Zitto ataja mawaziri mizigo

Zitto ataja mawaziri mizigo

Huyu mama hakuna lolote, ardhi ni shida sana kwa sasa nadhani wao ndiyo wanataka wamiliki kila sehemu especially maeneo yaliyopimwa.
Ardhi ni shida sana kwa watu kama sisi wa kawaida

Mama yaani Prof. hana tatizo, tatizo ni ukoo aliomo a.k.a ukoo wa panya, kila mmoja ni mwizi, hutaki kuiba kubaliana na wezi hutaki achia ngazi sasa hapo kuachia ngazi ndo huo utamaduni hatunao, Ma Anna tafadhali njoo uwajibu hawa wana nzengo, wengi ni wapiga kura wako!!!!
 
Ukinionesha tusi moja nitaomba samahani, vinginevyo lugha za kupamba wakati mapungufu na uhamna/emptiness ni mkubwa. Kama planning authorities ni Halmshauri je wewe wizara unafanya nini??? mimi ninaongelea kuweka sera na sheria za nchi zinazompatia kila mtanzania nafasi ya kupata fursa ya kuwa na kiwanja na hivyo makazi bora. Nchi ni yetu ardhi ni yetu kwa nini iwe aghali kwa mtanzania??? almost 95% hawawezi kununua ardhi/kiwanja-kama 80% wako vijijini hiyo 15% wako mjini na ni wapangaji wa kudumu. Labda 5% tu ndo nyinyi wenye majengo makubwa kama mahekalu. Waliojenga wengi mafisadi na wezi wa mali za umma, ukweli ni hawajakamatwa tu, wengine ni wale waliopata urithi kutoka kwa wazazi wao miaka mingi iliyopita. HOJA ZANGU Halmaushari zimekosa sera kutoka wizarani ya kutekeleza, wanajirusha kadri wanavyoweza, unakopa kupima viwanja kila mwaka tunalipa kodi zinaenda wapi??? mtu unalipa kodi zaidi ya milioni moja kila mwezi PAYE lakni hakuna huduma??? kila huduma unalipia MAJI, HOSPITALI, UMEME unadaiwa mita, nguzo ikibidi nyaya, ARDHI bei juu, MAHAKAMA, ELIMU, BARABARA road license, ZIMAMOTO etc hii ni mifano tu, kweli aibu. Ujanja ujanja mwingi mnatuingiza kwemye gharama kubwa, kule vijijini kiwanja wanapima heka moja miguu sabini kwa sabini, mbona viwanja winakuwepo, hapa kupima kwa GPS kweli TZS 8000/- kwa mita square moja???? kwa lipi hapo waziri??? kama technolojia ni gharama na hairahisishi kazi (maana hata hivyo viwanja havipatikani) basi haitufai, wanaikumbatia maana ni chanzo cha rushwa wanazozihitaji. Kosa lako ni kushindwa kuona hayo, NCHI YETU TUNAHITAJI VIWANJA VIPATIKANE SIO KWA KUOMBAOMBA NI HAKI YETU. Makudu yanapima viwanja vijijini na maisha yanakwenda. Teknolojia aghali kiasi wanaohitaji kuitumia hawana uwezo wa kuimudu haihitaji uwe profesa wa kweli kujua etknolojia hiyo haina tija kwa wananchi.
 
1. Ulanguzi wa viwanja umepigana nao vipi? is it fair watu wana-aply hawapati wanaopata wanakuwa wale wale maofisa wagawaji viwanja harafu wanawalangua wananchi, je hufahamu hili??? kama hufahamu basi serikali imepoteza maana ya kuwa serikali. 2. Dhibiti bei za viwanja za halmashauri njia mbadala zipo sio kila kitu benki na kuwatumbukiza wananchi kwenye gharama kubwa 3. Komesha viwanja vidogo vidogo mpaka maana inaisha 40x40 could be ideal kwa makazi hili unajua, maana wewe umejenga kwenye nafasi kubwa. 4 hata kama umepata kiharali viwanja sio biashara mtu ajilimbikizie harafu aanze kuuza kwa bei mara 10 ya bei halali, hayupo aliyelima na kuvuna ardhi wote tumezaliwa na kuitakuwa ni yetu, kutumia fursa kirafi na kuwanyima wengine fursa ni ufisadi upigwe vita na WAZIRI
 
Kwa kweli ameshindwa, nimesubiri kuona cheche lkn siku zinakwenda tuu, mafisadi wanaendelea tu kuuza na kujimilikisha ardhi yetu tukufu.
 
There is something Mama Tibaijuka must do to serve her office.Ardhi crisis and disputes are now song of the day.
 
To my side mimi nina na Matumaini makubwa sana juu yake.ila naona hapo ardhi matatizo ndo yamekuwa mingi.si umeona katibu mkuu wake aliamua kustaafu yaishe??
Anyways back to the topic
-Migogoro ya ardhi.
-watendaji wake wanaojimilikisha viwanja kila kona wanavizia hali ikiwa shwari wanaviuza kwa bei mara kumi.
-kwenye hotuba yake ya budget alidai wizara haina program ya kupima ardhi...je ni kweli? Au watu wamekalia mavyeo hawataki mabadiliko au kufundishwa???
Maana kuna vijana wazuri wa IT hapa tz wanaweza kuifanya hyo kazi tukapata mfumo mzuri tu..tena unaosyncronise between TRA,city,postal codes zake,na service zingine....
We need changes kwa kweli.serious on and not politics..

hapa tunapoongea na kuandika nina software tatu za kupima arthi kwa kutumia setellite, inafanya propertiy value, property management, Inatumia GIS na GPS, inatumia book map ambayo unaweza kuona hata picha ya mmiliki wa kiwanja na physcal address yake, inaonyesha kama analipa kodi zote, na kutathimini kila baada ya mwaka mmoja, hapa kusingekuwepo utapeli pamoja na gharama za kucheck unapotaka kukopa aua kuamisha bicon , kwa wale wajanja wa kujiongezea viwanja, kila kiwanja kinakuwa na barcode, hivyo na TRA hawana tabu ya kufuatana ni kubovya tu.
 
Kama ukiritimba wa mifumo ya serikali umekufanya ushindwe kutoa huduma kwa wananchi, kauli yako hapo juu "Waziri wa Ardhi anatenda kazi kwa mujibu wa sheria zilizopo. Hakurupuki. Hana mamlaka ya ki-imla unayoonekana kudhani anayo!" Wewe kama msomi na waziri ungeendesha mapambano ya kiuongozi kufuta ukiritimba na mifumo mibovu kwa faida ya umma. Kama kila waziri atakaa kimya juu ya mifumo mibovu, nani atairekebisha na nani atainufaisha jamii na lini? Waziri sio yes man popote kila wakati, wala sidhani rais alimanisha waziri aende kutekeleza yale tu yaliyopo tayari kwenye sheria na vitabu vya serikali bali anapaswa pima ku-review utaratibu mzima, mifumo na kutoa mapendekezo mapya kwa ajili ya kuboresha mifumo yetu, kuleta mbinu mpya na kuingiza mazingira halisi ya wakati husika. Hakuna suala la wishful thinking, we need you either to work on issues pertaining to land and land ownership, land management, and policies etc or resign to create space for another Tanzanian occupy the post for sole purpose of improving our living standards through affordable and quality sheltering for all.
 
Ukweli kuwa wabovu ni wengi sana ndo maana baadhi yetu tunashindwa kujua yupi ni mbovu kuliko wote, huyu prof nakumbuka nimewahi kumukuta gigiri pale Nairobi nikazani mpiga kazi,leo amezima kama kwamba alikuwa anabahatisha, au kulikuwa na jembe linalomfanyia kazi huko UN habitat, sasa anaiacha wizara na business as usual, hakuna tija kwa wananchi, hakuna sera ya ardhi ambayo mzawa angenufaika nayo, muda unakwenda. Mtalaamu anasema tunachuki, tunalalamika tu, tukasome, mimwabie tu tumesoma sana, na sio lazima wakaswa fursa tue sisi wenyewe mmoja mmoja waandishi wa mambo haya, ni watanzania kwa ujumla wao. YAANI HALI MBAYA KWA WATANZANIA HATA KAMA MIMI NIKO FIT VIPI SIO KITU CHA KUKALIA KIMYA, MAANA AMANI YAO AMANI YANGU, utapata wapia amani huna hata uwanja wa 40 kwa 40, unapanga kisa kiwanja hakipatikani ndani ya nchi yako, kikipatikana anaweza nunua ni mtu mkubwa tu wakati aslimi 95% ya watz ni watu wa kawaida wa hivi hivi tu kwa maneno ya mwalimu Nyerere.
 
Jimboni kimenuka,yuko huku anazunguka na loli la masufuria ya pilau ili hawashawishi watu waje kwenye mikutano yake.CHEZEA PROF. WEWE.
 
ukisema ukweli huo, utaambiwa unatoa matusi, ndo imekuwa fashion kuwapa watu pilau maprof wanafurahia sana.
 
Kweli hakuna mabadiliko, natafuta Hati mililiki ya kiwanja kwa ajili ya uwekezaji kule Kilwa, tangu aingie madarakani hadi leo, miaka mitatu tunaingia wa nne, sijapata.Nadhani wafanyakazi wa wizara hiyo wana utaalamu mkubwa wa mashairi/ngonjera, maana kila ukifuatilia majibu ni mistari mipya unaimbiwa!,Pesa nimetoa hadi nachanganyikiwa, sijui la kusema tena, nimekata tamaa, nimeacha tu watoe siku watakapotaka wao, ila uwekezaji nao unachelewa-hii ni kasi ya kale; si mpya tena!
 
huyu mtoa mada anatoka kigamboni nini? ana hasira kweli, madudu haya aliyoyasema yameshamiri huko!
 
Suala la ardhi limeangamizwa na rushwa.Namshauri waziri amuombe Rais aweke agenda ya ardhi katika kikao kijacho cha baraza la mawaziri,ili azimio liandaliwe mahsusi kuhamisha mamlaka kutoka serikali za mitaa na kurejeshwa serikali kuu.Na maamuzi yote ya ugawaji wa ardhi yasimame mara moja ili iandaliwe policy itakayo elekeza nguvu zake kwenye equity,transparency ,integrity na accountability.Hapa tuna tatizo la ardhi kwa wafugaji na wakulima,ardhi kwa ajili ya makazi,ardhi kwa ajili ya uwekezaji mkubwa ,wa kati na mdogo pamoja na ardhi kwa ajili ya uhifadhi wa mazingira na Mali ya asili.Tumesomesha watanzania wengi sana hapo Chuo cha ardhi na wengine wapo vyuoni hadi hivi Sasa.Ina maana wote hao hakuna kitu kichwani hadi tufikie hapa tulipo Sasa?Ushauri wangu tena,serikali iandae kongamano kubwa pale ardhi university,tupate mawazo ya watanzania wengi,yafanyike kazi mara moja katika kuandaa policy yenye muelekeo niliotaja hapo mwana..Nawasilisha.
 
Wa kuu mm namwamini huyu mama pia hoja ya mleta uzi ni nzuri hivyo tumtake aifanyie kazi.
Tatizo kubwa la nchi hii ni mfumo kuparaganyika na mfumo huu bila kubadilishwa hata uteuliwe ww utakukwama tu.

Mfano waziri wa mambo ya ndani ya nchi,hata uteuliwe ww utakwama tu bila ku overhall kwanza mfumo na sheria za kikoloni za polisi.
 
Matatizo yapo tena ya msingi, lakini inawezekana unayaaddress sehemu isiyo husika. Swala la bei kwa mjini haliwezi kuepukika. Kwa mfano sheria inakutaka udevelop eneo lako ndani ya miezi 36. Sasa kama utashindwa kununua kiwanja kwa milioni 2 hivi kweli wewe unaweza kujenga ndani ya miezi 36? Tatizo la ulanguzi wa viwanja nadhani tukianza kutumia teknolojia ya Land Information Systems tutaweza kubaini kirahisi nani anahujumu. Mimi nadhani tutumie muda mwingi kutafuta suluhisho la tatizo na sio kulalamika.
 
Hili suala kweli hatuliachii watu waendelee kuwa wageni nyumbani kwao, haiwezekani, waziri aje na majibu ya manufaa kwa jamii, aje na mipango ya kurekebisha miundo mibovu ardhi haiwezi kuwa biashara za watu wachache, ardhi ndo urithi wa pekee wa kuzaliwa, yaani huwezi kumuondelea mtz utanzania wake wa kuzaliwa hata akiuza nchi au ua watu wote, tunataka viwanja kwa kila mtz aliye over 25yrs. Iwe ni mkakati wa serikali kumpatia kiwanja japo kimoja cha 40x40, inawezekana. sio tunazaliwa tunalipa kodi mpaka tunakufa hakuna faida ya kodi zetu ukiacha kulipa mishahara ya wakubwa, yaani nilipe kodi umri wangu wote kukulisha tu waziri na familia yako, na mawaziri wenzako HAPANA LAZIMA UTUFANYIE KAZI NA UTUWEZESHE KUPATA MAKAZI BORA.
 
Back
Top Bottom