Zitto Kabwe kupeleka Bungeni hoja binafsi ya kutokuwa na Imani na Rais Magufuli

Jambo moja ni muhimu sana, Rais anapaswa kujua kuwa anafanya kazi kwa mujibu wa Katiba ya nchi. Na Katiba imetoa wajibu wa lazima kwa Serikali kulinda watu. Ndio kazi ya Serikali – kulinda wananchi pale ambapo yanatokea majanga ambayo yanazidi kimo wananchi hao.

Tunamwambia Rais kwamba, Mtanzania yeyote akifa kwa njaa kwa sababu Serikali imeshindwa kutekeleza wajibu wake Watanzania tutapaswa kuchukua hatua, Katiba inatulazimisha kumtoa Rais madarakani ikiwa yeye na Serikali yake watashindwa kutimiza wajibu wake wa kulinda uhai wa raia wake.

Tunamkumbusha Rais kuwa yeye sio mungu mtu. Yupo chini ya Katiba na kwa idadi ya wabunge wa upinzani waliopo Bungeni, na wakiamua kusimama na wananchi na kulinda Katiba, Rais wa sasa atakuwa Rais wa kwanza wa nchi yetu kutolewa hoja ya kutokuwa na imani naye bungeni. Katiba inahitaji asilimia 20 tu ya wabunge kuwasilisha hoja hiyo bungeni.

Ninatoa wito kwa Watanzania wote nchini, bila kujali vyama vyao, kuweka rekodi ya hali ya chakula popote walipo na kuweka takwimu ya maafa yeyote yanayotokana na njaa. Mtanzania yeyote akifa kwa njaa ni lazima tuchukue jukumu la kumwajibisha Rais kwa kusema waziwazi kwamba hajatimiza wajibu wake kama Mkuu wa Serikali kulinda wananchi wake.

Tunamkumbusha Rais kwamba kwa mujibu wa ibara ya 46A ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo yeye amekula kiapo kuilinda, kuihifadhi na kuitetea, Bunge laweza kumshataki yeye Rais kwa kosa la mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais.

Wananchi wanaona lugha za ubabe, vitisho, kuonea watu, kudhihaki waliopatwa na majanga kwamba ni mambo yanayodhalilisha kiti cha Rais.

Hivyo Rais achague maneno ya kusema mbele ya wananchi wake, atumie lugha ya kujenga matumaini badala ya kujenga hofu kwenye jamii, aache kuonea watu kwa kutumia madaraka yake, na akumbuke cheo ni dhamana.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo
Kijichi - Dar es salaam
Januari 15, 2017
Ndugu yangu Zitto unatishia kupeleka hoja ya kutokuwa na imani na Rais hahaha yani anaweza akasubiri unataka kuingia kwenye mlango wa bunge na akalivunja bunge hapo hapo..........
Zitto Kigoma kuna mvua nenda kahamasishe kilimo kuliko kupiga kelele facebook na twitter....
Umemshindwa Muhongo kamwe Magufuli hutomuweza unapoteza muda............
 
Ukisoma vizuri hili post utagundua hatua hii ya Zitto bado ni conditional kutegemea na jinsi serikali itakavyo-handle issue ya uhaba wa chakula katika siku zijazo.
Tatizo ni kuwa siasa zi.etukaa sana mbelembele na hatufikirii namna ya kulipeleka taifa kuzuri
Kama ni uhaba wa chakula mbna ishatokea mara kibao nyuma na mambo yakawa mazr baadae
 
Zitto akizidi kumwandama Magufuli atapotea Kama Ben Saa tisa.
ZK kwa sasa kinachomfaa ni kupuuzwa tu! Asizuiwe kutoa maoni, yenye tija yachukuliwe lakini yaliyo mengi hayana mashiko! Ili amuelewe rais wetu ni lazima ashuke kwenye uelewa wa masikini waliowengi na aachane na utaratibu wa kukariri kwa kusomea, watz wengi wanamtazamo tofauti kabisa na yeye! Kwa wananchi waliowengi waliokuwa wamezoea kudanganywa Magufuli is by far a more practical president. Aende tu na muswada wake hazuiliwi na mtu!
 
Asijaribu kuitisha hiyo kura hata nyumbani kwake maana atapata aibu ya mwaka! Zito amepoteza moral authority ya kuhoji lolote tokea anganganie uwenyekiti chadema na kwenda kuanzisha chama chake!

Ameonesha kua yeye ni mwanasiasa mbinafsi na mjivuni sana asiyetaka kuwa chini ya mtu yoyote!

Tabia hiyo anataka kuleta katika jamii ya Kitanzania iliyostaarabika!

Zito ni wa kuogopwa na kupingwa kwa nguvu zote!
Sijui kama umemuelewa mleta mada! Uliyoyaandika hayafanani na mada, jitafakari...
 
Jambo moja ni muhimu sana, Rais anapaswa kujua kuwa anafanya kazi kwa mujibu wa Katiba ya nchi. Na Katiba imetoa wajibu wa lazima kwa Serikali kulinda watu. Ndio kazi ya Serikali – kulinda wananchi pale ambapo yanatokea majanga ambayo yanazidi kimo wananchi hao.

Tunamwambia Rais kwamba, Mtanzania yeyote akifa kwa njaa kwa sababu Serikali imeshindwa kutekeleza wajibu wake Watanzania tutapaswa kuchukua hatua, Katiba inatulazimisha kumtoa Rais madarakani ikiwa yeye na Serikali yake watashindwa kutimiza wajibu wake wa kulinda uhai wa raia wake.

Tunamkumbusha Rais kuwa yeye sio mungu mtu. Yupo chini ya Katiba na kwa idadi ya wabunge wa upinzani waliopo Bungeni, na wakiamua kusimama na wananchi na kulinda Katiba, Rais wa sasa atakuwa Rais wa kwanza wa nchi yetu kutolewa hoja ya kutokuwa na imani naye bungeni. Katiba inahitaji asilimia 20 tu ya wabunge kuwasilisha hoja hiyo bungeni.

Ninatoa wito kwa Watanzania wote nchini, bila kujali vyama vyao, kuweka rekodi ya hali ya chakula popote walipo na kuweka takwimu ya maafa yeyote yanayotokana na njaa. Mtanzania yeyote akifa kwa njaa ni lazima tuchukue jukumu la kumwajibisha Rais kwa kusema waziwazi kwamba hajatimiza wajibu wake kama Mkuu wa Serikali kulinda wananchi wake.

Tunamkumbusha Rais kwamba kwa mujibu wa ibara ya 46A ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo yeye amekula kiapo kuilinda, kuihifadhi na kuitetea, Bunge laweza kumshataki yeye Rais kwa kosa la mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais.

Wananchi wanaona lugha za ubabe, vitisho, kuonea watu, kudhihaki waliopatwa na majanga kwamba ni mambo yanayodhalilisha kiti cha Rais.

Hivyo Rais achague maneno ya kusema mbele ya wananchi wake, atumie lugha ya kujenga matumaini badala ya kujenga hofu kwenye jamii, aache kuonea watu kwa kutumia madaraka yake, na akumbuke cheo ni dhamana.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo
Kijichi - Dar es salaam
Januari 15, 2017

Hakujua poleni.
 
Asijaribu kuitisha hiyo kura hata nyumbani kwake maana atapata aibu ya mwaka! Zito amepoteza moral authority ya kuhoji lolote tokea anganganie uwenyekiti chadema na kwenda kuanzisha chama chake!

Ameonesha kua yeye ni mwanasiasa mbinafsi na mjivuni sana asiyetaka kuwa chini ya mtu yoyote!

Tabia hiyo anataka kuleta katika jamii ya Kitanzania iliyostaarabika!

Zito ni wa kuogopwa na kupingwa kwa nguvu zote!
Leo ndo mnamkataa
 
Jambo moja ni muhimu sana, Rais anapaswa kujua kuwa anafanya kazi kwa mujibu wa Katiba ya nchi. Na Katiba imetoa wajibu wa lazima kwa Serikali kulinda watu. Ndio kazi ya Serikali – kulinda wananchi pale ambapo yanatokea majanga ambayo yanazidi kimo wananchi hao.

Tunamwambia Rais kwamba, Mtanzania yeyote akifa kwa njaa kwa sababu Serikali imeshindwa kutekeleza wajibu wake Watanzania tutapaswa kuchukua hatua, Katiba inatulazimisha kumtoa Rais madarakani ikiwa yeye na Serikali yake watashindwa kutimiza wajibu wake wa kulinda uhai wa raia wake.

Tunamkumbusha Rais kuwa yeye sio mungu mtu. Yupo chini ya Katiba na kwa idadi ya wabunge wa upinzani waliopo Bungeni, na wakiamua kusimama na wananchi na kulinda Katiba, Rais wa sasa atakuwa Rais wa kwanza wa nchi yetu kutolewa hoja ya kutokuwa na imani naye bungeni. Katiba inahitaji asilimia 20 tu ya wabunge kuwasilisha hoja hiyo bungeni.

Ninatoa wito kwa Watanzania wote nchini, bila kujali vyama vyao, kuweka rekodi ya hali ya chakula popote walipo na kuweka takwimu ya maafa yeyote yanayotokana na njaa. Mtanzania yeyote akifa kwa njaa ni lazima tuchukue jukumu la kumwajibisha Rais kwa kusema waziwazi kwamba hajatimiza wajibu wake kama Mkuu wa Serikali kulinda wananchi wake.

Tunamkumbusha Rais kwamba kwa mujibu wa ibara ya 46A ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo yeye amekula kiapo kuilinda, kuihifadhi na kuitetea, Bunge laweza kumshataki yeye Rais kwa kosa la mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais.

Wananchi wanaona lugha za ubabe, vitisho, kuonea watu, kudhihaki waliopatwa na majanga kwamba ni mambo yanayodhalilisha kiti cha Rais.

Hivyo Rais achague maneno ya kusema mbele ya wananchi wake, atumie lugha ya kujenga matumaini badala ya kujenga hofu kwenye jamii, aache kuonea watu kwa kutumia madaraka yake, na akumbuke cheo ni dhamana.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo
Kijichi - Dar es salaam
Januari 15, 2017
Unafiki wake tunaujua na hata chuo alitusumbua kwa roho ya ubinafsi. Yuko kimaslahi zaidi...kapewa lamba lamba kwa kuwa huwa hawezi kuchukua maada yeyote bila ....
 
Zitto ananifurahisha sana. Siasa za JK anampelekea Magu.
 
Binafsi Nina subiria Kwa hamu magazeti ya Kesho baada ya haya matukio matatu ya Leo

1. JPM kule Magu

2.Lowassa kule Kagera

3.Zito kule Dar
 
Nilikuwa namuelewa Zitto, lakini kwa kauli zake za kumpiga rais wetu wa ukweli hanipat tena, Zitto ndumilakuwili.
 
Back
Top Bottom