Zitto Kabwe na wapinzani wote, kwanini mnapiga tu kelele kuhusu udikteta bila kuchukua hatua zozote? Isn't it a nuisance? Je, 2020 ni CCM pekee?

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,503
113,616
Wanabodi,
Japo bandiko hili liko addressed kwa Mhe. Zitto, lakini hoja zake ni kwa Wapinzani wote, namuelekezea Zitto Kabwe kwa sababu kwa maoni yangu ndio mpinzani pekee kwa sasa anayeweza kusimama na rais Magufuli 2020, na Magufuli akahisi kijoto joto japo kwa mbali.

Ni kwa muda mrefu kumekuwa kukitolewa hoja za udikiteta wa rais Magufuli. Kama watu wale wale, wanatoa hoja zile zile miaka nenda miaka rudi bila kuchukua hatua zozote, then kuendelea kutumia hoja hizo ni kupiga tuu kelele, na kiukweli kabisa kelele zikizidi, zinageika a nuisances.

Swali ni hili

Swali kwa Zitto Kabwe na Wapinzani Wengine: Hoja ya Udikiteta wa Rais Magufuli, Kwa Nini Wewe Zitto na Wapinzani Mnapiga Tuu Kelele Bila Kuchukia Hatua Yoyoye?. Kelele zikizidi Zinageuka Nuisances, Jee Kelele Hizi za Udikiteta wa Rais Magufuli hivi sasa Isn't it a Nuisance?. Kama Upinzani Wenyewe wa Tanzania Ndio Upinzani Huu Ambao Umeishiwa Kabisa Hoja za Msingi!, Jee Tukisema Uchaguzi wa 2020 ni CCM Pekee?, Tutakuwa Tunawakatisha Tamaa Wapinzani? au Tunawaandaa Watanzania kupokea Ukweli Mchungu kuwa Tanzania Hatuna Kabisa Upinzani wa Maana?.

Bandiko hili linafuatia hoja ya Zitto kwenye bandiko hili Tanzania imetimiza Hatua 8 za kujenga Utawala wa Kidikteta?

Tanzania imetimiza Hatua 8 za kujenga Utawala wa Kidikteta?

Licha ushahidi wa wazi wa kusigina Katiba, vyama vya Upinzani hatuchukui hatua yeyote dhidi ya Rais Magufuli licha ya Katiba kutoa nafasi hiyo kwa mujibu wa Ibara ya 46A ya Katiba - kumshtaki Bungeni. Utadhani tumepigwa ganzi au tumesomewa kile Watu wa Ujiji huita Surat Zubaa!

Watanzania watavumilia kuishi kwenye nchi ya kidikteta inayokandamiza Uhuru wa watu? Tusubiri tuone

Zitto Kabwe

Nairobi
Mhe. Zitto, with due respect, kitendo cha kurudia rudia kauli hii ya Magufuli ni dikiteta bila kuchukua hatua zozote, nazo ni kelele tuu.

Watanzania wa sasa hawataki kelele, wanataka matendo. Kesho ni uchaguzi wa serikali za mitaa, mnatakiwa mje kwa wananchi mtuambie mmefanya nini au mtafanya nini ili mchaguliwe na sio hizi kelele za udikiteta!.

Naomba kukukumbusha siku ile tulipokutana pale Karimjee, nilikushauri nini kuhusu hii hoja ya Udikiteta ?. Jikumbushe.
View: https://youtu.be/A_YPEHtM9WM?si=iSm1YWvqtF8Fyd77

Watu wa mwanzo kuupinga udikiteta ni Chadema kwa kuanzisha Ukuta, na mtu wa mwanzo very vocal kuhusu udikiteta, nilitoa ushauri muhimu kwa Lissu kuhusu huu udikiteta, hivyo nakushauri Mhe. Zitto, niliisha kushauri kitu cha kufanya, na hapa kwa faida ya wengi, nashauri tena.

Kwa msio jua, udikiteta sio hoja ya kisiasa, ni hoja ya kisheria, matatizo ya kisiasa, yanahitaji ufumbuzi wa kisiasa na matatizo ya kisheria, yanahitaji ufumbuzi wa kisheria.

Hoja ya Udikteta wa Magufuli: Tundu Lissu isn't Right. Haupingwi kwa kupaza sauti kupiga tu Kelele! - JamiiForums
Udikiteta unapingwa kwa njia moja tuu, Court Review kupitia Mamlaka ya Mahakama Kuu kutoa kitu kinachoitwa Prerogative orders ziko 6, ila maarufu zaidi ni 3.
  • certiorari, an order by a higher court directing a lower court to send the record in a given case for review;
  • mandamus, an order issued by a higher court to compel or to direct a lower court or a government officer to perform mandatory duties correctly;
  • prohibition, directing a subordinate to stop doing something the law prohibits;
  • habeas corpus, demands that a prisoner be taken before the court to determine whether there is lawful authority to detain the person;
  • quo warranto, requiring a person to show by what authority they exercise a power.
  • procedendo, to send a case from an appellate court to a lower court with an order to proceed to judgment) mtanisamehe sizijui Kiswahili chake.
Hivyo Lisu kama mwanasheria mbobezi, Mwenyekiti wa TLS na Mwanasheria Mkuu wa Chadema alipaswa kwanza kutumia the legal local remedies available, kwanza kuuthibitisha huo udikiteta, zikishindikana ndipo sauti zipazwe ili kusaidiwa na jumuiya ya kimataifa.

Tukisema Tanzania hatuna kabisa any serious and credible opposition, viongozi wote wa upinzani mliopo ni wababaishaji tuu, na vyama vyote vya upinzani ni vyama vya upinzani uchwala, itakuwa ni kuwaonea?.

Kwa mwendo huu, acha tuu CCM itutawale milele, na wapinzani wanaojitambua na kuamua politics ndio full professional yao, tusiwalaumu wakijiunga CCM, wanaona mbali.

Kama haya yote unayaona, kwa nini hizo hatua usianze nazo wewe au na wewe pia kwa vile ni mtu wa Ujiji, hivyo unafanya kile Watu wa Ujiji wanachoita Surat Zubaa?.

Matokeo ya upinzani legelege na upinzani uchwara huu, tutayaona baada ya uchaguzi mkuu wa 2020, baada ya serikali ya Magufuli kugundua upinzani uliopo ni hakuna kitu, inakwenda kuufuta rasmi kwenye uchaguzi huo kwa CCM kukomba kila kitu, kwa kukomba mitaa yote, kata zote, majimbo yote ya huku bara na kuwa na Bunge la chama kimoja CCM.
Muda huo ukifika, upinzani wakagalagazwa, naombeni sana tusije anza kutafuta mchawi. Mchawi wa upinzani Tanzania ni wapinzani wenyewe!.

Paskali.
Cape Town.
RSA
Rejea kuhusu Udikiteta
Magufuli ni Dikiteta!, Tanzania Ilihitaji Dikiteta, Tumempata ...
If you can't beat them, join them! He is the worst dictator. Let's ...
Udikiteta ni Dhana Tuu or ni Real?. "Lets Call A Spade A Spade ...
Kauli huumba! Je, ni kweli Magufuli ni dikiteta? Kama ni kweli, ni ...
Udikiteta Tanzania: Je, Rais Magufuli kweli ni dikiteta au ...
Udikiteta: Uongo Ukisemwa Sana na Kuachwa Bila Kukanushwa Hugeuka ...
Kitendo cha Kukiuka Ilani ya CCM Bila Kikao Chochote, Sio ...
Character Assassination ni Modus Oparandi ya Madikiteta Katili ...
CHADEMA Chama cha Ajabu Sana!.Kwenda Mahakamani Kwa Non Issue ...
UDIKTETA: Hongera Sana TWAWEZA, TZ hakuna Udikteta! Ila ...
Kutoonyesha Hisia/Huruma wala pole za sauti si Udikteta bali ni ...
Fungia Fungia Magazeti: Ni Udikiteta wa Serikali Magufuli ...
CHADEMA Ikipewa Nchi, October 2015, Hakuna Hatari Kugeuka Utawala ...
Serikali ikanushe uongo huu wa SABC kumsema vibaya Rais wetu ...
Kama sio udikteta, Mhe. Rais futilia mbali utawala wa sheria ...
Kanda ya Ziwa na kuongea kwa ukali: Ukali wa Rais Magufuli ni ...
Rais Magufuli ni Simple, Genuine & Down To Earth-He is Simply A ...
Magufuli Kama Nyerere: Ni Mtu wa Watu, Hapapasi, Hamung'unyi, Ni ...
 
Mimi nafikiri mmnaweka a cart before a horse wanasema, kwanza mngeanza kumuuliza Zito Kabwe Chama chake kina Wabunge wangapi? Hakuna miujiza hapo, huyo jamaa anajikuza sana na kujidanganya na social media klk uhalisia, hana ushawishi wowote ule on the ground, ikumbukwe kwamba alizunguka TZ nzima kunadi Wabunge wake lkn hola, sasa ataanzia wapi kumtake down Raisi Magufuli ambaye anavuta Kanda ya Ziwa karibia yote?
 
Ni kweli mwaka 2015 chama kilikuwa kidogo. Lakini tumejitahidi kufanya kazi kwa bidii na sasa chama kinakua kwa kasi sana. Tunaomba utuunge mkono
 
Natamani ningekuwa na uwezo wa kuchukua hatua hiyo. Sina uwezo huo. Soma Katiba uone mahitaji yake. Nimejitahidi sana kushawishi wenzangu tufanye hilo lakini bado wana tafakari. Ninaendelea kuwashawishi.
Daah! Mhe Zitto jibu hili linaonesha umekata tamaa kabisa, na jibu hili limenivunja moyo sana mm ambaye niliweka matunaini yangu yote kwako. Niliamini una mbinu zaidi ya moja ya kupambana na ccm.

Utawala huu unatumia nguvu kukabiliana na upinzani, wakati ninyi mkiendeleza mbinu zile zile za kupambana kwa hoja. Ni dhahiri kwamba hamtaweza.

Kwani mhe' haiwezekani kubadili mbinu na upinzani ukaanza kutumia nguvu kupambana na ccm? Hata ikibidi kupeleka vijana kwenye kambi za mafunzo nchi za nje.
 
Natamani ningekuwa na uwezo wa kuchukua hatua hiyo. Sina uwezo huo. Soma Katiba uone mahitaji yake. Nimejitahidi sana kushawishi wenzangu tufanye hilo lakini bado wana tafakari. Ninaendelea kuwashawishi.
Miaka nenda rudi sheria inayosimamia tume ya uchaguzi ni ile ile isiyoruhusu tume huru ya uchaguzi na tunakwenda kwenye uchaguzi mwingine bila tume huru ilihali wapinzani hamjachukua hatua yoyote ile zaid ya kulalama kila uchaguzi kuibiwa kura.
 
Natamani ningekuwa na uwezo wa kuchukua hatua hiyo. Sina uwezo huo. Soma Katiba uone mahitaji yake. Nimejitahidi sana kushawishi wenzangu tufanye hilo lakini bado wana tafakari. Ninaendelea kuwashawishi.
Kwa jibu hili ni wazi kabisa hoja ya Pasco inamashiko, kuhusu upinzani uchwara..
Nasikitika mimi binafsi kama mwananchi wa kawaida ninayetegemea wapinzani ndio mnauwezo wa kushawishi mabadiliko ya katiba ila kama bado mpaka leo wenzako hawajaona umuhimu wa kuungana tena

Ni wazi mtaendelea kulia lia iwapo ushawishi huu hautafanikiwa.
 
Ng.
Mayalla umeeleza vyema sana lakini sababu za kwa nini hayo yanatokea unazijua, ingawa haujataka kuzitambua katika bandiko lako.

Katika nchi yetu na kwingineko Africa, kuwa mwanachama au kiongozi wa chama cha upinzani ni sawa na kuwa mhaini, mpinga maendeleo, mharibu amani ya nchi nk. Hata kama wananchi walio wengi waliojaa uoga watakuelewa bado haitasaidia katika harakati za kukiondoa chama tawala, bahati mbaya sana asilimia kubwa ya wanaoelewa umuhimu wa vyama vingi siyo tu kwamba hawapigi kura bali hawatoi sapoti ya harakati unazofanya. Hii ni changamoto sana katika harakati za kumuondoa unaemlalamikia.

Sasa turudi kwenye hoja ya msingi, Uimara wa vyama vya upinzani unategemea vitu viwili, mosi utayari wa kuvipokea pamoja na uelewa wa wananchi wenyewe kuhusu manufaa ya kuwepo kwa vyama vya upinzani, pili ni mfumo wa uendeshaji wa nchi usiwe bias sana. (Kwenye hili nauhakika umenielewa)

Kwa hiyo, unapokuwa na bunge linalojipendekeza kwa mhimili uliojichimbia, je unaweza ukafanikiwa kumshitaki mkuu wa mhimili uliojichimbia ili aondolewe madarakani?

Je unapokuwa na mahakama inayoogopa kusababisha mgogoro wa kikatiba, unafikiri mahakama hiyo inaweza ikasimama kidete na ikatamka kwamba mkuu wa mhimili uliojichimbia amevunja katiba?

Je unapokuwa na jeshi ambalo pamoja na matukio mengi ya utekaji, lakini hakuna mtekaji hata mmoja ambaye awewahi kutiwa hatiani, unafikiri jeshi hilo linaweza likachunguza uonevu wanaofanyiwa wanachama au viongozi wa vyama vya upinzani?

Kwa hiyo basi, usiwalaum sana viongozi wa upinzani, CCM itaondolewa na wananchi wenyewe siku wakiamua. hata kama wenye chama hicho wanaamini chama chao kitatawala milele, ingawa wao hawatatawala wala kuishi milele.
 
Wanabodi,
Japo bandiko hili liko addressed kwa Mhe. Zitto, lakini hoja zake ni kwa Wapinzani wote, namuelekezea Zitto Kabwe kwa sababu kwa maoni yangu ndio mpinzani pekee kwa sasa anayeweza kusimama na rais Magufuli 2020, na Magufuli akahisi kijoto joto japo kwa mbali.

Ni kwa muda mrefu kumekuwa kukitolewa hoja za udikiteta wa rais Magufuli. Kama watu wale wale, wanatoa hoja zile zile miaka nenda miaka rudi bila kuchukua hatua zozote, then kuendelea kutumia hoja hizo ni kupiga tuu kelele, na kiukweli kabisa kelele zikizidi, zinageika a nuisances.

Swali ni hili

Swali kwa Zitto Kabwe na Wapinzani Wengine: Hoja ya Udikiteta wa Rais Magufuli, Kwa Nini Wewe Zitto na Wapinzani Mnapiga Tuu Kelele Bila Kuchukia Hatua Yoyoye?. Kelele zikizidi Zinageuka Nuisances, Jee Kelele Hizi za Udikiteta wa Rais Magufuli hivi sasa Isn't it a Nuisance?. Kama Upinzani Wenyewe wa Tanzania Ndio Upinzani Huu Ambao Umeishiwa Kabisa Hoja za Msingi!, Jee Tukisema Uchaguzi wa 2020 ni CCM Pekee?, Tutakuwa Tunawakatisha Tamaa Wapinzani? au Tunawaandaa Watanzania kupokea Ukweli Mchungu kuwa Tanzania Hatuna Kabisa Upinzani wa Maana?.

Bandiko hili linafuatia hoja ya Zitto kwenye bandiko hili

Mhe. Zitto, with due respect, kitendo cha kurudia rudia kauli hii ya Magufuli ni dikiteta bila kuchukua hatua zozote, nazo ni kelele tuu.

Watanzania wa sasa hawataki kelele, wanataka matendo. Kesho ni uchaguzi wa serikali za mitaa, mnatakiwa mje kwa wananchi mtuambie mmefanya nini au mtafanya nini ili mchaguliwe na sio hizi kelele za udikiteta!.

Naomba kukukumbusha siku ile tulipokutana pale Karimjee, nilikushauri nini kuhusu hii hoja ya Udikiteta ?. Jikumbushe.

Tukisema Tanzania hatuna kabisa any serious and credible opposition, viongozi wote wa upinzani mliopo ni wababaishaji tuu, na vyama vyote vya upinzani ni vyama vya upinzani uchwala, itakuwa ni kuwaonea?.

Kwa mwendo huu, acha tuu CCM itutawale milele, na wapinzani wanaojitambua na kuamua politics ndio full professional yao, tusiwalaumu wakijiunga CCM, wanaona mbali.

Kama haya yote unayaona, kwa nini hizo hatua usianze nazo wewe au na wewe pia kwa vile ni mtu wa Ujiji, hivyo unafanya kile Watu wa Ujiji wanachoita Surat Zubaa?.

Paskali.
Cape Town.
RSA

Hatua za kuchukua ni kuvuka mipaka kwenda kwenya mahakama za uhalifu wa kimataifa lakini kuchukua hatua ni vigumu kupata haki
 
Back
Top Bottom