Zitto Kabwe, Halima Mdee na Dkt. Kigwangalla walienda JKT Ukubwani, Je Wana Uzalendo wa Kutuvusha kwenye suala la DP World?

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
84,035
142,141
Zamani kipimo cha Uzalendo ilikuwa ni Pamoja na kushiriki Mafunzo ya JKT miezi 9 au Mgambo miezi 3

Kadhalika ili kuwa mwanachama wa CCM ililazimu kuingia darasani kwa miezi 3

Panahitajika Wasomi Wazalendo katika Hili swala la kutoa Elimu ya Mkataba wa Bandari na DP World

Ndio nikawakumbuka Wanasiasa Watatu walioenda Jeshini JKT wakiwa Watu wazima Ili kunoa Uzalendo wao hawa si wengine bali Zitto Kabwe ( ACT Wazalendo), Halima Mdee ( Chadema) na Dr Kigwangalla ( CCM)

Tupo katikati ya safari Tulikotoka ni mbali na tunakoenda hatukujui

Mungu wa mbinguni Uturehemu Sisi!
 
JKT ya sasa hivi hamna kitu, JKT ilikuwa miaka yetu bana, Uzalendo wa kweli, ujasiri wa kuhoji lolote unaloona halina maslahi kitaifa. Mwaka mzima dadadeq sasa itakuwa hili la wiki 3.
Walioenda jkt ya miaka unayosema ndio hasa walioingia na bado wako kwenye position ya kuingia au ku-influence kuingia mikataba ya aina hiyo! Lostitamu mwenyewe kapiga jkt mwaka mzima. KATIBA!
 
JKT ya sasa hivi hamna kitu, JKT ilikuwa miaka yetu bana, Uzalendo wa kweli, ujasiri wa kuhoji lolote unaloona halina maslahi kitaifa. Mwaka mzima dadadeq sasa itakuwa hili la wiki 3.
Nakumbuka cheche za James Mbatia pale Mlimani akitokea JKT kwa mujibu wa sheria
 
Zamani kipimo cha Uzalendo ilikuwa ni Pamoja na kushiriki Mafunzo ya JKT miezi 9 au Mgambo miezi 3

Kadhalika ili kuwa mwanachama wa CCM ililazimu kuingia darasani kwa miezi 3

Panahitajika Wasomi Wazalendo katika Hili swala la kutoa Elimu ya Mkataba wa Bandari na DP World

Ndio nikawakumbuka Wanasiasa Watatu walioenda Jeshini JKT wakiwa Watu wazima Ili kunoa Uzalendo wao hawa si wengine bali Zitto Kabwe ( ACT Wazalendo), Halima Mdee ( Chadema) na Dr Kigwangalla ( CCM)

Tupo katikati ya safari Tulikotoka ni mbali na tunakoenda hatukujui

Mungu wa mbinguni Uturehemu Sisi!
Unafeli sana.Hivi,kwenda mafunzo hayo ndiyo kipimo chako cha uzalendo wakati waendaji huenda tu kutimiza wajibu? Uzalendo huwa upo kwa mtu bila kujali amekuaje!
 
Kwenda JKT ni kitu kimoja na uzalendo ni kingine.
JKT ya zamani ilifundisha na kuthibitisha umoja, undugu, mshikamano na usawa miongoni mwa vijana wa Tanzania kivitendo.
Huo ndiyo uliokuwa msingi wa uzalendo.
Kila kijana aliyehitimu kidato Cha sita au vyuo vya kati alihudhuria, akapata mafunzo bila ubaguzi wa kitabaka.
Mtoto wa waziri alihudhuria kama wa mkulima wa jembe la mkono.
Hii JKT ya kuigiza, yawezekana hata mgambo ana ukakamavu na uzalendo zaidi.
Ulegevu wa fikra umesababisha ubabaishaji kila kona.
Tunahitaji kujipanga upya, kujenga uzalendo kwa kuwapika vijana kivitendo na sito maneno matupu.
 
Zamani kipimo cha Uzalendo ilikuwa ni Pamoja na kushiriki Mafunzo ya JKT miezi 9 au Mgambo miezi 3

Kadhalika ili kuwa mwanachama wa CCM ililazimu kuingia darasani kwa miezi 3

Panahitajika Wasomi Wazalendo katika Hili swala la kutoa Elimu ya Mkataba wa Bandari na DP World

Ndio nikawakumbuka Wanasiasa Watatu walioenda Jeshini JKT wakiwa Watu wazima Ili kunoa Uzalendo wao hawa si wengine bali Zitto Kabwe ( ACT Wazalendo), Halima Mdee ( Chadema) na Dr Kigwangalla ( CCM)

Tupo katikati ya safari Tulikotoka ni mbali na tunakoenda hatukujui

Mungu wa mbinguni Uturehemu Sisi!
Ni ujinga wa hali ya juu kufikiri au kuamini kuwa mtu akipita jkt ni anahitimu kuwa mzalendo. Au mtu asipopitia jkt hawezi kuwa mzalendo.
 
Kwenda JKT ni kitu kimoja na uzalendo ni kingine.
JKT ya zamani ilifundisha na kuthibitisha umoja, undugu, mshikamano na usawa miongoni mwa vijana wa Tanzania kivitendo.
Huo ndiyo uliokuwa msingi wa uzalendo.
Kila kijana aliyehitimu kidato Cha sita au vyuo vya kati alihudhuria, akapata mafunzo bila ubaguzi wa kitabaka.
Mtoto wa waziri alihudhuria kama wa mkulima wa jembe la mkono.
Hii JKT ya kuigiza, yawezekana hata mgambo ana ukakamavu na uzalendo zaidi.
Ulegevu wa fikra umesababisha ubabaishaji kila kona.
Tunahitaji kujipanga upya, kujenga uzalendo kwa kuwapika vijana kivitendo na sito maneno matupu.
Nimekuelewa sana
 
Zamani kipimo cha Uzalendo ilikuwa ni Pamoja na kushiriki Mafunzo ya JKT miezi 9 au Mgambo miezi 3

Kadhalika ili kuwa mwanachama wa CCM ililazimu kuingia darasani kwa miezi 3

Panahitajika Wasomi Wazalendo katika Hili swala la kutoa Elimu ya Mkataba wa Bandari na DP World

Ndio nikawakumbuka Wanasiasa Watatu walioenda Jeshini JKT wakiwa Watu wazima Ili kunoa Uzalendo wao hawa si wengine bali Zitto Kabwe ( ACT Wazalendo), Halima Mdee ( Chadema) na Dr Kigwangalla ( CCM)

Tupo katikati ya safari Tulikotoka ni mbali na tunakoenda hatukujui

Mungu wa mbinguni Uturehemu Sisi!
Ndiyo akili matope ya CCM, JKT hainoi uzalendo wowote, ilikuwa ni falsafa ya Nyerere kudanganya watu kuwafanya makondoo. Nilikataa ukondoo huo pamoja na kukaa mwaka mzima JKT. Utakuwa mjinga gani unaona watu wanaiba wewe useme mimi ni mzalendo. Labda kama kwenda msituni kukomesha wizi wa CCM, kuonesha uzalendo wa kuitetea nchi toka wezi wa CCM, short of that nami nitaiba maan hata rais mwizi , why not me?
 
Back
Top Bottom