Francis12
JF-Expert Member
- Sep 30, 2016
- 7,533
- 22,278
Anaandika Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe
Unamkamata mtumishi wa Mungu kama Gwajima kwa kuliambia Taifa kuwa anahusika na dawa za kulevya. Unampekua. Unampima damu na mkojo. Unakuta hana kosa lolote. Unamwachia.
Dunia nzima imejulishwa kuwa Gwajima anahusika na madawa. Waumini wake, familia yake na ndugu na marafiki zake unawaweka katika hali gani?
Sasa wataita tena waandishi kumsafisha? Watamwomba radhi?
Tufuate misingi ya haki. Tukumbuke kuwa Cheo ni dhamana, usikitumie cheo chako au cha mtu mwengine kwa Faida yako.
Ushauri wangu kwa Askofu Gwajima, samehe. Kusamehe ni adhabu kubwa zaidi kwa anayekukosea. Samehe Baba Askofu