Zitto Kabwe Asifike katika eneo letu... Zitto asizungumze na watanzania, Period!

Status
Not open for further replies.
Miongoni mwa wananchi mizigo basi wewe nizigo. Katiba ya nchi inamruhusu kuzunguuka kokote ndani ya nchi na kuongea na wananchi wala usijitie ujinga na upumbavu wa kudhani una hati miliki kwa watanzania. Wewe kama una chuki siku ya mkutano ubaki kwako usiende.
Wazee wa gongo.
 
Hiyo nguvu inayotumika kufight against zzk ni mara ingepelekwa kujenga chama
 
mimi kwa upande wangu nadhani si vizuri zitto akakaa kimya,maana kila mikutano wanayohutubia wanataja sababu za kumvua uongozi zitto na ni vyema zitto pia akapita humo humo na kuzikubali ama kuzikataa sababu hizo hii itasaidia kusikia ya upande wa pili.

kwa mfano ukisoma hapa utaona kilichosemwa ktk moja ya mikutano

Lissu azungumzia maamuzi kuhusu Zitto...SOMA ZAIDI HAPA ~ PAPARAZI
paparazihuru.com
Lissu azungumzia maamuzi kuhusu Zitto...SOMA ZAIDI HAPA


Lissu azungumzia maamuzi kuhusu Zitto...SOMA ZAIDI HAPA ~ PAPARAZI


Sasa hii itasaidia kupata ukweli wa baadhi ya kauli za viongozi kama zinaukweli ama la,kwani muhusika mwenyewe zitto atakuwa akizijibu hoja zilizosemwa na wanaomtuhuma,na haitakuwa vizuri yasemwe na zitto akae kimya.

Hata mie nakubaliana na wewe. Unajua wao walidhani watammaliza kwa kupitia Jf na alivyo Gthinker hakuhangaika na akina Sa8 wanaojifanya maFBI wa jf. Sasa atapita kufutilia kabisa nyayo za boss wake ben
 
Nyie simulijiaminisha kuwa zitto kwisha habari yake sasa mbona mnahaha kumzuwia nawakati hana wafuasi? Nini wasiwasi wenu ni nini?
 
Watazania wengi wanasubiri maamuzi ya vikao halali vya chama juu ya hao wasaliti a k a mayuda iscariotes. Kwa sbb CDM ni chama makini, then uamuzi utakaotolewa utakuwa ni muafaka na uliozingatia taratibu na kanuni according to CDM constitution .
 
Siunajuwa Makamanda wameamua kuweka Akili mfukoni na kuwa Makasuku wanapenda kuongea yale yanayowapendezesha Slaa na Mbowe,we leo mtu kama Lisu ameingia katika ujinga huu!ukiongea tofauti na wanachotaka kusikia mbowe na Slaa....unaitwa Msaliti!Usaliti si upo katika Ndoa
#Mbowe na Slaa wanafanya Biashara Siasa:Zitto anafanya Siasa Jamii#
 
betlehem

Tokea Zitto avuliwe Nyadhifa zote ndani ya CHADEMA hadi leo umeshaanzisha thread ngapi juu ya Zitto na nini Mrejesho wa Thread zako ???

Huyu bethlehem ni TeamZitto kwa 100% na isitoshe ni teamCCM coz yuko huko sasa anajifanya yuko CDM. bethlehem ukiwa CDM unatakiwa uwe FIT ktk kila nyanja, watu hawaingiliki kijinga kama nyie watoto NJAA.
Dr Slaa aliambiwa na nyie asifike Kigoma sijui ni wapi uliweka bandiko lako, leo unakuja na uzushi eti jamaa yako Zitto asifike sehemu fulani??
Wapi?? Nani kasema?? Usituletee ujinga wako wa Sembe
 
Last edited by a moderator:
Hiyo nguvu inayotumika kufight against zzk ni mara ingepelekwa kujenga chama
Nyuvu ipi sasa wewe tope kutoka m.a.s.a.b.u.r.i.n.i chama kilikuwa na hiyo program ya kujenga chama na kukagua uhai wa chama maeneo yote hata kabla Zitto kuvuliwa madaraka hakiwezi kusitisha ziara kwa kumuogopa eti Zitto na propaganda zenu za kitoto.
 
Zitto, dr. Slaa, mbowe,jk, mlipuaji mwigulu na wengineo wana haki ya kufika kokote katika tanzania, nilishangaa sana wale waliokuwa wanamtisha dr. Slaa kuwa asiende kigoma huu ni ulevi wa fikra, zitto vilevile ana haki ya kwenda popote, lakini yeye kama mwanachama mtiifu anapaswa kuheshimu chama na viongozi wake, tatizo na unafiki unaanzia pale anapopokelewa na mabango yanayokidhalilisha chama chake na viongozi huku yakimtukuza yeye binafsi huku akiangalia tu, huu ni unafiki.
 
Kulewa sifa ni kitu kibaya mno. Utamsikia mtu mzima na akili zake akifoka "Zitto asifike katika eneo letu/mkoa fulani akifika atakiona!" au utasikia mtu mzima na akili zake anafoka "Zitto akae kimya! period!"

Ndugu zangu niulize!

Ni nani mwenye hati miliki ya kumruhusu mtanzania mwenzake kufika au kutofika katika eneo fulani?nani!

Ni nani basi mwenye hati miliki ya kumruhusu mtu kuongea na wenzake na kumzuia pale anapotaka?nani!

Kati yetu ni nani asiyejiamini; kama tunajiamini, tunapiga mayowe ya nini?

Je; si tumemfanyia haki zitto na tunaendelea kumfanyia haki tunaogopa nini?

Si tumemshutumu zitto na kisha tukazunguka nchi nzima kueleza alivyo na matatizo na jinsi asivyofaa? kama tumesema ya kweli, tunaogopa nini na yeye anapoongea na wananchi wale wale ambao sisi tuliongea nao mahali pale pale na hakuna alietuzuia?Tunaogopa nini?

Sisi si tunadai kwamba hoja ndio msingi wa uongozi, kwa maana hiyo tuna nguvu za hoja!, sasa tunaogopa nini Zitto akitoa hoja zake hata tunataka tumzibe mdomo? Au katukana mtu?

Katiba ya Tanzania inamkataza nani kufika wapi ndani ya Jamuhuri ya Tanzania?Au tunafuata muongozo gani?

Kuna katiba au sheria yeyote inayomkataza yeyote kufia kokote ndani ya Nchi hii? au ni nini muongozo wetu sisi tunaowapiga marufuku baadhi ya watu kufika baadhi ya maeneo?Kwa ujinga huu huu kuna siku utasikia Rais asije kwetu! Alaaaah!

Sidhani kama kuna haja ya kujishuku kama tunaamini kwa 100% kwamba tumemtendea Zitto Haki na sisi ni watenda haki daima.Kwani Zitto anapiga watu ngumi au anatoa hoja? Si siku zote tunasema hoja hujibiwa kwa hoja! au tumebadili msimamo wetu?.Natutulie ! au kama tunataka na sisi tuzungumze yetu na twende tunakotaka ndani ya mipaka ya nchi.Huo ndio ustaarabu.

Dr Slaa pia alipigwa marufuku kwenda mwanza na kigoma sikuona ukimtetea mkuu sana bethlehem
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom