Zitto Kabwe: Nini kifanyike Tanzania?

Zitto Kabwe: Nini kifanyike Tanzania?

Neno "democracy " linapendwa na kila mtu... Lakn masharti yake hakuna ayapendaye... Unalala, ukiamka unatoa tamko la kisera bila kupitisha vikao. Kuna democracy hapo?

Je, hili n tamko "binafsi" la Zitto au n msimamo wa ACT-Wazanyeti?

Tuchoree picha ya Tanzania utajayotuletea baada ya kuondoa hii iliyopo... Je, unataka kusema kuwa Tanzania yako:
(1) kila MTu atasema lolote na atatukana yeyote
(2) hakuna kulipa kodi
(3) uvuvi Haram ruksa
(4) Hakuna hifadhi za wanyama wala mapori yatakayohifadhiwa...tutachunga mifugo popote
(5) bunge Hakuna kutunga sheria
(6) nk... Au unamaanisha nini?

Populism inawasumbua sana...
Na huu ndio ukweli,hata wao tukiwapa nchi leo,hawataweza kutoa uhuru huo,ni wajinga tu ndio wanaweza kuamini maneno ya wanasiasa hawa.
 
Hata kutoka na uhakika wa mlo mmoja nayo ni hofu! Ni watu wangapi hapa hawana uhakika wa kula jioni? Na yote sababu ni John!

Acheni hoja zisizo na msingi bwana...Je, ni katika awamu hii tu ndiyo baadhi ya watu hawana uhakika wa hata mlo mmoja?? Mimi nilikuwapo wakati wa kiongozi wetu mpendwa Nyerere na tulikuwa tunapanga foleni kununua unga wa yanga, sukari, kiberiti, mche wa mbuni na mchele, lakini hatukupiga kelele eti tuiasi nchi yetu, tulimpenda Nyerere kwa kuwa alikuwa na nia njema na nchi hii na wala hakujilimbikizia mali...Akaja Mwinyi watu wakawa wanafanya watakavyo chakula kilikuwapo lakini wengine wengi walikuwa hawana uwezo,akaja Mkapa tukaona mashirika yanauzwa watu wakataka kuzuia wale makaburu wasichukue Tanesco lakini wakavurumishwa na polisi na kutandikwa kisawasawa lakini kuna positives zilikuwepo akaja JK hapo ndipo tukaona wenye fedha wakitamba na vyombo vya dola vikidharauliwa na wenye pesa na hata hapo wako ambao kupata mlo ilikuwa ni shida amekuja JPM ameanza kujenga misingi ya utawala bora na misingi imara ya uchumihuku mafisadi na vibaraka wao wakitikiswa na ndipo tunaanza kusikia kelele za eti wako ambao hawapati mlo mmoja na kwamba TZ kuna hofu...Yaani hofu gani hiyo mnaizungumzia???!! Mwacheni JPM achape kazi, acheni fujo, acheni uchochezi...
 
Huyu mtu au dogo anaitwa Zitto sijui yukoje???!!! Kuna hofu gani TZ?? Kama iko hofu basi ni miongoni mwa wachache sana tena sana ambaosidhani wanafika hata watano ambao wao hawataki kutii mamlaka na wanadhani wanajua kila kitu kwa niaba ya Watanzania...hakuna democracy without restrictions...ikiwemo democracy ya aina hiyo basi hiyo ni chaos....Mimi naona yaliyomo kwenye hoja iliyowekwa hapa ni ya kuchochea vurugu....Kuandika eti "tunaweza tukiamua, haya twenzetu tukaunda vuguvugu hili kuanzia mitaani tunamoishi, vijijini na mijini" ni maneno ya uchochezi ili kuleta vurugu katika nchi...kama maneno haya kweli ni ya zitto basi huyu dogo ana matatizo na ni sahihi kwa dola kumshughulikia....halafu kuandika kuwa eti "watanzania wapo tayari wanapaswa kuongozwa tu" kwa maana ya kuasi mamlaka ni uchochezi wa kiwango cha hali ya juu kabisa...huyu dogo kama kweli ameandika yeye ni vema afunzwe adabu..watanzania wa wapi hao ambao wapo tayari kuleta vurugu!!!???


Kwani na wewe una mamlaka ya kutafsiri maneno ya zito kwa niaba ya watanzania(au wanaosoma hilo andiko)???

Acha kila mtu awe na maoni yake na kuamua vile anaona sahihi......... na wala huna haja ya kuishawishi dola kumchkulia hatua, wacha nao kwa kuwa ni timamu watafanya kile kilicho sahihi..... vinginevyo unaleta upinzani
 
Hivi zile Terrible Teens zinakuja lini? Zitto ukitaka nikuamini niambie Terrible Teens zinakuja lini na zije kweli.
 
Sikuhizi kunamtindo. Kila jambo linalowaudhi wanalitungia sheria kali sana. Mwisho wa siku tutajikita kila kitu cha Kidemokrasia tulikuwa tunaenjoy niharamu mbele ya sheria.
 
Huyu Zito ni mpenda rushwa na hii tabia imejengeka miaka mingi akilini mwake anawatia jambajamba mkiwa dhaifu awavute fedha na amekuwa hivi hata alivyokuwa kwenye ile kamati ya PAC amewasumbua sana mifuko ya jamii akiwatetemesha anahongwa sasa kwenye serikali hii ameona hakuna anayemjali au kusikiliza na sasa anajidai kutaka kuwafarakanisha serikali na wananchi ili aitwe mezani apewe chochote lakini dili lake limekwama . Zito watanzania hawawaamini tena nyie wanasiasa uchwara na ukigeugeu wenu , achana na sisi fata yako sie sio wajinga waliwao pambana na hali yako tumekuchoka.
 
"Democracy is beautiful in theory, in practice it is a fallacy" - Benito Mussolini

Jambo la msingi kila upande uangalie jinsi gani ya kutekeleza kwa vitendo Mkataba wa Dunia wa Haki za Binadamu wa mwaka 1966 ambao kwa Tanzania ulianza kutekelezwa mwaka 1974. Kwa msingi huu sisi wananchi tutambuwe mipaka ya haki na uhuru wetu lkn pia kwa viongozi watambuwe mipaka ya kazi zao - dunia itakuwa mahali salama!

Tunapaswa kutengamana sana
MUNGU ATUONA
 
Zitto hana legacy ya kuzungumza lolote mbele ya watu wanaojielewa. Alizoea vihela hela awamu iliyopita mpaka akaamua kuwasaliti wenzie. Leo asimame aseme bado tumsikilize NO NO NO. Labda akaungane na wananchi wake Kigoma huko
 
Tofauti kati ya Zito Kabwe na Mtatiro ni ipi? Si wote walikuwa Jela/Rumande?
 
Humu naona wengi wanakimbilia kumshambulia Mh Zitto badala ya hoja yake.

Watu hao hao walikimbilia kumshambuli Fatma Karume kwa hoja yake lkn baada ya serikali kutoa msimamo wake wote walifyata. Hivyo hata kwa hili mnajivisha upofu hamyaoni yanayoendelea nchini mwetu but time'll tell.
 
CCM inajiua yenyewe kwa kishindo. (Self Destruction/Suicide Mission)

Their behavior presently is harmful or potentially harmful towards themselves, who engages in their own behavior and decisions, which exist on a continuum, with suicide at one extreme end of the scale.

Deliberate, Born of impulse, and Developed as a habit in their political time since their dawn. Now its time for other political parties to act wisely to wound their credibility/trust/belief/divide/overule them OR ELSE upinzani hawata kuja kupata nafasi nzuri ya kuimwaga CCM kama hii ya sasa hivi. They wont get this perfect opportunity to crush CCM.

Sasa hivi CCM wapo OFF-GUARD Psychological, na wanajipasua wenyewe kwa wenyewe, ni muda muafaka wa kuwapata vizuri kabla hawajavuka vikwazo vyao baina yao wanaavyopitia, wenyewe kwa wenyewe kichama. Upinzani wanaachohitaji ni kuwasetia CCM kaburi wajizike wenyewe kwa wenyewe.


Zitto #urais 2020 kwa kishindo
 
Nini kifanyike Tanzania?

Na Zitto Kabwe

Hali yetu ya sasa

Ni dhahiri kuwa hofu imetanda miongoni mwa Watanzania. Ingawa watawala na mashabiki wao hukanusha jambo hili, ukweli ni kuwa nina amini wao wenyewe ndani ya mioyo yao wanakiri kuwa nchi sasa inaendeshwa kwa hofu na wananchi wamejaa hofu kubwa.

Hivi sasa mwananchi akifanya jambo lolote linaloonekana kuwa kinyume na fikra za watawala, wenzake wanamtazama kwa jicho kuwa atakuwa mhanga wa vitisho, mateso, kutekwa, kupotea ama kubambikiwa kesi.

Hakika jamii iliyojaa hofu haiwezi kuwa jamii huru na kamwe haiwezi kupata maendeleo.

Hofu hii iliyotamalaki imekomazwa na matendo ya utawala kukandamiza uhuru wa watu kujieleza, kupata/kupasha habari, kukusanyika na kuhoji/kukosoa Serikali yao. Hizi ni haki za kikatiba ambazo wajibu wa Serikali ni kuzilinda.

Tumeshuhudia wananchi na haswa vijana wakishtakiwa mahakamani kwa makosa yatokanayo na haki yao ya kujieleza kwenye mitandao ya kijamii. Baadhi ya vijana wamehukumiwa vifungo ama kulipa faini.

Mmiliki wa mtandao wa JamiiForums, mtandao wenye kutoa mawazo huru kwa wananchi na kwa muda uliochangia kwa kiasi kikubwa vita dhidi ya ufisadi nchini, Maxence Melo bado anaendelea na kesi zilizofunguliwa dhidi yake ikiwa sehemu ya vitisho vya dola ambavyo pamoja na shauri hilo amekuwa akilazimishwa kutoa majina ya wachangiaji wa mtandao huo.

Licha ya kwamba katiba yetu inaruhusu vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara na kujitangaza, kuandikisha wanachama, kukosoa sera za Serikali na hata kueneza sera mbadala, Serikali kupitia amri isiyo ya kikatiba wala kisheria ya Rais imezuia vyama kufanya shughuli zake hizo halali.

Matamko halali kabisa ya kisiasa ya wanasiasa sasa yanachukuliwa kama ni uchochezi na watoa matamko kushtakiwa kwa makosa ya jinai ikiwemo kwa kutumia sheria mpya kandamizi ya huduma za habari (The Media Services Act 2016 ).

Tumeshuhudia wabunge wakifungwa jela kwa makosa ya matamko ya kisiasa ambayo yangepaswa kujibiwa kisiasa tu kutoka upande wa pili ( watawala ).

Hivi sasa viongozi wakuu wa vyama vya upinzani wanakwenda mahakamani kila wiki kujibu tuhuma za kisiasa, lengo likiwa ni kuwapotezea muda na kuwajaza hofu washindwe kufanya shughuli zao ipasavyo.

Utawala umeweza kusambaza hofu kwa kugusa kila kundi katika jamii. Wanasiasa wanatishiwa na kesi za uchochezi, kutekwa au majaribio ya kuuawa kwa kupigwa risasi mchana kweupe ndani ya eneo lenye ulinzi mkubwa.

Waandishi wa Habari wanatishwa kwa ama vyombo vya habari kama magazeti kufungiwa au kutekwa na kutoonekana kabisa; Wakulima bei za mazao yao zimeporomoshwa makusudi kutokana na maamuzi ya hovyo ya kisera ya Serikali; Wavuvi wanachomewa nyavu zao na mitumbu yao kuchomwa moto; Wafugaji wanaondolewa kwenye maeneo yao ya malisho ili kuanzisha ranchi binafsi na wengine kuuwawa; Wafanyabiashara wanabambikiwa kesi ama kodi kubwa ili kuwakomesha na kuweka utii kwa dola; Wanawake wanatukanwa na kudhalilishwa ikiwemo kuwanyima fursa ya kujiendeleza kimasomo watoto wa kike wanaopata uja uzito mashuleni.

Viongozi wa dini wanaojaribu kuhoji watawala wanachunguzwa uraia wao; Wanaharakati wa asasi za kijamii wanaotoa mawazo yasiyopendeza watawala wanatangazwa sio raia wa Tanzania na asasi zao kutishiwa kufutwa kwa kutungiwa kanuni kandamizi za uendeshaji wa asasi hizo.

Wananchi kwa ujumla wanaumizwa na hali mbaya ya uchumi inayotokana na maamuzi ya hovyo ya kisera ya Serikali katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo. Wananchi wa Zanzibar wamenyimwa haki ya kuongozwa na Serikali waliyoichagua katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Hakuna kundi katika jamii ambalo limebakizwa, kila kundi limeguswa.

Tunataka nini?
Kwa maoni yangu Watanzania wengi wanapenda kuwa huru; Uhuru wa Mawazo, kujieleza, kukusanyika nk. Nadhani tunataka Tanzania yenye raia wenye uhuru kwa mujibu wa Katiba. Vyama vya siasa viwe huru kufanya shughuli zao bila bugudha na kwa mujibu wa sheria, Bunge la Wananchi liwe huru kuisimamia Serikali bila kuzongwazongwa na Watendaji, vyombo vya habari viwe huru kuandika/kutangaza habari bila woga wala upendeleo; Wananchi wawe huru kuikosoa serikali dhidi ya sera zake kandamizi zinazowasokomeza kwenye umasikini, Wazanzibari wapate haki yao ya uchaguzi (electoral justice) waliyoporwa Oktoba 2015 na viongozi wa dini na asasi za kiraia wawe huru kufanya kazi zao bila vitisho. Kiufupi tunataka nchi ya kidemokrasia ambayo asasi za kidemokrasia zinatimiza wajibu wao kwa uhuru.

Tufanye nini?

Sasa wakati umefika wa kujenga mshikamano kurejesha demokrasia tuliyokuwa nayo nchini na kujenga demokrasia madhubuti ambayo haitachezewa tena na yeyote. Haitoshi kila mtu kusema lake kwa wakati wake anapoguswa na matendo ya kidikteta, tunapaswa kuwa na sauti nyingi lakini zinazoratibiwa ili kuhakikisha kuwa tunalinda haki za watu na kuhami uchumi wa nchi wetu usiendelee kuporomoka. Tunapaswa kuwa na harakati za kutetea haki za kijamii (social justice), haki za kujieleza (freedom of speech) na Demokrasia. Tunapaswa kujenga vuguvugu pana la watu a broad based popular movement) ili kuleta mabadiliko ya kijamii, kiuchumi na kisiasa.

Ili kujenga vuguvugu hili ni lazima kuweka mbele maslahi mapana ya Taifa letu na kuachana na maslahi binafsi ambayo yamekuwa yakitawala siasa za Tanzania kwa miongo miwili sasa bila mafanikio ya maana. Ni lazima kukubali ukweli kuwa, kwa hali ya nchi ilivyo sasa hakuna chama kimoja pekee ama kundi la jamii moja pekee linaweza kukabili utawala dhalimu wa kidikteta uliopo nchini na kushinda. Wasioweza kuukabili ubinafsi wao kwenye mambo haya tuwaombe basi wauweke kama akiba kisha tukimaliza kazi hii ya mabadiliko waendelee nao. Kila jambo tufanyalo lazima lijibu swali ‘ hili linatusaidia kutufikisha kwenye lengo la kuondoa utawala wa kidikteta nchini?’

Ni lazima tuwe na mshikamano katika kukabili dubwana tunalokabiliana nalo. Hatupaswi kuruhusu hata siku moja ya ziada baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 tukiwa na ‘regime’ hii tuliyonayo sasa.

Hili ni jambo linalowezekana iwapo tutakuwa na mshikamano madhubuti bila kujali vyama vyetu vya siasa.

Watanzania wapo tayari, wanapaswa kuongozwa tu. Uongozi huu ni lazima uwe na watu wasiopenda yanayoendelea nchini ndani ya watawala, walio nje ya watawala, Wafanyakazi, Wakulima, Wavuvi, Wafugaji, Vjana, Wanawake, Wafanyabiashara, wana harakati na kila mtu anayetaka Tanzania na Zanzibar zilizo njema zenye Uhuru na Demokrasia.

Tunaweza tukiamua. Haya #twenzetu tukaunde vuguvugu hili kuanzia mitaani tunamoishi, vijijini na mijini.

Dar Es Salaam
5/11/2018
Kaka nakuelewa sana...kwa kweli Magu anapaswa kufungashiwa virago vyake na kushtakiwa, siyo kwa uchafu huu anaoifanyia nchi!
 
Back
Top Bottom