Zitto Kabwe: Msimlinganishe Bernard Membe na Edward Lowassa

Zitto Kabwe: Msimlinganishe Bernard Membe na Edward Lowassa

NASEMA UCHAGUZI HUU KULIKO UPINZANI KUUNGANA KUMSIMAMISHA MEMBE KAMA MGOMBEA BORA WASISHIRIKI UCHAGUZI WA RAIS KABISA...!! Wakomae na ubunge na madiwani lakini kumpa dhamana membe ni sawa na kuwaambia CCM sisi ni wapumbavuu maana 2015 upinzani walikuwa wajinga wakauzwa leo hii wanataka warudie kosa lile lilee akati wanajua kabisa walishawahi kufanya upuuzi kama huo ukawacost.
 
Upinzani wawe watu wa kujifunza, waachane kabisa na Membe.. Membe ni Political Opportunist ana tamaa ya madaraka na ni wazi hawezi kuyapata na akishayakosa atarejea ccm kama Lowassa alivyofanya.

Upinzani wasimamishe wagombea wao waachane na watu ambao wao nia yao ni kugeuza upinzani kama jukwaa la kutafutia madaraka na wakishayakosa wanarudi tena ccm na kuvujisha siri za wapinzani...
Mkuu hata mtoto wa la kwanza atawashangaa wapinzani wakifanya upuuzi huu tena maana walishapewa funzo lakini naona wanataka kujitoa ufahamu tena
 
Basi Tanzania wanasiasa wa upinzani watakuwa wapumbavu sana,hawajiandai kwa uchaguzi kwa kufanya recruitment within their parties wanasubilia watoke ccm ndiyo wawatumie? Kwa style hii ccm inaweza kuongoza for more than 50 incoming years
 
Kosa moja kubwa watalolifanya upinzani ni kumpokea Membe na sasa napata wasiwasi kama kweli Maalim Seif ni mpinzani kwa kuungana na Zitto.
Z
 
Kwani hamna wagombea wengine jamani?Mimi binafsi naamini Membe ni mwana CCM ila kwa vile ndio siasa maji taka tutadanganyana hapa baada ya Muda utasikia nimerudi nyumbani hebu tuwe tunajifunza bora agombee hata Ado Shaibu mkuu Zito kama unanisikia braza
 
Zuberi yupo londo right now duh
Chakata kweli maana hapo panaitwa ikulu ndogo
Chakula chao kitamu sana nilikula mara ya mwisho 2014 december
 
Chadema iliundwa kwa ufadhili wa nani?rejea uchaguzi wa mwaka 2015

Cdm iliundwa wakati mfumo wa vyama vingi hapa uliporejea. Hao uliowaona 2015, walikuja na pesa mkono Mbowe na kundi lake hawakufanya ajizi.
 
Mtajadili sana lkn kwa nn Membe aje kupoteza rasilimali zake na za watu kwenye utupu huu?

Najaribu kumtafuta nikimpata ntamwambia asubiri 2025 japo afya naona haiko timamu sana kama trump lkn atatufaa kama biden licha ya afya kuzorota inayoathiri utoaji wa maamuzi lkn bado anataka kuwa rais na huenda wamarekani wakampa kwa kigezo cha nani atakuwa makamu wa rais
 
Kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe amewataka Wananchi kuondoa wasiwasi juu ya Bernard Membe endapo akipokelewa na kupewa nafasi kugombea Urais ndani ya Vyama vya Upinzani.

Mheshimiwa Zitto Kabwe amesema upinzani kumpokea Membe wakati huu siyo sawa na kilichofanyika mwaka 2015 kwani Bernard Membe hajagombea Urais ndani ya CCM na kukatwa bali Bernard Membe amefukuzwa.

Pia amesema kuhusu uwezekano wa kumpokea Membe ndani ya ACT Wazalendo amesema hilo siyo suala la ACT peke yake bali ni swala la upinzani kwa ujumla. Na kwamba atatakiwa kushindanishwa na Wagombea wengine wa upinzani ambao wametia nia ya kugombea Urais.

Akizungumzia kuhusu kauli ya ofisi msajili wa vyama vya siasa kuwa upinzani umechelewa kuungana amesema upinzani bado upo ndani ya muda bado hawajachelewa kuungana. Kwa mujibu wa Zitto Kabwe sheria ya vyama vya siasa inasema vyama vinatakiwa kuungana miezi mitatu kabla ya uchaguzi. Kwa maana hiyo kama uchaguzi ni mwishoni mwa oktoba bado muda upo.

Kuhusu kuwepo mkakati wa vyama vya upinzani kuungana Mheshimiwa Zitto Kabwe amewataka wananchi kuwa na subira muda ukifika watajulishwa.




Duh,
Ila CCM wanatuweza wapinzani!
Haki ya nani huyo Mungu wao wasijethubutu KUMUACHA.
 
Kama wapinzani hawataungana kutengeneza UKAWA 2 na kumkaribisha Membe kuwa mgombea wa Rais nachelea kusema kuwa ni wazi kuwa Magufuli atashinda kwa kishindo kikubwa sana kuliko awamu ilopita

Huo ndiyo ukweli mchungu ambao hamtaki kuusikia !

Wakati kumbe mngeungana na kumpokea agombee Membe mngeweza kugawa matokeo ya kura kama uchaguzi wa 2015 kiasi kwamba ingeweza kutoa ujumbe fulani.

Sasa nyie neng’enekeni tu subirini muone matokeo hamtaamini!

Actually mwelekeo wa matokeo hayo utaendana sambamba na matokeo ya kwenye udiwani na ubunge .
 
Kwanza awamu hii tangu ianze upinzani hamjaweza kufanya mikutano ya uhamasishaji kwa wananchi ili kupata wanachama wapya na ku bring political awareness pamoja na elimu ya uraia.

Kumbukeni hilo!

Mikoani huko awareness ya kujua kuwa kuwa mwanachama cha upinzani au kuchagua mpinzani siyo kosa ni haki wengi hawajui chochote!

Wengine wanatishiwa mkichagua upinzani mtaletewa vita wanawekewa na video za nchi zenye vita. Imagine halafu nao kwa ufahamu wao kuwa Mdogo wengine wanaamini kuwa ni kweli!

Katika hii miaka takribani 5 wapinzani hamjaweza kufanya mikutano kwa flexibility halafu Eti badala ya kuwa na multi strategies mnabaki kumlaumu Lowasa!

Nyie acheni kujiunga kuanzisha ukawa ya pili halafu Membe msimpokee halafu wacha wagombee hao mnaowataka kisha tusubiri matokeo tuone !
 
Zito hana ujanja lazima akubali masharti ya Membe. ACT ni chama kilichoundwa kwa ufadhili wa JK, Membe, Mwigulu nk. Na lengo lilikuwa ni kupambana na cdm. Baada ya Magufuli kuingia madarakani amekata supply yote ya kundi la kina JK, Membe nk. Hapo ndio uadui wa Zito na serikali ya ccm chini ya Magufuli ulipoanzia.

Zito anajua fika cdm ndio yenye wapiga kura wengi wa upinzani, kutokana na ukweli huu, Membe anamuagiza Zito kuwashawishi cdm ili waungane kisha Membe awatumie wapinzani kama ngazi. Ila tatizo liko kwetu sisi wapiga kura hasa wa cdm, kwani bado tunaugulia uhuni wa Lowassa, na hatuko tayari kurudia kosa. Na tumeapa kuwa hatuko tayari tena kusupport muhuni yoyote toka ccm.

Nyuma ya pazia inaonekana Cdm na ACT wanapokea hela za Membe na ccm asilia isiyo upande wa Magufuli, ili agombee urais kupitia upinzani. Tatizo ni kuwa Membe kuja cdm ni kurudia kosa la Lowassa, hivyo Zito ndio anatumika kama kete. Hao akina Membe ndio wameshawishi vyama vya upinzani viache kudai tume ya uchaguzi, ndio maana unaona hakuna kelele za kudai tena tume huru, ila kushiriki uchaguzi hivyo hivyo. Hapa bila wananchi kusimama kidete, ni lazima aletwe muhuni mwingine kama Lowassa.
Ni kama unanifungua akili yangu hivi
Mmmh kweli unaweza kuwa ni mpango kama uleeeeee wa Lowassa
 
Katika hili tafakuri yangu ipo hivi:
1. Membe hana ushawishi mkubwa, na hawezi kuusaidia upinzani kwa kiwango kikubwa kufikia athari chanya zilizoletwa na Lowasa, ikiwemo kuongezeka kwa kura za upinzani na hadi kupata wabunge. Hili hata Zitto Kabwe na Maalim Seif wanalifahamu.

2. Malengo ya ACT-Wazalendo katika uchaguzi huu sio kuchukua dola, ni kupata wabunge wengi. kwa hiyo, wakimpata Membe anaweza akawasaidia kuongeza wabunge hasa ukanda wa kusini anakotokea.

3. Kwa kuwa ACT-Wazalendo wanataka wabunge tu, wako radhi kushawishi Membe apewe nafasi ya kugombea urais wakijua kuwa hawezi kupata, lakini akawasaidia kupata wabunge wengi.
Nini cha kufanya?

4. Kama Membe anataka ajiunge na upinzani kweli, basi aje bila sharti hilo la kutaka agombee urais kwa sababu ataharibu saikolojia ya wapiga kura ambao wamejipanga kupigia kura mtu ambaye wanaamini kabisa ana roho ya upinzani piga ua! Wapiga kura walioko upinzani na CCM ambao wameamua mpaka sasa kumpigia mtu mwingine, lakini sio Magufuli wanatamani kumpigia kura mtu mwenye kumudu vilivyo Magufuli jukwaani na nje ya jukwaa, kama vyombo vya dola vinawekwa kando, na huyo hawezi kuwa Membe.

5. ACT-Wazalendo waachane na mtazamo kwamba Membe anaeza kuwasaidia kupata wabunge wengi, bali wajisimamie wenyewe kwa kuwatumia akina Bwege na watu mashuhuri ndani ya CCM ambao kiroho hawapo pamoja na CCM katika kupata Rais 2020, ambao ni wengi tu huko kusini kwenyewe ambako ni target yao.

6. Kama Zitto atalazimisha, kama inavyoonekana, kumvuta Membe kwa ahadi ya urais ataharibu kwa sababu ataanza kuandaa mapema utengano wa wapinzani ambao wameanza kuaminika kuelekea uchaguzi, yaani ACT-Wazalendo na Chadema.

lakini kubwa la mwisho katika ninachokiona sasa, na ambacho kinapaswa kutopuuzwa ni kwamba: Zitto ana historia ya kutumiwa na TISS, hivyo tusipuuze mtazamo kwamba Membe na Zitto wanaweza kushirikiana kupunguza threat kwa CCM. lazima mjue kuwa tofauti na wengi wanavyojidai, ukweli ni kwamba this time CCM kina wakati mgumu sana kuelekea uchaguzi mkuu. Hizo mbwembwe zinazoonyeshwa ni za nje tu ambazo ni sehemu ya propaganda, lakini anguko lake linaweza kuwa mwaka huu kupitia sanduku la kura!
Hahahaàaaaaaaa ya kweli hayo!!!!!!.Wacha miti basi ishangae law niaba
 
Kwani kurudi kwenu kuna ubaya gani? Sema tu hapo umetudanganya hiyo nchi badala ya kuitaja Rwanda ukataja Congo, lkn kwakuwa ulikuwa kwenye kundi la mayi mayi bado hujakosea
Mbona Zitto anakuwa na wasiwasi na mgombea wao? Wamlete tumkanyage kwa hoja, akipata hata 2% ya kura nahamia Congo.
 
Wewe kazi ya utabiri umeianza lini?
Teh! niliona kakipande cha interview ya Mh. BM ndani ya BBC swahili jana.. ah pale facial expression na body language alichemka, it was poorly choreographed and coordinated. But anyway ndio siasa..
 
Angekuwa ni mzigo kwanini mliamua kumfukuza baada ya kuwatangazia kuwa anataka kugombea urais?
Huyu Zitto nae aache kujikomba komba, Membe hana Upepo Wowote Ni Mzigo
 
Ni kama unanifungua akili yangu hivi
Mmmh kweli unaweza kuwa ni mpango kama uleeeeee wa Lowassa
Lowassa hakukuwa na mpango wowote. Lowassa alikuwa natafuta urais kwa udi na uvumba. Lowassa kuja Chadema ilikuwa ni njia tu ya kufikia lengo lake la kuwa rais. KIlichomrudisha CCM ni kuona hali yake kiafya siyo nzuri na hawezi kufikia tena lengo lake la kuwa rais. Nakuhakikishia angekuwa na afya nzuri kama yule Lowassa wa 2010, asingerudi CCM na safari hii angetoa bado angegombea tena. Na si ajabu wangeungana na Membe.
 
Mawazo kwamba Membe ana mtaji mkubwa wa watu wengi na eti atawaongezea kura/wabunge/ruzuku ni mawazo potofu mno. Ile bahati ya Lowassa haitokaa itokee tena. Wapinzani komaeni na watu mlionao.
 
Back
Top Bottom