Zitto Kabwe For Tanzanian President Candidate - Golden Chance | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Zitto Kabwe For Tanzanian President Candidate - Golden Chance

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mwiba, Sep 1, 2009.

Thread Status:
Not open for further replies.
 1. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #1
  Sep 1, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Naona Zitto ajibu mapigo kwa kujiunga na CUF ili arudishe hadhi yake .ni hapo tu atakapo anza kupaa na huenda hata nafasi ya kugombea Uraisi akapewa ,Zitto hiyo ni Golden Chance kuukwaa Uraisi wa Tanzania kupitia CUF kazi kwako.Hii ni tiketi ambayo ipo wazi kabisa na labda utaona kama masihara lakini nafasi ya kugombea Uraisi kwa tiketi ya CUF ipo wazi kabiza ,Lipumba ni mtu mwenye akili sana na nahisi angependa kupata kijana mbadala ambae ana msimamo wa kuikomboa Nchi hii na mwenye kukubalika katika jamii ,hivyo jishauri na utakuja kunikumbuka ,tatizo vijana mnakuwa mnashindwa kuelewa kuwa Chama kinachowafaa ni CUF ili kupambana na CCM na si chama kingine chochote kile ,ipeleke nguvu yako CUF ichanganywe na ya Maalim Seif tuone kama CCM hawakuanguka.
  Wakuu mnasemaje kwa hili ,mpeni ushauri wa bure Zitto.
  Nasikia Lwakatale ajuuuuuuta kujunga na Chadema.
   
 2. Josh Michael

  Josh Michael JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2009
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,525
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mwanzoni alianza vizuri lakini siku zinavyozidi kwenda mbele ndio anazidi kwenda kunani.. Inapaswa sana Zitto kuwa makini hata kushauriwa na watu makini sana kuliko sasa hivi anavyofanya mambo yake. Sijui kama hili linaweza kutokea kwake
   
 3. K

  Kyaruzi Member

  #3
  Sep 1, 2009
  Joined: Mar 23, 2007
  Messages: 83
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwiba unatega ndowano kabisa,nadhani ushauri wako ataufanyia kazi kama uenyekiti kanyimwa itakuwa na hiyo nafasi kubwa?
   
 4. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #4
  Sep 1, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Kweli kabisa Mwiba,

  Zitto aingie CUF apewe uenyekiti (natumaini kuwa yale madogo dhidi Prof Safari yaliyotolewa na kambi ya Lipumba wakati wa uchaguzi hayatakuwepo kipindi hiki) au wewe unasemaje?
   
 5. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #5
  Sep 1, 2009
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280

  tell them,,,,,,,,,,,,,,,,,,,,
   
 6. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #6
  Sep 1, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Nyinyi mnaongelea utani ,Safari ni pandikizi na hana backgorund ya kisiasa ,Zitto hawezi kupewa uenyekiti wa CUf kwani sheria za CUF ni baada ya miezi sita ndio mtu anaweza kugombea nafasi yeyote ile .ila tiketi ya kugombea Uraisi inakuwa ni free kwa kila mwanachama ambae sifa zake zitajitosheleza,vilevile backgound za Safari ni mbalimbali tena mbali sana ,Safari hakuonekana isipokuwa katika kugombea ,wakati ushauri ni kuwa hakuwemo hata ndani ya uongozi wa juu wa CUf, na hivyo utaona alipewa nafasi ya kugombea lakini hakushinda ,hakuambiwa ajitoe ,wala hakushauriwa afanye hivyo ,tofauti na yaliyomkuta Zitto Chadema,kitu ambacho waTz wote wanaona hakutendewa haki,isipokuwa mimi ambae naona kwa vile alikuwa tayari yumo ndani ya uongozi wa juu ,angetulia tu kulinda ile cabinet yao isivamiwe na mtu mgeni kama akina Safari ambao kama wangejitokeza wangelipewa nafasi lakini result yao ni kupata kura chache tu.

  Kwa hili la Zitto kuelekea CUF sio jambo baya ukiangalia kuwa CUF ni Chama ambacho kinakubalika karibuni mikoa yote ile na ni Chama kikuu cha kwanza Cha upinzani hapa Tz na hili Chadema na CCM wanalielewa kwa kina kabisa wala halina ubishi isipokuwa kwa wale ambao wanamatatizo ya kijazba.Rekodi za CUF katika kuusaka Uraisi zipo na result yake ipo na wapiga kura wake wapo mbali ya mizengwe ya CCM,bado CUF ni tishio iwapo uchaguzi utakuwa wa haki na huru,hivi jamani hamuoni majeshi na vifaru vinavyoelekezwa kwa CUF ?

  Hapa Zitto asifanye ucheleweshaji njia ni nyeupe kuukwaa Uraisi wa Tanzania ,hilo alielewe wazi halina ubishi kama nilivyoandika ni Golden Chance ambayo itamuweka katika chati nzuri kabisa kisiasa kuliko hali anayoendelea nayo sasa ambayo imepangwa kumuangusha.

  Zitto kama atasoma hapa basi ajue ni kama ameona lailatulkadiri na wanaJF mtakuja kuikumbuka hii na kusema kweli ,Mwiba aliona mbali.
   
 7. M

  Mwafrika JF-Expert Member

  #7
  Sep 1, 2009
  Joined: Nov 20, 2006
  Messages: 5,490
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 0
  Mkuu Mwiba,

  Ulijuaje kuwa Safari ni pandikizi? Je hata Zitto ni pandikizi kule CHADEMA?
   
 8. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #8
  Sep 1, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Zitto abaki CHADEMA. Agombee urais mwaka 2015.Mwakani agombee ubunge, na kuendeleza mapambano ya kuongeza nguvu za upinzani bungeni ili kuandaa mazingira mazuri ya uchaguzi 2015 i.e tume huru ya uchaguzi.
   
 9. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #9
  Sep 1, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Tatizo mnasoma na kuondoka na shida badala ya faida, Kwani Safari alifanywaje ? Maana mpaka sasa sijaliona tatizo la Safari na vipi utalinganisha ya Safari na Zitto ,hebu niwekeeni sawa ?
  Labda kwa kuwasaidia katika kupata maelezo yenu niambieni :-

  Safari alifanywa nini na Zitto amefanywa nini ?

  Ninavyoafahamu mimi ni kuwa Safari alishiriki uchaguzi na matokeo alishindwa,sina zaidi au sijui zaidi ,kama mnayo wekeni hapa tuchangie.Kuh.kuwa alikuwa pandikizi hizo ni internal factors hazina umuhimu kuziweka hapa ,si alisema anatunga kitabu ,vipi mshapata ronyo.

  Ninavyofahamu Zitto ameenguliwa kama wanavyoengua CCM (tiketi ya uraisi Zanzibar ,mnajua NEC walimfanya nini mtu na kumpisha Karume) ndicho kilichomkuta Zitto.
   
 10. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #10
  Sep 1, 2009
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Kugombea urais siyo lazima uwe mwanachama wa chama fulani.
   
 11. M

  Mkandara Verified User

  #11
  Sep 1, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mwiba,
  Mkuu unachanganya vitu viwili hapa.. Zitto hakatazwi kugombea Urais akiwa Chadema na utaratibu wake uko wazi kabisa..Kinachotakiwa yeye ni Kujipanga tu.. Huyo huyo Zitto hawezi kujiunga na CUF au TLP akadai kugombea Uenyekiti wa vyama hivyo... atapigwa chini kwa kuenguliwa kwani ni jambo la kawaida kabisa ktk mchezo wa siasa.

  Nina hakika Lipumba hawezi kumpisha kwani wapo vijana kibao toka Zanzibar au Bara wanaotaka sana kushika nafasi hiyo, tena wenye uwezo mkubwa kuliko Lipumba mwenyewe... nadhani unakumbuka kwamba hata hao CUF, huyo Limpumba alipitishwa kwa mapendekezo tu ikakatazwa kabisa upinzani dhidi yake na soo lake bado sijalisahau..
  Hivyo Lipumba ni mwenyekiti wa CUF ambaye hakupitia mtihani wa Demokrasia mnayotaka kuitangaza Chadema..Pia hakatazwi mtu kugombea Urais ndani ya CUF itakapo fika wakati wa kujiandikisha..

  Binafsi nilitegemea sana kumwona Zitto katika kugombea kiti cha Urais na akiweza kushinda hilo mara zote mgombea huyo huwa mwenyekiti wa chama..Ni utaratibu ambao nimeuona nchi nyingi maskini au za Kiafrika.
  hata CCM JK amekuwa mwenyekiti baada ya kukaa kiti cha Urais kwa mwaka mzima akipikwa. Hivyo hivyo ilikuwa kwa Mwinyi na Mkapa hakuna kati yao aliyegombea Uenyekiti wa chama kabla hajachukua kiti cha IKULU.

  Mimi nipo sana na Zitto na namuunga mkono siku zote isipokuwa anapofanya makosa siwezi kunyamaza kimya na kumpongeza wakati naelewa kabisa mshikaji kasmell na namwomba Mungu kila mara Zitto anielewe hasira zangu.
  Tatizo la vyama vya Upinzani ni kuwa pandikizi la chama CCM ili nchi yetu iondokane na vikwazo vya kiuchumi tulivyowekewa kwa sababu hatukuwa na Demokrasia. hatukuunda vyama vya Upinzani kwa hiari na kuhakikisha Demokrasia ya kweli inatumika ila vyama vya Upinzani vilitokana na mikwara ya IMF na World bank..
  Upinzani mkubwa wa NCCR chama cha kwanza kabla hakijavunjika na kuundwa kwa matabaka ndio ulikuwa upinzani wa kweli na laiti NCCR ingesimama uchaguzi wa kwanza baina yake na CCM basi biola shaka CCM ingeshindwa isipokuwa CCM ni zaidi ya tunavyofikiria.
  Nayapokea kabisa maneno ya mzee Malecela kwamba chama chake kina mbinu nyingi sana za kupata Ushindi na moja ya ilani ya chama inayotangulia ni Ushindi kwa kila hali..Hivyo mkuu wangu hatushindani ni chama gani chenye vijana au wazee ila tunachokitafuta ni ushindi dhidi ya CCM.
  Kama Zitto ataweza kuviunganisha vichwa vya CUF, Chadema, TLP na NCCR Mageuzi dhidi ya wazee wakongwe waliopandikizwa basi bila shaka nitakuwa mpambe wa hicho chama kipya..Kinyume cha hapo CUF TLP na sijui NCCR vyama vyote hivi ni vyama vinavyoongozwa na watu wanaopanga mstari kila mwisho wa mwezi IKULU kuchukua ruzuku zao..
   
 12. Mwiba

  Mwiba JF-Expert Member

  #12
  Sep 1, 2009
  Joined: Oct 23, 2007
  Messages: 7,606
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  Kupanga mstari kuchukua ruzuku hilo ni jambo la kawaida na ni haki yao.Sasa itakuwa unadharau na kuwasimbulia kwani CCM hawachukui ruzuku mbali wanayolwapua BOT ?

  Weka kando hayo ,yanayomkuta Zitto sasa hivi si mambo ya kawaida ndani ya Chadema na mnamuona kama Yuda msaliti.Mmemsikia mama yake akifoka kwamba mnamwita fisadi,ingawa ni kawaida katika siasa haswa inapofikia katika kugombea kila pro zitakuwepo.

  Mimi nawambia Zitto nafasi ya kugombea Uraisi ipo wazi kwa upande wa CUF ,ingawa Mkuu Mkandara umedai kuwa wapo vijana ndani ya CUF ambao wanaweza kugombea Uraisi ,wengi wa vijana hao ni kutoka Pemba na si vijana ni tayari weshakuwa watu wazima na wajukuu ,kwa siasa zilivyokalia ugombea wa Raisi wa Muungano kunahitajika kijana kutoka bara ,safu ya CUF bara haina kijana ambae yupo tayari kugombea nafasi hiyo au yule ,mapepe Safari ?

  Hivyo basi kama Zitto atabakia Chadema na kupewa ahadi kuwa agombee urais kwani wale wengi wao wamesema wanarudi kugombea ubunge sawa ,ila kwa nionavyo Zitto will not & never be the same again in Chadema ,ndio nikampa ushauri wa kuhama na kuhamia CUF na huko nyote mnakujua ikiwa mrundi Hiza aliweza kupanda chati ndani ya CUF,itakuwa Zitto ambae back ground zake zinaonyesha well propagated on Tz political system na zinakubalika ,halafu CUF ni very cool ndani ya utawala ,tofauti na vyama vingine vya upinzani ,hili linahitaji mwanasiasa makini kulielewa ili ajue ni wapi kwa kuanzia ,yaani ni lazima uweze kuelewa kuwa CUF inapakwa matope na hilo ndio muhimu ili kukwepa matapishi yanayotoka kule wasikoitakia mafanikio CUF.

  Hapa namshauri jamaa asifikiri sana ,njia ni moja tu ,aelekee CUF na mtazame kashkash ya waTanzania watakavyompokea na kuona sasa wamepata shujaa mwengine ambae ataendeleza mapambano ndani na nje ya Tanzania kupambana na CCM ,yaani ni kitu kidogo sana ni uamuzi tu ,yeye mwenyewe ataona kuwa alikuwa anapoteza muda wake pale Chadema na sasa amepata fadhila za punda.
   
 13. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #13
  Sep 1, 2009
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,837
  Likes Received: 125
  Trophy Points: 160
  Beauty and the Beast!!!
   
 14. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #14
  Sep 1, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  unajua kama prof saffari kajitolea mambo mengi sana kwa ajili ya cuf?kiasi cha kuharibu ajira yake chuo cha diplomasia.
  Jee mchukia ufisadi ambaye ni mwana jf mwenzetu kwanini hamkupa nafasi yake ya naibu?
   
 15. M

  Mkandara Verified User

  #15
  Sep 2, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mwiba,
  Sasa haya unayoongea ndio ya Lwakatare na CUF..na ajabu unaonyesha kuelewa ya Zitto ukashindwa ya Lwakatare.
  Kinachoendelea Chadema ni midomo ya baadhi ya wajinga ambao tunawajua vizuri, lakini sitegemei Zitto atakuwa mwepesi wa kutoa maamuzi kama alivyofanya Lwakatare. Pamoja na matukio yote haya inanipa wasiwasi sana tuhuma zinazoendelea mjini kuhusu CUF na Chadema.. Sidhani kama mambo yaliyowakuta Lwalatare na Zitto hayana ukweli ndani yake ila ni jinsi ya watu hawa walivyo respond ndio Umri unapogomba. Najua fika kinachomsumbua Mh. Kabwe Zitto zaidi ni umri ambapo hana experience kuwasoma watu na tabia zao kisha akachukua maamuzi yenye busara yaani ya majibu ya kati bila kusababisha madhara..
   
 16. K

  Koba JF-Expert Member

  #16
  Sep 2, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  nyie naona akili zimechoka,yaani fisadi Zitto awe raisi wetu kweli naamini nchi imeishiwa kabisa...tena waliofilisika kimawazo ni wapiga kura sio mafisadi!
   
 17. M

  Mkandara Verified User

  #17
  Sep 2, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Duh, U made Ur point!..ila tu hakuna aliyesema Zitto awe rais wa nchi isip[okuwa tunazungumzia nafasi ya Zitto kugombea kiti cha Urais ndani ya chama.
   
 18. Kichuguu

  Kichuguu Platinum Member

  #18
  Sep 2, 2009
  Joined: Oct 11, 2006
  Messages: 7,203
  Likes Received: 867
  Trophy Points: 280
  Wewe Mwiba unachoma kweli kweli.
   
 19. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #19
  Sep 2, 2009
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  kweli Kilwa Jazz walisema TENDA WEMA WENDE ZAKO.LEO ZITTO ANAPATA MATUSI HAYA?

  ZITTO NILIKWAMBIA HUKO NYUMA SHUGHULI NA WATU WAKO HAWA WAKAWA WANAKUSIFU KUWA WEWE NI MBUNGE WA TAIFA.USI DILI NA WATU WAKO.LEO WANAKUPONDA KIASI HIKI HATA MIEZI MINNE HAIJAPITA.WEKEZA KWA WATU WAKO KAMA WAO WALIVYOWEKEZA KWENYE CHAMA CHAO HIKI CHA WATU WA KASKAZINI.
   
 20. K

  Koba JF-Expert Member

  #20
  Sep 2, 2009
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  ...wee kipunga kama Zito unamwona father wako kanywe naye chai usituletee upuuzi wako!
   
Thread Status:
Not open for further replies.
Loading...