Ujumbe wa Askofu Kakobe, mtego kwa CHADEMA unaoelekea kuwashinda kuutegua

kioju

JF-Expert Member
Apr 28, 2014
804
271
Ni takribani siku Nne sasa toka taarifa zizagae hasa katka mitandao ya kijami,i kuhusu ujumbe na Neno alilotoa Askofu Mkuu wa kanisa la Full Gospel Bible Fellowship Z.Kakobe, kwa vyama vya upinzani hususani chama kikuu cha upinzani kwa sasa CHADEMA juu ya kauli za viongozi wake mbalimbali wakiwemo baadhi ya Wabunge wa chama hicho, dhidi ya viongozi wa kiroho walipokutana na Rais Magufuri. Kwa sasa ningependa kutoa mtazamo wangu juu ya hili linaloendelea sasa.
AINA YA UJUMBE ULIOTOLEWA NA KAKOBE
MSTARI WA KUKUMBUKA 1THESOLANIKE 2:13


Ilikuwa siku ya jumapili mida ya usiku nikakutana na taarifa kwa ndugu mmoja niliemfollow IG ameiweka na ilitoka katika ukurasa wa Nipashe ikinukuu maneno ya Kakobe kuwa hakuwahi kuwa pamoja na CHADEMA na huku imewekwa picha ya Kakobe akizungumza katika Mkutano wa chama hicho mwaka 2015, na nikasoma maelezo ya huyu jamaa chini yalikuwa yakimsuta Kakobe kuwa muongo na amuogope Mungu na Tekinolojia.

Mimi mwenyewe nilistuka kidogo ni kwa vipi huyu Mtu ambaye huwa namkubali hivi hata wakati mwingine nimekuwa nafuatilia mafundisho yake aseme uongo hadharani hivi? Sikupuuza habari hizi nikawaza aliitoa kwenye hafla ipi hii kauli Ndg Kakobe, kwasababu siku za hivi karibuni nimekuwa nikimuona akitokea sana katika hafla hizi za kiserikali.nikaanza kuzitafta taarifa kwa vyombo rasmi vya habari ninavyoviamini binafsi kama Azam Tv na Mwananchi katika kurasa zao za mitandao ya kijamii lakini sikuona hafla wala dalili za tukio hilo kuwepo kwa jumapili hiyo wala habari za Kakobe katika kurasa hizo.

Nilipoona hivyo tu nikaanza kupata na mashaka juu ya ile taarifa nikijua ni uzushi na ni mambo ya siasa tupu na editing ili kumchafua kwasababu amekuwa akionekana ktk hafla za Serikali kipindi hiki kifupi, nikapuuzia lkn haikupita muda mfupi nikaziona tena kwenye kurasa nyingi za wanachama na wapenzi wa CHADEMA ambao nimewafollow sana kwasababu ni mpenzi wa chama na sera za chama hiki kwa muda sana, niliamua kumuuliza mtu juu ya taarifa hizi zimesemwa wapi akaniambia ni leo kanisani pale Mwenge, nliposikia hivyo nikaonelea nianze kutafta washirika wa kanisa hilo wanisimlie ilikuwje leo Kakobe aseme uongo huu tena kanisani.

Nilifanikiwa kumpata mmoja wa waumini ambaye aliniambia nadhani nikupe audio usikilize ili nisipinguze wala kuongeza chochote nikasema itakuwa vyema, alinitumia Audio ya kile kilichozungumzwa na Kakobe jumapili kanisani.

Nilichokuta nikagundua ni “AINA YA UJUMBE” ilikuwa ni Neno kutoka madhabahuni kwa maneno mengine ilikwa ni moja ya mambo yaliyosemwa ndani ya Neno la siku ile “Ujumbe kutoka kwa Mungu”.

Nikazidi kuwa na nidhamu ya kusikia kuliko hapo mwanzo huku nikiwa na shauku kubwa ya kusikia kipengele cha kukana kutokuwahi kuwa na CHADEMA na kutokuwahi kuongea na Mh. Lowassa wakati alikuwepo Mlimani City siku Mh. Lowassa anapewa ridhaa rasmi na chama kuwakilisha chama.

Na ikafika muda nikasikia alichozungumza kiukweli vyombo vya Habari vinapaswa kuwa makini na uandishi na kuripoti taarifa ili kuweka maana sahihi ya kile mhusika anachokisema, na kwa bahati mbaya zaidi ni kuwa Watanzania huwa hatuna kawaida ya kufuatilia kwa undani sana huwa tunasubiri kulishwa habari na baadae kuzibeba na kuanza kuzishikia bango kama ilivyokuwa kwenye suala hili.

Kifupi yale aliyoyasema kwamba hakuwahi kuwa na na sisi alikuwa anamaanisha hakuwahi kuwa na ukarbu nao wala kushiriki mambo yao isipokuwa matukio mawili ya Mlimani City na kipindi cha Katiba Mpya haya maneno vyombo vya habari havikufafanua na wazee wa mtandaoni wakaanza kumsuta Askofu Kakobe muongo mbaya zaidi hata wale unaoamini kuwa ni watu wenye udadisi wa mambo na smart katika tafiti kwa hili waliangukia pua ikawa ni kejeli hadi baadhi ya Wabunge ambao kimsingi tunaamini wako smart kuchambua uongo wa Serikali walishindwa kujiridhisha na badala yake kumshutumu na kumsuta Kakobe.

Anyway pamoja na yote hayo tunapoendelea kusoma bandiko hili nenda na kitu kimoja akilini kuwa aina ya ujumbe ulikuwa ni Neno la siku kwa wanadamu wakiwemo CHADEMA ambalo kimsingi wanadamu wanatakiwa kulitendea kazi neon hilo la huwezi kaa kimya ni busara zaidi hil sio hotuba ya JIWE ulijadili na kulipinga kwa ushahidi wako wa madhaifu ya mtoa Neno ukifanya hivyo unafeli tu hakuna namna. 1Thesolanike 2:13

MTEGO KWA CHADEMA
Binafsi nimeanza kumwona Freeman Mbowe miaka ile anagombea Urais kupitia CHADEMA enzi hizo nilikuwa sijavutiwa na siasa sana ila alipokuja kipindi kile nilikuwa Mwnza nikaenda kumsikiliza nikavutiwa sana na siasa na sera za jamaa nikawa nafuatilia sana ziara zake za kampeni nyakati hizo CUF ilikuwa inaitwa Chama kikuu cha upinzani 2005.

Nimemzungumzia Mbowe kwasababu kwangu ni mmoja wa viongozi ambaye anajua wapi azungumze nini na ni kiongozi anayefikiri sana juu ya ustawi wa baadae wa Taasisi kama anayoiongoza na ni ukweli usiopingika kuwa Mbowe ni mmoja wa watu waliotoa mchango mkubwa sana katika ukuaji wa hiki chama hadi kufikia hapo kilipo,na asilimia kubwa ya watu waliotokea mikononi mwa Mbowe wamerithi hekima hizo na kujizuia katika kutoa kauli au kusema, mfano wa watu hao ni JJ Mnyika, na Zitto Kabwe.

Nimeyasema haya kwasababu kipo kizazi kilichoibuka kinachodhani kila neon linahitaji kujibiwa haijalishi ni mtu wa aina gani anajibiwa vipi, kizazi kinachoamini ujasiri ni kumtunishia kifua awayeyote anayeonekana anayekatiza mbele yako pasipokujuwa wako wengine hukatiza kukujulia hali na kukuamsha huwenda umelala adui atakupiga, kosa lako kwao kizazi hiki ni wewe kukanyaga kwenye anga lake utalipuliwa tu.

Sasa hii ni tatizo kubwa sana, sakata hili la Askofu Kakobe wamelichukuwa negative sana kiasi cha kuanza kumshambulia sana hadi wale Wabunge ambao binafsi huwa nawachukulia ni watu wenye hofu sana ya Mungu na wenye busara sana, wengine hadi kipindi huyu Kakobe amemwambia Magufuri atubu walipost taarifa hizi wakimhimiza Magufuri asimsumbue “MTUMISHI WA MUNGU” wala asibishane na Neno la MUNGU yeye atubu tu.

Nyakati zile mtu kama Waziri Kigwangala alimdhihaki Askofu Kakobe,RC wa Arusha ndg. Mrisho Gambo alidirki kumwita Kakobe MBURULA sijui kama nimeandika sahihi, lakin ilikuwa ni dhihaka sana, hawa CHADEMA walisimama na Kakobe wakimsifia sana kuwa ni Mtumishi wa Mungu na Kwamba neon lile lilitoka kwa Mungu kuja kwa Magufuri, Kigwangala alitupiwa maneno makali kumshutum Mtumishi wa Mungu mkubwa namna hiyo na kwamba anatetea tumbo n.k

Hatimae leo Neno kutubu limeingia anga za CHADEMA duh! Chama kinachoanza na Mungu na Kumaliza na Mungu kimekataa kutubu na kuanza kushambulia mjumbe aliyeleta habar kwa kuangalia udhaifu wake huko nyuma, kuna huyu Mchungaji Msigwa nae anahuo unaoitwa ujasiri wa kupinga neon TOBA na ni Mchungaji, anazungumza habari za Utabiri wa Kakobe juu ya Mrema kuwa Rais, sijui Umeme kupita eneo la kanisa alilopo Kakobe sijui CCM kuporomoka 2015, sembuse kuporomoka kwa CHADEMA, nilijiuliza hivi huyu Mchungaji wakati anamtetea Kakobe kipindi cha TOBA kwa Magufuri huyu Kakobe alikuwa sio Yule aliyeyatabiri hayo aliyoyataja?

Anyway ukiachana na hayo inamaana huyu Mchungaji hajui lile andiko linalosema wakati mwingine unabii huwa hautimii ikiwa kuna vitu vimefanyika? Lkn tuachane na habr ya Uchungaji wake tujiulize yeye anafurahia viongozi wenzie wa kisiasa na wanachama wenzie kuendeea kutoa kauli nzito kama zile kwa viongozi wa Kiroho, kwa maneno mengine amejipambanua kuwa yeye kwake chama kwanza Mungu baadae.

Sio huyo tu aliyemshambulia Kakobe baada ya kuambiwa Watubu lakin viongozi wengi wa chama na wanakuja na hoja za MBONA Fulani alikutusi hukutoa kauli kama hizo, wameenda mbali sana hadi wakafukua makaburi kuleta kejeri za jamaa wa CCM waziri na RC wa Arusha walivyofanya na Kakobe kukaa kimya wakiamini hicho kinawapa hualali na wao kumkejeli kumfanyia dhihaka hivyohivyo kama wale, yupo ndugu mmoja anasema hasapoti matusi ila inakuwaje hakuwakemea wale aje awakemee wao?

Dah na Diwani kutoka pande za Sombetini nae maskini wa Mungu akasema anataka kumkera zaidi Kakobe akasema yake humo wakiamini kwamba kufanya hivyo ni kama kumkomoa Kakobe aliyewaambia watubu ni hawa ndio wanapiga vifua huko Magufuri anakiburi asikilizi na kuwadharau watumishi wa Mungu hadi wanaposti video zake alipotoa kauli kipindi cha sekeseke la Gwajima, huku wao wakisahau kuwa wanamkejeli Kakobe wakati huohuo.

Hili jambo limenikumbusha enzi za Adamu na Hawa walipofanya dhambi kimsingi alianza Hawa baadae Hawa akamshawishi Adam, Adamu akakubali kula lile tunda walilokatazwa kula, wakawa wamemuasi Mungu, kwakuwa Mungu aliwapenda hawa viumbe akaja kumuuliza Adamu amefanya nini sasa kwa kufanya asiyoambiwa kufanya, Adam badala ya KUTUBU akaanza kutoa sababu kuwa ni mwanamke uliyonipa hizi habari ni katika Mwanzo 3:9-13. Yaan Adamu hapo alikuwa anaona si halali yake kuitwa mkosa hili hali mwanamke aliyeletewa kamsababishia hilo.

Lakini pia huenda Mungu anawapenda sana CHADEMA ana mpango mzuri sana na Chama hiki, niwape mfano mzuri tu, ni vigumu sana Mzazi kumuadhibu mtoto wa jirani yake kwa makosa aliyofanya au kukosa heshima kuliko kumuadhibu mtoto wake, utaona anamuadhibu vilivyo mtoto lengo ni kumpa malezi bora kwa maisha yake baadae wakati akienda kuishi na jamii. Huwenda ndivyo ilivyo kwa Mungu na CHADEMA kupitia kwa Kakobe soma UFUNUO 3:19 . Nyie msingeleta habari za kupinga na kuleta ushahidi mwiiiiingi huu ni mtego kwenu kuona je hawa watu wanaunyenyekevu mbele za Huyo Mungu wanaeamini kuanza naye na kumaliza naye? Biblia inasema Adhabu inapokuja huonekana ni kitu kisicho na furaha ni kero lkn kumbe mbeleni huleta furaha na Amani lkn zaidi sana HAKI,ambayo mnaitafuta kila siku katika taifa angalieni maandiko haya WAEBRANIA 12:11

Ndugu zanguni CHADEMA mnaelekea kushindwa mtego huu wa kutubu muda bado upo niwashauri tu na hili mimi naamini kabisa mgetubu na kuomba msamaha juu ya kauli zenu kwa viongozi mbalimbali wa kiroho, leo tungekuwa tunazungumza mengine kabisa, mgefungua uwanja mkubwa sana wa utatuzi wa masuala mengi mno ya kisiasa yanayokabili vyama hivi vya siasa katika nchi kupitia hawa viongozi wa dini, mkiendelea na hii tabia ya kutunishia misuri kila anaewashauri na kuwapa muongozo mnampuuza hakuna kundi litakalo saidia hata hao umma wenyewe walishajikatia tamaa.

Nimalizie kwa kuwashauri wanasiasa hasa upinzani si kila neono au jambo ni la kupazia sauti mengine ni mtego yaache yapite, jifunzeni kwa wenzenu wenye hofu ya Mungu ndani yao,wanaamini juu ya kusema panapostahili kusema na kuzungumza nini wakati gani, watu kama Joseph Haule (MB), Salome Makamba (MB), Sugu (MB), Elia Michaeli Diwani na Mbunge nje ya Bunge, na wengine wengi sijawataja hapa.

ILEWEKE NINAPOSEMA KUNYAMAZA KATIKA BANDIKO HILI SIMAANISHI KUFUNGA MDOMO KUTETEA HAKI ZAKO ZA MSINGI, ASANTENI
 
Umeongea vitu vya msingi sana mpaka mwili wote umesisimuka.Ni kweli hili swala ni mtego kwetu CHADEMA ila tatizo kubwa kwenye chama chetu hakina msemaji maalum wa Chama ila kila mtu anajifanya kujua kropoka na kuongea ovyon anavyojisikia
 
"……….chama chenu kitaingia kwenye shimo kubwa na hakitatoka tena-Kakobe". Hawa jamaa walikuwa wanakuja vizuri sana sema ndo hivyo walikosa wisdom ya kujua what to overlook!! Knowing what you want to accomplish in the end (long term goals) will help you weed out the essential from the nonessential.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom