FIKIRIKWANZA Nilitegemea michango yako ingefanana fanana na NICKNAME yako lakini kumbe ni tofauti kabisa!. Pole. Bora ungelikuwa Verified User nikakufahamu kama unavyonifahamu na mimi ningelipata nafasi ya kukutathmini katika elimu na utendaji wako pale ulipo! Nakutoa maksi? Labda na mimi ningelijikuta ninamshauri mwajiri wako kutafuta mtu mwingine! Unajua mkuki kwa nguruwe, kwa mwanadamu mchungu! Hasira na chuki zitakutafuna, utabaki kutukana, hatimaye kukosa amani, kukata tamaa na maisha. Kila mtu utamwona mbaya, mjinga, fisadi, nkd. Utashindwa kujielimisha kwa kukata tamaa! Sasa nikusaidie kama ifuatavyo: Waziri wa Ardhi anatenda kazi kwa mujibu wa sheria zilizopo. Hakurupuki. Hana mamlaka ya ki-imla unayoonekana kudhani anayo! Usimamizi wa mipango miji, na maafisa ARDHI wote wapo chini ya Himaya ya TAMISEMI, Halmashauri ndizo Planning Authorities. Uliyosema mengi, kama vile kutopanga viwanja chini ya sqm400 (20X20) tayari Halmashauri zimeelekezwa kuzingatia ila wengine wanaweza kuwa hawatekelezi! Hapo wanakiuka mipango na jukumu la wananchi ni kuwa macho na kutujulisha. Viwanja ni aghali kwa sababu bajeti ya serikali haitoshi kuvipima, Halmashauri zinakopa benki kupima, na riba ziko juu! Wanarejesha mikopo kwa kuuza viwanja. Waziri na hata mamlaka za juu huwezi kuwaingilia bila kuwa na RUZUKU ya kuwapa! Kama wewe ni kijana nikusihi usikate tamaa na kufikiri kwanza utukane, tena watu wazima! Utajipotezea muda kwa sababu pamoja na mapungufu niliyonayo mimi naona nimeweza tena sana!. You cannot take that away from me! Ni wishful thinking! Jenga hoja. Dai haki yako kwa heshima na kujiamini ( ujitambulishe rasmi) nikusaidie? Mama T