Zitto Kabwe: Msimlinganishe Bernard Membe na Edward Lowassa

Zitto Kabwe: Msimlinganishe Bernard Membe na Edward Lowassa

Katika hili tafakuri yangu ipo hivi:
1. Membe hana ushawishi mkubwa, na hawezi kuusaidia upinzani kwa kiwango kikubwa kufikia athari chanya zilizoletwa na Lowasa, ikiwemo kuongezeka kwa kura za upinzani na hadi kupata wabunge. Hili hata Zitto Kabwe na Maalim Seif wanalifahamu.

2. Malengo ya ACT-Wazalendo katika uchaguzi huu sio kuchukua dola, ni kupata wabunge wengi. kwa hiyo, wakimpata Membe anaweza akawasaidia kuongeza wabunge hasa ukanda wa kusini anakotokea.

3. Kwa kuwa ACT-Wazalendo wanataka wabunge tu, wako radhi kushawishi Membe apewe nafasi ya kugombea urais wakijua kuwa hawezi kupata, lakini akawasaidia kupata wabunge wengi.
Nini cha kufanya?

4. Kama Membe anataka ajiunge na upinzani kweli, basi aje bila sharti hilo la kutaka agombee urais kwa sababu ataharibu saikolojia ya wapiga kura ambao wamejipanga kupigia kura mtu ambaye wanaamini kabisa ana roho ya upinzani piga ua! Wapiga kura walioko upinzani na CCM ambao wameamua mpaka sasa kumpigia mtu mwingine, lakini sio Magufuli wanatamani kumpigia kura mtu mwenye kumudu vilivyo Magufuli jukwaani na nje ya jukwaa, kama vyombo vya dola vinawekwa kando, na huyo hawezi kuwa Membe.

5. ACT-Wazalendo waachane na mtazamo kwamba Membe anaeza kuwasaidia kupata wabunge wengi, bali wajisimamie wenyewe kwa kuwatumia akina Bwege na watu mashuhuri ndani ya CCM ambao kiroho hawapo pamoja na CCM katika kupata Rais 2020, ambao ni wengi tu huko kusini kwenyewe ambako ni target yao.

6. Kama Zitto atalazimisha, kama inavyoonekana, kumvuta Membe kwa ahadi ya urais ataharibu kwa sababu ataanza kuandaa mapema utengano wa wapinzani ambao wameanza kuaminika kuelekea uchaguzi, yaani ACT-Wazalendo na Chadema.

lakini kubwa la mwisho katika ninachokiona sasa, na ambacho kinapaswa kutopuuzwa ni kwamba: Zitto ana historia ya kutumiwa na TISS, hivyo tusipuuze mtazamo kwamba Membe na Zitto wanaweza kushirikiana kupunguza threat kwa CCM. lazima mjue kuwa tofauti na wengi wanavyojidai, ukweli ni kwamba this time CCM kina wakati mgumu sana kuelekea uchaguzi mkuu. Hizo mbwembwe zinazoonyeshwa ni za nje tu ambazo ni sehemu ya propaganda, lakini anguko lake linaweza kuwa mwaka huu kupitia sanduku la kura!

Mchango murua kabisa huu.
 
Mawazo kwamba Membe ana mtaji mkubwa wa watu wengi na eti atawaongezea kura/wabunge/ruzuku ni mawazo potofu mno. Ile bahati ya Lowassa haitokaa itokee tena. Wapinzani komaeni na watu mlionao.

Uko sahihi mno, tena hata Lowassa mwenyewe ni kama alirukia kuendesha gari lililokuwa katika mteremko. Angekosea aende chama cha upinzani nje ya cdm angechekesha.
 
Kama wapinzani hawataungana kutengeneza UKAWA 2 na kumkaribisha Membe kuwa mgombea wa Rais nachelea kusema kuwa ni wazi kuwa Magufuli atashinda kwa kishindo kikubwa sana kuliko awamu ilopita

Huo ndiyo ukweli mchungu ambao hamtaki kuusikia !

Wakati kumbe mngeungana na kumpokea agombee Membe mngeweza kugawa matokeo ya kura kama uchaguzi wa 2015 kiasi kwamba ingeweza kutoa ujumbe fulani.

Sasa nyie neng’enekeni tu subirini muone matokeo hamtaamini!

Actually mwelekeo wa matokeo hayo utaendana sambamba na matokeo ya kwenye udiwani na ubunge .
Angalau wewe unachemsha bongo yako tofauti na watanzania wengi. Kwa hii tume ya uchaguzi inayofanya kazi kwa kupokea maelekezo kutoka kwa rais ni bora kumsimamisha mtu kama Membe ataweza kuwa na propability kubwa zaidi ya kupata kura nyingi kuliko mtu kama Lissu. Siyo kama Lissu siyo hafai ila uchaguzi ni zaidi ya kukubalika. Uwezekano wa Membe kupata support (hata ya kimya kimya) kutoka ndani ya system ni mkubwa zaidi kuliko Lissu. Membe ameshakuwa CCM na ataondoka na mashabiki huko + wale ambao wako upinzani. CCM kuna watu wengi wazito ambao hawakubali kabisa utawala wa Magufuli lakini wanakufa na tai shingoni ambao wako tayari kumsapoti Membe kwa kificho lakini sioni wakifanya hivyo kwa Lissu.
 
JASUSI MBOBEZI NDANI YA UPINZANI. Safi sana...

Acheze karata zake kama alivyoagizwa...2024 ataleta mrejesho wa hii assignment!
 
Uko sahihi mno, tena hata Lowassa mwenyewe ni kama alirukia kuendesha gari lililokuwa katika mteremko. Angekosea aende chama cha upinzani nje ya cdm angechekesha.
Hivi unataka kuniambia kama Chadema na UKAWA wangemuweka Dr Slaa awe mgombea wake 2015, angepata kura alizopata Lowassa? Magufuli alipata 8,882,935 na Lowassa alipata 6,072,848. Mimi sioni namna dr Slaa angepata hizi kura. Tatizo lipo kwenye lengo la wanasiasa wengi wa kiafrika: hawasimamii itikadi yoyote bali wanasimamia maslahi yao binafsi. Kwa hiyo Lowassa kilimpeleka Chadema ni maslahi binafsi ya kutimiza ndoto yake ya kuwa rais na kilichomtoa ni baada ya kuona ndoto yake haiwezi kutimia tena kutokana na hali ya afya yake. Lowassa hakurudi CCM kwa sababu anaipenda au alitumwa kuja upinzani kuvuruga. Angekuwa mzima kiafya hata safari hii angekuwa mgombea wa upinzani. Kwa hali ya tume tuliyonayo mtu kama Lissu au mpinzani yeyote kusimama na Magufuli uwezekano wa kumshinda ni finyu zaidi kuliko mtu ambaye ametoka CCM kama Membe ambaye anaweza kuwa bado na ushawishi ndani ya sytem.
 
Mawazo kwamba Membe ana mtaji mkubwa wa watu wengi na eti atawaongezea kura/wabunge/ruzuku ni mawazo potofu mno. Ile bahati ya Lowassa haitokaa itokee tena. Wapinzani komaeni na watu mlionao.
Wapinzani kukomaa na watu walionao ni hasara zaidi kuliko kumsimamisha Membe. Nafuu asimamishwe Membe na Magufuli kwani Membe uungwaji wake mkono ni mkubwa kulinganisha na Lissu. (Japo mimi nilitamani sana Lissu asimame na Magufuli lakini uchaguzi ukiwa rigid sana hufiki popote.
 
Nani ni nani kati ya hawa. Anafaa kuwa Rais?View attachment 1496538View attachment 1496539
Hawa wote wana faa kuwa maraisi,
Tundu ana 70% ya credibility ya kuwa raisi akisimamishwa ,lakni usalama wake na pia uzima wake (phisical fitness yake ) inaweza ikawa kikwazo.

Membe ni kama vile mgombe a Binfsi anayetafuta chama cha kumbeba ili afikie ndoto zake,
Kuingi kwa membe ACT ni kama vile alivyoingia Lowas Chadema 2015. lakini akishinda ndio upinzani ulioshinda ni si CCM, Pamoja na hivyo hana mvuto mkubwa kisiasa
Pengine nimpe 40%

hatokuwa na Uchama zaidi wa ACT au Chadema bali atakuwa Neutral. na kwa maana hiyo anatufaa sanaa kwa kutusogeza na pengine hadi kuingoa ccm. Yeye anaijua ccm kwa undani na ana maraiki wengi kule wanaweza kumpa kura zao.

Kwa makubaliano ya 2015 chadema wlitowa Mgombea na kura za uraisi zilineemesha chadema kwa ruzuku nono baada ya kukosa Uraisi.

2020 zamu hii ilikuwa iwe CUF kama isingelisambaratika ,lakini badala yake alipo Maalim Seif ndio kwenye Upinzani haswa, kwa hiyo mwaka huu ni ACT wafaidike na ruzuku kama hawakupata Uraisi.
IMANI YANGU MWAKA HUU NI WETU WAPINZANI, TUJIUNGE NA KUACHA MIZENGWE,
CCM WEPESI SANA, UKITOWA WIZI wa kura NA MABAVU ya vyombo vya dola HAWANA PA KUTOKEA, WATU WAMEWACHOKA MNO

MATUMBO YA WATANZANIA YANAFUKA MOTO KWA NJAA,

KILA CONA YA TZ, HELA HAMNA, KAZI HAMNA, MAISHA MAGUMU, ILIMRADI CCM WANATAKA MISIFA TUU.
 
Yaani hata hamjitambui nyie, can't you opposition see that Membe is a puppet, and so is Zitto? Kweli nchi hii haipigi hatua kisiasa coz upinzani umejaa viazi.
Upinzani hawapendi kuambiwa ukweli.

Lowassa walianza hivi hivi...sema wengi wamebadili ID tungewakumbusha.

Wangetumia huu mwaka kujijenga maana nafasi ya kumshinda Magufuli walikuwa nayo 2015. Mwaka huu wakiambulia kura milioni kadhaa washukuru.
 
Jibu swali, angegombea kupitia UDP angepata hizo kura 6m+?
Ni kweli angeenda UDP, TADEA na hata (ACT ya wakati huo) asingeweza kupata hizo 6 mil. Lakini pia hata CDM pamoja na kuwa tayari walikuwa na mizizi ya kutosha, wasingeweza kufikisha hizo 6 mil. Lowasa alikuwa mchezaji mzuri aliyekaribia kuipa ubingwa timu ambayo pia haikuwa mbovu. Kwa hiyo ikiwa alikuwa mbovu ama vinginevyo, bado kuna kaukweli aliongeza vikura vingi kadhaa.
 
Hivi unataka kuniambia kama Chadema na UKAWA wangemuweka Dr Slaa awe mgombea wake 2015, angepata kura alizopata Lowassa? Magufuli alipata 8,882,935 na Lowassa alipata 6,072,848. Mimi sioni namna dr Slaa angepata hizi kura. Tatizo lipo kwenye lengo la wanasiasa wengi wa kiafrika: hawasimamii itikadi yoyote bali wanasimamia maslahi yao binafsi. Kwa hiyo Lowassa kilimpeleka Chadema ni maslahi binafsi ya kutimiza ndoto yake ya kuwa rais na kilichomtoa ni baada ya kuona ndoto yake haiwezi kutimia tena kutokana na hali ya afya yake. Lowassa hakurudi CCM kwa sababu anaipenda au alitumwa kuja upinzani kuvuruga. Angekuwa mzima kiafya hata safari hii angekuwa mgombea wa upinzani. Kwa hali ya tume tuliyonayo mtu kama Lissu au mpinzani yeyote kusimama na Magufuli uwezekano wa kumshinda ni finyu zaidi kuliko mtu ambaye ametoka CCM kama Membe ambaye anaweza kuwa bado na ushawishi ndani ya sytem.

Mkuu naona hata ww umeingia kwenye hii propaganda mfu kuwa kura za cdm 2015 zililetwa na Lowassa! Kwa taarifa yako baada ya uchaguzi wa 2010, cdm ndio chama kilichofanya kazi ya kisiasa, na kutoa elimu ya uraia kuliko chama chochote. Ndio chama cha siasa kilichofanya mikutano mingi kuliko chama chochote cha siasa ikiwemo ccm. Huko kote Dr. Slaa ndiye aliyekuwa jemadari wa kuijenga cdm.

Iwapo cdm ingemsimamisha Dr. Slaa sio tu ingepata kura nyingi lakini zaidi ingebaki kwenye njia na haiba yake. Watu walijiandikisha kwa hasira wakijua Lowassa ndio atakuwa mgombea wa ccm, na Slaa angekuwa mgombea wa cdm. Humo ndio jina kitambulisho cha kura kilipopata jina kichinjio, ili kumchinja Lowassa. Alaaniwe Mbowe na genge lake kumpokea Lowassa na kuitoa cdm kwenye haiba yake. Mengine kwa sasa ni historia. Sasa ngoja nikuulize ili twende sawa, iwapo Lowassa angegombea kupitia TLP, UDP nk angepata kura 6m+? Msitake kumpa mtu sifa asiyostahili. Lowassa namfananisha na mchezaji aliyeingia dakika ya 90 na kufunga goli la ushindi, kisha ionekane yeye ndio shujaa.

Hiyo kwamba Membe ndio anaweza kushindana na Magufuli eti sijui kwakuwa alikuwa kwenye system, aende UDP au TADEA kisha uje utoe mrejesho hapa. Kusimama na Magufuli sio lazima kumshinda, tunataka ushindani halisi, na mwenye uwezo wa hilo ni Lisu. Huyo Membe anataka kusafiria nyota za watu, lakini hana mvuto wowote.
 
Huyo Lissu mwenyewe yuko wapi sasa?

Yani mtu afanye kuja kama mgeni jamani saa za lala salama ?!

Mikakati mnaipangaje mkiwa mbali mbali?!

Kazi ipo!
 
Ni kweli angeenda UDP, TADEA na hata (ACT ya wakati huo) asingeweza kupata hizo 6 mil. Lakini pia hata CDM pamoja na kuwa tayari walikuwa na mizizi ya kutosha, wasingeweza kufikisha hizo 6 mil. Lowasa alikuwa mchezaji mzuri aliyekaribia kuipa ubingwa timu ambayo pia haikuwa mbovu. Kwa hiyo ikiwa alikuwa mbovu ama vinginevyo, bado kuna kaukweli aliongeza vikura vingi kadhaa.

Hilo la kuwa aliongeza kura kadhaa siwezi kulikataa, lakini alikuta 90% ya kura ziko tayari. Kama aliweza kuleta kura milioni sita wabunge na madiwani akiwa na miezi miwili ndani vya cdm, alileta viti vingapi na wabunge wangapi kwa muda wa miaka miwili aliyokaa? Au nitajie alifungua matawi mangapi ya cdm ndani ya hiyo miaka miwili? Asipewe mtu sifa asiyostahili pls. Ndio maana sasa hivi nasisitiza sana Membe asiitumie cdm, ili tuone akienda chama kingine avune hizo kura.
 
Huyo Lissu mwenyewe yuko wapi sasa?

Yani mtu afanye kuja kama mgeni jamani saa za lala salama ?!

Mikakati mnaipangaje mkiwa mbali mbali?!

Kazi ipo!

Lissu sio mgeni, hakuna mtu wa upinzani na yoyote anayejua siasa asiyemfahamu. Yuko nje kwa matibabu, na sababu nyingine za kibinafsi hasa usalama wake.
 
Mkuu naona hata ww umeingia kwenye hii propaganda mfu kuwa kura za cdm 2015 zililetwa na Lowassa! Kwa taarifa yako baada ya uchaguzi wa 2010, cdm ndio chama kilichofanya kazi ya kisiasa, na kutoa elimu ya uraia kuliko chama chochote. Ndio chama cha siasa kilichofanya mikutano mingi kuliko chama chochote cha siasa ikiwemo ccm. Huko kote Dr. Slaa ndiye aliyekuwa jemadari wa kuijenga cdm.

Iwapo cdm ingemsimamisha Dr. Slaa sio tu ingepata kura nyingi lakini zaidi ingebaki kwenye njia na haiba yake. Watu walijiandikisha kwa hasira wakijua Lowassa ndio atakuwa mgombea wa ccm, na Slaa angekuwa mgombea wa cdm. Humo ndio jina kitambulisho cha kura kilipopata jina kichinjio, ili kumchinja Lowassa. Alaaniwe Mbowe na genge lake kumpokea Lowassa na kuitoa cdm kwenye haiba yake. Mengine kwa sasa ni historia. Sasa ngoja nikuulize ili twende sawa, iwapo Lowassa angegombea kupitia TLP, UDP nk angepata kura 6m+? Msitake kumpa mtu sifa asiyostahili. Lowassa namfananisha na mchezaji aliyeingia dakika ya 90 na kufunga goli la ushindi, kisha ionekane yeye ndio shujaa.

Hiyo kwamba Membe ndio anaweza kushindana na Magufuli eti sijui kwakuwa alikuwa kwenye system, aende UDP au TADEA kisha uje utoe mrejesho hapa. Kusimama na Magufuli sio lazima kumshinda, tunataka ushindani halisi, na mwenye uwezo wa hilo ni Lisu. Huyo Membe anataka kusafiria nyota za watu, lakini hana mvuto wowote.
Mkuu tukumbuke Lowassa kura zake alipata baada ya muungano unaoitwa UKAWA! Hata angekuwa TLP lakini UKAWA ukawa ule ule nina imani angezipata, japo zipingi kuwa Chadema ilikuwa na contribution kubwa sana kwenye kura za UKAWA. Vinginevyo kama angeenda CUF, na kusiwe na UKAWA, na wakapambana Magufuli, Lowassa na Slaa, bado nina imani bado Magufuli angeshinda na kura walizopata UKAWA zingeenda nusu kwa Lowassa (akiwa na CUF) na nusu Chadema ikiwa na Slaa.
 
Kiongozi mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Zuberi Kabwe amewataka Wananchi kuondoa wasiwasi juu ya Bernard Membe endapo akipokelewa na kupewa nafasi kugombea Urais ndani ya Vyama vya Upinzani.

Mheshimiwa Zitto Kabwe amesema upinzani kumpokea Membe wakati huu siyo sawa na kilichofanyika mwaka 2015 kwani Bernard Membe hajagombea Urais ndani ya CCM na kukatwa bali Bernard Membe amefukuzwa.

Pia amesema kuhusu uwezekano wa kumpokea Membe ndani ya ACT Wazalendo amesema hilo siyo suala la ACT peke yake bali ni swala la upinzani kwa ujumla. Na kwamba atatakiwa kushindanishwa na Wagombea wengine wa upinzani ambao wametia nia ya kugombea Urais.

Akizungumzia kuhusu kauli ya ofisi msajili wa vyama vya siasa kuwa upinzani umechelewa kuungana amesema upinzani bado upo ndani ya muda bado hawajachelewa kuungana. Kwa mujibu wa Zitto Kabwe sheria ya vyama vya siasa inasema vyama vinatakiwa kuungana miezi mitatu kabla ya uchaguzi. Kwa maana hiyo kama uchaguzi ni mwishoni mwa oktoba bado muda upo.

Kuhusu kuwepo mkakati wa vyama vya upinzani kuungana Mheshimiwa Zitto Kabwe amewataka wananchi kuwa na subira muda ukifika watajulishwa.

mama Mgirwa vipi?!
 
...kwani Membe uungwaji wake mkono ni mkubwa kulinganisha na Lissu. (Japo mimi nilitamani sana Lissu..
Hao wengi wanaomuunga Mkono Membe zaidi ya Lissu ni akina nani? Wana CCM au Wapinzani? Ukipenda chongo kweli utaita kengeza😎
 
Lipumba anatafuta mwanachama yeyote kugombea kiti cha rais, Kwanini asimualike Membe kwenye chama chake? Cdm wanaijua michezo ianayochezwa na ccm, Kila mara chaguzi zinapokaribia, Janja ya ccm imebaki kwa Membe kuvuruga upinzani, Upinzani uingie kwenye uchaguzi ukiwa na mgombea kutoka Upinzani
 
Back
Top Bottom