Zitto Kabwe ananikwaza sana, simuelewi anafanya siasa zake kwa maslahi ya nani?

J

JINOME

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2017
Messages
889
Likes
1,301
Points
180
J

JINOME

JF-Expert Member
Joined May 29, 2017
889 1,301 180
Oktoba 29, 2017
Naitwa Luhimbila Makalyusi Mtule, Nipo masomoni Finland.
Naomba niwe mkweli Zitto Kabwe ananikwaza sana, simuelewi anafanya siasa zake kwa maslahi ya nani?

Nilimuelewa awali kuwa kijana aliyejitolea kupigania maslahi ya nchi yetu lakini hapa katikati akaanza kunichanganya na sasa naanza kuamini waliyoyasema kwenye chama chake cha zamani CHADEMA kuwa ni mtu anayetumika kwa maslahi yake.

Mimi na Watanzania wengi tuliopo Ulaya, Marekani na hata China ambako mwezi Juni mwaka huu nilikwenda tunatembea kifua mbele kwa sababu kila unaposema unatoka Tanzania basi moja kwa moja mjadala unaegemea kumsifu Rais Magufuli kwa kazi kubwa, ya uzalendo na kukataa utumwa wa mataifa makubwa anayoifanya.

Sielewi kwa nini Zitto Kabwe kajipa kazi ya kumchafua Rais Magufuli na kuichafua TANZANIA, nikifuatilia akaunti yake ya twitter, facebook na mikutano anayofanya na waandishi wa habari naona sasa hivi kajipa kazi ya kuitangazia dunia kuwa Tanzania ina Rais wa hovyo, uchumi wa nchi umekufa, Serikali inaendeshwa kisanii na zaidi anatoa kauli za kumdhalilisha Rais ambayo ni nembo ya Taifa kwa sasa.

Rais ndiye Baba wa Tanzania kwa sasa, na hakujiweka kwenye nafasi hiyo aliwekwa na Watanzania wenye akili timamu kupitia sanduku la kura, kwa kweli inauma sana, sasa hata huku ughaibuni watu wanashindwa kuelewa.

Hili jambo halikubaliki, kama Zitto anajiona yeye ni bora asiichafue nchi, asimchafue Rais kwa kiasi hicho, Na kwa sababu wakati Zitto anawika kwa siasa zilizowashawishi vijana wengi mimi pia alinishawishi nilifanikiwa kujua mambo yake mengi.

Haikuwa nia yangu na wala sio tabia yangu, lakini kama atasoma ujumbe huu ama wapambe wake watausoma naomba wamwambie sitakuwa tayari kumuacha aendelee kumdhalilisha Rais, sitakubali aendelee kuichafua Tanzania, nitaanza kufichua na mambo yake ya hovyo anayowafanyia sanaa Watanzania.

Na kwa sababu anaona kudhalilisha wenzie kunoga sasa na yeye atakapoguswa avumilia asilie kama alivyofanya bunge. Waswahili wana msemo "usianzishe ugomvi wa mawe wakati unaishi kwenye nyumba ya vioo"

Tutafichua usanii uliofanya kwenye kifo cha Mama yako mzazi, tutafichue usanii wako na maslahi yako binafsi kwa hili la kujifanya wewe ndio ulikuwa rafiki mkubwa wa Deo Filikunjombe, tutafichua usanii wako na Wajerumani na ajenda mliyonayo, tutafichua usanii wake na Dkt. Ramadhan Dau aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,

Tutafichua mapesa yote uliyopiga ukiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge (PAC) na tutafichua mbinu unazozifanya ndani ya UKAWA ili ujiimarishe na chama chako cha ACT Wazalendo.

Kwanza namshukuru sana Rais kwa kuwaondoa Prof. Kitila Mkumbo na Mama Anna Mngwilla kwenye ACT Wazalendo, hawa watu wana heshima kubwa na haikuwa sawa hata kidogo kuendelea kuongozwa na Msanii Zitto Kabwe, nawapongeza Advocate Msando, Samson Mwigamba na wote waliofanya uamuzi wa kuondoka ACT Wazalendo.

Mmefanya jambo jema kujiepusha na aibu ya kuwa na mtu huyu. Huyu panapomfaa ni UKAWA akaungane na Wasanii wenzake akina Mbowe, Lema, Nassari, Kubenea, Mch Msigwa, Mdee, Bulaya na mgonjwa ambaye simtaji hapa ambao wamejipa kazi ya kufanya siasa za uchochezi, uanaharakati, fitina na uchonganishi badala ya kufanya siasa za upinzani zenye lengo la kuisimamia Serikali iwaletee wananchi maendeleo na kuondoa Dosari.

Hivi kwa anayoyafanya leo Rais Magufuli mtu mwenye akili na nia njema na nchi huwezi kuwa unafanya kampeni za kumdhohofisha, unataka kudhohofisha vita dhidi ya rushwa, unataka kudhohofisha mapambano ya kuwaondoa wanyonyaji wa uchumi, unadhohofisha mipango ya maendeleo.

Yaani Zitto na genge lake wangefurahi sana kuona wazungu wa makinikia wameshinda, wanaombea sana uchumi wa Tanzania uporomoke, wanaombea sana wadau wa maendeleo wajiondoe kuungana na Tanzania, wanatamani sana wawekezaji wasije kuwekeza Tanzania, wanatamani sana kuona miradi inakwamba, wanatamani sana wezi wa mali za umma waendelee kutamba mitaani.

Sasa naanza kumuelewa Magufuli kwa nini alipiga marufuku mikutano ya siasa na kuelekeza kila mmoja afanye mkutano kwake, maana leo nchi ingekuwa inashinda kwenye maandamano badala ya kazi, Lakini nataka kuuliza hawa wapuuzi wanafanya ujinga huu vijana wa CCM mpo wapi? Wabunge wa CCM mpo wapi? Vijana wazalendo wa Tanzania mnawaachaje hawa wanafanya upuuzi huu?

Hivi vyombo vya dola pamoja na Rais kusema chukueni hatua za kisheria kwa wanapotosha ukweli kwa nini mnamuacha Zitto Kabwe anatamba namna hii? Yeye nani?
Mbona Msemaji wa Serikali Dk. Abbas anafungia magazeti yanayochapisha uongo, nyie mna kigugumizi cha nini? Mtu anatoa takwimu za uongo mnaishia kufafanua tu? Nooo.
Afanye hivyo nchi kama China aone cha moto. Kwenye mapambano hakuna kuangaliana usoni jamani.
Ujumbe wangu ndio huo.

Salamu zangu kwenu ndugu zangu watanzania kutoka Finland
 
Lambardi

Lambardi

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2008
Messages
10,406
Likes
5,796
Points
280
Lambardi

Lambardi

JF-Expert Member
Joined Feb 7, 2008
10,406 5,796 280
Mkuu jibu kwa takwimu zile hoja....umejibu porojo tupu!! Yeye alitoa takwimu...tafadhali kwa usomi wako hadi Ufini tujibu tukuelewe wewe na wenzako unaowakilisha nje huko...ila kwa porojo hizo hata hutakiwi kujibiwa!!! Utadhihirisha usomi wako ni wa kukariri makaratasi si wa kutukomboa jamii nzima ya watanzania...!!! Tunasubiri mkuu
 
mjumbe wa bwana

mjumbe wa bwana

JF-Expert Member
Joined
Sep 19, 2016
Messages
3,516
Likes
2,922
Points
280
mjumbe wa bwana

mjumbe wa bwana

JF-Expert Member
Joined Sep 19, 2016
3,516 2,922 280
ulikunywa balimi nini jana maana naona Unaandika kimipasho pingana kwa takwimu sio mipasho
by Roma mkatoliki weka risasi chini tubishane kwa hoja maana lengo letu ni kuijenga Tanzania
 
bigmind

bigmind

JF-Expert Member
Joined
Oct 28, 2015
Messages
9,498
Likes
8,889
Points
280
bigmind

bigmind

JF-Expert Member
Joined Oct 28, 2015
9,498 8,889 280
Shida hao ssm unaowaita wenzio zitto ni mzito kuwazidi mbali mno..! Pamoja na unafiki wake ssm small brain wanachoweza ni propaganda tu, mambo ya kisomi wako shallow labda watumie SMG.
 
kipara kipya

kipara kipya

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2016
Messages
5,387
Likes
5,383
Points
280
kipara kipya

kipara kipya

JF-Expert Member
Joined May 2, 2016
5,387 5,383 280
zitto ni mnafiki wa kutupwa!
 
Kimbunga

Kimbunga

Platinum Member
Joined
Oct 4, 2007
Messages
13,389
Likes
2,290
Points
280
Kimbunga

Kimbunga

Platinum Member
Joined Oct 4, 2007
13,389 2,290 280
Kumbe mbwembwe zooooote zile wakati akiwa Mwenyekiti PAC ilikuwa ni upigaji? Tunasubiri umuweke hadharani Mkuu manake hakuna giza mbele ya jua.
 
Al Zagawi

Al Zagawi

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2009
Messages
1,848
Likes
396
Points
180
Al Zagawi

Al Zagawi

JF-Expert Member
Joined Mar 17, 2009
1,848 396 180
Oktoba 29, 2017
Naitwa Luhimbila Makalyusi Mtule, Nipo masomoni Finland.
Naomba niwe mkweli Zitto Kabwe ananikwaza sana, simuelewi anafanya siasa zake kwa maslahi ya nani?

Nilimuelewa awali kuwa kijana aliyejitolea kupigania maslahi ya nchi yetu lakini hapa katikati akaanza kunichanganya na sasa naanza kuamini waliyoyasema kwenye chama chake cha zamani CHADEMA kuwa ni mtu anayetumika kwa maslahi yake.

Mimi na Watanzania wengi tuliopo Ulaya, Marekani na hata China ambako mwezi Juni mwaka huu nilikwenda tunatembea kifua mbele kwa sababu kila unaposema unatoka Tanzania basi moja kwa moja mjadala unaegemea kumsifu Rais Magufuli kwa kazi kubwa, ya uzalendo na kukataa utumwa wa mataifa makubwa anayoifanya.

Sielewi kwa nini Zitto Kabwe kajipa kazi ya kumchafua Rais Magufuli na kuichafua TANZANIA, nikifuatilia akaunti yake ya twitter, facebook na mikutano anayofanya na waandishi wa habari naona sasa hivi kajipa kazi ya kuitangazia dunia kuwa Tanzania ina Rais wa hovyo, uchumi wa nchi umekufa, Serikali inaendeshwa kisanii na zaidi anatoa kauli za kumdhalilisha Rais ambayo ni nembo ya Taifa kwa sasa.

Rais ndiye Baba wa Tanzania kwa sasa, na hakujiweka kwenye nafasi hiyo aliwekwa na Watanzania wenye akili timamu kupitia sanduku la kura, kwa kweli inauma sana, sasa hata huku ughaibuni watu wanashindwa kuelewa.

Hili jambo halikubaliki, kama Zitto anajiona yeye ni bora asiichafue nchi, asimchafue Rais kwa kiasi hicho, Na kwa sababu wakati Zitto anawika kwa siasa zilizowashawishi vijana wengi mimi pia alinishawishi nilifanikiwa kujua mambo yake mengi.

Haikuwa nia yangu na wala sio tabia yangu, lakini kama atasoma ujumbe huu ama wapambe wake watausoma naomba wamwambie sitakuwa tayari kumuacha aendelee kumdhalilisha Rais, sitakubali aendelee kuichafua Tanzania, nitaanza kufichua na mambo yake ya hovyo anayowafanyia sanaa Watanzania.

Na kwa sababu anaona kudhalilisha wenzie kunoga sasa na yeye atakapoguswa avumilia asilie kama alivyofanya bunge. Waswahili wana msemo "usianzishe ugomvi wa mawe wakati unaishi kwenye nyumba ya vioo"

Tutafichua usanii uliofanya kwenye kifo cha Mama yako mzazi, tutafichue usanii wako na maslahi yako binafsi kwa hili la kujifanya wewe ndio ulikuwa rafiki mkubwa wa Deo Filikunjombe, tutafichua usanii wako na Wajerumani na ajenda mliyonayo, tutafichua usanii wake na Dkt. Ramadhan Dau aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,

Tutafichua mapesa yote uliyopiga ukiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge (PAC) na tutafichua mbinu unazozifanya ndani ya UKAWA ili ujiimarishe na chama chako cha ACT Wazalendo.

Kwanza namshukuru sana Rais kwa kuwaondoa Prof. Kitila Mkumbo na Mama Anna Mngwilla kwenye ACT Wazalendo, hawa watu wana heshima kubwa na haikuwa sawa hata kidogo kuendelea kuongozwa na Msanii Zitto Kabwe, nawapongeza Advocate Msando, Samson Mwigamba na wote waliofanya uamuzi wa kuondoka ACT Wazalendo.

Mmefanya jambo jema kujiepusha na aibu ya kuwa na mtu huyu. Huyu panapomfaa ni UKAWA akaungane na Wasanii wenzake akina Mbowe, Lema, Nassari, Kubenea, Mch Msigwa, Mdee, Bulaya na mgonjwa ambaye simtaji hapa ambao wamejipa kazi ya kufanya siasa za uchochezi, uanaharakati, fitina na uchonganishi badala ya kufanya siasa za upinzani zenye lengo la kuisimamia Serikali iwaletee wananchi maendeleo na kuondoa Dosari.

Hivi kwa anayoyafanya leo Rais Magufuli mtu mwenye akili na nia njema na nchi huwezi kuwa unafanya kampeni za kumdhohofisha, unataka kudhohofisha vita dhidi ya rushwa, unataka kudhohofisha mapambano ya kuwaondoa wanyonyaji wa uchumi, unadhohofisha mipango ya maendeleo.

Yaani Zitto na genge lake wangefurahi sana kuona wazungu wa makinikia wameshinda, wanaombea sana uchumi wa Tanzania uporomoke, wanaombea sana wadau wa maendeleo wajiondoe kuungana na Tanzania, wanatamani sana wawekezaji wasije kuwekeza Tanzania, wanatamani sana kuona miradi inakwamba, wanatamani sana wezi wa mali za umma waendelee kutamba mitaani.

Sasa naanza kumuelewa Magufuli kwa nini alipiga marufuku mikutano ya siasa na kuelekeza kila mmoja afanye mkutano kwake, maana leo nchi ingekuwa inashinda kwenye maandamano badala ya kazi, Lakini nataka kuuliza hawa wapuuzi wanafanya ujinga huu vijana wa CCM mpo wapi? Wabunge wa CCM mpo wapi? Vijana wazalendo wa Tanzania mnawaachaje hawa wanafanya upuuzi huu?

Hivi vyombo vya dola pamoja na Rais kusema chukueni hatua za kisheria kwa wanapotosha ukweli kwa nini mnamuacha Zitto Kabwe anatamba namna hii? Yeye nani?
Mbona Msemaji wa Serikali Dk. Abbas anafungia magazeti yanayochapisha uongo, nyie mna kigugumizi cha nini? Mtu anatoa takwimu za uongo mnaishia kufafanua tu? Nooo.
Afanye hivyo nchi kama China aone cha moto. Kwenye mapambano hakuna kuangaliana usoni jamani.
Ujumbe wangu ndio huo.

Salamu zangu kwenu ndugu zangu watanzania kutoka Finland
Waliokupa hiyo scholarship wamepoteza resources....huonyeshi ukomavu wa fikra wala usomi wa kiwango cha huko first world uliko....

Hoja hujibiwa kwa hoja, kama hoja za Zitto zinawachafua basi leteni hoja za kujisafisha....otherwise ni porojo na vitisho tu....
 
Masanja

Masanja

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2007
Messages
3,928
Likes
4,794
Points
280
Masanja

Masanja

JF-Expert Member
Joined Aug 1, 2007
3,928 4,794 280
Kama hawa ndo wasomi tulio nao Tanzania. Twafaaaaa! Yaani jamaa kichwani ni vumbi tupu!!!.

Nilisoma hili bandiko nikiwa na shuku ya kuona counter facts! Nilitegemea huyu bwana aje na takwimu mbadala kuonyesha uongo wa Zitto ni upi! Lakini kumbe ni wale wale wanaotafuta U-DC na U-DAS! Poor Tanzanian in Finland. Porojo tuu mwanzo mwisho....

Kijana tunategemea mawazo yanayoonyesha usomi wako. Lakini ulivyoandika huna tofauti na Jerry Muro na H. Polepole. Sasa faida yako kwenda Ulaya ni ipi? Si mara kumi ungebaki Tanzania hiyo nafasi akapewa mwingine?
 
K

kindikwili

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2016
Messages
1,698
Likes
2,477
Points
280
K

kindikwili

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2016
1,698 2,477 280
Jamaa anasema na "yule mgonjwa" mkuu una kibuti cha uzima, kiburi kinachokusahaulisha kwamba uzima wako kuna mtu kaushikilia na akiamua kuichukua huna cha kusema. Yaani unataka kusema "mgonjwa" ni jina la mtu au ni sifa ya? By the way kuna watu wanamjua zzk kuliko wewe, wana vyombo vya kiuchunguzi na vyombo vya dola pamoja na vyanzo muhimu vya kupata taarifa ,sasa kama hao wameshindwa kumshughulikia zzk wewe mwanafunzi utaweza? Kazi njema mkuu tunasubiri unavyomuumbua zzk
 
balimar

balimar

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2015
Messages
3,449
Likes
4,297
Points
280
balimar

balimar

JF-Expert Member
Joined Sep 18, 2015
3,449 4,297 280
Ndg.ungeleta na ka-altenative analysis kako na sisi tungeanzia hapo

Yaani wewe ni sawa MTU anaeulizwa wewe jina lako Nani? Wewe unajibu Mimi ni mchaga wa kibololoni.

To make story short malizia, malizia hayo masomo yako ya diploma in file managment and arrangment in local offices along the coast and besides the shores. Ndio uje sasa na hizo sentensi zako
 
amadeusity

amadeusity

JF-Expert Member
Joined
May 30, 2016
Messages
561
Likes
287
Points
80
amadeusity

amadeusity

JF-Expert Member
Joined May 30, 2016
561 287 80
nyie mnaojiita wasomi nje ya nchi mnaidhalilisha Tz. no evidence no right to speak..!!
Umeandika maneno mengi lakin unapata shida sana kuupata uhalisia wa kile unachokisema
 
Forum statistics

Threads 1,235,132
Members 474,353
Posts 29,212,887