Zitto Kabwe ananikwaza sana, simuelewi anafanya siasa zake kwa maslahi ya nani?

Wewe unastahili ukirudi ukamatwe uwekwe ndani. Haiwezekani ukawa unajua maovu mengi ya Zitto halafu ukakaa kimya bila kutoa taarifa kwa vyombo vya dola, you are a complicity of the wrong doings of Zitto if what you are saying here is true and not fabricated. Mtu anayeficha muovu ni muovu pia. Kama una evidence zitoe usisubiri hadi Zitto amkashfu mh. Rais ndio uanze kutishia huo sio uzalendo ni unafiki mkubwa kwa msomi kama wewe.
 
Oktoba 29, 2017
Naitwa Luhimbila Makalyusi Mtule, Nipo masomoni Finland.
Naomba niwe mkweli Zitto Kabwe ananikwaza sana, simuelewi anafanya siasa zake kwa maslahi ya nani?

Nilimuelewa awali kuwa kijana aliyejitolea kupigania maslahi ya nchi yetu lakini hapa katikati akaanza kunichanganya na sasa naanza kuamini waliyoyasema kwenye chama chake cha zamani CHADEMA kuwa ni mtu anayetumika kwa maslahi yake.

Mimi na Watanzania wengi tuliopo Ulaya, Marekani na hata China ambako mwezi Juni mwaka huu nilikwenda tunatembea kifua mbele kwa sababu kila unaposema unatoka Tanzania basi moja kwa moja mjadala unaegemea kumsifu Rais Magufuli kwa kazi kubwa, ya uzalendo na kukataa utumwa wa mataifa makubwa anayoifanya.

Sielewi kwa nini Zitto Kabwe kajipa kazi ya kumchafua Rais Magufuli na kuichafua TANZANIA, nikifuatilia akaunti yake ya twitter, facebook na mikutano anayofanya na waandishi wa habari naona sasa hivi kajipa kazi ya kuitangazia dunia kuwa Tanzania ina Rais wa hovyo, uchumi wa nchi umekufa, Serikali inaendeshwa kisanii na zaidi anatoa kauli za kumdhalilisha Rais ambayo ni nembo ya Taifa kwa sasa.

Rais ndiye Baba wa Tanzania kwa sasa, na hakujiweka kwenye nafasi hiyo aliwekwa na Watanzania wenye akili timamu kupitia sanduku la kura, kwa kweli inauma sana, sasa hata huku ughaibuni watu wanashindwa kuelewa.

Hili jambo halikubaliki, kama Zitto anajiona yeye ni bora asiichafue nchi, asimchafue Rais kwa kiasi hicho, Na kwa sababu wakati Zitto anawika kwa siasa zilizowashawishi vijana wengi mimi pia alinishawishi nilifanikiwa kujua mambo yake mengi.

Haikuwa nia yangu na wala sio tabia yangu, lakini kama atasoma ujumbe huu ama wapambe wake watausoma naomba wamwambie sitakuwa tayari kumuacha aendelee kumdhalilisha Rais, sitakubali aendelee kuichafua Tanzania, nitaanza kufichua na mambo yake ya hovyo anayowafanyia sanaa Watanzania.

Na kwa sababu anaona kudhalilisha wenzie kunoga sasa na yeye atakapoguswa avumilia asilie kama alivyofanya bunge. Waswahili wana msemo "usianzishe ugomvi wa mawe wakati unaishi kwenye nyumba ya vioo"

Tutafichua usanii uliofanya kwenye kifo cha Mama yako mzazi, tutafichue usanii wako na maslahi yako binafsi kwa hili la kujifanya wewe ndio ulikuwa rafiki mkubwa wa Deo Filikunjombe, tutafichua usanii wako na Wajerumani na ajenda mliyonayo, tutafichua usanii wake na Dkt. Ramadhan Dau aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa NSSF,

Tutafichua mapesa yote uliyopiga ukiwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge (PAC) na tutafichua mbinu unazozifanya ndani ya UKAWA ili ujiimarishe na chama chako cha ACT Wazalendo.

Kwanza namshukuru sana Rais kwa kuwaondoa Prof. Kitila Mkumbo na Mama Anna Mngwilla kwenye ACT Wazalendo, hawa watu wana heshima kubwa na haikuwa sawa hata kidogo kuendelea kuongozwa na Msanii Zitto Kabwe, nawapongeza Advocate Msando, Samson Mwigamba na wote waliofanya uamuzi wa kuondoka ACT Wazalendo.

Mmefanya jambo jema kujiepusha na aibu ya kuwa na mtu huyu. Huyu panapomfaa ni UKAWA akaungane na Wasanii wenzake akina Mbowe, Lema, Nassari, Kubenea, Mch Msigwa, Mdee, Bulaya na mgonjwa ambaye simtaji hapa ambao wamejipa kazi ya kufanya siasa za uchochezi, uanaharakati, fitina na uchonganishi badala ya kufanya siasa za upinzani zenye lengo la kuisimamia Serikali iwaletee wananchi maendeleo na kuondoa Dosari.

Hivi kwa anayoyafanya leo Rais Magufuli mtu mwenye akili na nia njema na nchi huwezi kuwa unafanya kampeni za kumdhohofisha, unataka kudhohofisha vita dhidi ya rushwa, unataka kudhohofisha mapambano ya kuwaondoa wanyonyaji wa uchumi, unadhohofisha mipango ya maendeleo.

Yaani Zitto na genge lake wangefurahi sana kuona wazungu wa makinikia wameshinda, wanaombea sana uchumi wa Tanzania uporomoke, wanaombea sana wadau wa maendeleo wajiondoe kuungana na Tanzania, wanatamani sana wawekezaji wasije kuwekeza Tanzania, wanatamani sana kuona miradi inakwamba, wanatamani sana wezi wa mali za umma waendelee kutamba mitaani.

Sasa naanza kumuelewa Magufuli kwa nini alipiga marufuku mikutano ya siasa na kuelekeza kila mmoja afanye mkutano kwake, maana leo nchi ingekuwa inashinda kwenye maandamano badala ya kazi, Lakini nataka kuuliza hawa wapuuzi wanafanya ujinga huu vijana wa CCM mpo wapi? Wabunge wa CCM mpo wapi? Vijana wazalendo wa Tanzania mnawaachaje hawa wanafanya upuuzi huu?

Hivi vyombo vya dola pamoja na Rais kusema chukueni hatua za kisheria kwa wanapotosha ukweli kwa nini mnamuacha Zitto Kabwe anatamba namna hii? Yeye nani?
Mbona Msemaji wa Serikali Dk. Abbas anafungia magazeti yanayochapisha uongo, nyie mna kigugumizi cha nini? Mtu anatoa takwimu za uongo mnaishia kufafanua tu? Nooo.
Afanye hivyo nchi kama China aone cha moto. Kwenye mapambano hakuna kuangaliana usoni jamani.
Ujumbe wangu ndio huo.

Salamu zangu kwenu ndugu zangu watanzania kutoka Finland

Ugemjibu kwa HOJA na vielelezo kupinga maneno yake,lakini naona umekuja zaidi na vihoja vya kusifu na kuabudu.Pole kwanza endelea kukaa ugenini U-enjoy maisha ya kuwa huru na kuwa mtumwa na maneno ya WATAWALA kwa sababu ya kuamini kila asemacho mfalme ni sahihi as if Mfalme ni Malaika
 
Uwa mnapenda positive tu.
Mkikutana na negative mnachukia.
Kwa kuwa uko masomoni mnasifiwa na wazungu kwa ajili ya magufuli.
Ndo Zito asiseme ukweli kuhusu hii nchi.
Kumbe wewe ni Mr misifa.
 
Oktoba 29, 2017...Naitwa Luhimbila Makalyusi Mtule, Nipo masomoni Finland.

Mimi na Watanzania wengi tuliopo Ulaya, Marekani na hata China ambako mwezi Juni mwaka huu nilikwenda tunatembea kifua mbele kwa sababu kila unaposema unatoka Tanzania basi moja kwa moja mjadala unaegemea kumsifu Rais Magufuli kwa kazi kubwa, ya uzalendo na kukataa utumwa wa mataifa makubwa anayoifanya.
JINOME naomba umwambie huyo Luhimbila Makalyusi Mtule aiondoe Marekani katika hiyo list yake...huko naambiwa vilaza ni wachache sana na si kama unavyofikiria.
 
msalimie Jerry muro mwambie kilio chake na njaaa yake tumeiona nafile lake linafanyiwa kazi,Tukutane magogoni anytime
 
Mi hua nasema kila Siku Tanzania kwa sasa hakuna vyama vya upinzani vyenye malengo mema na taifa hili. Tumebaki na genge la wahuni ambao hawajui nini wanataka. Wengine wanafika mahali wanajipinga hadi wao wenyewe. Kwahali hii wanatakiwa kukemewa na kila mtanzania.
 
Zitto km ni kiongozi mzuri atwaambie kaifanyie nini kigoma vijijin kwa miaka kumi aloongoza na anaifanyia nini kigoma mjini baada ya kuchukua almashaur ya mji...
 
hapa kazi tunayo wabongo, kama huyu ndo msomi anayejivunia kuwa finland mbona ajabu? kwel mtu mwenye level ya kuwa finland ndo unaandika uzi kama huu? ungetuwekea basi ata takwim zako ndo utuaminishe,
 
Yaani wewe msomi tena nje ya nchi ndio unaandika ngonjera utadhani hujawahi toka hata nje ya kijiji chenu. Ktk hizo nchi ulizotembea wapi hawaishauri serikali, wapi hawaruhusiwi kutoa maoni yao. Anachofanya Zitto sio kuiponda serikali, ila anaishauri namna bora ya kufikia maendeleo ya nchi. Sasa kila mtu akinyamaza kimya bila kushauri si hata serikali yenyewe itabweteka.
 
Mtoa post pambana na hali yako achana na mambo ya huku we soma kwanza ukimaliza njoo ujiunge na watu wasiojulikana ndio umuondoe zito kabwe kwasababu kwa povu lako unamaanisha unatamani umuondoe duniani na hizo ndio kauli kama za rais wako unayemtetea huna lolote
 
Kipindi akina Lissu wanaanza harakati katika sekta ya madini, kulitokea watu kama nyie waliokuwa wanapinga harakatu zile. Ona hivi sasa mpaka rais nae ameshikia bango yupi mbele kabisa wakati naue alikuwa ni miongonu mwa watu waliokuwa wanampinga.
Ndo kinachotokea sasa. Zitto anaonekana mtu wa ajabu na asiye mzalendo.. Ila kuna kipindi watu watakuwa fed up na siasa za upopurarity na wataona mambo jinsi yalivyo na hapo ndo Ushujaa wa Zitto utakapoonekana..!
 
Waliokupa hiyo scholarship wamepoteza resources....huonyeshi ukomavu wa fikra wala usomi wa kiwango cha huko first world uliko....

Hoja hujibiwa kwa hoja, kama hoja za Zitto zinawachafua basi leteni hoja za kujisafisha....otherwise ni porojo na vitisho tu....
Huo muda aliondika hizi pointless afadhali angeutumia kupublish paper ambayo itasaidia wengine kuelimika zaidi juu ya elimu yake
 
Mi nikajua kuna utofaut mkubwa kwa wasomi mnaosomea nje tena finland?...
..hv unasomea nn?
yaani zito azuiwe kuongea tena kitakwimu..ila ww unaleta mipasho ..unaongelea maisha binafsi kuhusu zito+mama yake...kuhusu PAC)Hata kama kapiga ela sawa...wale wa escrow unawajua!..wizi wa ccm miaka 50+ Unauonaje!?
 
Ni lini Tanzania unayoisema iliwahi kuwa safi?

Halafu kinachomchafua(?) Mkuu au nchi ni kauli na matendo ya Mkuu mwenyewe. Sio mimi wala wewe wala Zitto anayeweza kumchafua Mkuu au Nchi. Lakini kwa maneno na matendo yake nakwambia hata ukienda Samoa watasikia....kumbuka ubaya unaenda mbali na kwa haraka zaidi.

Mshaurini ajirekebishe tu, hivyo ndiyo dawa na tiba pekee sahihi.
 
Anaboa sana analazimisha kukaa kwenye chat wakati tumeshamshtukia ni MNAFKI fulani amazing na tumeshamchoka.
 
Back
Top Bottom