Zitto hayuko tayari kuwa kiongozi!

Jamani hebu mtufafanulie hivi huyu Zito ni mtu wa aina gani mbona anajadiliwa sana mitandaoni na kwenye media mbalimbali kuliko wanasiasa wengine?
 
4th December 2010 21:08
#1
JF Senior Expert MemberArray


Join Date : 22nd November 2006
Posts : 1,726
Rep Power : 1059
Likes Received498
Likes Given19


[h=2]
icon1.png
Zitto hayuko tayari kuwa kiongozi![/h]
Nilitokea kumjua zitto kutokana na marafiki zangu waliosoma naye kule Galanos. Vilevile mimi nilisoma Galonos form five mwaka 1994-1995 miaka miwili kabla ya zitto. Vilevile zitto nimempita mwaka moja kwani yeye kazaliwa 1976 na mimi 1975. Kwa ujumla mimi nilijiona nafanana sana na huyu kijana mpya ambaye ameingia kwenye siasa na hivyo alivyotembelea USA nilihakikisha ninaongea naye kwani niliona ni watu wa rika moja na tutaelewana zaidi kuliko wazee wengi wanakuja huku.
Zitto alivyokuja aliniambia mimi na vijana wengine anataka kupumzika siasa na kwenda kusoma PHD. Vilevile tulimuuliza kama anataka msaada wowote atwambie akasema kapata shule nyingi ikiwa pamoja na Preston University amboyo ni chuo kizuri sana kiko State ya New Jersey. Alisema alitaka kusoma mambo ya economics contracts ili aweze kufundisha kwenye chuo kimoja nafikiri Dodoma kuhusu mikataba kama ya madini na n.k kwani alisema nchi yetu inahitaji wataalamu wa mikataba. Vilevile tuliongea mambo mengi na kibinafsi ambayo sitataka kuyasema. Kwa ujumla Zitto alituambia na kuonekani waziwazi hapendi siasa na hana furaha na kitu anachofanya. Vilevile alionyesha waziwazi anapenda kuwa Professor wa chuo kikuu chochote. Zitto alitoa ahadi nyingi ikiwa ni pamoja ya kujibu email zetu na kutusaidia kuelezea mambo fulani muhimu ambayo watu wengi wa diaspora tulikuwa tunaona kama yanahitaji mwangeaji.
Zitto alishangaza wengi kwani hajafanya hata kitu kimoja alishokuwa anasema ikiwa ni pamoja na kwenda chuo, kujibu email na kuwasiliana na kuongea mambo muhimu ya diaspora ambayo tulikubaliana naye kutusaidia ku lobby. Vilevile Zitto alionekana hana experience ya maisha kama kufanya kazi ya kawaida au kufanya biashara!.
Kwa mawazo yangu Zitto ni mapepe ni kijana mwenye akini lakini anatakiwa kutulia na kujua anataka kufanya nini hasa kwenye maisha. Vilevile Zitto haelewi kwa undani ni kwanini Chadema iko imara kuliko nyama vingine.
Chadema iko imara kwasababu
(1)Viongozi na waanzilishi wa Chadema wamejitosheleza kiuchumi na hawana tamaa. Uhodari wa kuongea na ushabiki hautoshi kukuza chama kikubwa kama Chadema. Mrema alikuwa ni hodari na mwenye kipaji cha mvuto kwa wananchi lakini kwasababu ya umasikini wake alikuwa nategemea sana serikali kuanzia ruzuku hadi nyumba aliyokuwa anakaa. Hii ilimfanya Mrema kutangatanga bila mafanikia na kuhama vyama bila mafanikio makubwa kwasababu Mrema alikuwa hajajitosheleza na maisha aliyokuwa nayo na alitegemea sana serikali. Zitto ni kama Mrema ingawa Tatizo lake hajui anachotaka bado!
(2)Mboe, Slaa, Ndesamburo na Mtei. Dr Slaa alikuwa padre ambaye alishazoea kuishi maisha marahisi na ya wito hivyo hawezi kutapatapa. Mboe, Ndesamburo na Mtei ni wafanya biashara wakubwa wenye akili ya biashara na wanafanya biashara ambazo hazitegemei serikali hivyo serikali haiwezi kuwatisha. Mtei ana biashara ya kupeleka maua nje, Ndesamburo ana viwanda na hoteli na Mboe ana hoteli hivyo hawa watu hawawezi kudanganya na watu wa serikalini. Ndesamburo kununua Helikopta mbili kwa chama ni mfano kwani ameonyesha anafanya vitu kwa wito na sio shida.
(3)Viongozi wa Chadema wana ongoza chama kibiashara hii inawezekana isionekane waziwazi lakini Mboe ni mtu muhimu kuliko Zitto kwasababu anajua kuongoza. Zitto anafikiri kidemokrasia lakini kwenye kampuni hakuna demokrasia bali productivity. Mboe ana results na Zitto hana, Mboe ana experience za utawala Zitto hana, Mboe anajua anachokitaka na Zitto hajui. Hivyo Zitto anaweza akawa ni mtu mwenye kipaji cha akili zaidi ya Zitto na Mvuto zaidi ya Mboe lakini hana uwezo wa kuongoza kwasasa zaidi ya Mboe!. Mboe vilevile anavitu kama magazeti n.k ambavyo ni muhimu kutoa habari na Zitto hata email hajibu!. Chadema ingekuwa haina watu matajiri kwenye chama na wenye wito chama kingeshakufa sikunyingi sana. Huwezi kupambana na CCM kwa sera pekee! Zitto.
Zitto ni lazima uelewe kwamba mafanikio ya Chadema ni ya wito na utajiri wa waanzilishi na viongozi na si uhodari wa kuongea pekee. Kuna watu watakudanganya uhame chama kwa kuweka udini na kukupa kichwa kwamba wewe una kipaji utafanikiwa popote lakini kuwa mwanasiasa hodari si sawa na kuwa kiongozi hodari!. Mboe ni muhimu kwa Chadema kuliko wewe. Je ni mfanya biashara gani mkubwa ni muha wa kigoma!!. Ni lazima uwaheshimu watu waliokutoa kigoma mpaka hapo ulipo kwani hawa wanaokushauri uhame ndiyo wa kwanza watakao kuita Muha wa kigoma anayetangatanga na hutakuwa na watu wenye nia nzuri kwako bali kukutumia tu. Hivyo Zitto tukia na jenga imani na jifunze kutoka kwa kina ndesamburo, Slaa na Mboe jinsi ya kufanikiwa kimaisha bila siasa!.Muda wako utakuja hapo utakapojua ni kitu gani unataka kufanya, vilevile acha uongo!.
Zitto kwasasa hauko tajari kuwa mwenyekiti wa Chadema.​

hexacyanoferrate likes this.


 
Kuna waliosema nimetukana watu wa Kigoma lakini nia yangu ilikuwa kuonyesha fikra za wanasiasa sio binafsi. Number hazidanganyi. Tunaona mbali wengine
 
Kamundu. Naona leo upo na Muha mwenzako bwana Zitto
 
Last edited by a moderator:
Kuna waliosema nimetukana watu wa Kigoma lakini nia yangu ilikuwa kuonyesha fikra za wanasiasa sio binafsi. Number hazidanganyi. Tunaona mbali wengine

Mkuu wewe ni genius, mambo yako ya 2010 sasa hivi yanamuelezea Zitto kiuhalisia kabisa. Kila ulichosema kimekuwa realized, kweli unamjua vizuri Zitto...

Kwa sasa akiitisha mkutano hawezi kupata watu wa kujaza hata basi moja la Yutong
 
Huko kigoma watu wamemshtukia.....anazomewa kila kona mpenda rushwa huyu....iwapo kamati ya kushughulikia madini ilimshinda,akachagua rushwa kuliko wananchi huyo ni wakuogopa km ebola.
 
Payroll zinazotoka kwenye mifuko ya jamii ya masikini ni mbaya sana ni kama laana kwa anayechukua
 
akili ya zitto imeenda likizo baada ya kuandamwa nap msongo wa mawazo kwa yaliyomsibu,kila siku anazidi kupotea kwa hali anayoishi hana tofauti na mgonjwa wa akili,nilimkubali sana huyu kijana ila kw unafiki na uroho wa madaraka hatufai hata team# lowassa aishie hukohuko ACT
 
Ushauri mzuri,umaarufu ni kama jua,huchomoza na kuzama.Hivyo,umaarufu sio tija,bali jali wale waliokupa huo umaarufu.
 
Laiti mgalijua!.ZZK ni habari nyingine kabisa!. Endeleeni kujifariji!.

P.

Nadhani wewe pamoja na maccm ndio mliomfikisha hapo alipo kwa hizi sifa zenu uchwara kwake! Alishapotea huyo kwenye siasa za bongo na hata yeye analijua hilo.hicho chama chake cha wasaliti na mamluki kikipata hata mbunge mmoja mimi najinyonga! Sioni jimbo la kuchukuliwa na act hapo 2015
 
Kweli mleta mada anamfahamu uzuri Zitto. Hayo aliyowafanyia diaspora ndio anaowafanyia wana jimbo lake, wafanyakazi vijana wa halmashauri yake na hata wageni, HATIMIZI AHADI KABISA, na PROMISE KWAKE YEYE INA MAANA TOFAUTI.
Aliwadanganya wajerumani waje wafanye field mwamgongo na kwamba TANAPA watawasupport matokeo yake akawatelekeza huku TANAPA hawana hata moja wanalolijua.
Kipindi cha pili cha ubunge wake amekipata kwa heshima ya diwani wa Mwandiga aliyezunguka jimbo lote kumuombea msamaha, lkn kama kawa alivyoahidi hajatimiza hata nusu ya robo.
Na ndio maana alianza kujisemesha kuliacha jimbo na kufikiria kugombea kigoma mjini (wabadilishane na serukamba) coz anajua hawezi kuchagulia kamwe kaskazini, jimboni mwake kawa MSALITI hata kabla hajawa msaliti wa watanzania na CHADEMA
 
Zitto ni tumaini LETU jipya mtamtukana kumkebehi ila mwisho wa siku mtamkubali wenyewe
 
Back
Top Bottom