uvuvi Haram ruksa
(4) Hakuna hifadhi za wanyama wala mapori yatakayohifadhiwa...tutachunga mifugo popote
(5) bunge Hakuna kutunga sheria
(6) nk... Au unamaanisha nini?

Populism inawasumbua sana...
 
Neno "democracy " linapendwa na kila mtu... Lakn masharti yake hakuna ayapendaye... Unalala, ukiamka unatoa tamko la kisera bila kupitisha vikao. Kuna democracy hapo?

Je, hili n tamko "binafsi" la Zitto au n msimamo wa ACT-Wazanyeti?

Tuchoree picha ya Tanzania utajayotuletea baada ya kuondoa hii iliyopo... Je, unataka kusema kuwa Tanzania yako:
(1) kila MTu atasema lolote na atatukana yeyote
(2) hakuna kulipa kodi
(3) uvuvi Haram ruksa
(4) Hakuna hifadhi za wanyama wala mapori yatakayohifadhiwa...tutachunga mifugo popote
(5) bunge Hakuna kutunga sheria
(6) nk... Au unamaanisha nini?

Populism inawasumbua sana...
Hivyo vyote ulivyo orodhesha ni sawa tatzo lipo hapa..... Unatumia njia gani kudhibiti ama kurekebisha ....je unatumia katiba?? Je unafata sheria stahiki?? Sasa kama unatumia medula yako pekeako unadhan nini kita happen.....lazma utazingua tuuu
 
Nini kifanyike Tanzania?

Na Zitto Kabwe

Hali yetu ya sasa

Ni dhahiri kuwa hofu imetanda miongoni mwa Watanzania. Ingawa watawala na mashabiki wao hukanusha jambo hili, ukweli ni kuwa nina amini wao wenyewe ndani ya mioyo yao wanakiri kuwa nchi sasa inaendeshwa kwa hofu na wananchi wamejaa hofu kubwa.

Hivi sasa mwananchi akifanya jambo lolote linaloonekana kuwa kinyume na fikra za watawala, wenzake wanamtazama kwa jicho kuwa atakuwa mhanga wa vitisho, mateso, kutekwa, kupotea ama kubambikiwa kesi.

Hakika jamii iliyojaa hofu haiwezi kuwa jamii huru na kamwe haiwezi kupata maendeleo.

Hofu hii iliyotamalaki imekomazwa na matendo ya utawala kukandamiza uhuru wa watu kujieleza, kupata/kupasha habari, kukusanyika na kuhoji/kukosoa Serikali yao. Hizi ni haki za kikatiba ambazo wajibu wa Serikali ni kuzilinda.

Tumeshuhudia wananchi na haswa vijana wakishtakiwa mahakamani kwa makosa yatokanayo na haki yao ya kujieleza kwenye mitandao ya kijamii. Baadhi ya vijana wamehukumiwa vifungo ama kulipa faini.

Mmiliki wa mtandao wa JamiiForums, mtandao wenye kutoa mawazo huru kwa wananchi na kwa muda uliochangia kwa kiasi kikubwa vita dhidi ya ufisadi nchini, Maxence Melo bado anaendelea na kesi zilizofunguliwa dhidi yake ikiwa sehemu ya vitisho vya dola ambavyo pamoja na shauri hilo amekuwa akilazimishwa kutoa majina ya wachangiaji wa mtandao huo.

Licha ya kwamba katiba yetu inaruhusu vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara na kujitangaza, kuandikisha wanachama, kukosoa sera za Serikali na hata kueneza sera mbadala, Serikali kupitia amri isiyo ya kikatiba wala kisheria ya Rais imezuia vyama kufanya shughuli zake hizo halali.

Matamko halali kabisa ya kisiasa ya wanasiasa sasa yanachukuliwa kama ni uchochezi na watoa matamko kushtakiwa kwa makosa ya jinai ikiwemo kwa kutumia sheria mpya kandamizi ya huduma za habari (The Media Services Act 2016 ).

Tumeshuhudia wabunge wakifungwa jela kwa makosa ya matamko ya kisiasa ambayo yangepaswa kujibiwa kisiasa tu kutoka upande wa pili ( watawala ).

Hivi sasa viongozi wakuu wa vyama vya upinzani wanakwenda mahakamani kila wiki kujibu tuhuma za kisiasa, lengo likiwa ni kuwapotezea muda na kuwajaza hofu washindwe kufanya shughuli zao ipasavyo.

Utawala umeweza kusambaza hofu kwa kugusa kila kundi katika jamii. Wanasiasa wanatishiwa na kesi za uchochezi, kutekwa au majaribio ya kuuawa kwa kupigwa risasi mchana kweupe ndani ya eneo lenye ulinzi mkubwa.

Waandishi wa Habari wanatishwa kwa ama vyombo vya habari kama magazeti kufungiwa au kutekwa na kutoonekana kabisa; Wakulima bei za mazao yao zimeporomoshwa makusudi kutokana na maamuzi ya hovyo ya kisera ya Serikali; Wavuvi wanachomewa nyavu zao na mitumbu yao kuchomwa moto; Wafugaji wanaondolewa kwenye maeneo yao ya malisho ili kuanzisha ranchi binafsi na wengine kuuwawa; Wafanyabiashara wanabambikiwa kesi ama kodi kubwa ili kuwakomesha na kuweka utii kwa dola; Wanawake wanatukanwa na kudhalilishwa ikiwemo kuwanyima fursa ya kujiendeleza kimasomo watoto wa kike wanaopata uja uzito mashuleni.

Viongozi wa dini wanaojaribu kuhoji watawala wanachunguzwa uraia wao; Wanaharakati wa asasi za kijamii wanaotoa mawazo yasiyopendeza watawala wanatangazwa sio raia wa Tanzania na asasi zao kutishiwa kufutwa kwa kutungiwa kanuni kandamizi za uendeshaji wa asasi hizo.

Wananchi kwa ujumla wanaumizwa na hali mbaya ya uchumi inayotokana na maamuzi ya hovyo ya kisera ya Serikali katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo. Wananchi wa Zanzibar wamenyimwa haki ya kuongozwa na Serikali waliyoichagua katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Hakuna kundi katika jamii ambalo limebakizwa, kila kundi limeguswa.

Tunataka nini?
Kwa maoni yangu Watanzania wengi wanapenda kuwa huru; Uhuru wa Mawazo, kujieleza, kukusanyika nk. Nadhani tunataka Tanzania yenye raia wenye uhuru kwa mujibu wa Katiba. Vyama vya siasa viwe huru kufanya shughuli zao bila bugudha na kwa mujibu wa sheria, Bunge la Wananchi liwe huru kuisimamia Serikali bila kuzongwazongwa na Watendaji, vyombo vya habari viwe huru kuandika/kutangaza habari bila woga wala upendeleo; Wananchi wawe huru kuikosoa serikali dhidi ya sera zake kandamizi zinazowasokomeza kwenye umasikini, Wazanzibari wapate haki yao ya uchaguzi (electoral justice) waliyoporwa Oktoba 2015 na viongozi wa dini na asasi za kiraia wawe huru kufanya kazi zao bila vitisho. Kiufupi tunataka nchi ya kidemokrasia ambayo asasi za kidemokrasia zinatimiza wajibu wao kwa uhuru.

Tufanye nini?

Sasa wakati umefika wa kujenga mshikamano kurejesha demokrasia tuliyokuwa nayo nchini na kujenga demokrasia madhubuti ambayo haitachezewa tena na yeyote. Haitoshi kila mtu kusema lake kwa wakati wake anapoguswa na matendo ya kidikteta, tunapaswa kuwa na sauti nyingi lakini zinazoratibiwa ili kuhakikisha kuwa tunalinda haki za watu na kuhami uchumi wa nchi wetu usiendelee kuporomoka. Tunapaswa kuwa na harakati za kutetea haki za kijamii (social justice), haki za kujieleza (freedom of speech) na Demokrasia. Tunapaswa kujenga vuguvugu pana la watu a broad based popular movement) ili kuleta mabadiliko ya kijamii, kiuchumi na kisiasa.

Ili kujenga vuguvugu hili ni lazima kuweka mbele maslahi mapana ya Taifa letu na kuachana na maslahi binafsi ambayo yamekuwa yakitawala siasa za Tanzania kwa miongo miwili sasa bila mafanikio ya maana. Ni lazima kukubali ukweli kuwa, kwa hali ya nchi ilivyo sasa hakuna chama kimoja pekee ama kundi la jamii moja pekee linaweza kukabili utawala dhalimu wa kidikteta uliopo nchini na kushinda. Wasioweza kuukabili ubinafsi wao kwenye mambo haya tuwaombe basi wauweke kama akiba kisha tukimaliza kazi hii ya mabadiliko waendelee nao. Kila jambo tufanyalo lazima lijibu swali ‘ hili linatusaidia kutufikisha kwenye lengo la kuondoa utawala wa kidikteta nchini?’

Ni lazima tuwe na mshikamano katika kukabili dubwana tunalokabiliana nalo. Hatupaswi kuruhusu hata siku moja ya ziada baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 tukiwa na ‘regime’ hii tuliyonayo sasa.

Hili ni jambo linalowezekana iwapo tutakuwa na mshikamano madhubuti bila kujali vyama vyetu vya siasa.

Watanzania wapo tayari, wanapaswa kuongozwa tu. Uongozi huu ni lazima uwe na watu wasiopenda yanayoendelea nchini ndani ya watawala, walio nje ya watawala, Wafanyakazi, Wakulima, Wavuvi, Wafugaji, Vjana, Wanawake, Wafanyabiashara, wana harakati na kila mtu anayetaka Tanzania na Zanzibar zilizo njema zenye Uhuru na Demokrasia.

Tunaweza tukiamua. Haya #twenzetu tukaunde vuguvugu hili kuanzia mitaani tunamoishi, vijijini na mijini.

Dar Es Salaam
5/11/2018
Hii ndo tunataka kutoka kwa viongozi wa level yako, hata siku moja baada ya October 2020, Lissu raisi, fatma karume makamu, zito PM na mbowe speaker, tunamaliza kazi asubuhi. Asante zito
 
Huyu mtu au dogo anaitwa Zitto sijui yukoje???!!! Kuna hofu gani TZ?? Kama iko hofu basi ni miongoni mwa wachache sana tena sana ambaosidhani wanafika hata watano ambao wao hawataki kutii mamlaka na wanadhani wanajua kila kitu kwa niaba ya Watanzania...hakuna democracy without restrictions...ikiwemo democracy ya aina hiyo basi hiyo ni chaos....Mimi naona yaliyomo kwenye hoja iliyowekwa hapa ni ya kuchochea vurugu....Kuandika eti "tunaweza tukiamua, haya twenzetu tukaunda vuguvugu hili kuanzia mitaani tunamoishi, vijijini na mijini" ni maneno ya uchochezi ili kuleta vurugu katika nchi...kama maneno haya kweli ni ya zitto basi huyu dogo ana matatizo na ni sahihi kwa dola kumshughulikia....halafu kuandika kuwa eti "watanzania wapo tayari wanapaswa kuongozwa tu" kwa maana ya kuasi mamlaka ni uchochezi wa kiwango cha hali ya juu kabisa...huyu dogo kama kweli ameandika yeye ni vema afunzwe adabu..watanzania wa wapi hao ambao wapo tayari kuleta vurugu!!!???
Unaonaje ukimshtaki?
 
Tatizo nyie wapinzani mmekuwa wasaliti wa wananchi, bado hatujasahau wewe mh zitto na wenzako mlivyofanya harakati za kudhoofisha chadema .. na sasa unakuja na swali ati tufanyeje? acheni unafiki na ubinafsi , vinginevyo mtaendelea kukosa imani ya wananchi.. waacheni wananchi wapambane na hali zao sio kuwahadaa ...
Wewe mpaka sasa hujajua tu nani anaidhoofisha Chadema na upinzani?

Matukio mangapi yametokea ya kuhatarisha sana umoja wetu lakini zaidi ya Zito umemsikia nani akisema. Angalau na Lema.
Mbowe kwa Taarifa yako alikua ni kati ya mitandao miovu kabisa ndani ya CCM.
Amekifanya Chama kimekua kama Kamati ya Send off. Hakisikiki tena wala hakina hoja ya maana zaidi ya kejeli tu.

Zito sio Mnafiki haya anayoyakemea Leo
aliyakemea pia akiwa ndani ya Chadema. Alipinga udikteta ndani ya Chama ,alipinga matumizi mabaya ya fedha za ruzuku, alipinga usiri ,alipinga ukabila ,alipinga udini. Alifukuzwa kwa sababu ya kuwa Mpinzani wa Kweli. Leo hii hata Lissu ukimuuliza ndani ya roho yake atakuambia kuwa Walioonekana kuwa ni wapinzani wa kweli sio Bali ni kundi la mawakala wa CCM na maadui wa Demokrasia.

Ingia kwenye mtandao yote kama kuna cha maana anachoandika Mbowe. Ni mwoga wa kukosolewa kama ilivyo kwa madikteta wote duniani.

Niambie ni lini Mbowe ameleta hoja hata ya kijinga hapa ili tumshauri au tumkosoe au tumpe makavu ajifunze.
Woga umemjaa.
Kwa sasa wanasiasa na wanaharakati ni wawili Tu ,Zito na Tundu.
 
Solutions ni ngumu cos wanasiasa waTz wengi wenu ni wanafiki na wachumia tumbo, leo unasema hivi kesho unasema lile....hamuaminiki
 
Back
Top Bottom