Zitto Kabwe afunguliwa kesi na Harbinder Singh kisa sakata la IPTL

Zitto Kabwe afunguliwa kesi na Harbinder Singh kisa sakata la IPTL

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
137,306
Reaction score
271,600
Kiongozi Mkuu mstaafu wa Chama cha ACT Wazalendo na Mbunge wa zamani Zitto Kabwe amefunguliwa Kesi na Harbinder Singh Seth akidaiwa kumkashifu mfanyabiashara huyo na kumvunjia heshima mbele ya jamii

Akizungumza na wanahabari leo Zitto Kabwe amesema kuwa kesi hiyo imetokana na yeye kuzungumzia sakata la IPTL (Kampuni ya kufua umeme) ambapo Seth ameomba kulipwa ‘mabilioni’ ya fedha

"Nimewaita hivi leo kwasababu ya kesi ambayo nimefunguliwa na mtu anayeitwa bwana Harbinder Singh Seth kuwa nimemkashifu na kumshushia heshima mbele ya jamii kwa vile eti nimezungumzia sakata la IPTL (Kampuni ya kufua umeme), na ameomba mahakama mbali na mambo mengine nimlipe ‘mabilioni’ ya fedha"

"Tuhuma hizo za bwana Seth kwanza si za kweli, kwasababu sijamkashifu na wala kumshushia heshima, lakini ninampongeza sana na kumshukuru kwa ujasiri wake wa kunishitaki kwasababu kesi hii itatoa fursa ya kumaliza jambo hili linaloweka wingu kwa muda mrefu sana katika taifa letu, lakini pia kesi hii itanipa nafasi ya kuweka ukweli wote wazi na mwisho kuufukia kabisa huu mzoga unaoitwa sakata la IPTL"

"Binafsi sikatai kuandika maneno ambayo bwana Seth (Harbinder Seth- Mmiliki wa kampuni ya IPTL ya ufuaji wa umeme) ananituhumu nayo kwamba nimemkashifu , maneno hayo niliyaandika na kuyachapisha katika akaunti yangu ya X zamani Twitter, na maneno yale yanaakisi picha halisi na yenye ukweli wa jambo zima hili la IPTL"

"Pili maneno haya mimi niliyaongea kwa nia njema kabisa, ya kutaka kupata ufumbuzi wa sakata hili, na tatu, maneno yale niliyasema kwavile mimi nilibahatika kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) iliyoshughulikia sakata la IPTL"

"Kama unakumbuka wakati ule maarufu lilivyojulikana kama sakata la Escrow, hivyo nilitumia fursa hiyo kuwaeleza Watanzania wenzangu ukweli wa jambo hili, kwasababu ninafahamu ukweli wa jambo hilo, na ni wajibu wangu kama raia kulinda rasilimali za taifa dhidi ya njama zozote zile za kupora rasilimali hizo kwa kisingizio cha uwekezaji".


 
Zitto atatumia nafasi hiyo kurudi ktk siasa za mjukwaani huku Seth kashaangalia upepo wa kushinda kesi ili arudi ktk dili za tenda. Nionavyo, kanjibai hana haja ya kulipwa pesa. Anachotaka ni kusafishwa awe msafi ili aweze kugombania tenda.
 
Amfungulie na Kafulila, aliyepigania hizo pesa mpaka akaitwa tumbili.
Huyo alikosa Mgao

Tofautisha kupigania na kuwalipua watu.

Kumbuka hizo pesa zilimfanya akakosa hadi ubunge na wakati alishinda.

Kilichotokea aliwalipua wenzake baada ya kukosa mgao
 
Bwana Zitto Kabwe amewaambia Waandishi wa Habari wa Tanzania kwamba Yule jamaa wa Escrow akaunti amemfungulia kesi Mahakamani.

Zaidi soma hapa

View attachment 3338039View attachment 3338040
Ni vema kaliweka jambo hili hadharani na ninafahamu wakati issue hii iko bungeni Zitto alikuwa miongoni wa wabunge waliochangia jambo hili.na kwa mantiki hii sasa Zitto ataliweka wazi ili hata sisi tuliokuwa tunalijua juuju tutapata ufahamu endapo kuna mtu alionewa au lilikuwa na ukweli.
 
Zitto atatumia nafasi hiyo kurudi ktk siasa za mjukwaani huku Seth kashaangalia upepo wa kushinda kesi ili arudi ktk dili za tenda. Nionavyo, kanjibai hana haja ya kulipwa pesa. Anachotaka ni kusafishwa awe msafi ili aweze kugombania tenda.
You definitely spoke my mind!

Wote lao moja! Ni marafiki hawa!
 
HARBINDER SINGH HATOBOI, niite mbwa

Harbinger Singh alipata hisa za Mechmar kupitia Piper Links na hatimaye PAP kwa udanganyifu uliopata baraka za Jaji Werema kama AG.

1. Wakati Piper Links ikipata hisa 70% za Mechmar katika IPTL mwaka 2010 Kampuni ya Mechmar ya Malaysia ilikuwa tayari mufilisi (Under receivership).

2. Baadhi ya wanahisa wa iliyokuwa Mechmar waliizunguka Serikali pamoja na Mahakama Kuu ya Malaysia mpaka wakauza hisa zao

3. Mechmar walimuuzia Piper Links (Harbinger Singh) ambayo ni kampuni ya kufikirika ambayo ilizitunza hisa hizo kwanza kwenye visiwa vya Virgin Island.

4. Wafilisi wa Mechmar wanasema Mkurugenzi mmoja wa iliyokuwa Mechmar Fatuk Baharudwn bin Abdul Najid alikiuka amri ya Mahakama ya tarehe 03/ 10/ 2010 kwa kuidanganya Mahakama kwa kuingia Mkataba wa
Umiliki Hisa (Share Purchase Agreement) ya USD 9.0 Million na Piper Link Investments Ltd mnamo 09/ 09/ 2010.

5. Wafilisi walifanikiwa kufungua kesi kwenye Mahakama ya BVK ya Malaysia na waliweza kushinda kesi ya kurudisha hati za hisa.

6. Swali, Je Piper Links waliwezaje kuuza hisa kwa PAP (Mali ya Harbinger Singh) wakati kulikuwa na amri ya tarehe 03/ 04/ 2011 inayowakataza Wakurugenzi wa Piper Links kufanya miamala yeyote ya hisa za Mechmar?.

7. Je ni nyaraka zipi ambazo PAP walizitumia kuwasilisha Wizara ya Nishati na Madini kuonyesha umiliki wao wa hisa 70% za IPTL?

8.Nyaraka zinaonyesha kuwa Piper Links walinunua hisa kutoka Mechmar kwa USD 9.0 Milion na kuziuza siku hiyo hiyo kwa PAP kwa USD 300,000 siku ya tarehe 05/ 12/ 2013 ambayo ni siku moja baada ya BOT kuziachia fedha za ESCROW kwa PAP.

Harbinder Singh ana kesi ya kughushi na kuiba kisha kutakatisha fedha. Jaji Fredrick Werema (Aliyekuwa AG) na Prof Sospeter Muhongo (Aliyekuwa Waziri wa Nishati) wao ndiyo waliothibitisha nyaraka za PAP na kumshawishi James Rugemalira wa VIPEM kuuza hisa zake 30% kwa PAP.
 
Sasa kuita waandishi wa habari, kujitetea na kesi ipo mahakamani!

Au anataka public sympathy?
Hayo angepaswa akayaseme, mahakamani, maana ameshashitakiwa na wenda tayari ana "summons" ya mahakama mkononi.
Amevunja sheria?

Kwa hiyo asiuhabarishe umma?
 
Kwenye mada za namna hii ndio utajua uwezo halisi wa akili za watu.

Kama umefatilia press ya Zitto na ukazisikia zile hoja zake kama ni kweli basi Taifa letu linahitaji neema ya MUNGU.

Mtu kabadili hadi wamiliki wa HISA wakati akiwa hana hayo mamlaka kisheria.Na bado alikubali kisheria kuwa atalipa pesa kama ikitokea WaTanzania tunadaiwa lakini hajalipa.

La ziada alikubali kulipa katika Pre bargain kwa DPP ila matokeo yake yeye ndio anadai.

Kiukweli inasikitisha sana hata kama watu wanaimbishwa nyimbo za uzalendo lakini kwa namna hii tunatengeneza Taifa la watu wengi kuwaza upigaji tu.
 
Back
Top Bottom