Azizi Mussa
JF-Expert Member
- May 9, 2012
- 9,172
- 7,427
Kulewa sifa ni kitu kibaya mno. Utamsikia mtu mzima na akili zake akifoka "Zitto asifike katika eneo letu/mkoa fulani akifika atakiona!" au utasikia mtu mzima na akili zake anafoka "Zitto akae kimya! period!"
Ndugu zangu niulize!
Ni nani mwenye hati miliki ya kumruhusu mtanzania mwenzake kufika au kutofika katika eneo fulani?nani!
Ni nani basi mwenye hati miliki ya kumruhusu mtu kuongea na wenzake na kumzuia pale anapotaka?nani!
Kati yetu ni nani asiyejiamini; kama tunajiamini, tunapiga mayowe ya nini?
Je; si tumemfanyia haki zitto na tunaendelea kumfanyia haki tunaogopa nini?
Si tumemshutumu zitto na kisha tukazunguka nchi nzima kueleza alivyo na matatizo na jinsi asivyofaa? kama tumesema ya kweli, tunaogopa nini na yeye anapoongea na wananchi wale wale ambao sisi tuliongea nao mahali pale pale na hakuna alietuzuia?Tunaogopa nini?
Sisi si tunadai kwamba hoja ndio msingi wa uongozi, kwa maana hiyo tuna nguvu za hoja!, sasa tunaogopa nini Zitto akitoa hoja zake hata tunataka tumzibe mdomo? Au katukana mtu?
Katiba ya Tanzania inamkataza nani kufika wapi ndani ya Jamuhuri ya Tanzania?Au tunafuata muongozo gani?
Kuna katiba au sheria yeyote inayomkataza yeyote kufia kokote ndani ya Nchi hii? au ni nini muongozo wetu sisi tunaowapiga marufuku baadhi ya watu kufika baadhi ya maeneo?Kwa ujinga huu huu kuna siku utasikia Rais asije kwetu! Alaaaah!
Sidhani kama kuna haja ya kujishuku kama tunaamini kwa 100% kwamba tumemtendea Zitto Haki na sisi ni watenda haki daima.Kwani Zitto anapiga watu ngumi au anatoa hoja? Si siku zote tunasema hoja hujibiwa kwa hoja! au tumebadili msimamo wetu?.Natutulie ! au kama tunataka na sisi tuzungumze yetu na twende tunakotaka ndani ya mipaka ya nchi.Huo ndio ustaarabu.