zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 19,039
- 28,690
Leo ndio nimegundua nchi yetu ina watu wa ajabu kabisa. Kma lissu ndio hafai vp vyama vingine vyenye wagombea wastaarabu kma Membe ana madiwani wangapi? Lipumba je? Mbatia sio moderate ilikuaje kaanguka?Ukirejea majadiliano yetu ya awali utabaini kuwa unajitahidi kujiondoa mwenyewe kwenye mjadala. Mfano wa Trump nimeutoa kujibu mifano yako ya nchi za nje, unayopenda kutumia badala ya uhalisia wa nchini kwetu, kwa sababu uchaguzi uliomalizika siyo wa kwanza hapa.
Takwimu nilizokuwa nimemtoa hazihusiani kabisa na hicho unachotaka wanaJF wakuelewe, ambacho hutumika kwenye tafiti za kisayansi.
Kwamba, siasa za uchaguzi, kiuhalisia ni kama maji yayotiririka ambayo ufuata mkondo wowote yakielekezwa lakini yakilazimishwa yatafurika na kuleta athari. Na ndicho kilichotokea Uchaguzi Mkuu huu uliomalizika. Lissu, mgombea Urais kupitia CHADEMA, alitaka kulazimisha wapiga kura kuamini upuuzi wake, nao wamemjibu. Nawe umekiri udhaifu wake.
Ni kweli most voters expected an incumbent to win by a narrow margin possibly 60:40 ratio or rather 70:30!! But 85:15? No one saw it coming to be honest. Kwa hii hoja napenda kurudia na kusisitiza kuwa viongozi wa CHADEMA walifanya makosa makubwa kumsimamisha Lissu kama mgombea wao wa Urais wakati wanajua:
√ ni mtu jeuri, mwenye majivuno, haambiliki na mbinafsi wa kutupwa;
√ hana na hatakuwa na nguvu ya kisiasa ya Lowassa iliyokipa CHADEMA wabunge na madiwani wengi kiasi cha kuongoza Halmashauri ya miji mikubwa na kuwa chama kikuu cha upinzani; na
√ alizunguka dunia kuinanga nchi yake itengwe na Jumuiya ya Kimataifa. Kila mpiga kura alilijua hilo.
Itoshe kihitimisha kuwa vyama vya upinzani vijifunze kwa makosa yao wenyewe yaliyotendeka katika Uchaguzi Mkuu uliomalizika km kutokushirikiana na badala yake kuanza kuumbuana hadharani.
Maalim naye kaanguka kwa sababu ni mgombea mbaya au ni Lissu pekee ndio mbaya?
Kma wapinzani wote wameangushwa ina maana kuna common problem na sio specific to Lissu only? Yaani CHADEMA ikianguka ni sababu ya Lissu ila vyama vingine una maoni gani? Mbadala wa CHADEMA ni upi kwa upinzani ili wajifunzie huko kwa wagombea waliowekwa?
Kuhusu Lissu kuwa na ushawishi kma Lowassa ni subjective zaidi. Maadam kampeni za Lissu zilikua energetic kuliko wapinzani wengine wote naweza conclude alikua na ushawishi mkubwa sana. Sadly uchaguzi umeamuliwa na Tume na sio wapiga kura, ssa kma huwezi liona hilo basi tusemw tuna raia wapumbavu kuliko wote duniani.