SHIGELLA
Member
- Jun 17, 2011
- 63
- 6
Hata kama anapendwa na wananchi wengi isiwe ndo njia ya kukisaliti chama, hata hao unaowaona kina magufuli, mwakyembe wanashine kwa sababu wako ndani ya chama na hawakisaliti. Ukisaliti chama na kutolewa huwezi tena kushine. Kama mnabisha wajaribu kujiunga na vyama vingine mwone kama watashine kama walivyo sasa. Uzuri wa Chadema wako well-informed na kwa kutolewa kwa Zitto kwenye uongozi haiwezi kuifanya chama kutetereka, watu watapiga kelele na baada ya siku mbili watanyamaza na chama kinaendelea. Tunatakiwa kujenga taasisi si kujenga jina la mtu. Nawashukuru sana CDM kwa kujitahidi kujenga taasisi badala ya watu binafsi. Hata CCM wao wamejitahidi sana kujenga taasisi si majina ya watu. Kama wewe unadhani kwamba unakubalika sana na watu si utoke ukaunde chama chako na hao watu watakufuata huko huko, Kwa nini ung'ang'anie sehemu moja?
Kitu ambacho mimi nasisitiza ni kwamba vyama vya kisiasa na serikali kwa ujumla vijenge taasisi imara na si watu maana watu hawa wanakuja na kupita. Kwa mfano serikali yetu ikiweza kujenga taasisi imara basi tutakuwa tumeshinda maana hatutategemea watu ndo binafsi ndo watuletee maendeleo. Watanzania tunategemea watu binafsi kuleta maendeleo. Mathalani kwa kuwa Tanesco haikujengwa kuwa imara basi hata awe nani kiongozi pale hawezi kufanya mabadiko.
Kuwaondo wenye mawazo tofauti na mabos zenu..eti kuimarisha taasisi/chama..eti usaliti..unaushahidi? yakuambiwa changanya na yako!
Mchango wa zzk kwa taifa hili na kwa chama chake ni wa kiwango cha kupigiwa mifano, badala yakumtia moyo au kujifunza na kufanya vizuri zaidi yake.. wengi wenu inawauma kwa wivu wa kijinga.....!Acheni porojo, majungu na unafiki!
Propaganda na Ushabiki wakujipendekeza upande wa wenye madaraka/fedha hauta wapeleka kokote kisiasa!