Zitto hayuko tayari kuwa kiongozi!

Kamundu

Platinum Member
Nov 22, 2006
4,812
2,000
Nilitokea kumjua zitto kutokana na marafiki zangu waliosoma naye kule Galanos. Vilevile mimi nilisoma Galonos form five mwaka 1994-1995 miaka miwili kabla ya zitto. Vilevile zitto nimempita mwaka moja kwani yeye kazaliwa 1976 na mimi 1975. Kwa ujumla mimi nilijiona nafanana sana na huyu kijana mpya ambaye ameingia kwenye siasa na hivyo alivyotembelea USA nilihakikisha ninaongea naye kwani niliona ni watu wa rika moja na tutaelewana zaidi kuliko wazee wengi wanakuja huku.

Zitto alivyokuja aliniambia mimi na vijana wengine anataka kupumzika siasa na kwenda kusoma PHD. Vilevile tulimuuliza kama anataka msaada wowote atwambie akasema kapata shule nyingi ikiwa pamoja na Preston University amboyo ni chuo kizuri sana kiko State ya New Jersey. Alisema alitaka kusoma mambo ya economics contracts ili aweze kufundisha kwenye chuo kimoja nafikiri Dodoma kuhusu mikataba kama ya madini na n.k kwani alisema nchi yetu inahitaji wataalamu wa mikataba. Vilevile tuliongea mambo mengi na kibinafsi ambayo sitataka kuyasema. Kwa ujumla Zitto alituambia na kuonekani waziwazi hapendi siasa na hana furaha na kitu anachofanya.

Vilevile alionyesha waziwazi anapenda kuwa Professor wa chuo kikuu chochote. Zitto alitoa ahadi nyingi ikiwa ni pamoja ya kujibu email zetu na kutusaidia kuelezea mambo fulani muhimu ambayo watu wengi wa diaspora tulikuwa tunaona kama yanahitaji mwangeaji.

Zitto alishangaza wengi kwani hajafanya hata kitu kimoja alishokuwa anasema ikiwa ni pamoja na kwenda chuo, kujibu email na kuwasiliana na kuongea mambo muhimu ya diaspora ambayo tulikubaliana naye kutusaidia ku lobby. Vilevile Zitto alionekana hana experience ya maisha kama kufanya kazi ya kawaida au kufanya biashara!.

Kwa mawazo yangu Zitto ni mapepe ni kijana mwenye akini lakini anatakiwa kutulia na kujua anataka kufanya nini hasa kwenye maisha. Vilevile Zitto haelewi kwa undani ni kwanini Chadema iko imara kuliko nyama vingine.

Chadema iko imara kwasababu
(1)Viongozi na waanzilishi wa Chadema wamejitosheleza kiuchumi na hawana tamaa. Uhodari wa kuongea na ushabiki hautoshi kukuza chama kikubwa kama Chadema. Mrema alikuwa ni hodari na mwenye kipaji cha mvuto kwa wananchi lakini kwasababu ya umasikini wake alikuwa nategemea sana serikali kuanzia ruzuku hadi nyumba aliyokuwa anakaa. Hii ilimfanya Mrema kutangatanga bila mafanikia na kuhama vyama bila mafanikio makubwa kwasababu Mrema alikuwa hajajitosheleza na maisha aliyokuwa nayo na alitegemea sana serikali. Zitto ni kama Mrema ingawa Tatizo lake hajui anachotaka bado!

(2)Mboe, Slaa, Ndesamburo na Mtei. Dr Slaa alikuwa padre ambaye alishazoea kuishi maisha marahisi na ya wito hivyo hawezi kutapatapa. Mboe, Ndesamburo na Mtei ni wafanya biashara wakubwa wenye akili ya biashara na wanafanya biashara ambazo hazitegemei serikali hivyo serikali haiwezi kuwatisha. Mtei ana biashara ya kupeleka maua nje, Ndesamburo ana viwanda na hoteli na Mboe ana hoteli hivyo hawa watu hawawezi kudanganya na watu wa serikalini. Ndesamburo kununua Helikopta mbili kwa chama ni mfano kwani ameonyesha anafanya vitu kwa wito na sio shida.

(3)Viongozi wa Chadema wana ongoza chama kibiashara hii inawezekana isionekane waziwazi lakini Mboe ni mtu muhimu kuliko Zitto kwasababu anajua kuongoza. Zitto anafikiri kidemokrasia lakini kwenye kampuni hakuna demokrasia bali productivity. Mboe ana results na Zitto hana, Mboe ana experience za utawala Zitto hana, Mboe anajua anachokitaka na Zitto hajui. Hivyo Zitto anaweza akawa ni mtu mwenye kipaji cha akili zaidi ya Zitto na Mvuto zaidi ya Mboe lakini hana uwezo wa kuongoza kwasasa zaidi ya Mboe!.

Mboe vilevile anavitu kama magazeti n.k ambavyo ni muhimu kutoa habari na Zitto hata email hajibu!. Chadema ingekuwa haina watu matajiri kwenye chama na wenye wito chama kingeshakufa sikunyingi sana. Huwezi kupambana na CCM kwa sera pekee! Zitto.

Zitto ni lazima uelewe kwamba mafanikio ya Chadema ni ya wito na utajiri wa waanzilishi na viongozi na si uhodari wa kuongea pekee. Kuna watu watakudanganya uhame chama kwa kuweka udini na kukupa kichwa kwamba wewe una kipaji utafanikiwa popote lakini kuwa mwanasiasa hodari si sawa na kuwa kiongozi hodari!. Mboe ni muhimu kwa Chadema kuliko wewe. Je ni mfanya biashara gani mkubwa ni muha wa kigoma!!.

Ni lazima uwaheshimu watu waliokutoa kigoma mpaka hapo ulipo kwani hawa wanaokushauri uhame ndiyo wa kwanza watakao kuita Muha wa kigoma anayetangatanga na hutakuwa na watu wenye nia nzuri kwako bali kukutumia tu. Hivyo Zitto tulia na jenga imani na jifunze kutoka kwa kina ndesamburo, Slaa na Mboe jinsi ya kufanikiwa kimaisha bila siasa!.Muda wako utakuja hapo utakapojua ni kitu gani unataka kufanya, vilevile acha uongo!.

Zitto kwasasa hauko tajari kuwa mwenyekiti wa Chadema.
 
Mpasuajipu

JF-Expert Member
Oct 22, 2010
836
0
Hapo umemchokora PWEZA. Maana Pweza pamoja na kuwa na mikono nane bado hunaswa na bin-adamu mwenye mikono miwili tu.
 
mshikachuma

JF-Expert Member
Dec 2, 2010
2,853
0
Nafikiri ni meseji mzuri sana kwa zitto!
Kama ataisoma basi nahisi kuna sehemu itamgusa kiasi fulani.
 
tumpale

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
200
0
meseji sent and i think delivered, zitto achukue ujumbe huo utamsaidia sana akiuzingatia.
 
Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
0
Chadema ingekuwa haina watu matajiri kwenye chama na wenye wito chama kingeshakufa sikunyingi sana. Huwezi kupambana na CCM kwa sera pekee! Zitto.
Well said, mfano wa Mrema ni live kabisa hakuna atakayebisha kuwa maisha anayoishi Mrema ni ya kubahatisha na kutegemea wahisani kuanzia nyumba, afya, elimu nk. Kwa hali hiyo huwezi kuwa mwenyekiti wa chama na kupambana na CCM iliyo na kila kitu kuanzia pesa nk wakihitaji pesa ya kumnunua Mbunge ni kiasi cha kunyanyua simu na kumpigia Ndullu.

Kweli Zitto kaa kwanza ujifunze kukaa na kuishi na watu umemaliza shule juzi huna experience yeyote ya mambo yanavyokwenda uraiani ni tofauti na unavyosoma vitabuni, ni sawa na maisha ya ndoa kwa nje unaweza sema ni rahisi kuishi mme na mke ingia uone. Jifunze kwanza kwa uliowakuta usikimbilie kuongoza kwa sifa za JF uongozi ni zaidi ya kupigiwa makofi.
 
Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
9,952
2,000
Huyu Bwana amenena bila kumung'unya maneno. Katika siasa kuna mambo mengine watu hawasemi sana lakini ni muhimu sana katika kuleta mafankio, nayo ni 'Pesa'. Wanaosema kuwa pesa siyo muhimu katika siasa ni kama wale wanaosema kuwa unaweza kuishi vizuri katika mapenzi/ndoa bila pesa lakini ukweli ni kuwa mapenzi/ndoa katika umaskini ni ngumu sana.

Tukienda katika hali ya kawaida, ukivitazama vyama vya upinzani Tanzania bara, kwa jinsi vinavyojengewa mazingira magumu ili vife, ukiona vinaendelea kuna watu wamevitegemeza sana kwa pesa zao binafsi lakini ukiwapata watu wenye akili ndogo utawasikia mara Mbowe kwa signatory wa account za Chama, mara hiki mara kile, unashindwa kuelewa kama hao watu wanajua Mtei, Ndesamburo na Mbowe walivyokitegemeza chama kwa pesa yao binafsi.

Mimi nakubaliana sana na huyu Bwana kuwa kijana Zito ana akili lakini asipoaangalia akili yake haitaweza kuwasaidia watu wala yeye mwenyewe, na kilicho muhimu siyo kuwa na akili tu bali kuwa na matumizi sahihi ya akili. Unaweza kuwa na akili sana lakini ukaitumia akili hiyo kuwavuruga watu, kuwahadaa, au kupanga mipango ya kuwaibia watu bila kugundulika. Na ukifikia hapo, ni aheri asiye na akili atakuwa na madhara madogo kwa jamii kuliko mwenye akili sana lakini wa namna hiyo.
 
Waberoya

Platinum Member
Aug 3, 2008
15,149
2,000
Kamundu

Yaani umekichana chadema live kabisa bila wewe kujua, umefikiri unajenga kumbe unamaliza kabisa

Chama chenye sera nzuri kinaongozwa na watu na michango ya watu, ni sawa na harusi hata kama una fedha nyingi bila watu kuchanga haifurahishi, maana haishirikikiki!! umenena live chadema ni cha wachache wafanyabiashara!!! wafanya bishara hawako tayari kwenda jela kwa ajili ya manufaa ya wananchi wako tayari kulinda fedha na status zao!

Hivi umefikiria ulichoandika maan naona umeeleza ukweli wa moyoni kitu ambacho chadema wengi huwa wanabisha na wewe live umeeleza ni wafanyabiashara, believe me, Ndesamburo na hao wengine lazima wanapata faida!!!how?? au wanajitolea tu lwa sababu wanakupenda sana!!!

Huyo slaa ni mroho wa hela na alihaidiwa mshahara fulani akikosa urais, unalijua hilo

Kuhusu Zito well, kuna mawali mengi BEING PROFESSOR AU ACADEMICIAN AS NOTHING TO DO WITH POLITICS!!! POLITICS IS NOT PROFESSIONAL FOR PARTICIPANTS; IS OPTION ONLY FOR POLITICAL SCIENTIST!!
Ndiyo maana kuna mainjinia akina Mwandosya, chemist Dr.Magufuli, n.k you can be politician still you can excell to your professional , hapa inahitaji akili kidogo tu, na siamini kabisa kuwa una umri huo. Dr.Magufuli amepata masters na PhD akiwa kiongozi/mwanasiasa (record this)

Umeweka vijembe eti hakuna mfanyabiashara mkubwa Mha!!! yaani umeleta ukabila live ule tunaopigana nao humu!!! ar you sure

FYI Zito ameingia chadema akiwa na miaka 16!!! na amepokelewa na hao unaowasema na leo hii wamempa unabibu katibu mkuu!! japo unafikiri unawasemea akina Slaa ila wengi wanakushangaa lengo la hii post ni nini?? wapi umemkamata amefanya kosa gani (with evidence) na maoni yako ya kutokuwa na imani naye yanapingana na maoni ya kamati kuu ya chadema akiwamo meti na ndesamburo!!

By the way unasoma chuo gani huko marekani? maan paragraph hamna I mean post yako haivutii kabisa
 
Last edited by a moderator:

JAY2da4

JF-Expert Member
Nov 11, 2008
213
250
Naunga mkono hoja yako.Mwandishi karopoka inaonekana ana chuki binafsi tu,kadhihirisha kuwa ni limbukeni na mbaguzi mkubwa.
Chadema bila kuwa na watu wa matabaka yote siyo chama,eti matajiri,njaa tu hakuna cha tajiri hapo bana.Kwa hiyo wanakupenda sana
ndo maana wanakidhani chama ?

Yaani umekichana chadema live kabisa bila wewe kujua, umefikiri unajenga kumbe unamaliza kabisa

Chama chenye sera nzuri kinaongozwa na watu na michango ya watu, ni sawa na harusi hata kama una fedha nyingi bila watu kuchanga haifurahishi, maana haishirikikiki!! umenena live chadema ni cha wachache wafanyabiashara!!! wafanya bishara hawako tayari kwenda jela kwa ajili ya manufaa ya wananchi wako tayari kulinda fedha na status zao!

Hivi umefikiria ulichoandika maan naona umeeleza ukweli wa moyoni kitu ambacho chadema wengi huwa wanabisha na wewe live umeeleza ni wafanyabiashara, believe me, Ndesamburo na hao wengine lazima wanapata faida!!!how?? au wanajitolea tu lwa sababu wanakupenda sana!!!

Huyo slaa ni mroho wa hela na alihaidiwa mshahara fulani akikosa urais, unalijua hilo

Kuhusu Zito well, kuna mawali mengi BEING PROFESSOR AU ACADEMICIAN AS NOTHING TO DO WITH POLITICS!!! POLITICS IS NOT PROFESSIONAL FOR PARTICIPANTS; IS OPTION ONLY FOR POLITICAL SCIENTIST!!
Ndiyo maana kuna mainjinia akina Mwandosya, chemist Dr.Magufuli, n.k you can be politician still you can excell to your professional , hapa inahitaji akili kidogo tu, na siamini kabisa kuwa una umri huo. Dr.Magufuli amepata masters na PhD akiwa kiongozi/mwanasiasa (record this)

Umeweka vijembe eti hakuna mfanyabiashara mkubwa Mha!!! yaani umeleta ukabila live ule tunaopigana nao humu!!! ar you sure

FYI Zito ameingia chadema akiwa na miaka 16!!! na amepokelewa na hao unaowasema na leo hii wamempa unabibu katibu mkuu!! japo unafikiri unawasemea akina Slaa ila wengi wanakushangaa lengo la hii post ni nini?? wapi umemkamata amefanya kosa gani (with evidence) na maoni yako ya kutokuwa na imani naye yanapingana na maoni ya kamati kuu ya chadema akiwamo meti na ndesamburo!!

By the way unasoma chuo gani huko marekani? maan paragraph hamna I mean post yako haivutii kabisa
 
Lekanjobe Kubinika

JF-Expert Member
Dec 6, 2006
3,022
2,000
lakini sikio la kufa bahati mbaya halisikii dawa. Umri wake huo na social status vina conflict kubwa mno hata anajikuta anafunikwa kwa kuzidiwa na kutamani aonekane kuwa anayo sifa kuwa yuko juu zaidi.

Mtu yeyote anayetanguliza kutafuta sifa hawezi kuona madhara halisi ya purukushani zake kwa jamii. Akikua ataacha. Kwa sasa dunia inaendelea kumfunza. Chochote atakachoambiwa nje ya kumpatia sifa ataamini kwamba anaonewa.

Akijifunza japo kwa maangamizi ya jamii na tena kwa njia ngumu labda, anaweza kuwa mwalimu mzuri sana kwa watu wanaopitia mapito yake.
 
Gagnija

JF-Expert Member
Apr 28, 2006
9,377
2,000
Kama viongozi wa CHADEMA wangekuwa na mawazo mfu kama ya Kamundu ningeichanachana kadi yangu ya chama. Huyu mpumbav angefanya utafiti kidogo angejua kuwa Kigoma ilianza kuwa stronghold ya chama kabla hata ya huko kwao, na miongoni mwa waasisi wa chama walikuwemo pia watu wa Kigoma, not necessarily waha.

AmaniKatoshi

Senior Member
Mar 31, 2009
158
195
Yaani umekichana chadema live kabisa bila wewe kujua, umefikiri unajenga kumbe unamaliza kabisa

Chama chenye sera nzuri kinaongozwa na watu na michango ya watu, ni sawa na harusi hata kama una fedha nyingi bila watu kuchanga haifurahishi, maana haishirikikiki!! umenena live chadema ni cha wachache wafanyabiashara!!! wafanya bishara hawako tayari kwenda jela kwa ajili ya manufaa ya wananchi wako tayari kulinda fedha na status zao!

Hivi umefikiria ulichoandika maan naona umeeleza ukweli wa moyoni kitu ambacho chadema wengi huwa wanabisha na wewe live umeeleza ni wafanyabiashara, believe me, Ndesamburo na hao wengine lazima wanapata faida!!!how?? au wanajitolea tu lwa sababu wanakupenda sana!!!

Huyo slaa ni mroho wa hela na alihaidiwa mshahara fulani akikosa urais, unalijua hilo

Kuhusu Zito well, kuna mawali mengi BEING PROFESSOR AU ACADEMICIAN AS NOTHING TO DO WITH POLITICS!!! POLITICS IS NOT PROFESSIONAL FOR PARTICIPANTS; IS OPTION ONLY FOR POLITICAL SCIENTIST!!
Ndiyo maana kuna mainjinia akina Mwandosya, chemist Dr.Magufuli, n.k you can be politician still you can excell to your professional , hapa inahitaji akili kidogo tu, na siamini kabisa kuwa una umri huo. Dr.Magufuli amepata masters na PhD akiwa kiongozi/mwanasiasa (record this)

Umeweka vijembe eti hakuna mfanyabiashara mkubwa Mha!!! yaani umeleta ukabila live ule tunaopigana nao humu!!! ar you sure

FYI Zito ameingia chadema akiwa na miaka 16!!! na amepokelewa na hao unaowasema na leo hii wamempa unabibu katibu mkuu!! japo unafikiri unawasemea akina Slaa ila wengi wanakushangaa lengo la hii post ni nini?? wapi umemkamata amefanya kosa gani (with evidence) na maoni yako ya kutokuwa na imani naye yanapingana na maoni ya kamati kuu ya chadema akiwamo meti na ndesamburo!!

By the way unasoma chuo gani huko marekani? maan paragraph hamna I mean post yako haivutii kabisa

Weberoya, uwezo wa kukaa mbele ya PC na kutype sio kilelelezo cha kuyaelewa yale unayoandika. Ninakushauri uusome tena ujumbe wako vizuri alafu urekebishe pale inapofaa...

Kwa kifupi tuu...wewe ni mmoja kati ya wengi ambao hawaitakii CHADEMA mema.

Kuwa mfanyabiashara haihusiani na ukabila bali akili ya kufikiri na kuamua bila kuamrishwa. Je unakubali hilo?

Welll ningefurahi sana kama ungetuambia source ya sentensi hii....BEING PROFESSOR AU ACADEMICIAN AS NOTHING TO DO WITH POLITICS!!! POLITICS IS NOT PROFESSIONAL FOR PARTICIPANTS; IS OPTION ONLY FOR POLITICAL SCIENTIST!! maana sio ya kwako. Nasikitika pia kuwa umeiquote bila kuielewa...hapa unamsema nani?

Hawa waliongia kwenye siasa ambazo zio mahali pao kama akina Mwandosya unaowataja umeona wanachofanya? Wizara ngapi amezunguka? Zipi amezifanikisha walao kwa kiwango kidogo...? Nenda kule Afya, nenda elimu kwa akina Msolwa etc.

Sasa nakubali kuwa IS OPTION FOR POLITICAL SCIENTISA mbao sio lazima wawe wamesomea na kupata vyeti bali kwa kufanya mambo makubwa, angalia akina Berluscony, Mandela etc.
 
andrewk

JF-Expert Member
Apr 13, 2010
3,102
1,500
Tehe teh....... mamabo hayo, kuna mtu anasema sera nzuri zitawafanya watu wachangie chama kama harusi?... dhubutu! ...... kwa serikali za afrika changia uone kwa sasa ni sabodo tu kwani CCM wanamuogopa, lakini wakati Nyerere anaijenga Tanu na CCM si akina Bukuku ndio walikuwa karibu sana, mbona atukusema CCM au Tanu ni chama cha watu wa Musoma.

Naunga mkono hoja bila kujali kama yote aliyosema yanaweza kuwa na mvuto kwa watu wote, especially ndugu zangu Wahaaa,... maana miseme inaweza tuktumika na isipendeze kwa watu. Nyerere aliwahi sema hawezi kukaa kimya wakati nchi inachukuliwa na mbwa.... sasa huo ni msemo unafahamika sana, lakini ukiuweka kwa kiswahili ndio linakuwa kama tusi vile....Lakini pale jamaa alipowasema wahaa , sidhani alimaanisha wahaa wote hawawezi biashara. Nadharia ilikuwa ni kuonyesha kwamba kufanikiwa katika siasa kunahitaji uvumilivu wa wa hali ya juu ambaoviongoziwa sasa wa chadema (ambao ni wachaga wameweza, kwani sifa pekee ya wachaga ni kutoogopa kujaribu jambo ambalo anaamini lina manufaa kwake na jamii inayomzunguka)

Nyerere aliaamini tanzania inaweza kujitawala, ila hakuwa na uwezo kifedha, aliwaheshimu waliomuwezesha kutimiza dhamira yake...

Maada hii ndefu sana na ni nzuri sana kuichangia.. ila kazi sasa, by
 
Butola

JF-Expert Member
Jan 19, 2010
2,290
2,000
Ndesamburo kununua Helikopta mbili kwa chama ni mfano kwani ameonyesha anafanya vitu kwa wito na sio shida

Kanunua kwa ajili ya chama au kwa ajili ya biashara? Ndesa ameshiriki kwenye maamuzi ya kutumia rasilimali za chama kwa faida zake za kibiashara, huu ni mgongano mkubwa wa kimaslahi ambao tunaupinga sikuzote.

(2)Dr Slaa alikuwa padre ambaye alishazoea kuishi maisha marahisi na ya wito hivyo hawezi kutapatapa..

Angekuwa hivyo, asingetoa sharti la kulipwa "mshahara mkubwa" wakati makatibu wa mikoa na wilaya hawapati ata posho, huu ni ubinafsi wa kiwangi kikubwa, hapa Dr.Slaa anajali zaidi maslahi yake binafsi na katu usijidanganye kuwa ni wito.

(3)Viongozi wa Chadema wana ongoza chama kibiashara hii inawezekana isionekane waziwazi. Zitto anafikiri kidemokrasia lakini kwenye kampuni hakuna demokrasia bali productivity. .

Kibiashara kwa faida ya nani? hili ndio tatizo kubwa zaidi kwa chama kinachopaswa kuwa cha siasa.
 
spencer

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
3,593
2,000
ZitTo- Ushauri wa Bure,
A wise person thinks before talking, a fool person talks then thinks.

"Think Grobally acT Locally"
 
Albedo

JF-Expert Member
Feb 24, 2008
5,559
1,195
Butola

Kanunua kwa ajili ya chama au kwa ajili ya biashara? Ndesa ameshiriki kwenye maamuzi ya kutumia rasilimali za chama kwa faida zake za kibiashara, huu ni mgongano mkubwa wa kimaslahi ambao tunaupinga sikuzote.
Kabla ya Kufikia hiyo Conclusion ni vyema ungetafuta jawabu la swali ulilouliza hapo la sivyo watu watakuona una chuki tu na ndesa, ni Angalizo tu mkuu maana huwa naheshimu sana michango yako

Angekuwa hivyo, asingetoa sharti la kulipwa "mshahara mkubwa" wakati makatibu wa mikoa na wilaya hawapati ata posho, huu ni ubinafsi wa kiwangi kikubwa, hapa Dr.Slaa anajali zaidi maslahi yake binafsi na katu usijidanganye kuwa ni wito
.

Mkuu ungeambiwa utoe huo Ushahidi wa Slaa kudai mshahara mkubwa ungeweza? Ongea vitu ambavyo vina mashiko ili ujitofautishe na mashabiki wengi hapa JF
 
Nyauba

JF-Expert Member
Jul 10, 2008
1,098
1,195
Ujumbe mzuri wenye maudhui ya uongozi unahitaji uvumilivu na usikivuu mkubwaa..akili ya kujua mambo sio kigezoo cha kuwa kiongozi mzuri.

Ni kweli CDM kimekuwa imara kutokana na misingi ya uongozi wake waanzilishi ambao kuwa na uwezo binafsi kiuchumi kumekifanya chama hiki kiwe imara bila kusukwasukwa kirahisi na CCM.

Zitto tafakari kwa kina ujumbe huu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom