Zitto Kabwe 'azitoboa' bajeti 5 za serikali ya CCM Mpya

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,305
24,193
June 14 2020

Source : Wazalendo TV

KIONGOZI wa chama cha siasa cha ACT- Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe, amekosoa Bajeti kuu ya serikali na kusema, kila bajeti inapaswa kutafsiri maono, malengo na shabaha, ambazo hazijawahi kuonekana tangu Rais John Magufuli, kuingia madarakani.”

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo Jumapili, tarehe 14 Juni 2020, Zitto amesema, “tangu serikali ya Rais Magufuli, iingie madarakani, haijawahi kutimiza malengo yaliyowekwa katika bajeti zake.”

Ametoa kauli hiyo, siku tatu baada ya Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk. Philip Mpango, kuwasilisha mapendekezo ya makadirio ya mapato na matumizi ya serikali katika mwaka wa fedha wa 2020/21.

Akichambua bajeti moja baada ya nyingine – kuanzia mwaka wa fedha 2016/2017 hadi 2020/2021 – Zitto amesema, kila mwaka serikali imekuwa ikukusanya pungufu ya kile inachokikadiria.

Amesema, “katika bajeti ya kwanza ya Rais Magufuli (2016/2017), serikali serikali ilipanga kukusanya Sh. 29.5 trilioni. Lakini iliishia kukusanya kiasi cha Sh. 25.3 trilioni tu.

“Kushindwa kukusanya kwa kiwango hicho, kukafanya kutokufikia lengo la makusanyo hayo, kwa asilimia 14.33.Ukuzaji huu wa makisio kwa asilimia 31, ni mkubwa sana, ukulinganisha na wastani wa ukuzaji wa makisio ya bajeti wa asilimia 11 katika miaka miwili ya nyuma,” ameeleza.

Amesema, “Sababu kubwa ya serikali ya kushindwa kufikia malengo, ni kuweka makisio makubwa mno bila ushahidi wa takwimu za kutosha kuhusu hali ya uchumi wa nchi.

“Jambo hili lilisababisha ukamuaji mkubwa wa kodi kwa wafanyabishara, jambo ambalo lilisababisha biashara nyingi kufungwa, na hivyo kusababisha athari kubwa kwenye uchumi wa taifa hili.”

Bajeti ya mwaka wa fedha wa 2016/2017, ilikuwa bajeti ya kwanza ya serikali ya Rais Magufuli.

“Licha ya serikali kutambua makosa yake haya ya kuweka makisio makubwa katika bajeti yake ya kwanza, bado haitaki kubadilika,” ameeleza.

Amesema, “kwa kuanza kushusha kasi ya kupandisha makisio kutoka asilimia 31 mpaka asilimia asilimia 7 mwaka 2017/18; asilimia 2 mwaka 2018/19, asilimia 2 mwaka 2019/2020 na asilimia 4 mwaka 2020/2021, tayari uchumi umeshaharibiwa kwa shughuli za uzalishaji kushuka na hivyo malengo ya makusanyo kuporomoka zaidi kuliko mwaka uliopita.”

Amesema, mwaka 2018/19 jumla ya Sh. 32.5 trilioni, zilitarajiwa kukusanywa, lakini kwa mujibu wa taarifa ya CAG, serikali ilikusanya Sh. 25.8 trilioni pekee na hivyo kutofikia lengo la makusanyo kwa asilimia 21.

Amesema, “mwaka 2019/20 jumla ya Sh. 33.1 trilioni, zilitarajiwa kukusanywa, lakini kwa mujibu wa taarifa ya Dk. Mpango, mpaka Aprili mwaka huu, makusanyo yamefikia Sh. 24.85 trilioni tu, ikiwa imebakia miezi 2 kabla ya mwaka wa fedha kuisha.”

Anasema, mpaka Aprili 2020, lengo la mapato ya kibajeti, halijafikiwa kwa asilimia 25 na kwamba makusanyo ya mapato yote ya serikali katika mwaka 2018/19, yalikuwa madogo kuliko bajeti ya mwaka uliotangulia wa 2017/18.

Kwenye uchambuzi wake huo Zitto anasema, kwa mujibu wa taarifa ya Mwaka ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Kamati ya Bunge ya Bajeti, licha ya makadiro na makusanyo halisi yaliyotarajiwa, utekelezaji wa bajeti uko chini ya asilimia 70.

Zitto ambaye ni mbunge wa Kigoma Mjini, ameeleza kuwa katika mwaka wa fedha 2016/17, bajeti ya serikali ilitekelezwa kwa asilimia 66.5, mwaka 2017/18, asilimia 64.5, mwaka 2018/19 asilimia 68.6 na 2019/2020, ilitekelezwa kwa asilimia 62 pekee.

“Kwa ujumla bajeti zote tano za Serikali ya Awamu ya Tano, baada ya hii ya mwaka 2020/2021 kupitishwa na Bunge, zitakuwa ni jumla ya Sh. 162 trilioni. Je, fedha hizi zinaendana na hali halisi ya maendeleo ya wananchi,” amehoji Zitto.

Amesema, taarifa ya hali ya uchumi wa taifa 2019 iliyotolewa na Dk. Mpango, tarehe 11 Juni 2020, inaonyesha kuwa pato la taifa (GDP) limekua kwa asilimia 7, kama ilivyokuwa kwa mwaka 2018.

Hii maana yake ni kwamba, ukuaji wa uchumi haukuongezeka; bali ulibaki pale pale katika viwango vya mwaka uliopita.

Mwanasiasa huyo kijana amesema, katika miaka hiyo mitano ya utawala wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), serikali imeshindwa kutumia rasilimali fedha za nchi kuchochea maendeleo kwa wananchi wake
 
Zito ni msaliti kwa mujibu wa pro chadema na sasa ni msaliti wa taifa anajiuza kwa mabeberu kwa pesa ya mihogo na migebuka hafai kitu
 
June 14 2020
ZITTO KABWE "HAMNA RAIS AMBAYE HAJAKOPA/SIO KUKOPA TU, UNAKOPAJE?"

Mpango wa CCM Mpya wa Nishati umeitia hasara kubwa nchi

Malengo ya kuzalisha nishati yameshindwa kufikiwa. Nchi imebakiwa na madeni makubwa ya miradi ambayo katika miaka 2016 - 2020 imeshindwa kuongeza MegaWatts zaidi ya 1500 ktk gridi ya taifa huku lengo lilikuwa 4,000 MegaWatts.

Gesi ya Mtwara inayosafirishwa kwa bomba lilogharimu pesa nyingi linatumia uwezo wa 6% tu kusafirisha gesi huku 94% ya uwezo wa bomba linabaki bila kutumiwa.

Stieglers Gorge kuchukua zaidi ya miaka 10 kukamilika .

Hali ni mbaya sana ktk ulinganifu wa mikopo iliyochukuliwa na muda ambao umeme wa Stieglers Gorge utaigia ktk gridi ya taifa siyo value for money yaani mikopo hailingani na thamani itokanayo na miradi.

Source : Mwanahalisi TV
 
Ishu ni kuchua miaka mingi au ishu ni kuwepo kwa mradi

Tunaona miradi mingi ya mzee mkapa ilikamilika wakati wa jk na miradi ya jk imekamilika sasa hoja ni kuwa miradi inatija kwa taifa
 
June 14 2020

Source : Wazalendo TV

KIONGOZI wa chama cha siasa cha ACT- Wazalendo, Zitto Zuberi Kabwe, amekosoa Bajeti kuu ya serikali na kusema, kila bajeti inapaswa kutafsiri maono, malengo na shabaha, ambazo hazijawahi kuonekana tangu Rais John Magufuli, kuingia madarakani.”

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo Jumapili, tarehe 14 Juni 2020, Zitto amesema, “tangu serikali ya Rais Magufuli, iingie madarakani, haijawahi kutimiza malengo yaliyowekwa katika bajeti zake.”

Ametoa kauli hiyo, siku tatu baada ya Waziri wa Fedha na Uchumi, Dk. Philip Mpango, kuwasilisha mapendekezo ya makadirio ya mapato na matumizi ya serikali katika mwaka wa fedha wa 2020/21.

Akichambua bajeti moja baada ya nyingine – kuanzia mwaka wa fedha 2016/2017 hadi 2020/2021 – Zitto amesema, kila mwaka serikali imekuwa ikukusanya pungufu ya kile inachokikadiria.

Amesema, “katika bajeti ya kwanza ya Rais Magufuli (2016/2017), serikali serikali ilipanga kukusanya Sh. 29.5 trilioni. Lakini iliishia kukusanya kiasi cha Sh. 25.3 trilioni tu.

“Kushindwa kukusanya kwa kiwango hicho, kukafanya kutokufikia lengo la makusanyo hayo, kwa asilimia 14.33.Ukuzaji huu wa makisio kwa asilimia 31, ni mkubwa sana, ukulinganisha na wastani wa ukuzaji wa makisio ya bajeti wa asilimia 11 katika miaka miwili ya nyuma,” ameeleza.

Amesema, “Sababu kubwa ya serikali ya kushindwa kufikia malengo, ni kuweka makisio makubwa mno bila ushahidi wa takwimu za kutosha kuhusu hali ya uchumi wa nchi.

“Jambo hili lilisababisha ukamuaji mkubwa wa kodi kwa wafanyabishara, jambo ambalo lilisababisha biashara nyingi kufungwa, na hivyo kusababisha athari kubwa kwenye uchumi wa taifa hili.”

Bajeti ya mwaka wa fedha wa 2016/2017, ilikuwa bajeti ya kwanza ya serikali ya Rais Magufuli.

“Licha ya serikali kutambua makosa yake haya ya kuweka makisio makubwa katika bajeti yake ya kwanza, bado haitaki kubadilika,” ameeleza.

Amesema, “kwa kuanza kushusha kasi ya kupandisha makisio kutoka asilimia 31 mpaka asilimia asilimia 7 mwaka 2017/18; asilimia 2 mwaka 2018/19, asilimia 2 mwaka 2019/2020 na asilimia 4 mwaka 2020/2021, tayari uchumi umeshaharibiwa kwa shughuli za uzalishaji kushuka na hivyo malengo ya makusanyo kuporomoka zaidi kuliko mwaka uliopita.”

Amesema, mwaka 2018/19 jumla ya Sh. 32.5 trilioni, zilitarajiwa kukusanywa, lakini kwa mujibu wa taarifa ya CAG, serikali ilikusanya Sh. 25.8 trilioni pekee na hivyo kutofikia lengo la makusanyo kwa asilimia 21.

Amesema, “mwaka 2019/20 jumla ya Sh. 33.1 trilioni, zilitarajiwa kukusanywa, lakini kwa mujibu wa taarifa ya Dk. Mpango, mpaka Aprili mwaka huu, makusanyo yamefikia Sh. 24.85 trilioni tu, ikiwa imebakia miezi 2 kabla ya mwaka wa fedha kuisha.”

Anasema, mpaka Aprili 2020, lengo la mapato ya kibajeti, halijafikiwa kwa asilimia 25 na kwamba makusanyo ya mapato yote ya serikali katika mwaka 2018/19, yalikuwa madogo kuliko bajeti ya mwaka uliotangulia wa 2017/18.

Kwenye uchambuzi wake huo Zitto anasema, kwa mujibu wa taarifa ya Mwaka ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT) na Kamati ya Bunge ya Bajeti, licha ya makadiro na makusanyo halisi yaliyotarajiwa, utekelezaji wa bajeti uko chini ya asilimia 70.

Zitto ambaye ni mbunge wa Kigoma Mjini, ameeleza kuwa katika mwaka wa fedha 2016/17, bajeti ya serikali ilitekelezwa kwa asilimia 66.5, mwaka 2017/18, asilimia 64.5, mwaka 2018/19 asilimia 68.6 na 2019/2020, ilitekelezwa kwa asilimia 62 pekee.

“Kwa ujumla bajeti zote tano za Serikali ya Awamu ya Tano, baada ya hii ya mwaka 2020/2021 kupitishwa na Bunge, zitakuwa ni jumla ya Sh. 162 trilioni. Je, fedha hizi zinaendana na hali halisi ya maendeleo ya wananchi,” amehoji Zitto.

Amesema, taarifa ya hali ya uchumi wa taifa 2019 iliyotolewa na Dk. Mpango, tarehe 11 Juni 2020, inaonyesha kuwa pato la taifa (GDP) limekua kwa asilimia 7, kama ilivyokuwa kwa mwaka 2018.

Hii maana yake ni kwamba, ukuaji wa uchumi haukuongezeka; bali ulibaki pale pale katika viwango vya mwaka uliopita.

Mwanasiasa huyo kijana amesema, katika miaka hiyo mitano ya utawala wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), serikali imeshindwa kutumia rasilimali fedha za nchi kuchochea maendeleo kwa wananchi wake

Source : Zitto Kabwe, ‘azitoboa ’ Bajeti 5 za Rais Magufuli

Zitto Kabwe ni Msaliti wa Chadema, Taifa na Ukoo wake maana walimtenga nao na jawakumtaka atumie Jina lao la ukoo la Kabwe.
 
Zito ni msaliti kwa mujibu wa pro chadema na sasa ni msaliti wa taifa anajiuza kwa mabeberu kwa pesa ya mihogo na migebuka hafai kitu
Zitto yupo kundi moja na Tundu Lissu, Freeman Mbowe, Maalim Seif, Jenerali Ulimwengu, Sugu, Rev Msigwa, Lema, Fatma Karume, Maria Sarungi, Prof Assad - ambao sisi Watanzania tusio misukule tunawatambua kama wazalendo wa kujivunia wa taifa letu.
 
June 15, 2020
Dodoma , Tanzania
MBUNGE ZITTO KABWE BUNGENI LEO "MAMBO KAMA HAYA HATUWEZI KUYAACHA TU YAENDE"

  • Korosho
  • Utalii
  • Ukusanyaji mapato mbuga za wanyama TANAPA n.k
  • Covid-19
  • N.k

Source : Millard Ayo
 
Back
Top Bottom