Drifter
JF-Expert Member
- Jan 4, 2010
- 5,371
- 5,516
Anachohitaji Zitto hivi sasa ni kutafakari kikamilifumwelekeo wake kisiasa - kama bado anaamini ana mustakabali (future) katika fanihiyo baada ya mwanga (spotlight) wa enzi za Buzwagi kuanza kufifia. Hizi dhanaza rejareja anazohangaika nazo leo hii hazina maana wala umuhimu kwake yeye nataifa kwa ujumla. Hakuna falsafa wala itikadi mpya anayoileta zaidi yakuonekana kama mtu anayehaha kushindana au kupambana na wale anaowaona maaduizake binafsi katika ulimwengu wa siasa (defensive mindset).
Prof. Shivji amewasilisha maswali ya msingi. Azimio la Arusha haliendani kabisana mfumo wa kiuchumi na kijamii tulio nao wakati huu. Hata hayomaadili anayodai yako katika Azimio la Tabora si ainisho kamili la maadilikatika mfumo tulio nalo sasa. Yeye kashikilia kipengele cha "viongozikutangaza mali". Hiyo sio falsafa wala itikadi; ni sehemu ya utaratibutu (procedure) wa udhibiti na ufuatiliaji wa mienendo ya viongozi katikakigezo cha wizi wa mali za umma na ufisadi.
Hata katika mifumo inayoongozwa na falsafa/itikadi za kibepari wanazo taratibuza kuhakikisha kwamba wenye dhamana ya dola hawatumii nafasi zao kuhujumuuchumi wa taifa kwa wizi na rushwa. Hakuna falsafa/itikadi inayoshabikia wiziwa mali za umma. Tatizo la wizi/ufisadi hapa kwetu si la kifalsafa walakiitikadi. Ni tatizo la kukosa uongozi wa kweli (tumefilisika kiuongozi). Kwamfumo tulio nao, hata viongozi wa Serikali na vyama wakitangaza mali zao leohii bado wataendelea kutuibia bila hatua kuchukuliwa.