Zitto Kabwe afunguka kuhusu Dr. Bashiru kumtaka CCM

Zitto Kabwe afunguka kuhusu Dr. Bashiru kumtaka CCM

Zitto Kabwe afunguka kutimkia CCM

Zitto ametoa kauli hiyo baada ya kukaribishwa na Katibu Mkuu wa CCM kujiunga na chama hicho, ambapo alimpongeza kwa kuibua mijadala yenye maslahi ya kiuchumi.

"Mimi kujiunga CCM sio jawabu la shida za Watanzania na changamoto zinazoikabili nchi kama vile watu kukosa Uhuru wa mawazo, kukosoa, kupashana Habari na ukandamizwaji mkubwa wa vyama vya upinzani, Wananchi wanyonge kama Wakulima, Wavuvi, Wafugaji na uporaji wa Mali za watu wakiwemo Wafanyabiashara", amesema Zitto.

Zitto ameongeza kuwa, "Namwomba Bashiru CCM ni kundi la wasaka vyeo na walinda vyeo. Chama pekee cha Kijamaa nchini ni ACT Wazalendo kupitia Azimio la Tabora. Namtaka Mjamaa Bashiru Ally aachane na CCM iliyofilisika kiitikadi na ajiunge na ACT Wazalendo, Chama pekee cha Kijamaa Nchini na Afrika Mashariki".

Mapema leo akizungumza na wanachama wa CCM mkoani Iringa, Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Bashiru Ally ikiwa ni ziara yake ya kikazi mkoani humo amesema kuwa Zitto Kabwe anatakiwa kujiunga na chama hicho, kwani busara zake zinafaa kukitumikia chama hicho chenye Itikadi ya Kijamaa.

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe amefunguka kuwa kuhamia kwake CCM hakutomaliza changamoto za Watanzania.

SOURCE: Zitto Kabwe afunguka kutimkia CCM | East Africa Television
Bashiru Katumwa na Magufuli amekwa kisiki.
Hahahaaa
 
CCM isiwe kama timu ya mpira wa miguu ya Simba ambayo inataka kusajili kila mchezaji mzuri inayomwona na kupunguza upinzani kwa kurundika wachezaji wengi wenye vipaji lakini hawatumiki ipavyo kitu kinachosababisha kuua vipaji vyao.
CCM kutaka watu wote wenye vipaji na karama za uongozi kujiunga na chama tawala kutaifanya CCM iwe lege lege na dhaifu.
Upinzani imara uniimarisha CCM na kuleta maendeleo kwa Watanzania.
Tunataka viongozi wa upinzani wenye nguvu ya hoja na si hoja za nguvu kwa kuitukana Serikali iliyoko madarakani.
Tungependa akina Zito kabwe wengi kwenye upinzani na si kuwapunguza.
 
Eti CCM Chama dume wakati kinaogopa Vyama Vingine ukweli ni kwamba CCM ni Chama Shoga.kama wao ni wanaume waruhusu Mikutano halafu waone CHADEMA itakavyowanyoosha watu wana hamu kubwa nchi nzima,Buyungu tu Uharo ulikuwa unagonga chupi

Walati yule dogo wala hajulikani kitaifa lakini wananchi walijaa mikutano ya CHADEMA ilikua AIBU kuu kwa Chama Shoga.
Nilikuwepo na Polisi
Ukali wa maneno mkuu
 
Na kuwepo kwake ACT hakutamaliza shida za watanzania.....Zaidi ya maslahi
 
Back
Top Bottom