Zitto hayuko tayari kuwa kiongozi!

Zitto hayuko tayari kuwa kiongozi!

Ujumbe umeeleweka lakini napingana na mtoa hoja sidhani kama issue ya kuwa kiongozi au mwenyekiti wa taasisi lazima uwe tajiri kwa hili sikubaliani naye hata kidogo. Inawezekana anamfaham Zitto kama alivyosema na sikatai kwa kuwa simfahamu zaidi ya kumuona bungeni au akijadiliwa hoja na tabia zake kama hivi jamvini. Unaweza ukawa sahihi katika hoja yako lakini si ki vile kama ulivyosema kuwa alitolewa Kigoma kwa hiyo atachekwa kwangu mimi hayo bwana Kamundu umeenda mbali zaidi ya kinachotakiwa kujadiliwa katika hii mada yako. Labda niulize nini malengo ya mada yako kumbomoa au kumjenga bwana Zitto? Kama vijana inabidi tuelimishane na kuelewa tunachotakiwa kukifanya. Ni kweli katika hatua za mwanzo kama hizi hatuwezi kuwa sahihi kwa kila kitu ndiyo maana tunahitaji mawazo chanya ya wazee na si kwamba hatuwezi fanya kitu kwa kuwa hatuna utajiri sikubaliani na wewe katika hili. Simtetei Zitto kwani amekosea kama mwanachama na kiongozi wa juu katika chama lakini si mtazamo wa chama kama CHADEMA kuwa lazima uwe tajir ndiyo uwe kiongozi au mwenyekiti, la hasha!!!!
 
Kanunua kwa ajili ya chama au kwa ajili ya biashara? Ndesa ameshiriki kwenye maamuzi ya kutumia rasilimali za chama kwa faida zake za kibiashara, huu ni mgongano mkubwa wa kimaslahi ambao tunaupinga sikuzote.



Angekuwa hivyo, asingetoa sharti la kulipwa "mshahara mkubwa" wakati makatibu wa mikoa na wilaya hawapati ata posho, huu ni ubinafsi wa kiwangi kikubwa, hapa Dr.Slaa anajali zaidi maslahi yake binafsi na katu usijidanganye kuwa ni wito.



Kibiashara kwa faida ya nani? hili ndio tatizo kubwa zaidi kwa chama kinachopaswa kuwa cha siasa.

Butola unaweza usielewe falsafa ya kuendesha chama au nchi kibiashara kwa sababu ya kuharibiwa kwa miaka mingi na CCM kuwa siasa ni maneno au propaganda. Siasa za kimaendeleo sasa hivi zinatafsiri kuwa siasa ni uchumi. Na uchumi huwezi kuujenga kama hutazingatia misingi ya biashara, yaani biashara inayotoa faida. Uzalishe sana lakini utumie kidogo. Hapa kwetu kwa kuwa CCM bado wana siasa za kizamani wameshindwa kuoanisha siasa na uchumi ndiyo maana wanaweza hata kutumia zaidi kuliko wanavyozalisha, na pia kufanya mambo mengi ambayo hawajiulizi kabla ya kufanya juu ya faida na hasara ya kufanya mambo hayo kiuchumi.

Kule Singapore waliendelea baada ya kumpata Rais mmoja (jina nimesahau) ambaye alikuwa ni mfanyabiashara na ambaye baada ya kuombwa awe Rais alieleza kuwa ataiendesha Singapore siyo kama nchi bali kama kampuni yenye tija. Matokeo yake ni hayo maendeleo ya Singapore ambayo ni miracle ya Dunia.

Tunahitaji viongozi wanaoweza kuiongoza Tanzania kama kampuni inayoleta tija, viongozi ambao katika kila wanalotenda kwanza wanajiuliza faida na hasara zake katika uchumi, siyo hawa ambao wanaiendesha Tanzania kama bwalo la starehe.
 
Ninaona nichukuwe muda huu kufafanua vizuri vitu vichache.

(1) Kwanza kibinafsi nampenda Zitto kuliko viongozi wengine wa Chadema. Hii sio unafiki bali ni ukweli na labda inasababishwa na ukweli kwamba mimi na Zitto ni watu wa rika moja na ninaona kama anaweka kuelewa vitu zaidi kuliko wazee.
(2) Kuhusu Kigoma: Sina maana mbaya kwa watu waliotokea Kigoma na kama kuna mtu ameona nimebagua naomba msamaha kwani nilikuwa sina nia mbaya. Kuna watu wengi wengi wanafahamu kwamba mtoto wa Kikwete alikuwa rafiki wa Zitto walipokuwa Chuo kikuu hivyo basi ingekuwa rahisi kwa Kikwete kumuamini Zitto wakati anaonyesha nia yake ya kugombea. Ukweli ni kwamba CCM na Kikwete hawakuamini kama kijana mdogo kama Zitto alivyokuwa angeweza kuwa mbunge!. Chadema walimuamini Zitto kuliko CCM ingawa Zitto hakusoma na mtoto wa kiongozi yeyote wa Chadema wala hakukuwa na urafiki wa aina yeyote bali waliona kipaji na walimuamini Zitto. Ukweli ni kwamba hata sasa hivi CCM haiwezi kumpa Kijana wa Kigoma ambae hana pesa nafasi ya kuwa mgombea wao. Serikali ya CCM imesahau Kigoma kwa miaka mingi na ilikuwa inacheka wabunge wa CCM zamani walipokuwa wanaomba barabara na miradi mingine ya maendeleo. Serikali imeanza kuamini Kigoma baada ya Chadema kushinda. Kuwaita waha wa Kigoma ndivyo CCM ilivyokuwa inasema kichinichini na mimi nimejaribu kuisema hadharani.
(3) Kuhusu wafanyabiashara wa kutokea Kigoma: Ni kweli kwamba hakuna wafanyabiashara na kama wapo ni wa chache. Mimi nilikuwa nataka kumuelewesha Zitto kwamba alisokuwa mwangalifu atabaki mwenyewe kwani hao CCM kwa miaka mingi hawakusaidia watu wa Kigoma na hakutakuwa na watu wengi mtaani wa kumsaidia pale atakapo anguka. Kigoma sio stable kwasasa na Zitto anatakiwa asaidie maendeleo badala ya kutangatanga. Movement ya maendeleo ya Kigoma haitapata mvuto kama utahama kwasababu hakuna watu wengi wenye nguvu za kiuchumi na kisiasa waliotokea huko. Kikitokea kitu Arusha, Kilimanaro, Mwanza au Mbeya utaona kinatangazwa kwasababu kuna wanasiasa na wafanyabiashara wengi wametokea huko! Mengi atatangaza kwenye TV, Mboe ataandika kwenye gazeti n.k. Zitto huna hiyo nguvu kwasasa na nina wasiwasi ukianza kutangatanga hao CCM ndiyo wa kwanza kukucheka. Zitto nyumbani Kigoma bado hakujatulia. Mboe mwenzako analami mpaka kijijini kwasababu lami ya mboe na mengi ni hiyohiyo.
Huu ni ukweli nilazima ujue uko nafasi gani ili uweze kuleta maendeleo kwa jamii yako.Usipigane hata simu moja kama unajua utashidwa na hauko tayari. Zitto ukiwa mvumilivu utashinda lakini kwasasa hauko tayari unahitaji muda kujua ni kitu gani unataka kufanya.
 
Zitto hajatulia na ana tamaa. Zitto anajiua kisiasa na imani ya watanzania kwake inapungua kwa kasi kubwa. Nitafurahi sana nikisikia amehama CHADEMA na kujiunga na CCM kwani naamini kuwa akifanya hivyo ataondoka moja kwa moja kwenye ulingo wa siasa na ndiyo furaha yetu kwani amelewa madaraka na ana tamaa na ni msaliti....
 
Yaani umekichana chadema live kabisa bila wewe kujua, umefikiri unajenga kumbe unamaliza kabisa

Chama chenye sera nzuri kinaongozwa na watu na michango ya watu, ni sawa na harusi hata kama una fedha nyingi bila watu kuchanga haifurahishi, maana haishirikikiki!! umenena live chadema ni cha wachache wafanyabiashara!!! wafanya bishara hawako tayari kwenda jela kwa ajili ya manufaa ya wananchi wako tayari kulinda fedha na status zao!

Hivi umefikiria ulichoandika maan naona umeeleza ukweli wa moyoni kitu ambacho chadema wengi huwa wanabisha na wewe live umeeleza ni wafanyabiashara, believe me, Ndesamburo na hao wengine lazima wanapata faida!!!how?? au wanajitolea tu lwa sababu wanakupenda sana!!!

Huyo slaa ni mroho wa hela na alihaidiwa mshahara fulani akikosa urais, unalijua hilo

Kuhusu Zito well, kuna mawali mengi BEING PROFESSOR AU ACADEMICIAN AS NOTHING TO DO WITH POLITICS!!! POLITICS IS NOT PROFESSIONAL FOR PARTICIPANTS; IS OPTION ONLY FOR POLITICAL SCIENTIST!!
Ndiyo maana kuna mainjinia akina Mwandosya, chemist Dr.Magufuli, n.k you can be politician still you can excell to your professional , hapa inahitaji akili kidogo tu, na siamini kabisa kuwa una umri huo. Dr.Magufuli amepata masters na PhD akiwa kiongozi/mwanasiasa (record this)

Umeweka vijembe eti hakuna mfanyabiashara mkubwa Mha!!! yaani umeleta ukabila live ule tunaopigana nao humu!!! ar you sure

FYI Zito ameingia chadema akiwa na miaka 16!!! na amepokelewa na hao unaowasema na leo hii wamempa unabibu katibu mkuu!! japo unafikiri unawasemea akina Slaa ila wengi wanakushangaa lengo la hii post ni nini?? wapi umemkamata amefanya kosa gani (with evidence) na maoni yako ya kutokuwa na imani naye yanapingana na maoni ya kamati kuu ya chadema akiwamo meti na ndesamburo!!

By the way unasoma chuo gani huko marekani? maan paragraph hamna I mean post yako haivutii kabisa

Hapo kwenye blue unaweza fafanua kidogo? Nijauvyo mimi vyama vingi vilianza Tanzania mwaka 1992 ni vigumu (??) kwa Zitto kuingia CHADEMA akiwa na umri huo.
Being a politician and excel in profession???? Hard to imagine
 
classic mawazo ya 2010 je yalifuatwa na sasa tuko wapi?
 
classic mawazo ya 2010 je yalifuatwa na sasa tuko wapi?
Kamundu unachosema kinaakisi uhalisia.
Tatizo la baadhi ya wanajukwaa wameligeuza kuwa sehemu ya propaganda ambazo nyingi haziakisi uhalisia bali ni sehemu ya kutetea maslahi binafsi, chama, et all na kamwe hawafikirii critically with an open mind.
Nijuavyo mawazo na fikra zitokazo kwa mchangiaji asiyeegemea upande wowote baada ya kusoma historia na wakati uliopo basi kupata picha ya mbele ni rahisi. Ndio maana leo bado tunatumia principal hata zenye zaidi ya miaka 300 iliyopita, na kama zina marekebisho basi ni machache.
Ulichokisema kuhusu ZZK binafsi naona bado yuko katikati, huko aendako kama hatoacha tamaa na kuridhika na hali yake ya kiuchumi atazidi kupotea zaidi kisiasa. Pia hata akawa academician kwa upopo huu atakuwa ni academician asiye na credibilite, kitu ambacho ni kibaya zaidi kwa anayeelewa na atakuwa hana tofauti na mtu mwingine yeyote asiye na elimu.
 
natn zaid ya chuki.

mleta mada ni mbaguzi xana, mkabila nahisi utakuwa mdini wakutupwa, naona muha muha muha wa kigoma,

huu c ubaguzi na dhihaka hz? ulikuwa una hoja nzuri ila niseme tu hujui unachokiandika. na kama unalipwa kuxema haya

yote kamwambie bosi wako umeshindwa.

leta hoja na ushahidi co kujadili mtu na kabila lake hapa.

only middle mind can discuss this.
 
Basi mtoa post hamjui vizuri zito. Zito ni zaidi ya wenye akili zako 100. Zito ana mambo mengi ya kitaifa. Unataka akujibu wewe aache wajibu. Kwanza ulishaongea naye, ulitaka nini tena.
 
Basi mtoa post hamjui vizuri zito. Zito ni zaidi ya wenye akili zako 100. Zito ana mambo mengi ya kitaifa. Unataka akujibu wewe aache wajibu. Kwanza ulishaongea naye, ulitaka nini tena.

Mtoa post hii ni rofa fulani! Kwa nini unajifananisha na ZZK? Huu ni moto wa kuotea mbali sana - jaribu usome au usikilize statements zake ulinganishe na utumbo wako huo uone havifanani kabisa! Hta hivyo hawezi kusimama na akina mbowe wako chini sawa na binadamu asimamapo na sisimizi!

ZZK, Mnyika na January Makamba ni wawakilishi wazuri wa kundi la vijana!
 
Basi mtoa post hamjui vizuri zito. Zito ni zaidi ya wenye akili zako 100. Zito ana mambo mengi ya kitaifa. Unataka akujibu wewe aache wajibu. Kwanza ulishaongea naye, ulitaka nini tena.

Zitto hana lolote jipya zaidi ya kupiga kelele ili mafisadi ya ccm yamnunue.Rejea inshu ya Buzwagi alivyozimishwa kwa kuhongwa na hili la mabilioni ya Uswis!
 
hili pia ni somo zuri kwake....kuna mwana JF alilitoa juzi juzi.

SOMA KISA HIKI CHA MWANAPUNDA ALIYEMBEBA YESU

Leo katika kujifunza zaiidi nilikuwa nasoma Biblia takatifu,katika kusomasoma nikasoma kisa cha Punda aliyembeba yesu wakati anaingia Yerusalem,punda alishangazwa na aina ya mapokezi aliyoyapata,watu wengi walijitokeza barabarani kumlaki,walimwimbia kila nyimbo,wakamwagia kila sifa na mwishowe wakamtandikia nguo chini ili apite juu ya kanga zile.maandiko yanasema Punda yule alivimba kichwa na kujiona yeye ndo yeye,kwamba yeye ndo mfalme,kwamba anakubarika sana,asijue kumbe nderemo na vifijo vyote vile vilitokana na yule aliyekuwa amembeba ambaye alikuwa ni Yesu.

Unaambiwa siku aliyoamua kutembea peke yake na kurudi mji ule tena kwa kupitia njia ileile,alistaajabu kuona watu wanampita kama hawamwoni hata pale alipotembea kwa mikogo na mbwembwe,kuona hivyo akataka kuingia kwenye lile hekalu aliloingia wakati amembeba Yesu anaambiwa alichezea kichapo cha haja,akatandikwa bakora za kutosha akatimua mbio huku akijiuliza nini chanzo?
 
huu ujumbe ni murua kwake kama atasoma na kuzingatia na kwa wengine wanaopenda sana sifa kuliko kutenda jambo

mkuu umefanya jambo la mbolea hapa
 
Haya ni mawazo yangu binafsi cha kushangaza pamoja na madongo Zitto mwenyewe ananiomba mimi mawazo na nilimpa mawazo miaka michache nyuma kuhusu biashara ya mafuta. Hao wanaosema ni moto wa kuotea mbali ndiyo wanaompoteza hamjui mambo kiundani siasa sio ushabiki pekee. Zitto alikuwa anataka mwongozo wakati nilipoandika hii topiki mwaka 2010 lakini hajafuata ushauri wangu wa kutulia.
 
Siasa bwana! Sikuwahi kuwaza kuwa Zito atakuja kupoteza reputation yake kiasi hiki! Nikijiuliza sana juu ya kuanguka kwa zito huwa sipati majibu kosa ni la nani? Jamaa siasa zake kutakuwa na sehemu alizikosea aisee. Inaniuma sana huyu jamaa hali yake kwa sasa.
 
Zito ni 97% yes. Namfahamu since akiwa katibu wa chuo Udsm. Ni kiongozi mzuri.
 
Back
Top Bottom