Zitto Kabwe: Msimlinganishe Bernard Membe na Edward Lowassa

Mkuu tukumbuke Lowassa kura zake alipata baada ya muungano unaoitwa UKAWA! Hata angekuwa TLP lakini UKAWA ukawa ule ule nina imani angezipata, japo zipingi kuwa Chadema ilikuwa na contribution kubwa sana kwenye kura za UKAWA. Vinginevyo kama angeenda CUF, na kusiwe na UKAWA, na wakapambana Magufuli, Lowassa na Slaa, bado nina imani bado Magufuli angeshinda na kura walizopata UKAWA zingeenda nusu kwa Lowassa (akiwa na CUF) na nusu Chadema ikiwa na Slaa.

Mkuu you can't be serious, angepata kura nje ya cdm kwa kusema kipaombele chake ni "elimu, elimu, elimu, mambo mengine utayakuta mitandaoni"!

Mkuu Lowassa ni kama ng'ombe aliyenenepea mnadani. Kuna mtu nimemuuliza kama Lowassa ndio aliyeleta kura zote hizo cdm akiwa na miezi miwili tu. Je, akiwa na miaka miwili alileta wabunge na madiwani wangapi? Nitajie tu hata alifungua matawi mangapi ya cdm, ili niamini unachosema. Usikwepe swali hili ili tuwe na mtazamo wa pamoja.
 
Anachotaka Zito ni kitu kimoja tu fedha ya ruzuku kupitia kura za urais anajua Membe atapata kura japo laki sita kwa hiyo kuna mshiko wa ruzuku hapo. Lakini pia anajua Membe anazo fedha kama Lowassa kwa hiyo ananyatia nyatia
Chadema hawatakubali kwa sababu wao ndio wanaaminiwa zaidi na wananchi upande wa upinzani, Hata kama membe atajiunga na Act , Bado kura nyingi za rais zitaenda kwa mgombea wa chadema, Na chadema wanajua hata kama hawatashinda kiti cha rais, Bado zie kura watakazozipata zitawaongezea ruzuku katika maendeleo ya chama
 
Hilo la kuwa aliongeza kura kadhaa siwezi kulikataa, lakini alikuta 90% ya kura ziko tayari. Kama aliweza kuleta kura milioni sita wabunge na madiwani akiwa na miezi miwili ndani vya cdm, alileta viti vingapi na wabunge wangapi kwa muda wa miaka miwili aliyokaa? Au nitajie alifungua matawi mangapi ya cdm ndani ya hiyo miaka miwili? Asipewe mtu sifa asiyostahili pls. Ndio maana sasa hivi nasisitiza sana Membe asiitumie cdm, ili tuone akienda chama kingine avune hizo kura.
Hizo siasa za kufungua matawi, kuingiza wanachama wapya na A,B,C,D,E,F..... zingine katika kuimarisha chama kama taasisi inawezekana hakuzifanya akiwa CDM. Aichokuwa amefanya ni kutafuta kura wakati akingali CCM na nadhani alikuwa amefanikiwa kuzipata kwa kiasi kikubwa. Na nadhani kama utakuwa mkweli inawezekana 50% + ya hiyo 6mil ya ukawa ametoka nayo ccm. Na labda ndicho hicho tena kinachowasukuma akina Zitto kuweka matamanio kwa Membe kwamba ataleta kura kadhaa toka ccm ili kuongezea kwenye kapu la upinzani ambalo already lipo. Pengine tupunguze misimamo mikali na iwe hivi, huyo Membe or who ever comes from anywhere asipate automatic chance kwa niaba ya upinzani. Achunguzwe kwa kina na baadaye Apambanishwe na waliopo fairy, akiwashinda hapo sawa. Au namna gani mkuu?
 
Hivi unataka kuniambia kama Chadema na UKAWA wangemuweka Dr Slaa awe mgombea wake 2015, angepata kura alizopata Lowassa? Magufuli alipata 8,882,935 na Lowassa alipata 6,072,848. Mimi sioni namna dr Slaa angepata hizi kura. Tatizo lipo kwenye lengo la wanasiasa wengi wa kiafrika: hawasimamii itikadi yoyote bali wanasimamia maslahi yao binafsi. Kwa hiyo Lowassa kilimpeleka Chadema ni maslahi binafsi ya kutimiza ndoto yake ya kuwa rais na kilichomtoa ni baada ya kuona ndoto yake haiwezi kutimia tena kutokana na hali ya afya yake. Lowassa hakurudi CCM kwa sababu anaipenda au alitumwa kuja upinzani kuvuruga. Angekuwa mzima kiafya hata safari hii angekuwa mgombea wa upinzani. Kwa hali ya tume tuliyonayo mtu kama Lissu au mpinzani yeyote kusimama na Magufuli uwezekano wa kumshinda ni finyu zaidi kuliko mtu ambaye ametoka CCM kama Membe ambaye anaweza kuwa bado na ushawishi ndani ya sytem.

mkuu ungejiunga na CCM tu kama unawakubali wagombea wao
 
Ni kweli Membe si sawa na Lowasa na Nyakati ni tofauti

Lowasa alikuwa ana ushawishi na ufuasi mkubwa kuliko mwanasiasa mwingine kwa kipindi kile kwenye kugombea Urais

Lowasa aligombea nyakati ambazo ilikuwa ni rahisi kupata Urais kuliko wakati huu (Rais anaporudia muhula wa pili ni ngumu kumuondoa, kuliko mgombea wa Chama tawala ambaye si Rais kwa wakati huo)

Siasa za sasa ni ngumu kwa upinzani kuliko wakati ule

Kuna watu wenye akili zao watawadharau wapinzani wakijaribu kurudia kosa ambalo lilifanyika huko nyuma
 
Zitto anatofauti gani na Mbowe aliemkaribisha Eddo chadema, mpaka Zitto anaongea hivo huwezi jua kashamalizana na Mbowe.

Utofauti ni Mbowe alikua na wabunge zaidi ya 40 na madiwani mamia huku Zitto alikua na Mbunge mmoja na madiwani 10 na usheee hapo.
 
Ni kweli Membe si sawa na Lowasa na Nyakati ni tofauti

Lowasa alikuwa ana ushawishi na ufuasi mkubwa kuliko mwanasiasa mwingine kwa kipindi kile kwenye kugombea Urais

Lowasa aligombea nyakati ambazo ilikuwa ni rahisi kupata Urais kuliko wakati huu (Rais anaporudia muhula wa pili ni ngumu kumuondoa, kuliko mgombea wa Chama tawala ambaye si Rais kwa wakati huo)

Siasa za sasa ni ngumu kwa upinzani kuliko wakati ule

Kuna watu wenye akili zao watawadharau wapinzani wakijaribu kurudia kosa ambalo lilifanyika huko nyuma
Hakuna kosa lililo fanywa na wapinzani huko nyuma.
Kumsimamisha lowasa haikuwa kosa, tulikusudia kuingoa CCm na tulikaribia kufikia lengo.
Ndo maana Tume ya Uchaguzi wakaweka utaratibu kandamizi wa kushirikiana kwa vyama ili kuipa CCM break isije ikatokezea Ukawa Nyingine yenye nguvu kama ile ya wakati ule,
Lowasa kurudi CCM si tatizo kamwe kwa Upinzani, Hakutusaliti,bali aliisaliti CCM baada ya kufutwa kwenye kura za maoni mapema na kuondowa ndotozake jinsi alivojiandaa kuwa raisi mapema.

Kushusu Membe ni kweli hana Ushawishi kutokana na hali ya Upinzani ulivyo pigika kutokana na ukandamizaji wa Upinzani kwa miaka 5 iliyopitia.
Hata hivyo Kuna faid akubwa ujio wa Membe Upinzani,
Membe si Mfuasi wa Chama chochote kile cha upinzani ,hata kama atajiunga ACT bado anaweza kuungwa mkono na Chadema na wengineo kama mgombea wa pamoja kwa vile vyama vyetu vya upinzani havina wagombea wenye Ushawishi mkubwa wanaoweza kupendwa pande zote,.
 
HAWA NDIO WAPINZANI WANAOPIGANIA KUIPUMZISHA CCM ILIYOCHOKA KWA KUTUMIA WAGOMBEA WANAOTOKA CCM ILIYOCHOKA!
 
Zito hana ujanja lazima akubali masharti ya Membe. ACT ni chama kilichoundwa kwa ufadhili wa JK, Membe, Mwigulu nk. Na lengo lilikuwa ni kupambana na cdm. Baada ya Magufuli kuingia madarakani amekata supply yote ya kundi la kina JK, Membe nk. Hapo ndio uadui wa Zito na serikali ya ccm chini ya Magufuli ulipoanzia.

Zito anajua fika cdm ndio yenye wapiga kura wengi wa upinzani, kutokana na ukweli huu, Membe anamuagiza Zito kuwashawishi cdm ili waungane kisha Membe awatumie wapinzani kama ngazi. Ila tatizo liko kwetu sisi wapiga kura hasa wa cdm, kwani bado tunaugulia uhuni wa Lowassa, na hatuko tayari kurudia kosa. Na tumeapa kuwa hatuko tayari tena kusupport muhuni yoyote toka ccm.

Nyuma ya pazia inaonekana Cdm na ACT wanapokea hela za Membe na ccm asilia isiyo upande wa Magufuli, ili agombee urais kupitia upinzani. Tatizo ni kuwa Membe kuja cdm ni kurudia kosa la Lowassa, hivyo Zito ndio anatumika kama kete. Hao akina Membe ndio wameshawishi vyama vya upinzani viache kudai tume ya uchaguzi, ndio maana unaona hakuna kelele za kudai tena tume huru, ila kushiriki uchaguzi hivyo hivyo. Hapa bila wananchi kusimama kidete, ni lazima aletwe muhuni mwingine kama Lowassa.
Hongera sana mkuu kwa kuwa na fikra huru, hakika wewe ni great thinker
 
Back
Top Bottom