Zitto Kabwe: ACT- Wazalendo, hatutajiunga na UKAWA

Zitto Kabwe: ACT- Wazalendo, hatutajiunga na UKAWA

Si kuna kipindi Mwenyekiti wa ACT yule mwanamama alinukuliwa na vyombo vya habari akisema kuwa wameiandikia UKAWA barua ya kuomba kujiunga?

Barua ile hadi Leo haijajibiwa inasemakana chadema wamegoma kuwakaribisha act kwa sababu ya zito.
Kama kuna ugonjwa sugu ambao unaweza pelekea kifo cha chadema ni ubinafisi na ukabila.
 
Hivi Mbowe anaweza kutangaza mali zake hadharani?

Kwa hiyo alitakiwa kuto ongea kwa kuwa UKAWA(FUTUHI) wameahirisha mambo yao?

Kamwambie Rizone aaanze kutangaza maana aliambiwa mwizi na DK Slaa na Mtikila akatishia kwwnda mahamani hajaenda hadi leo, baada ya hapo mwambie Chenge huko orodha ni ndefu sana anza na hao halafu tuendelee na wengine na ili upate uhalali wa kumwambia Mbowe atangaze mali zake
 
Zitto kabwe kiongozi mkuu wa act ,hatuko tayari kuungana na ukawa,hayo yamesemwa na kiongozi mkuu wa act zito kabwe leo akiwa anaongea na wanachama wa act jijini dar es salam.
Mm kama mwana chama wa act kiongozi wangu ananichanganya sana miezi miwili iliyopita kiongozi wangu wa act alinukuliwa na redio dw ya ujerumani akisema act wako tayari kujiunga na ukawa,kulikoni tena leo kiongozi wangu amebalika?

Zitto hana uhakika wa kurudi mjengoni akiwa nje ya UKAWA!
Hivyo ametarget maslahi yake binafsi akitumia mgogo wa Lowasa (Muanzilishi na mfadhili wa ACT).
 
Act walituma barua ukawa kutaka kujiunga hadi leo haijajibiwa unafikiri watafanyaje zaidi ya kujipanga upya kivyao.
Wa kulaumiwa ni chadema ambao ni wabinafisi wanaofikiri wanaweza kuingia ikulu bila kushirikiana na vyama vingine.
Usishangae hata huu ukawa ukavunjika.

Siasa Bana eti hawana mpango wakati waliomba kujiunga.
 
Mawio limekuwa likimtukana na kumpa shutuma mbalimbali bwana zito kabwe,gazeti hilo ambalo mwandish wake ni kubenea limesababisha mtafaruku na kushindwa kutangazwa kwa mgombea ukawa kweny kikao cha Jana baada ya zito wanatakaje sapot take wakati hilo gazet LA chadema linamsimanga?? inakuwaje wanataka ushirikiano ghafla wakat hawakujibu barua ya April 24 namna ya kujiunga ukawa? Lowassa amesisitiza hawez kugombea bila wapinzan kuwa wamoja.mbowe kamaind vibaya kubenea

Mkuu, huyo Kubenea hata kwenye forum yake ya Mwanahalisi zipo thread nyingi za kumchafua Zitto, nafikiri huyo Kubenea anatumika vibaya, yeye na mabwana zake vita hii hawatashinda kwasababu Zitto ni mjanja na anaweza kucheza michezo yote michafu!
 
Last edited by a moderator:
Hivi vyama vinavyoibuka au kuundwa muda mfupi kabla ya uchaguzi havina agenda yeyote zaidi kutumika kupunguza nguvu ya upinzani,sioni sababu nyengine yeyote, maana tofauti zengine zozote zinaweza jadiliwa, sera iwe ni moja tu ya umoja wa kutaka kuleta mabadiliko.
 
Zitto nilikuamini sana kipindi cha nyumalakini kwa sasa sikusomi kaka, Unajipinga mwenyewe kauli zako,

Kwa haswa swala la UKaWA, kwanza Mwenyekiti wako alitangaza mwana ACT yeyote atakae shabikia UKAWa atachukuliwa hatu, Ukaja wewe ukatangaza kuutaka umoja huo na kuandika Barua ya Kujiunga na ukatoa shutuma kwa Chadema kuwa hawakutaki, ila ukasema wakikubali hata leo unajiunga na kutamka wazi hakuna mtu asiye utaka umoja,

Leo unakuja na tamko jingine, ACT haita jiunga na UKAWA eti vyama vingine havina Sera nzuri kama ACT, kwanza kina azimio la Tabora, Je mwanzo ulipo andika barua haukuliona hilo? na je wangekukubalia ungejitoa? Zitto kwanini usiwe unafikiria kabla ya kutenda?

Swali jingine kwa Zitto, Je kama wewe ni Mkuu wa chama, kuna uchaguzi wowote ulifanyika kukuchagua? na kama hakuna utaratibu huo, wewe ni kiongozi wa Chama mpaka kufa kwako? na kama ni hivyo, nikikuita wewe ni mroho wa madaraka nitakuwa nafanya makosa?

Zitto hiki Chama kweli ni cha Watanzania? na akama cha Watanzania, kwanini ulitangaza kushinda majimbo yote ya kigoma na sii Mbeya? na ukijua wewe ni mwanakigoma? unamaanisha hiki chama ni cha watu wa kigoma? kwahiyo uanataka kutuambia kila atakae kuwa na uwezo wa kuanzisha chama akipeleke kwao? huoni kuwa kila kabila litakuwa na Chama chake? na hauoni ukabila na ukwetu utaanzia hapo?

Sawa kaka unajenga chama chako ila jaribu kujielewa na kuelewa kile unafanya

yangu ni hayo tu
 
ZZK anaweza akawa spilit UKAWA, anavyopenda sifa utafikiri yeye ndo chama, kama wazee wa cdm na busara zao baregu, marando, slaa, safari na wengineo wamemshindwa ni nani atamweze. I think abaki ACT panamtosha, akipata hapo jimbo moja na madiwani 5 karuzuku tosha.
 
Kiongozi wa ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe amesema kuwa chama chake hakitashirikiana na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), badala yake kitasimama chenyewe kwenye Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.
Kauli hiyo inazima minong’ono iliyotawala miongoni mwa wanachama wa ACT-Wazalendo waliokuwa wakimuuliza Zitto kuhusu chama hicho kujiunga na Ukawa. Zitto alimaliza uvumi huo jana jijini hapa katika mkutano na viongozi wa chama, wanachama na watiania wa nafasi mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu. Alisema ACT-Wazalendo haiwezi kuungana na Ukawa inayoundwa na vyama vya Chadema, CUF, NCCR-Mageuzi na NLD kwa vile sera ya chama hicho tofauti na vyama hivyo.
 
Ni kweli hata malengo ya kuanzishwa kwake ni tofauti na vyama vingine vya upinzani
 
Barua ile hadi Leo haijajibiwa inasemakana chadema wamegoma kuwakaribisha act kwa sababu ya zito.
Kama kuna ugonjwa sugu ambao unaweza pelekea kifo cha chadema ni ubinafisi na ukabila.

Zzt hajielewi
kwanini aliomba kujiunga Mara ya kwanza wakati anajua misingi take haiendana na ya vyama vingine?
 
Zitto is a great leader of our time. Only critical thinkers can understand this. He is the only leader with vision and who can articulate it to his followers. Big up Zitto

Zitto ni mpumbavu tu. Huku unaandika Barua ya kutaka kujiunga na Ukawa, Huku unadai kuwa kwa chama chochote makini lazima kujiunga katika Umoja. Barua haijajibiwa, UKAWA haujakubali kujiunga na wewe. Leo unakurupuka eti hatutajiunga na Ukawa. Kwani umekubaliwa kujiunga lini??. Acha short cut Kijana. Kujenga chama sio rahisi hivyo
 
Kamwambie Rizone aaanze kutangaza maana aliambiwa mwizi na DK Slaa na Mtikila akatishia kwwnda mahamani hajaenda hadi leo, baada ya hapo mwambie Chenge huko orodha ni ndefu sana anza na hao halafu tuendelee na wengine na ili upate uhalali wa kumwambia Mbowe atangaze mali zake

Safi Mkuu, Ila jibu ni kwamba Tume ya maadili ina mali za Viongozi. Kwa nini wasiiombe Serikali yao ibadili sheria ili mali za Viongozi iwe wazi na sio siri
 
“Hatuwezi kujiunga na Ukawa kwa kuwa CCM na vyama vingine hawana tofauti kwa sera, lakini ACT ni tofauti kwa kuwa inaheshimu miiko ya uongozi na kubwa zaidi chama chetu kinaongozwa na azimio la Tabora,” alisema Zitto Kabwe. Una neno gani kwa Zitto Kabwe?
 
Haumuwezi kujiunga na ukawa!mnachekesha sana . wakati mnaomba kujiunga mlikuwa mna taka kujiunga na nani?
 
Back
Top Bottom