Zitto Kabwe: Nini kifanyike Tanzania?

Zitto Kabwe: Nini kifanyike Tanzania?

Dah! Mbona lugha mbaya tena mkuu? Nimeuliza kwa nia ya kupenda kujadili hoja yako.

Pili, utamaduni wa Kiafrika ndiyo utamaduni wa Kitanzania? Afrika ni kubwa mno! Hata kusema utamaduni wa Kitanzania, inaweza kuwa ni simplistic assertion tu!

Tatu, ukitaka “utamaduni wa Kitanzania” uakisi kwenye vitu vinavyotoka Magharibi/Kaskazini basi usi-cherrypick. Demokrasia ni moja ya matrilioni ya vitu na masuala yaliyoletwa.

Nne, tujadili kwa lugha ya staha.
Ukimuona mtu ni mwelevu lakini anaamua kuifanya hamnazo huwa ananipa shida sana.
Uhuru wa kujieleza sawa lakini uzingatie adabu ya Kitanzania na kiafrika. Matusi bezo kwa watu waliokuzidi umri si jadi yetu. Huo ni mfano mdogo tu
 
Tatizo la kwanza kubwa la wanasiasa wa Tanzania ni kujaliwa unafiki uliopitiliza ,Rais alipokuwa jimboni kwako ulitamka mbele ya umati wa watu wa Kigoma kuwa "wananchi wa Kigoma wanataka maendeleo na wewe Mhe Rais unawaletea maendeleo" .Kwa macho yako mwenyewe umeona maendeleo na kwa kinywa chako ukatamka leo hii tena unapingana na maneno yako.Au ulitamka hayo kwa kuwa ulikuwa naye uso kwa uso? Na sisi wewe tuu hata mwenzako wa Chadema Mchg Msigwa alifanya hivi hivi.Mkipata fursa ya kuonana ana kwa ana hamsemi mkimbilia kwenye social media kulia lia mpate huruma za wananchi afu hapo hapo mtaka tuwaamin kwamba mna dhamira ya dhati ya kutuongoza.Wewe pia Zitto Kabwe ni "Ndumilakuwili" ni hatari sanaa kukuamini mtu kama wewe.

Tatizo lingine ni kila mmoja wenu katika vyama vya siasa anauchu wa kuongoza, kwangu mimi ninavyohisi nyinyi mnaweza kuwa hatari zaidi kutokea katika historia ya taifa letu kwa sababu zifuatazo:-
1.Kuna watu wako nyuma yenu wanaowaongoza hivyo hamatakuwa na maamuzi bali mtakuwa mnaamuliwa
2.Mtaligawa taifa vipande vipande mtakuwa na dhamira ya kumtoa aliye madarakani lakini mioyoni mwenu kila mmoja atakuwa ana dhamira yake hivyo mbeleni mtashindwana tu na kuligharimu taifa letu.
3.Mataifa yanayowatumia kila moja lina interest zake baada ya kutekeleza lengo kuu la kumtoa aliye madarakani yataanza kutekeleza interest zao amabapo hapo itakuwa gharama kwa taifa letu
 
Kweli kabisa siku hizi hata tunavyojadili siasa kwenye vilinge vyetu tunaangaliana kwanza sura kama tunajuana....mkiona sura ngeni kati yenu....ghafla mnaanza stori za kuiponda Manchester United....

Kwa hili la kutujaza hofu watawala wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa, japo haimaanishi watu hatuongei.
Yaaani ninyi mna aliki sana.
 
Tatizo nyie wapinzani mmekuwa wasaliti wa wananchi, bado hatujasahau wewe mh zitto na wenzako mlivyofanya harakati za kudhoofisha chadema .. na sasa unakuja na swali ati tufanyeje? acheni unafiki na ubinafsi , vinginevyo mtaendelea kukosa imani ya wananchi.. waacheni wananchi wapambane na hali zao sio kuwahadaa ...
Ukweli wako nimeuelewa. Wote ni wachumia tumbo, mi huwa naikumbuka sana kauli ya Lema ya NI HESHIMA KUMTUKANA NA KUMZOMEA LOWASA leo hii Lowasa ni msafi duh!
 
Zito acheni kutuahada wananchi, hivi unakumbuka uliyoyafanya Chadema, hata kama huwa tunasahaulishwa kwa matukio ya kila aina, naomba mkumbuke kuwa huwa hatusau bali huwa tunaacha tu na kupokea kipya kilichokuja lakin katika ubongo kumbukumbu hudumu na hubakia miliele. Kaka hakuna mtu mnafiki kama wewe, Siasa za kiki zitaisha muda wake ni suala la muda tu, sio kwa watawala au wapinzani, muda utafika kila jambo litakuwa wazi
 
Tukianza kuangalia nyuma badala ya mbele tunaokoenda tutakuwa tunakosea. Sema wewe ni lisisiemu tu unaogopa umoja wa wanasiasa wa upinzani sasa hivi. Wewe una uchungu kuliko Lema, Heche na Mbowe ambao wameamua kuungana na kina Zitto kuhakikisha hali iliyopo sasa inaondoka. Furaha yako ni kuona hawapatani na kupatana kwako kunakutia chuki. Pole sana

Misiba hukutanisha maadui
Usidanganywe na muungano, tumia akili yako kufikiria sio kila wanachofanya upinzani kiko sawa, tumia ikili yako vizuri usifuate mkumbo kisa fulani kasema, tatizo tunaishi kwa matukio nyie ndio mliomporomoshea Zito matusi kipindi kile mnasema anatumika na watawala leo hii zito msafi. Acha kufuata mkumbo kila mtu hapo ni mchumia tumbo.
 
Umetoka lini selo? Watu zaidi ya 100 kufariki ndani ya kijiji kimoja siyo jambo dogo, yafaa ukaoneshe makaburi.

Hongera kwa kutoka mikononi boss
huyu kaka ni muongo, zito acha kiki fanya siasa zitazoleta faida kwa badae TZ
 
Usidanganywe na muungano, tumia akili yako kufikiria sio kila wanachofanya upinzani kiko sawa, tumia ikili yako vizuri usifuate mkumbo kisa fulani kasema, tatizo tunaishi kwa matukio nyie ndio mliomporomoshea Zito matusi kipindi kile mnasema anatumika na watawala leo hii zito msafi. Acha kufuata mkumbo kila mtu hapo ni mchumia tumbo.
Sawa sio kila wanachofanya kiko sawa, kwa hiyo unakiri kuna wanayofanya yako sawa. Inatosha, wasalimie Lumumba
 
Nini kifanyike Tanzania?

Na Zitto Kabwe

Hali yetu ya sasa

Ni dhahiri kuwa hofu imetanda miongoni mwa Watanzania. Ingawa watawala na mashabiki wao hukanusha jambo hili, ukweli ni kuwa nina amini wao wenyewe ndani ya mioyo yao wanakiri kuwa nchi sasa inaendeshwa kwa hofu na wananchi wamejaa hofu kubwa.

Hivi sasa mwananchi akifanya jambo lolote linaloonekana kuwa kinyume na fikra za watawala, wenzake wanamtazama kwa jicho kuwa atakuwa mhanga wa vitisho, mateso, kutekwa, kupotea ama kubambikiwa kesi.

Hakika jamii iliyojaa hofu haiwezi kuwa jamii huru na kamwe haiwezi kupata maendeleo.

Hofu hii iliyotamalaki imekomazwa na matendo ya utawala kukandamiza uhuru wa watu kujieleza, kupata/kupasha habari, kukusanyika na kuhoji/kukosoa Serikali yao. Hizi ni haki za kikatiba ambazo wajibu wa Serikali ni kuzilinda.

Tumeshuhudia wananchi na haswa vijana wakishtakiwa mahakamani kwa makosa yatokanayo na haki yao ya kujieleza kwenye mitandao ya kijamii. Baadhi ya vijana wamehukumiwa vifungo ama kulipa faini.

Mmiliki wa mtandao wa JamiiForums, mtandao wenye kutoa mawazo huru kwa wananchi na kwa muda uliochangia kwa kiasi kikubwa vita dhidi ya ufisadi nchini, Maxence Melo bado anaendelea na kesi zilizofunguliwa dhidi yake ikiwa sehemu ya vitisho vya dola ambavyo pamoja na shauri hilo amekuwa akilazimishwa kutoa majina ya wachangiaji wa mtandao huo.

Licha ya kwamba katiba yetu inaruhusu vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara na kujitangaza, kuandikisha wanachama, kukosoa sera za Serikali na hata kueneza sera mbadala, Serikali kupitia amri isiyo ya kikatiba wala kisheria ya Rais imezuia vyama kufanya shughuli zake hizo halali.

Matamko halali kabisa ya kisiasa ya wanasiasa sasa yanachukuliwa kama ni uchochezi na watoa matamko kushtakiwa kwa makosa ya jinai ikiwemo kwa kutumia sheria mpya kandamizi ya huduma za habari (The Media Services Act 2016 ).

Tumeshuhudia wabunge wakifungwa jela kwa makosa ya matamko ya kisiasa ambayo yangepaswa kujibiwa kisiasa tu kutoka upande wa pili ( watawala ).

Hivi sasa viongozi wakuu wa vyama vya upinzani wanakwenda mahakamani kila wiki kujibu tuhuma za kisiasa, lengo likiwa ni kuwapotezea muda na kuwajaza hofu washindwe kufanya shughuli zao ipasavyo.

Utawala umeweza kusambaza hofu kwa kugusa kila kundi katika jamii. Wanasiasa wanatishiwa na kesi za uchochezi, kutekwa au majaribio ya kuuawa kwa kupigwa risasi mchana kweupe ndani ya eneo lenye ulinzi mkubwa.

Waandishi wa Habari wanatishwa kwa ama vyombo vya habari kama magazeti kufungiwa au kutekwa na kutoonekana kabisa; Wakulima bei za mazao yao zimeporomoshwa makusudi kutokana na maamuzi ya hovyo ya kisera ya Serikali; Wavuvi wanachomewa nyavu zao na mitumbu yao kuchomwa moto; Wafugaji wanaondolewa kwenye maeneo yao ya malisho ili kuanzisha ranchi binafsi na wengine kuuwawa; Wafanyabiashara wanabambikiwa kesi ama kodi kubwa ili kuwakomesha na kuweka utii kwa dola; Wanawake wanatukanwa na kudhalilishwa ikiwemo kuwanyima fursa ya kujiendeleza kimasomo watoto wa kike wanaopata uja uzito mashuleni.

Viongozi wa dini wanaojaribu kuhoji watawala wanachunguzwa uraia wao; Wanaharakati wa asasi za kijamii wanaotoa mawazo yasiyopendeza watawala wanatangazwa sio raia wa Tanzania na asasi zao kutishiwa kufutwa kwa kutungiwa kanuni kandamizi za uendeshaji wa asasi hizo.

Wananchi kwa ujumla wanaumizwa na hali mbaya ya uchumi inayotokana na maamuzi ya hovyo ya kisera ya Serikali katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo. Wananchi wa Zanzibar wamenyimwa haki ya kuongozwa na Serikali waliyoichagua katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Hakuna kundi katika jamii ambalo limebakizwa, kila kundi limeguswa.

Tunataka nini?
Kwa maoni yangu Watanzania wengi wanapenda kuwa huru; Uhuru wa Mawazo, kujieleza, kukusanyika nk. Nadhani tunataka Tanzania yenye raia wenye uhuru kwa mujibu wa Katiba. Vyama vya siasa viwe huru kufanya shughuli zao bila bugudha na kwa mujibu wa sheria, Bunge la Wananchi liwe huru kuisimamia Serikali bila kuzongwazongwa na Watendaji, vyombo vya habari viwe huru kuandika/kutangaza habari bila woga wala upendeleo; Wananchi wawe huru kuikosoa serikali dhidi ya sera zake kandamizi zinazowasokomeza kwenye umasikini, Wazanzibari wapate haki yao ya uchaguzi (electoral justice) waliyoporwa Oktoba 2015 na viongozi wa dini na asasi za kiraia wawe huru kufanya kazi zao bila vitisho. Kiufupi tunataka nchi ya kidemokrasia ambayo asasi za kidemokrasia zinatimiza wajibu wao kwa uhuru.

Tufanye nini?

Sasa wakati umefika wa kujenga mshikamano kurejesha demokrasia tuliyokuwa nayo nchini na kujenga demokrasia madhubuti ambayo haitachezewa tena na yeyote. Haitoshi kila mtu kusema lake kwa wakati wake anapoguswa na matendo ya kidikteta, tunapaswa kuwa na sauti nyingi lakini zinazoratibiwa ili kuhakikisha kuwa tunalinda haki za watu na kuhami uchumi wa nchi wetu usiendelee kuporomoka. Tunapaswa kuwa na harakati za kutetea haki za kijamii (social justice), haki za kujieleza (freedom of speech) na Demokrasia. Tunapaswa kujenga vuguvugu pana la watu a broad based popular movement) ili kuleta mabadiliko ya kijamii, kiuchumi na kisiasa.

Ili kujenga vuguvugu hili ni lazima kuweka mbele maslahi mapana ya Taifa letu na kuachana na maslahi binafsi ambayo yamekuwa yakitawala siasa za Tanzania kwa miongo miwili sasa bila mafanikio ya maana. Ni lazima kukubali ukweli kuwa, kwa hali ya nchi ilivyo sasa hakuna chama kimoja pekee ama kundi la jamii moja pekee linaweza kukabili utawala dhalimu wa kidikteta uliopo nchini na kushinda. Wasioweza kuukabili ubinafsi wao kwenye mambo haya tuwaombe basi wauweke kama akiba kisha tukimaliza kazi hii ya mabadiliko waendelee nao. Kila jambo tufanyalo lazima lijibu swali ‘ hili linatusaidia kutufikisha kwenye lengo la kuondoa utawala wa kidikteta nchini?’

Ni lazima tuwe na mshikamano katika kukabili dubwana tunalokabiliana nalo. Hatupaswi kuruhusu hata siku moja ya ziada baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 tukiwa na ‘regime’ hii tuliyonayo sasa.

Hili ni jambo linalowezekana iwapo tutakuwa na mshikamano madhubuti bila kujali vyama vyetu vya siasa.

Watanzania wapo tayari, wanapaswa kuongozwa tu. Uongozi huu ni lazima uwe na watu wasiopenda yanayoendelea nchini ndani ya watawala, walio nje ya watawala, Wafanyakazi, Wakulima, Wavuvi, Wafugaji, Vjana, Wanawake, Wafanyabiashara, wana harakati na kila mtu anayetaka Tanzania na Zanzibar zilizo njema zenye Uhuru na Demokrasia.

Tunaweza tukiamua. Haya #twenzetu tukaunde vuguvugu hili kuanzia mitaani tunamoishi, vijijini na mijini.

Dar Es Salaam
5/11/2018
Kwanza nikiri kuwa sikuusoma waraka wote huu. Hii inatokana na sentenso ya kwanza kuwa mwandishi "ANA AMINI" hivyo ni suala la imani zaidi, imani ya Zitto na siyo kwa facts and figures! Hapo ndio penye tatizo. Ni vigumu sana kufuata "imani" ya mtu hasa hasa inapokuja kwenye mambo ya siasa.
 
Kweli kabisa siku hizi hata tunavyojadili siasa kwenye vilinge vyetu tunaangaliana kwanza sura kama tunajuana....mkiona sura ngeni kati yenu....ghafla mnaanza stori za kuiponda Manchester United....

Kwa hili la kutujaza hofu watawala wamefanikiwa kwa kiasi kikubwa, japo haimaanishi watu hatuongei.
 
Nikiona post kama hizi najikumbusha nyimbo tulizoimbishwa zamani kama kasuku kumbe utendaji kazi wake unazuiliwa na wale waliokuwa wakituimbisha nyimbo hizo:-
Naanza kuimba nena ....Afadhali kuwa na taifa ambalo
Halina siraha za kisasa lakini
Lina moyo wa ushujaa
Kuliko kuwa na taifa
Lenye siraha za kisasa lakini vijana wake ni waoga. *Mwisho*
Vijana watanzania ni waoga kwa sababu wana elimu ya kikoloni, wamejifunza kukubali kila kitu hata kama wanaumia.
 
Pamoja na kujifunza to let go some of the things, lakini ni kazi kweli kweli kumwamini ZZK, alitumika na jK kuharibia Watz future, sasa kama JPM hamuhitaji asituijie na story za nini kifanyike, kama sio yeye na hujuma zake huenda suala la nini kifanyike lisingekuwepo wala lisingekuwa na mantiki, kwa maana tungekuwa na kitu kingine kabisaaa TZ. TUKIJIDANGANYA KUTAFUTA UKOMBOZI KWA KUUNGANA NA WASALITI grade ya ZZK, TUTAKUWA TUMEFANYA KOSA from the start. Heri ukawie ufike.
 
Urafiki na nyoka tena chatu ni jambo hatari sana, wakati wowote njaa ikimshika anakumeza, ndio huyo kijana
 
Nini kifanyike Tanzania?

Na Zitto Kabwe

Hali yetu ya sasa

Ni dhahiri kuwa hofu imetanda miongoni mwa Watanzania. Ingawa watawala na mashabiki wao hukanusha jambo hili, ukweli ni kuwa nina amini wao wenyewe ndani ya mioyo yao wanakiri kuwa nchi sasa inaendeshwa kwa hofu na wananchi wamejaa hofu kubwa.

Hivi sasa mwananchi akifanya jambo lolote linaloonekana kuwa kinyume na fikra za watawala, wenzake wanamtazama kwa jicho kuwa atakuwa mhanga wa vitisho, mateso, kutekwa, kupotea ama kubambikiwa kesi.

Hakika jamii iliyojaa hofu haiwezi kuwa jamii huru na kamwe haiwezi kupata maendeleo.

Hofu hii iliyotamalaki imekomazwa na matendo ya utawala kukandamiza uhuru wa watu kujieleza, kupata/kupasha habari, kukusanyika na kuhoji/kukosoa Serikali yao. Hizi ni haki za kikatiba ambazo wajibu wa Serikali ni kuzilinda.

Tumeshuhudia wananchi na haswa vijana wakishtakiwa mahakamani kwa makosa yatokanayo na haki yao ya kujieleza kwenye mitandao ya kijamii. Baadhi ya vijana wamehukumiwa vifungo ama kulipa faini.

Mmiliki wa mtandao wa JamiiForums, mtandao wenye kutoa mawazo huru kwa wananchi na kwa muda uliochangia kwa kiasi kikubwa vita dhidi ya ufisadi nchini, Maxence Melo bado anaendelea na kesi zilizofunguliwa dhidi yake ikiwa sehemu ya vitisho vya dola ambavyo pamoja na shauri hilo amekuwa akilazimishwa kutoa majina ya wachangiaji wa mtandao huo.

Licha ya kwamba katiba yetu inaruhusu vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara na kujitangaza, kuandikisha wanachama, kukosoa sera za Serikali na hata kueneza sera mbadala, Serikali kupitia amri isiyo ya kikatiba wala kisheria ya Rais imezuia vyama kufanya shughuli zake hizo halali.

Matamko halali kabisa ya kisiasa ya wanasiasa sasa yanachukuliwa kama ni uchochezi na watoa matamko kushtakiwa kwa makosa ya jinai ikiwemo kwa kutumia sheria mpya kandamizi ya huduma za habari (The Media Services Act 2016 ).

Tumeshuhudia wabunge wakifungwa jela kwa makosa ya matamko ya kisiasa ambayo yangepaswa kujibiwa kisiasa tu kutoka upande wa pili ( watawala ).

Hivi sasa viongozi wakuu wa vyama vya upinzani wanakwenda mahakamani kila wiki kujibu tuhuma za kisiasa, lengo likiwa ni kuwapotezea muda na kuwajaza hofu washindwe kufanya shughuli zao ipasavyo.

Utawala umeweza kusambaza hofu kwa kugusa kila kundi katika jamii. Wanasiasa wanatishiwa na kesi za uchochezi, kutekwa au majaribio ya kuuawa kwa kupigwa risasi mchana kweupe ndani ya eneo lenye ulinzi mkubwa.

Waandishi wa Habari wanatishwa kwa ama vyombo vya habari kama magazeti kufungiwa au kutekwa na kutoonekana kabisa; Wakulima bei za mazao yao zimeporomoshwa makusudi kutokana na maamuzi ya hovyo ya kisera ya Serikali; Wavuvi wanachomewa nyavu zao na mitumbu yao kuchomwa moto; Wafugaji wanaondolewa kwenye maeneo yao ya malisho ili kuanzisha ranchi binafsi na wengine kuuwawa; Wafanyabiashara wanabambikiwa kesi ama kodi kubwa ili kuwakomesha na kuweka utii kwa dola; Wanawake wanatukanwa na kudhalilishwa ikiwemo kuwanyima fursa ya kujiendeleza kimasomo watoto wa kike wanaopata uja uzito mashuleni.

Viongozi wa dini wanaojaribu kuhoji watawala wanachunguzwa uraia wao; Wanaharakati wa asasi za kijamii wanaotoa mawazo yasiyopendeza watawala wanatangazwa sio raia wa Tanzania na asasi zao kutishiwa kufutwa kwa kutungiwa kanuni kandamizi za uendeshaji wa asasi hizo.

Wananchi kwa ujumla wanaumizwa na hali mbaya ya uchumi inayotokana na maamuzi ya hovyo ya kisera ya Serikali katika utekelezaji wa miradi mikubwa ya maendeleo. Wananchi wa Zanzibar wamenyimwa haki ya kuongozwa na Serikali waliyoichagua katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015. Hakuna kundi katika jamii ambalo limebakizwa, kila kundi limeguswa.

Tunataka nini?
Kwa maoni yangu Watanzania wengi wanapenda kuwa huru; Uhuru wa Mawazo, kujieleza, kukusanyika nk. Nadhani tunataka Tanzania yenye raia wenye uhuru kwa mujibu wa Katiba. Vyama vya siasa viwe huru kufanya shughuli zao bila bugudha na kwa mujibu wa sheria, Bunge la Wananchi liwe huru kuisimamia Serikali bila kuzongwazongwa na Watendaji, vyombo vya habari viwe huru kuandika/kutangaza habari bila woga wala upendeleo; Wananchi wawe huru kuikosoa serikali dhidi ya sera zake kandamizi zinazowasokomeza kwenye umasikini, Wazanzibari wapate haki yao ya uchaguzi (electoral justice) waliyoporwa Oktoba 2015 na viongozi wa dini na asasi za kiraia wawe huru kufanya kazi zao bila vitisho. Kiufupi tunataka nchi ya kidemokrasia ambayo asasi za kidemokrasia zinatimiza wajibu wao kwa uhuru.

Tufanye nini?

Sasa wakati umefika wa kujenga mshikamano kurejesha demokrasia tuliyokuwa nayo nchini na kujenga demokrasia madhubuti ambayo haitachezewa tena na yeyote. Haitoshi kila mtu kusema lake kwa wakati wake anapoguswa na matendo ya kidikteta, tunapaswa kuwa na sauti nyingi lakini zinazoratibiwa ili kuhakikisha kuwa tunalinda haki za watu na kuhami uchumi wa nchi wetu usiendelee kuporomoka. Tunapaswa kuwa na harakati za kutetea haki za kijamii (social justice), haki za kujieleza (freedom of speech) na Demokrasia. Tunapaswa kujenga vuguvugu pana la watu a broad based popular movement) ili kuleta mabadiliko ya kijamii, kiuchumi na kisiasa.

Ili kujenga vuguvugu hili ni lazima kuweka mbele maslahi mapana ya Taifa letu na kuachana na maslahi binafsi ambayo yamekuwa yakitawala siasa za Tanzania kwa miongo miwili sasa bila mafanikio ya maana. Ni lazima kukubali ukweli kuwa, kwa hali ya nchi ilivyo sasa hakuna chama kimoja pekee ama kundi la jamii moja pekee linaweza kukabili utawala dhalimu wa kidikteta uliopo nchini na kushinda. Wasioweza kuukabili ubinafsi wao kwenye mambo haya tuwaombe basi wauweke kama akiba kisha tukimaliza kazi hii ya mabadiliko waendelee nao. Kila jambo tufanyalo lazima lijibu swali ‘ hili linatusaidia kutufikisha kwenye lengo la kuondoa utawala wa kidikteta nchini?’

Ni lazima tuwe na mshikamano katika kukabili dubwana tunalokabiliana nalo. Hatupaswi kuruhusu hata siku moja ya ziada baada ya uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 tukiwa na ‘regime’ hii tuliyonayo sasa.

Hili ni jambo linalowezekana iwapo tutakuwa na mshikamano madhubuti bila kujali vyama vyetu vya siasa.

Watanzania wapo tayari, wanapaswa kuongozwa tu. Uongozi huu ni lazima uwe na watu wasiopenda yanayoendelea nchini ndani ya watawala, walio nje ya watawala, Wafanyakazi, Wakulima, Wavuvi, Wafugaji, Vjana, Wanawake, Wafanyabiashara, wana harakati na kila mtu anayetaka Tanzania na Zanzibar zilizo njema zenye Uhuru na Demokrasia.

Tunaweza tukiamua. Haya #twenzetu tukaunde vuguvugu hili kuanzia mitaani tunamoishi, vijijini na mijini.

Dar Es Salaam
5/11/2018
Serikali za kidikteta hazina maisha marefu.
 
Jamani jamani jamani huyu jamaa anataka nini? Anataka watanzania tuipindue serikali ya Magufuli?
Hivyo haya aliyo yasema anaamini kuwa ni demokrasia? Kwanini Zitto Kabwe hachukuliwi hatua? Ina maana serikali inamwogopa?

Huyu mtu ni hatari kubwa sana kwa amani ya nchi yetu. Rais Magufuli huyu mtu kwanini anatuchezea hivi? Ana nini cha msingi?
 
Ad hominem is a fallacious argumentative strategy whereby genuine discussion of the topic at hand is avoided by instead attacking the character, motive, or other attribute of the person making the argument, or persons associated with the argument, rather than attacking the substance of the argument itself.
€&£€
 
Back
Top Bottom