Zitto Kabwe kupeleka Bungeni hoja binafsi ya kutokuwa na Imani na Rais Magufuli

Asijaribu kuitisha hiyo kura hata nyumbani kwake maana atapata aibu ya mwaka! Zito amepoteza moral authority ya kuhoji lolote tokea anganganie uwenyekiti chadema na kwenda kuanzisha chama chake!

Ameonesha kua yeye ni mwanasiasa mbinafsi na mjivuni sana asiyetaka kuwa chini ya mtu yoyote!

Tabia hiyo anataka kuleta katika jamii ya Kitanzania iliyostaarabika!

Zito ni wa kuogopwa na kupingwa kwa nguvu zote!
 
Safi sana watakubeza lakini utakuwa umeandika historia yenye heshima na uzalendo.

Hii hatua imechelewa sana.

Tumezidi kulalamika tu bila kuonyesha uthubutu ndio maana tumefika hapa tulipo.Matamko juu ya matamko wameshayazoea.It is enough.

Najua hoja haitapita ila ujumbe utakuwa umefika na historia itakuwa imeandikwa.
Ningeshangaa usingeandika
 
Zito amenza kuchanganyikiwa sasa!Maghala ya chakula yamejaa chakula na bado ukienda sokoni unapata unachokitaka japo kwa bei juu kwa sasa kutokana na msimu.

Wataalamu wanasema kwa kipindi hiki bei za vyakula kupanda ni kawaida sana, pia kilichopo kwa sasa ni upungufu wa mvua kwa baadhi ya maeneo sio TZ yote..Sasa anataka ajiimarishe kisiasa kwa hoja yake ambayo wengi bado hatukubaliane nae..Akitaka tumuone wa maana aimarishe hoja yake kwenye kuingalia sera ya kilimo huko bungeni kuwa badala ya kutegemea mvua serikali ije na mpango wa kuwawezesha wakulima kwenye kilimo cha kisasa, umwagiliaji na kutumia maziwa kama Victoria na Tanganyika!Ufugaji pia uwe wenye tija..Kifupi aelekeze nguvu kwenye solution zaidi kuliko lawama..

Huyu jamaa naye kwa sasa anaweweseka baada ya kushuka umaarufu wa kisiasa..Namshauri atulize mshono au kipele chake na aelekeze nguvu kwenye sera ya kilimo ili kiwe cha kisasa badala ya ilivyo sasa kutegemea mvua..

Mheshimiwa rais endelea kukaza hapo hapo wananchi tulizoea kudeka..Hata bungeni wakisema hawana imani na wewe huku mtaani bado tunakukubali kinoma..UKAWA MWAFAA!
 
MAHAKAMA YA MAFISADI imeundwa kuwa mapambo ya Ikulu au kushughulikia mafisadi? Sasa kwa nini hao Mafisadi wa Richmond waliofukuzwa CCM wasifikishwe mbele ya mahakama hiyo badala ya kuachwa na sasa 'wanamtumia Zitto kuidhoofisha Serikali kwny Maoambano yake dhidi ua ufisadi'?

Kesi ya Jinai haina lapse of time!
 
Asijaribu kuitisha hiyo kura hata nyumbani kwake maana atapata aibu ya mwaka! Zito amepoteza moral authority ya kuhoji lolote tokea anganganie uwenyekiti chadema na kwenda kuanzisha chama chake!

Ameonesha kua yeye ni mwanasiasa mbinafsi na mjivuni sana asiyetaka kuwa chini ya mtu yoyote!

Tabia hiyo anataka kuleta katika jamii ya Kitanzania iliyostaarabika!

Zito ni wa kuogopwa na kupingwa kwa nguvu zote!
Chuki zako, anaongelea katiba wewe unasema chadema. Yaani kama haujaelewa kaa kimy tu.
 
Ivi raisi aliefuta ufisadi mchini na kuleta usawa bado watanzania mnampinga???
Mnataka ufisadi urudi au???

Tatizo watanzania wengi wamejaliwa na sifa binafsi na si kuliweka taifa mbele
Ukisoma vizuri hili post utagundua hatua hii ya Zitto bado ni conditional kutegemea na jinsi serikali itakavyo-handle issue ya uhaba wa chakula katika siku zijazo.
 
Jambo moja ni muhimu sana, Rais anapaswa kujua kuwa anafanya kazi kwa mujibu wa Katiba ya nchi. Na Katiba imetoa wajibu wa lazima kwa Serikali kulinda watu. Ndio kazi ya Serikali – kulinda wananchi pale ambapo yanatokea majanga ambayo yanazidi kimo wananchi hao.

Tunamwambia Rais kwamba, Mtanzania yeyote akifa kwa njaa kwa sababu Serikali imeshindwa kutekeleza wajibu wake Watanzania tutapaswa kuchukua hatua, Katiba inatulazimisha kumtoa Rais madarakani ikiwa yeye na Serikali yake watashindwa kutimiza wajibu wake wa kulinda uhai wa raia wake.

Tunamkumbusha Rais kuwa yeye sio mungu mtu. Yupo chini ya Katiba na kwa idadi ya wabunge wa upinzani waliopo Bungeni, na wakiamua kusimama na wananchi na kulinda Katiba, Rais wa sasa atakuwa Rais wa kwanza wa nchi yetu kutolewa hoja ya kutokuwa na imani naye bungeni. Katiba inahitaji asilimia 20 tu ya wabunge kuwasilisha hoja hiyo bungeni.

Ninatoa wito kwa Watanzania wote nchini, bila kujali vyama vyao, kuweka rekodi ya hali ya chakula popote walipo na kuweka takwimu ya maafa yeyote yanayotokana na njaa. Mtanzania yeyote akifa kwa njaa ni lazima tuchukue jukumu la kumwajibisha Rais kwa kusema waziwazi kwamba hajatimiza wajibu wake kama Mkuu wa Serikali kulinda wananchi wake.

Tunamkumbusha Rais kwamba kwa mujibu wa ibara ya 46A ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambayo yeye amekula kiapo kuilinda, kuihifadhi na kuitetea, Bunge laweza kumshataki yeye Rais kwa kosa la mwenendo unaodhalilisha kiti cha Rais.

Wananchi wanaona lugha za ubabe, vitisho, kuonea watu, kudhihaki waliopatwa na majanga kwamba ni mambo yanayodhalilisha kiti cha Rais.

Hivyo Rais achague maneno ya kusema mbele ya wananchi wake, atumie lugha ya kujenga matumaini badala ya kujenga hofu kwenye jamii, aache kuonea watu kwa kutumia madaraka yake, na akumbuke cheo ni dhamana.

Kabwe Z. Ruyagwa Zitto
Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo
Kijichi - Dar es salaam
Januari 15, 2017


JPM mulika huyu mtu, kachukua hela za NSSF.

Ni makelele tuuu utadhani jipu linakamuliwa
 
FB_IMG_1480342998100.jpg
 
Back
Top Bottom