Nyota ya zitto kabwe ni kali sana fuatilia haya..

malkiamrembo

JF-Expert Member
Mar 29, 2015
386
231
Ndugu zangu naomba nianze kwanza na kuwapa pongezi wananchi wote waliohama kutoka CUF na kuhamia ACT WAZALENDO, Kimsingi sijaona umuhimu wa Prof. Kuendelea kung'ang'ania madaraka kwasababu angefanya uungwana tu kumuachia Maalim, kwa sababu kwa sasa kwenye mioyo ya watanzania sidhani kama ana nafasi ile aliyokuwa nayo zamani hususani alichokifanya mwaka 2015 alicho wafanyia UKAWA kwa kubadili gia angani.(maoni yangu)
Pili napenda kurejea ktk mada yangu kuwa Mh. Zitto Kabwe ni wa hatari sana ktk medari hizi za siasa...nyota yake ktk siasa ni kubwa sana....hebu tukumbuke haya..

1. Alipokuwa CHADEMA alileta utisho sana kwa uongozi wa juu na hata kujiona kama anafaa kuwa Mwenyekiti..
2. Wakati wa Mchakato wa Mgombea Binafsi, Mh. Zitto alikuwa kimbelembele katika kudai hilo sana na alikwama kugombea Uraisi kwa sababu ya umri tuu lakini alithubutu kufanya vitu fulani
3. Alipohamia ktk chama cha ACT mbali na Presidential candidate wake kukihama hicho chama yeye alibaki imara na kukijenga chama yaani kana kwamba chama kizima yupo mwenyewe,lkn kina vuma sana
4. Umaarufu wake ktk medani hizi za siasa haushuki, hapa utaona wapo wanasiasa ambao umaarufu unapanda na kushuka lakini sio kwa ZITTO KABWE.
5. Uwezo wa kujenga hoja na kubishana kwa uhakika na thabiti, ktk hili hakuna asiyefahamu kama Mh. Zitto akiwa bungeni ni machachari sana ktk hoja nakuibua uovu mwingi wa Taifa.
6. Kuhama kwa wafuasi wa Cuf na kuhamia ACT. Jambo hili mimi nimeliona kwa jicho la tatu kwanza nikawaza kwann wasiende CHADEMA au TLP?na wakaamua waende ACT, nikapata jibu kuwa Maalimu seif kuna nukta ambayo anamkubali sana Mh. Zitto.

MWISHO

Huyu Zitto ipo siku watu watatamani wawe nae tena.... kama mtu aliweza kukipigania chama chake bila Back up yyte nyuma yaani Man Alone....itakuwaje kama akipewa dhamana yenye back up....
WATANZANIA TUJIFUNZE KUWASIFIA WATU WAKIWA HAI SIO MPAKA WAFE NDIO TUTOE SIFA ZAO....MIMI NAKUSIFU ZITTO WEWE NI MPAMBANAJI SANA. MINGU AKUBARIKI NA NDOTO ZAKO ZI TIMIE.
:::::::^:::^^^^Huo ni mtazamo wangu::::::::::^:^^

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hilo nililiona mapema sana

Zitto ana ushawishi mkubwa sana, hata hivyo ni kwakuwa mikutano ilizuiliwa; jamaa angekuwa na wafuasi wengi mno.

Akizua hoja yeyote ile, anajua kuijenga na kuilinda. Hatoki nje ya mstari

Anapotoa hoja, huwa anakuwa na ushahidi wa kutosha kabisa.
Akianza kutoa hoja zake waweza jikuta unaonekana mtuhumiwa badala yake.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom