Zitto Kabwe Asifike katika eneo letu... Zitto asizungumze na watanzania, Period!

Status
Not open for further replies.

Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,605
2,000
Kulewa sifa ni kitu kibaya mno. Utamsikia mtu mzima na akili zake akifoka "Zitto asifike katika eneo letu/mkoa fulani akifika atakiona!" au utasikia mtu mzima na akili zake anafoka "Zitto akae kimya! period!"

Ndugu zangu niulize!

Ni nani mwenye hati miliki ya kumruhusu mtanzania mwenzake kufika au kutofika katika eneo fulani?nani!

Ni nani basi mwenye hati miliki ya kumruhusu mtu kuongea na wenzake na kumzuia pale anapotaka?nani!

Kati yetu ni nani asiyejiamini; kama tunajiamini, tunapiga mayowe ya nini?

Je; si tumemfanyia haki zitto na tunaendelea kumfanyia haki tunaogopa nini?

Si tumemshutumu zitto na kisha tukazunguka nchi nzima kueleza alivyo na matatizo na jinsi asivyofaa? kama tumesema ya kweli, tunaogopa nini na yeye anapoongea na wananchi wale wale ambao sisi tuliongea nao mahali pale pale na hakuna alietuzuia?Tunaogopa nini?

Sisi si tunadai kwamba hoja ndio msingi wa uongozi, kwa maana hiyo tuna nguvu za hoja!, sasa tunaogopa nini Zitto akitoa hoja zake hata tunataka tumzibe mdomo? Au katukana mtu?

Katiba ya Tanzania inamkataza nani kufika wapi ndani ya Jamuhuri ya Tanzania?Au tunafuata muongozo gani?

Kuna katiba au sheria yeyote inayomkataza yeyote kufia kokote ndani ya Nchi hii? au ni nini muongozo wetu sisi tunaowapiga marufuku baadhi ya watu kufika baadhi ya maeneo?Kwa ujinga huu huu kuna siku utasikia Rais asije kwetu! Alaaaah!

Sidhani kama kuna haja ya kujishuku kama tunaamini kwa 100% kwamba tumemtendea Zitto Haki na sisi ni watenda haki daima.Kwani Zitto anapiga watu ngumi au anatoa hoja? Si siku zote tunasema hoja hujibiwa kwa hoja! au tumebadili msimamo wetu?.Natutulie ! au kama tunataka na sisi tuzungumze yetu na twende tunakotaka ndani ya mipaka ya nchi.Huo ndio ustaarabu.
 
The lost son

Senior Member
Dec 14, 2010
102
225
Mimi ni mganga maarufu toka Chigoma. Nasaidia kujiunga na freemason, zittophobia, kuonana na mwigulu, Hela za haraka toka ccm na n.k karibuni woteeeeeeeeeeeeeee
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,605
2,000
Ni ujinga kumzuia mtu mwingine kufanya tendo ambalo legallay sheria Mama Kama Katiba inamruhusu
Haki sawa! haki sawa! haki sawa! haki kwa naniiiiiiiiiii! haki kwa woteeeeeee! asiependa hakiiiiiii.................................!

Mara nyingi nimesema! si busara mtu kudhani yeye ana haki ambazo wengine hawana.Ni bora mtu ajizoeshe kufanya jambo analopenda kufanyiwa ili siku akiona mwenzake anafanya vile vile asipate pressure.Huo ndio uadilifu.Zitto aacwe huru aende apendako ndani ya nchi yake.Zitto ni mtanzania na ana haki zake za kiraia.Na anayemtishia au anayemuhujumu kwa namna yeyote afanye hivyo akijua mwisho wa ubaya aibu.
 
DCONSCIOUS

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
1,269
1,500
Baada ya kuwa zitto wamemuonea kwa kiasi kikubwa sasa wanahaha watafanya kuzima moto ambao wamewasha wenyewe zito hakuna wa kumzuia kupita na kwenda popote atakapo.

Km ambavyo Zitto alijaribu kumzuia Slaa kutua kigoma lakin alishidwa
 
Azizi Mussa

Verified Member
May 9, 2012
8,605
2,000
Km ambavyo Zitto alijaribu kumzuia Slaa kutua kigoma lakin alishidwa
Swali! unawaambia nini wanaojifanya wao ni watu wa muhimu sana na wenye maguvu sana katika nchi hii kiasi cha kujifanya eti wanawapiga marafuku watanzania wenzao kufika eneo fulani au kuzungumza hadharani?
 
Somoche

JF-Expert Member
Oct 6, 2010
4,689
2,000
Nyie mlianza kusema Slaa asikanyage Kigoma au sio Nyie akili hamna, mliposema hivo sheria za nchi mlikua mmeziweka wapi au leo ndio zinafanya kazi tu?!!
 
mnyakarema

Member
May 27, 2013
16
0
mimi natangaza nia leo ya kugombea nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa wa CHADEMA, naomba mnisapoti, mbowe lazima nimpige chini!
 
makomelo

Senior Member
Jun 28, 2013
110
170
Kulewa sifa ni kitu kibaya mno. Utamsikia mtu mzima na akili zake akifoka "Zitto asifike katika eneo letu/mkoa fulani akifika atakiona!" au utasikia mtu mzima na akili zake anafoka "Zitto akae kimya! period!"

Ndugu zangu niulize!

Ni nani mwenye hati miliki ya kumruhusu mtanzania mwenzake kufika au kutofika katika eneo fulani?nani!

Ni nani basi mwenye hati miliki ya kumruhusu mtu kuongea na wenzake na kumzuia pale anapotaka?nani!

Kati yetu ni nani asiyejiamini; kama tunajiamini, tunapiga mayowe ya nini?

Je; si tumemfanyia haki zitto na tunaendelea kumfanyia haki tunaogopa nini?

Si tumemshutumu zitto na kisha tukazunguka nchi nzima kueleza alivyo na matatizo na jinsi asivyofaa? kama tumesema ya kweli, tunaogopa nini na yeye anapoongea na wananchi wale wale ambao sisi tuliongea nao mahali pale pale na hakuna alietuzuia?Tunaogopa nini?

Sisi si tunadai kwamba hoja ndio msingi wa uongozi, kwa maana hiyo tuna nguvu za hoja!, sasa tunaogopa nini Zitto akitoa hoja zake hata tunataka tumzibe mdomo? Au katukana mtu?

Katiba ya Tanzania inamkataza nani kufika wapi ndani ya Jamuhuri ya Tanzania?Au tunafuata muongozo gani?

Kuna katiba au sheria yeyote inayomkataza yeyote kufia kokote ndani ya Nchi hii? au ni nini muongozo wetu sisi tunaowapiga marufuku baadhi ya watu kufika baadhi ya maeneo?Kwa ujinga huu huu kuna siku utasikia Rais asije kwetu! Alaaaah!

Sidhani kama kuna haja ya kujishuku kama tunaamini kwa 100% kwamba tumemtendea Zitto Haki na sisi ni watenda haki daima.Kwani Zitto anapiga watu ngumi au anatoa hoja? Si siku zote tunasema hoja hujibiwa kwa hoja! au tumebadili msimamo wetu?.Natutulie ! au kama tunataka na sisi tuzungumze yetu na twende tunakotaka ndani ya mipaka ya nchi.Huo ndio ustaarabu.

hata wewe umesahau tu kwani wafuasi wa huyo zigo ndo walikuwa wa kwanza kusema dr asifike kigoma! Hukuliona hilo
 
mjepo

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
4,917
1,225
Km ambavyo Zitto alijaribu kumzuia Slaa kutua kigoma lakin alishidwa
Badaye au kesho tukutane pale bavicha tufanye tathimini mikutano ya slaa na zitto nani zaidi tuzingatie vigezo vifuatavyo.
-nani kaongoza kwa kuzomewa kukejeliwa kwa mabango na kulindwa na polisi.
-idadi ya watu waliohudhuria kwenye mikutano yao na nani anayeonekana kupagawa na kuongea bila mpangilio.
 
Jile79

JF-Expert Member
May 28, 2009
17,363
2,000
Kwa uhuni wake haki miliki ataiona na utaiona. Kwa taarifa yako hata unayemwita raid kuna maeneo mengi amekataliwa asihutubie na amepopolewa had I Mawr sembuse huyo mnafiki! Kwa mfano pale mbaya wanasema sugu ndiyo raised wa utawakataza vp. Halikadhalika watu wanahaki miliki na maeneo yao hasa kwa watu waovu km zitto. Nasema asikanyage mkoa wetu
 
mjepo

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
4,917
1,225
hata wewe umesahau tu kwani wafuasi wa huyo zigo ndo walikuwa wa kwanza kusema dr asifike kigoma! Hukuliona hilo
Taratibu mkuu punguza hasila zito niwapolepole mkienda kasi mtapasuka msamba mapema sana kwa lazima mjue zitto ni nani.
 
mjepo

JF-Expert Member
Aug 8, 2013
4,917
1,225
Kwa uhuni wake haki miliki ataiona na utaiona. Kwa taarifa yako hata unayemwita raid kuna maeneo mengi amekataliwa asihutubie na amepopolewa had I Mawr sembuse huyo mnafiki! Kwa mfano pale mbaya wanasema sugu ndiyo raised wa utawakataza vp. Halikadhalika watu wanahaki miliki na maeneo yao hasa kwa watu waovu km zitto. Nasema asikanyage mkoa wetu
Da! Pole naona unaugulia maumivu makali kweli zito noma kweli.
 
Status
Not open for further replies.

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom