Zitto Kabwe afunguka kuhusu Dr. Bashiru kumtaka CCM

Zitto Kabwe afunguka kuhusu Dr. Bashiru kumtaka CCM

Trust None

JF-Expert Member
Joined
Feb 12, 2018
Posts
1,260
Reaction score
4,421
Zitto Kabwe afunguka kutimkia CCM

Zitto ametoa kauli hiyo baada ya kukaribishwa na Katibu Mkuu wa CCM kujiunga na chama hicho, ambapo alimpongeza kwa kuibua mijadala yenye maslahi ya kiuchumi.

"Mimi kujiunga CCM sio jawabu la shida za Watanzania na changamoto zinazoikabili nchi kama vile watu kukosa Uhuru wa mawazo, kukosoa, kupashana Habari na ukandamizwaji mkubwa wa vyama vya upinzani, Wananchi wanyonge kama Wakulima, Wavuvi, Wafugaji na uporaji wa Mali za watu wakiwemo Wafanyabiashara", amesema Zitto.

Zitto ameongeza kuwa, "Namwomba Bashiru CCM ni kundi la wasaka vyeo na walinda vyeo. Chama pekee cha Kijamaa nchini ni ACT Wazalendo kupitia Azimio la Tabora. Namtaka Mjamaa Bashiru Ally aachane na CCM iliyofilisika kiitikadi na ajiunge na ACT Wazalendo, Chama pekee cha Kijamaa Nchini na Afrika Mashariki".

Mapema leo akizungumza na wanachama wa CCM mkoani Iringa, Katibu Mkuu wa chama hicho Dkt. Bashiru Ally ikiwa ni ziara yake ya kikazi mkoani humo amesema kuwa Zitto Kabwe anatakiwa kujiunga na chama hicho, kwani busara zake zinafaa kukitumikia chama hicho chenye Itikadi ya Kijamaa.

Kiongozi wa Chama cha ACT-Wazalendo na Mbunge wa Kigoma mjini, Zitto Kabwe amefunguka kuwa kuhamia kwake CCM hakutomaliza changamoto za Watanzania.

SOURCE: Zitto Kabwe afunguka kutimkia CCM | East Africa Television
 
Bashiru Ally aache kukidhalilisha Chama Kikongwe Duniani

Msitu wa Amazon hauwezi kupungiwa na kitu Kwa kukosekana Mti mmoja

Bashiru asituletee damu za Kikongo kwenye chama chetu Pendwa
 
CCM ni watu wa ajabu sana, wana wenyeviti wa mitaa/vijiji, madiwani, wabunge wengi zaidi kuliko chama kingine chochote kile, lakini kwa kuwa hawajui ni kwa nini wako madarakani, wanaona hawawezi kuongoza nchi mpaka walioko kwenye vyama vingine nao wajiunge na chama chao!!

Hivi CCM wanataka wapewe nini ama wawe na nani ili waweze kuongoza nchi kwa ufanisi!? Siku nchi ikiongozwa na Rais toka chama kingine si CCM watawehuka!?
 
Zitto ni mwanafalsafa asiyeweza kuficha imani na hisia..
hawezi kwenda kwa jiwe maana mdomo unaweza ukashonwa kwa vile visent atakavyohongwa !
 
CCM ni watu wa ajabu sana, wana wenyeviti wa mitaa/vijiji, madiwani, wabunge wengi zaidi kuliko chama kingine chochote kile, lakini kwa kuwa hawajui ni kwa nini wako madarakani, wanaona hawawezi kuongoza nchi mpaka walioko kwenye vyama vingine nao wajiunge na chama chao!!

Hivi CCM wanataka wapewe nini ama wawe na nani ili waweze kuongoza nchi kwa ufanisi!? Siku nchi ikiongozwa na Rais toka chama kingine si CCM watawehuka!?
Umenifurahisha sana kwani umewaza nje ya box
 
Eti CCM Chama dume wakati kinaogopa Vyama Vingine ukweli ni kwamba CCM ni Chama Shoga.kama wao ni wanaume waruhusu Mikutano halafu waone CHADEMA itakavyowanyoosha watu wana hamu kubwa nchi nzima,Buyungu tu Uharo ulikuwa unagonga chupi

Walati yule dogo wala hajulikani kitaifa lakini wananchi walijaa mikutano ya CHADEMA ilikua AIBU kuu kwa Chama Shoga.
Nilikuwepo na Polisi
 
CCM ni watu wa ajabu sana, wana wenyeviti wa mitaa/vijiji, madiwani, wabunge wengi zaidi kuliko chama kingine chochote kile, lakini kwa kuwa hawajui ni kwa nini wako madarakani, wanaona hawawezi kuongoza nchi mpaka walioko kwenye vyama vingine nao wajiunge na chama chao!!

Hivi CCM wanataka wapewe nini ama wawe na nani ili waweze kuongoza nchi kwa ufanisi!? Siku nchi ikiongozwa na Rais toka chama kingine si CCM watawehuka!?

They prove one thing: hata wao wenyewe wanajijua kuwa ni incompetent.
 
CCM hakuna fursa ya kuibua mijadala yenye maslahi ya kiuchumi,kumkaribisha Zitto CCM nikumatakia ya Bashe ya kuambiwa kuwa ni watu wanaotafuta kuteuliwa.
 
Eti CCM Chama dume wakati kinaogopa Vyama Vingine ukweli ni kwamba CCM ni Chama Shoga.kama wao ni wanaume waruhusu Mikutano halafu waone CHADEMA itakavyowanyoosha watu wana hamu kubwa nchi nzima,Buyungu tu Uharo ulikuwa unagonga chupi

Walati yule dogo wala hajulikani kitaifa lakini wananchi walijaa mikutano ya CHADEMA ilikua AIBU kuu kwa Chama Shoga.
Nilikuwepo na Polisi
Aisee hii u turn yako bado naitafakari ,Jiwe kakugusa wapi ?
 
Back
Top Bottom