Zitto Kabwe na wapinzani wote, kwanini mnapiga tu kelele kuhusu udikteta bila kuchukua hatua zozote? Isn't it a nuisance? Je, 2020 ni CCM pekee?

upinzani ni dhaifu mno, mpinzani pekee mwenye nguvu ni Tundu Lisu, Tatizo hapati sapoti kutoka kwa wenzake
o
Wenzake akina nani? Tatizo la nchi hii liko kwa wananchi siyo wapinzani. Wananchi hawajielewi.

Hao unaowaita wapinzani ni watu waliojitokeza mbele kwa lengo la kuwahamasisha, kuwasemea na kuwaongoza wananchi kuukataa udhalimu na kuitafuta haki. Sasa kama wananchi wenyewe wamelala, unataka Zitto na wenzake wafanye nn?
 
Ccm wakiminywa kama wanavyo minywa upinzani ccm ingesha futika kitambo sana, kila mtu anajua mazingira ya siasa za Tanzania yalivyo lakini bado tunawalaumu, basi tuwapongeze hata kwa ule uvumilivu wao....

Fatuma Karume amepigania haki na demokrasia na kuheshimu utawala wa sheria wote mnajua nn kimempata...
 
Ng.
Mayalla umeeleza vyema sana lakini sababu za kwa nini hayo yanatokea unazijua, ingawa haujataka kuzitambua katika bandiko lako.
Katika nchi yetu na kwingineko Africa, kuwa mwanachama au kiongozi wa chama cha upinzani ni sawa na kuwa mhaini, mpinga maendeleo, mharibu amani ya nchi nk. Hata kama wananchi walio wengi waliojaa uoga watakuelewa bado haitasaidia katika harakati za kukiondoa chama tawala, bahati mbaya sana asilimia kubwa ya wanaoelewa umuhimu wa vyama vingi siyo tu kwamba hawapigi kura bali hawatoi sapoti ya harakati unazofanya. Hii ni changamoto sana katika harakati za kumuondoa unaemlalamikia.


Sasa turudi kwenye hoja ya msingi, Uimara wa vyama vya upinzani unategemea vitu viwili, mosi utayari wa kuvipokea pamoja na uelewa wa wananchi wenyewe kuhusu manufaa ya kuwepo kwa vyama vya upinzani, pili ni mfumo wa uendeshaji wa nchi usiwe bias sana. (Kwenye hili nauhakika umenielewa)

Kwa hiyo, unapokuwa na bunge linalojipendekeza kwa mhimili uliojichimbia, je unaweza ukafanikiwa kumshitaki mkuu wa mhimili uliojichimbia ili aondolewe madarakani??
Je unapokuwa na mahakama inayoogopa kusababisha mgogoro wa kikatiba, unafikiri mahakama hiyo inaweza ikasimama kidete na ikatamka kwamba mkuu wa mhimili uliojichimbia amevunja katiba??
Je unapokuwa na jeshi ambalo pamoja na matukio mengi ya utekaji, lakini hakuna mtekaji hata mmoja ambaye awewahi kutiwa hatiani, unafikiri jeshi hilo linaweza likachunguza uonevu wanaofanyiwa wanachama au viongozi wa vyama vya upinzani??
Kwa hiyo basi, usiwalaum sana viongozi wa upinzani, CCM itaondolewa na wananchi wenyewe siku wakiamua. hata kama wenye chama hicho wanaamini chama chao kitatawala milele, ingawa wao hawatatawala wala kuishi milele.
Chaguzi zote CCM huwa hawapati kura nyingi lakini kwa kutumia Dola huzawadiwa ushindi wa bure, hatua za kuchukua ni kuomba jumuia za kimataifa kuwatuma waangalizi wengi sana toka huko Ulaya kuja kusimamia uchaguzi uwe huru na haki ili CCM wasiibe kura na chaguo za wananchi zichukue Hatamu.
 
Mayala hoja yako umeijenga kwenye premise ya uongo. Suala la kuilinda na kuitetea katiba ni jukumu letu wote na sio issue ya upinzani pekee. Kwa hiyo, swali lako lilitakiwa lielekezwe kwa Watanzania “Kwa nini wanakaa kimya wakati...” Ushauri wangu ni kuwa uliza hilo swali halafu uone kama utaendelea kula dona mtaani.
 
o
Wenzake akina nani? Tatizo la nchi hii liko kwa wananchi siyo wapinzani. Wananchi awajielewi.

Hao unaowaita wapinzani ni watu waliojitokeza mbele kwa lengo la kuwahamasisha, kuwasemea na kuwaongoza wananchi kuukataa udhalimu na kuitafuta haki. Sasa kama wananchi wenyewe wamelala, unataka Zitto na wenzake wafanye nn?
Wakafungue kesi kwenye mahakama za kimataifa kudai Uhuru upya toka kwa mkoloni mweusi asiye taka demokrasia
 
Natamani ningekuwa na uwezo wa kuchukua hatua hiyo. Sina uwezo huo. Soma Katiba uone mahitaji yake. Nimejitahidi sana kushawishi wenzangu tufanye hilo lakini bado wana tafakari. Ninaendelea kuwashawishi.

yaani wewe unadhani kuna siku utafanikiwa kuwafanya Watanzania wakuamini?

Wanakujua kuwa wewe ni Mnafiki,Mbinafsi,Msaliti,Unapenda kujipendekeza....sema awamu hii haijakuona kabisa.

Ukitaka watu wakuamini tena......labda ufe.
Yaani unazuaga mambo yako huko,wenyeakili wanapima wanakuona punguwani.

Nimesoma bandiko lako humu,hivi unadhani watanzania wenye akili timamu hawaijui historia ya Hitler?....hata kama alikua na mabaya yake unajua kwa Wajerumani wanamuheshimu mno?

Acha ujinga,jenga chama chako kwanza,vinginevyo uelekeo wako utawapita kwa speed ya ajabu akina UDP,TLP,NCCR na wengine kwa kifo.

Pia wewe kama msomi,kubali kuwa nyakati zimebadilika,watu wanafuatilia mambo,wanazijua siasa,wanajua kipi chuya upi mchele.

Kidumu CHAMA CHA MAPINDUZI.
 
Mimi naamini suala hili si la "wapinzani" pekee,ni la Watanzania wote wanaoamini katika utawala unaofuata katiba,sheria kanuni ma taratibu za nchi tulizojiwekea.
Kama Watanzania tunaamini "wapinzani" au wanasiasa wanapaswa kutupigania kwenye kuifanya Tanzania iwe mahala salama pa uhai,usalama,ustawi wa kimaendeleo na kiuchumi,basi tunakosea sana.
Kila mwenye macho haambiwi ona,na sote tunaoishi leo hii tutakuwa tunastahili kuchapwa viboko kwa makaburi yetu pindi watoto,wajukuu na vitukuu vyetu huko mbeleni watakapogundua kuwa hatukuchukua hatua kuwarithisha nnchi iloyo bora na salama kwao.
 
Mayala hoja yako umeijenga kwenye premise ya uongo. Suala la kuilinda na kuitetea katiba ni jukumu letu wote na sio issue ya upinzani pekee. Kwa hiyo, swali lako lilitakiwa lielekezwe kwa Watanzania “Kwa nini wanakaa kimya wakati...” Ushauri wangu ni kuwa uliza hilo swali halafu uone kama utaendelea kula dona mtaani.
Una maana akiuliza hilo swali ataambulia kesi ya uhujumu uchumi? au una maana gani?
 
Japo mimi ni CCM siyo vibaya kutoa ushauri kwa vyama vya upinzani 2020 wawekeze zaidi kwenye kupata wabunge wengi waachane na mambo ya Urais ila 2025 wawekeze nguvu kubwa kwenye Urais. Waanze mapema maandalizi ya nani asimame 2025 na siyo kuchukua watakaokatwa CCM...Zitto, Lisu na wengineo wakiandaliwa vizuri 2025 wanaweza kushinda ya Mungu mengi
 
Kama Magufuli asingezuia mikutano ya hadhara ya wapinzani wake angetawala kwa tabu sana.

Sema hili la kuzuia vyama vingine kufanya kazi yake halafu ccm kikaendelea kufanya mikutano linawadanganya ccm kuwa wamesharudisha imani ya wananchi ukweli hauko hivyo.

Waruhusu uwanja huru wa siasa hata kwa miezi miwili tu kina Bashiru watapoteana kila mtanzania analia hali ngumu mpaka viongozi chini kwa chini nao sema wanaogopa kufunguka wazi wazi kukwepa kesi za uhujumu uchumi na kutekwa.

Hoja ya Pascal inaweza kuwa na mashiko lakini hatua zozote watakazochukua wapinzani zinaweza kuwa na gharama kubwa ya uhai wao na wananchi huu ni utawala wa kinyama kupita kiasi na hauna hata chembe ya utu.

Je Mayala yuko tayari kuona raia wasio na hatia wakiangamia kwa risasi za polisi wanaokilinda chama tawala ?

Je Mayala hukuyashuhudia yaliyotokea kwenye chaguzi ndogo zilizofanyika kiasi kila uchuguzi zilitokea kadhia za wapinzani kuuwawa na hata raia wasio na hatia kama kina Aquelina.

Je haoni kuwa karibu viongozi wote wa vyama vya upinzani wanakesi za kubambikwa kila siku wako mahakamani kujitetea ?
Wapinzani wanafanya kila wanaloweza lakini tuwe wakweli bila mikutano ya nje na ndani ni kitu gani kitaendelea kwenye siasa. In short uwanja wa siasa sio rafiki kwa wapinzani....so hakuna sababu ya kuwalaumu au kuwaona hawafanyi sehemu yao.....
 
Watumie nguvu zipi hebu fafanua ?
Daah! Mhe Zitto jibu hili linaonesha umekata tamaa kabisa, na jibu hili limenivunja moyo sana mm ambaye niliweka matunaini yangu yote kwako. Niliamini una mbinu zaidi ya moja ya kupambana na ccm.

Utawala huu unatumia nguvu kukabiliana na upinzani, wakati ninyi mkiendeleza mbinu zile zile za kupambana kwa hoja. Ni dhahiri kwamba hamtaweza.

Kwani mhe' haiwezekani kubadili mbinu na upinzani ukaanza kutumia nguvu kupambana na ccm? Hata ikibidi kupeleka vijana kwenye kambi za mafunzo nchi za nje.
 
Umoja ni nguvu, Utengano ni udhaifu. Mnamuonea tu Zitto, peke yake hataweza.

Tofauti ya CCM na vyama vya Upinzani ni kuwa; CCM wana Umoja na wanayajua kuyatumia mamlaka waliyonayo.

Upinzani wao kila mtu yupo kwa maslahi binafsi na ni wabinafsi sana ukilinganisha na wenzao wa CCM. Na ndio maana kamwe hawawezi kuiondoa CCM.

Huu ni ukweli mchungu kwao.
 
MKUU UNATAKA WACHUKUE HATUA ZIPI WAKATI HARAKATI ZA WAPINZANI ZINAZIMWA KWA RISASI NA UTEKAJI??!
Nabii Ibrahim Aleih Salaam, alipokua akipinga ibada za masanamu, hakuangalia wako wangapi wanaomuunga mkono, alichofanya Ni kuchukua hatua.

Yule aliyeenda kufungua kesi ya kikatiba juu ya ukomo wa Rais hakupita jamiiforums kubwata alienda mahakamani.

Magufuli alipoona nchi inasumbukia shimoni hakuitisha mjadala wa kitaifa juu ya kitu gani wafanye, ame take action, akikosea au akipatia lawama au hongera zitakwenda kwake.

Kama Rais huyu Ni dikteta Kama mnavyodai, na hamna Imani na mahakama za ndani, nendeni mkafungue shauri kwenye mahakama za nje.

MKUU MAYALA UKO SAHIHI KABISA WALA USIPATWE NA NYONG'ONYI JUU YA ULICHOKIANDIKA "WAPINZANI WA TANZANIA NI UCHWARA"
 
Na ukichukua hzo hata unatanguliza mapema, wewe mbowe, waoga tu, sijui ni wachumia tumbo...
Natamani ningekuwa na uwezo wa kuchukua hatua hiyo. Sina uwezo huo. Soma Katiba uone mahitaji yake. Nimejitahidi sana kushawishi wenzangu tufanye hilo lakini bado wana tafakari. Ninaendelea kuwashawishi.
 
MKUU UNATAKA WACHUKUE HATUA ZIPI WAKATI HARAKATI ZA WAPINZANI ZINAZIMWA KWA RISASI NA UTEKAJI??!

Huyu kiongozi anayeimba kuwa Rais ni dictator, cha ajabu anafufanya sisi wa Tanzania mazuzu kwani yeye mwenyewe ndiye Alizunguka nchi nzima 2015 akimshambulia mpinzani mwenzake Mhe Lowassa na kumpa sapoti kubwa saaana Rais wa sasa Dr Magufuli John! Mwenzake alikimbilia nchi jirani Rwanda kupata vinywaji wakati CCM ilikuwa imelazwa ICU katika hospitali maalum ya Apollo India!!!! Mwacheni huyu Mwl Nyerere II aendelee kunyoosha taifa. Kama siyo Rais Magufuli, just imagine taifa lingekuwa wapi! Viongozi wote katika upinzani ni wa binafsi(egoistic), angalia jinsi Maalim alivyosema kwa sababu kakosa kuwa Rais wa Zanzibar basi na wawakilishi wote waachie ngazi(tukose wote), maanake CCM ikaachiwa ukumbi wenyewe, wafanye wanavyotaka, wabadilishe vitu/sheria bungeni watakavyo, sababu tu”tukose wote”!!!! Yaonekana upinzani hautakuwa na nafasi kama ile ya 2015 tena labda mpaka kizazi cha sasa cha upinzani kitoweke - mpaka 2090 A.D.!!!!!
 
Halafu CCM wapo organised zaidi ya Upinzani, ndio maana unaona wanaachana uongozi, watakorofishana Ila wanakaa wanayamaliza.

Tunaweza kuwa tunasema na kulalamika kila siku kuwa wanabebwa na Tume ya Uchaguzi au Polisi, na visingizio vingine vingi.

Lakini, ukweli ni kuwa; hayo yote ni mamlaka waliyonayo, na kuyatumia vizuri ni moja ya akili tu za ushindani. Duniani kote hakuna haki, hata huko tunakoaminishwa kuna demokrasia ya kutosha, ila bado wapinzani huingia madarakani.

Wapinzani wanapaswa kuja na mbinu mbadala sio hii ya kulialia kama Pascal Mayalla alivyowaambia. Humu mitandaoni wanaweza kuwa na wafuasi wengi, ila hawaendi kupiga kura.

Wabadili mbinu, hii ya kulalamika kila siku, hasa mitandaoni, haitawafikisha mahali popote. Na ukweli mchungu ni kuwa mwakani asimame Lissu au Zitto au mtu awaye yote, Mheshimiwa Rais Magufuli atashinda kwa kishindo.

Msiniponde mawe, wala hakuna haja ya povu, take this as an eye opener.

Declaration of interest: currently sio mwanachama ama shabiki wa Chama Chochote.
 
Kaka Paskali utaambiwa kuwa uwanja wa kufanya siasa haipo sawa kwa vyama vyote. Utaambiwa habari ya Hai CDM wanafanya mkutano ndani ya nje wamejaa FFU.

Utaambiwa habari ya kusitikisha sana ya Aquilina, na mambo mengi kama hayo. Bwana mkubwa hapandi ndege na kwenda kuhutubia viti vitupu kule UN kama ile hali aliyokutana nayo Mnangagwa.

Yeye ni wa hapa hapa, hivyo hatoi nafasi ya zile operesheni za kaka wa Hai za kuzunguka mikoa yote na kuongea kana kwamba muda wowote ule hapa bongo kitawaka.
 
Back
Top Bottom