Zitto Kabwe For Tanzanian President Candidate - Golden Chance

Status
Not open for further replies.
Zitto hana kosa kugombea uenyekiti wa CHADEMA (au chama chochote kile atakachopenda).

Kinachoongelewa na wengi hapa ni flip flop aliyoonyesha kwenye hii process.

He is the ultimate flip flopper and he's not in my books anymore as a promising, vibrant, young lawmaker. He's just like the rest of them
 
Kweli kabisa NN,

Kijana kalikoroga na sasa badala ya kulinywa haraka haraka, anazidi kuongeza sukari .... yatakayofuatia hapo ni zaidi ya Absolut Vodka
 
Colleagues, your opinions sound rather fiddly and therefore one needs to take them literally. I doubt the kind of political analysis you people are doing. Tanzania politics is not as simple as you think. Perhaps you need more information than you currently have. Why are you forgetting so early? Why do we still have political conflicts in Zanzibar? Why do you think Mrema did not become the president during the first multiparty election? Why do you think Cheyo finally opted for MP? Leo mnamshauri Zitto ahame CHADEMA akagombee urais CUF!!! I think we need to be critical in our analyses and also give practical or evidence based suggestions if we are all heading to the same destination.

"Zittto aende CUF" Why?. Some of you remember what happened in Dodoma few years ago when our current President, His Excellency, Hon. Jakaya Mrisho Kikwete was stop and Mkapa took over the presidency. Did Kikwete move to another party? My suggestion is that irrespective of what happened to Zitto in his party, he should continue being a respective and true member of the party.

Mkubwa we jiandikie tu kwa lugha yetu hii tamu ya taifa kiingereza .....mh!
 
Bhaghosha,

Me kwa mtazamo wangu kwa hiyo Hoja ulio toa hapo juu, Kweli Zitto akigombea Urais kuna uwezekano mkubwa sana aka compete sasa na JK na wana CCM hawato lala kwani ni wazi zitto atapata nguvu kubwa toka kwa vijana sio tu kwa CHADEMA,CUF,TLP,NCCR,wala CCM vijana wote wa vyama hivyo watata kuuthibitishi umma kuwa kijana mwenzio bila kuangalia itikadi yoyote wanampa kura na Urais anauchukua, ingwawa watu wanaliona ni kama ndoto ila mjue Democrasia iko mpaka vijijini jamani, kwenye kupiga kura me huangalia yule atakaenitetea me mwananchi kwanza siangalii chama hata kidogo.

Kijana kalikoroga na sasa badala ya kulinywa haraka haraka, anazidi kuongeza sukari ....

Nimecheka hadi nasikia maumivu ya mgongo. Kumbe ukilikoroga ni budi ulinywe harakara haraka kabla halijageuka zege! hehehehehe, heheheheh.
 
Toa Maoni yako:

UCHAGUZI WA RAIS 2010 KATI YA WAGOMBEA

Mh.JAKAYA M. KIKWETE (CCM)
vs
Mh.ZITTO Z. KABWE (CHADEMA)
 
Kwa logic ipi? futa tu thread yako wala haina maana. Tanzania haruhusiwi mtu kugombea Urais akiwa chini ya miaka 40. Zitto ana 33 sasa. Ni vema ukafuta thread yako.
 
Hii nayo inahesabika kama moja ya thread za JF! Please MOD do the necessary!
 
Kweli kabisa NN,

Kijana kalikoroga na sasa badala ya kulinywa haraka haraka, anazidi kuongeza sukari .... yatakayofuatia hapo ni zaidi ya Absolut Vodka

Bora angekua anaongeza sukari....huyu anaweza chumvi kwenye kikombe cha chai.
 
Kwa logic ipi? futa tu thread yako wala haina maana. Tanzania haruhusiwi mtu kugombea Urais akiwa chini ya miaka 40. Zitto ana 33 sasa. Ni vema ukafuta thread yako.
imi

UMEMUAMBIA sawa katiba inasema ni miaka 40....,nadhani hata wadhamini wa chadema walitumia kigezo hicho kumuomba avumilie hata kwenye uwenyekiti agombee mwaka 2013 ,,,akimridhi mbowe...,na atakuwa na miaka 2 ya kujiandaa kugombea urais mwaka 2015 ikiwa kufikia wakati wa uchaguzi atakuwa ametimiza miaka 40.....ndio sababu kuu ya kumuomba asubiri.Wakijuwa wazi kuwa mwaka 2015 na mwaka 2020 ...ndio miaka hasa ya muheshimiwa zitti kambwe kufikia kilele za siasa za tanzania...

kwa umri wa miaka 33 alionao ...anahitaji bado kuongozwa na hata ikiwa kuna maoni aliyotoa humu ndani watu hawakupendwa ...basi tunahitaji kumuangalia kwa jicho la mdogo wetu,kaka,au mwanetu....wengi hapa tunao vijana wa umri huu nyumbani na bado ni kula kulala ....sasa hatuoni kuwa zitto kwa umri wake huu kapiga hatua....
nadhani ni busara kumuelewa kama na yeye ataliona hilo ....ikiwa anaweza kikiri kughafirika ...na kujutia matamshi yake hata kwa moyo tu[kimyakimya].Wengi hapa wanaomuambia ukweli ndio wanaompenda ....wanaomsifia na kumpa kichwa ..eti aendelee kuropoka ni watu wabaya,hawampendi.Ni kama wale watoto wanaoshinda nje ya vilabu vya pombe kusubiri walevi watoke na kuwafuata nyuma wakiwashangilia...pale wanaposema "nivue ,nisivue" watajibu "vuaaaaa""...lengo lao ni kumdhalilisha "mlevi"
akitokea rafiki au ndugu yake kumvika nguo basi ...wale waliokuwa wakisheherekea kudhalilika kwake ..wapo tayari hata kumpiga aliyekuja kumsitiri na kumtukana .....na hata yule "mlevi" atamuona aliyekuja msitiri kuwa ni mbaya ....lakini mara "pombe" au "hasira" zikiisha ....aliyekuwa mlevi atamuendea rafikiye aliyemsitiri na kumtaka radhi ...na kumshukuru ....na wale waliokuwa wakimshangilia aendelee kuharibu....atawaona ni wachawi na wabaya sana!!
 
Kusema kweli nipo nikisoma maoni yenu kimsingi kabisa na hayana wasiwasi juu ya uchambuzi ninaoufuatilia ,nilichokigundua ni kuzidi kumpaka matope Zitto na shutuma nyingi zinatoka kwa wafuasi wa Chadema ,sielewi kwanini leo hii Zitto amekuwa anawasababishia kichefuchefu wadau wa Chama hiki cha Chadema.

Ukiangalia kwa kina kabisa utaona wafuasi wa Chadema wapo katika mikakati ya kumuangamiza kama matarajio ya CCM yalivyo ,wammalize na asitajike katika duru za kisiasa.Yeye kuwemo katika kamati ya Raisi hatakuwa ni mtu wa mwanzo yupo Hamad Rashid mpinzani nambari one ndani ya Tanzania na ni mtu wa kuheshimika sana na CCM na Serikali yake inalielewa hilo ,pili hakuna mzozo kati ya Hamad Rashid na CUF.

Kumchukia Zitto na kumfanya si lolote si chochote na kusema kuwa ameanza kusahaulika hapo Chadema watakuwa wanalipa fadhila za kipunda ,fahamuni tu kuna vingunge kibao wamehama CUF na hatukuona mtiririko wa mawimbi yaliyochafua uhusiano kati ya nomads hao na uongozi wa CUF ,yalipita kama maneno ya siku mbili tu ambayo yakichochewa na waandishi na vitimba kwiri wengine ,lakini bahari ilitulia na leo watu wanendelea na kuheshimiana ,CUF haikuanika wala kutafuta vyombo vya habari na kumlaani aliehama zaidi ya kumtaka huyo aliehama ajiheshimu na kuheshimiana na hadi leo husikii tena maneno maneno ,ila hapa Chadema Zitto bado ni mwanachama lakini kumekuwa na masimango makubwa sana ambayo yatamfanya awe mnyonge siku zote na vile vile kuonekana si mwenye hekima ,nasema mnachomfanyia mwanachama ambae bado ni mwenzenu ni kuzidi kumhujumu na kutaka kile mlichokuwa nacho kukidhihirisha ,ukweli ambao ni ushauri wa bure ili kuzima majaribu haya aidha viongozi wa Chadema wakemee juu ya hujuma hizi au kwa Zitto kuwaepuka Chadema kwa salama na amani kabisa.

Rai niliyoitoa ni kujaribu kumrudisha Zitto kwenye chati za ulingo wa siasa ambazo kwa imani yangu zinaweza kurudi na kuzidi pale alipofikia ikiwa tu atajiunga na Chama cha CUF ,hilo halina mbadala kuliko kuendelea kuishi ndani ya jeneza la Chadema na kuonekana kama mtu aliefiliwa na kuondokewaa na wazazi wake na hana wa kumsaidia ,waChadema wote wanaonekana wamemsaliti.

Naamini kabisa kuwa vijana wengi bado wana imani nae na ikiwa atakuja kwa mshindo wa kuhamia CUF basi nawahakikishia hakuna atakaerudi nyuma katika kumuunga mkono, zaidi ya wapiga makelele na wapiga debe wa CCM na Chadema kumwandama kwa mijineno, lakini aminia kabisa nguvu ya upinzani Tanzania itakuwa kama imezaliwa upya na msukumo wake utakuwa si wa kawaida maana CUF shughuli za kupambana na wafuasi wa Sultani CCM wanaziweza na hilo mwengi wenu mnalielewa na halina ubishi.Maana kashkash za CUF hazina kurudi nyuma kilichobakia ni uamuzi wa viongozi tu ambao wamekuwa kila kukicha wakiionya serikali iliyoko madarakani isicheze na amani ya nchi hii siku CUF wakiamua kufungulia basi hakuna cha jeshi wala polisi ni lazima CCM waje na sare ya East & central Afrika ya kupika mseto ,natumai Zitto anahitajika kujiunga na CUF na hili ni jambo ambalo CCM na marafiki zake wanaliogopa kikweli.

Na WaTanzania walio wengi wanamtazama Zitto kwa jicho la tamaa kabisa ikiwa atajiunga na CUF basi mambo yatazidi kutimia.Na kutakuwa hakuna wa kulalamika kwani mambo yatakuwa ni mbele kwa mbele.
 
Supported; I said I like JF!
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom