Zitto apendekeza Dowans itaifishwe; Serikali yapinga! Mgao waendelea...

Very good comments na observation. Bravo Zitto.
Nakubaliana naye 100% kwenye issue ya IPTL kwa kuwa tuko kwenye CRISIS na ukizingatia tunacholose it is better tu-run IPTL at any cost kulinganisha na harasa zinazolikumba taifa kama alivyo comment.

Issue ya kutaifisha dowans iko wazi kabisa, na ilishajadiliwa hapa, nashangaa ni kwa nini serikali haichukui haya maamuzi haraka iwezekanavyo. Sijui wanasubiri nini.

Kuna wakati Daudi(kabla hajawa mfalme) na kundi lake walikuwa wanamkimbia mfalme Saulo wa Israel asiwaue nao wakaishiwa chakula. Zama hizo ilkuwa marafuku kabisa kula mikate iliyokuwa imetoewa madhabauni isipokuwa kwa makuhani tu.

Daudi na wenzake wakamwendea kuhani ni kumwambia awape mikate ile wale hata kama ni marufuku kuila wao. Kuhani akawapa ile mikate wakala wakapona njaa na kusonga mbele na safari yao.

IPTL na Dowans ni kama "mikate" ya madhabauni inayokatazwa kuliwa. Lakini watanzania tuna njaa ya umeme vibaya sana. Tumwambie "kuhani" kwamba sasa ni ruksa kuila ile "mikate" ili tupone. Kama asemavyo Kabwe "Desparate situations call for desparate measures". Kudos brother Kabwe.
 
Very good comments na observation. Bravo Zitto.
Nakubaliana naye 100% kwenye issue ya IPTL kwa kuwa tuko kwenye CRISIS na ukizingatia tunacholose it is better tu-run IPTL at any cost kulinganisha na harasa zinazolikumba taifa kama alivyo comment.

Issue ya kutaifisha dowans iko wazi kabisa, na ilishajadiliwa hapa, nashangaa ni kwa nini serikali haichukui haya maamuzi haraka iwezekanavyo. Sijui wanasubiri nini.
Nani wakutaifisha? unaweza kujitaifisha mwenyewe? Huwezi kukata mkoni unaokulisha wakati wewe huna mkono bana.

Kama tusipolipa umeme wanakata kwa mbwembwe, kwa nini wasipotupa umeme huo kwa kisingizio cha mgao tusigome kulipa then wakate kwa watu wote basi, after all hatupati huo umeme wenyewe/
 
......... Pia kumekuwa na shutma mbalimbali, mojawapo ikidai kuwa baadhi ya watendaji wa TANESCO wanajaribu kuthibitisha madai yao ya kitaalumu ya kununua mitambo ya DOWANS. Shutma kama hizi, ni dhahiri zinauelewa finyu juu ya vyanzo vya mgao wa umeme uliopo sasa, ambao unasababishwa na uhaba wa mashine na upungufu wa maji. Uelewa huu finyu si tu hauna manufaa, bali hautoi ufumbuzi juu ya tatizo lililopo sasa ili kuepuka madhara ya kiuchumi kwa taifa na wananchi wake.

.............. Wakati Taifa linakabiliwa na upungufu wa 90MW za umeme, na uchumi wa kila mtanzania unaathirika, hapa nchini tuna mitambo ya IPTL yenye uwezo wa kuzalisha 100MW, ambayo imezimwa kwa sababu ‘eti' ina kesi dhidi ya serikali. Majadiliano kuhusu mgogoro huu bado yanaendelea bila kwisha. Hapa nchini tuna mitambo ya Dowans yenye uwezo wa kuzalisha 125MW, ambayo ni ya kuwasha tu. Lakini kwasababu tu serikali imeshindwa kufikia maamuzi, inaendelea kuwepo nchini huku Taifa linayumba kwa giza. ......

•Kwa kuwa mapendekezo ya TANESCO ya kununua mitambo ya kampuni ya Dowans yalipingwa na baadhi ya wanasiasa wenzangu na hatimaye kutonunuliwa na hivyo kusababisha mgawo uliopo hivi sasa, na kwa kuwa mitambo ile inaweza kuingiza 125MW katika gridi ndani ya siku moja na kumaliza kabisa mgawo uliopo hivi sasa na kuliokoa Taifa na kuhami uchumi wetu,
na kwa kuwa mitambo ya Dowans inahusishwa na mkataba wa kifisadi wa Richmond, ninaishauri serikali itaifishe mara moja kampuni ya Dowans.........


Mazingira magumu kama haya yanahitaji maamuzi magumu (extra ordinary circumstances require extra ordinary decisions). Ninaamini serikali itazingatia ushauri wangu.

Asante sana.

KABWE ZUBERI ZITTO,MB
Dar es Salaam.


Patamu hapo. Hatukukubali kununua nguo chakavu kwa pesa yetu inayowezanunua nguo mpya kabisa, tena kwa muuzaji tapeli.

Kutaifisha sawa, kama hawataki kuondoa uchafu wao, au sivyo waanze kulipia nafasi wanayotumia kutunza marapurapu yao DOWANS. Swala la kununua pia ua halikubaliki kwa sababu inaashiria kuna watu wenzetu kabisa wanataka kunufaika kwa kuikalia migongo yetu. Kuna ubaya gani kwenda dukani kununua mipya ila wanakaa na pesa ambayo thamani yake huko walikoficha inaendelea kushuka?

Leka
 
•Serikali ihakikishe mitambo ya IPTL inawashwa mara moja wakati mazungumzo yake na IPTL yakiendelea kwa kuharakishwa (fast tracking). Hali ya nchi ni mbaya, ni sawa na vita, haiwezekani serikali yenye mamlaka ishindwe kuhakikisha IPTL inazalisha umeme wakati mazungumzo yakiendelea. Haiwezekani.Labda kama haina uchungu na maisha ya watu wake.

Hii nimeandika tu jana kuwa kama wangelikuwa wanania njema, wangelitangaza hali ya hatari na wakanunua moja kwa moja kwa watengenezaji mitambo mipya. Swala la Maji, Umeme ni kama kama VITA. SI vitu vya kufanyia ufisadi.

Kama kila kitu kingelifanyika kwa UWAZI na hata data kuwekwa kwenye Internet kwa kila mtu kuona, hakuna mtu angelilaani na kusema kweli hata kama tungelikula nyasi, basi si vibaya ila hili swala kulisolve.

Tatizo anapokuja mtu badala ya kusolve anakaa na kufikiri na yeye afaidike vipi kwenye hii shida. Sintashangaa sana kuwa wao ndiyo wanaouza sasa generator ili watu wawashe majumbani kwao..... bruuuuuuuuuuuu...........
 
Hapa cha kuongea ilikuwa kwa nini serikali na Tanesco hawajafanya juhudi za kununua mitambo mingine toka ile ya Richmond ilipokataliwa, tena toka kwa reputable manufacturer's leo hii tusingekuwa hapa, hilo la kutaifisha linaweza kuonekana sawa, lakini process iliyo bora na more diplomatic ni kufungua kesi au kesi ingekuwa imeishaamuliwa dhidi ya wahusika na kuhukumiwa na mahakama na mahakama kumfidia aliye umia kwa kumpa hiyo mitambo au baada ya hapo ndipo serikali ingetaifisha, lakini mpaka leo hii utashi huo au nia hiyo inaonekana haipo na ndio maana report ya richmond au maamuzi yake haya tekelezwa na serikali.

Huo wa IPTL ukishakuwa na mgogoro na mtu hasa wa pricing huwezi sema nipe for three day kwa hiyo bei yako ambayo wewe unaiipinga, walipoingia mgogoro huo ilikuwa ni kuamua kuachana nao na kuleta mwingine, haya yanayo fanyika ni hatua zinazopangwa na mafisadi kutafuta kuiibiwa serikali/wananchi wa tanzania kwa kutumia haya matatizo, maaana miradi yote ya umeme ndi wao wanayo imiliki na bei ni wao wanayo ipangilia, iwe IPTL, iwe Kiwira etc.

Nasikitika Mbunge mtoa mada kwanini hatuelezi serikali/Tanesco wamefanya nini toka wananchi na kamati ya shelukindo na baadae serikali walipo sema hawata-nunua mitambo ta dowans walifanya nini ili kuzuiawa jambo hili kutokea tena, aidha kuwa na 100mw za dharura endapo hale au pangani mitambo inpo haribika.

Haramu itaendelea kuwa haramu, sijawahi sikia haramu kwenye hali fulani inakuwa halali, labda kwenye ule msemo wa "msafiri kafiri" kwa Sababu Allah, asingependa kukuona unakufa. lakini hili la umeme tena unaliona mapema kabisa halafu huchukui hatua zozote, dakika za lala salama ndio unaamka na kusema hivi mitambo si ipo.

Kweli Tanzania tumekosa viongozi.
 
Mkuu heshima mbele,
Hivi wewe unaelewaje haya maneno EMERGENCY or CRISIS?
Hiyo mitambo mipya unayoongelea itakuja baada ya siku moja au wiki moja??? Jamani hivi tunaelewa sasa tuko kwenye hali mbaya sana kutokana na kukosa umeme. Sio wakati wa kusubiri plan ni wakati wa kufanya maamuzi ya haraka na machungu basi.
This is what we call state of emergency...

And this is exactly what they wanted to happen, watu wawe desparate ili wapate urahisi wa ya kununua mitambo hiyo ya Dowans. Kama unakumbukumbu nzuri this was also what produced Ze Richmond Saga. Emergency and Crisis!
 
Kuna wakati Daudi(kabla hajawa mfalme) na kundi lake walikuwa wanamkimbia mfalme Saulo wa Israel asiwaue nao wakaishiwa chakula. Zama hizo ilkuwa marafuku kabisa kula mikate iliyokuwa imetoewa madhabauni isipokuwa kwa makuhani tu.

Daudi na wenzake wakamwendea kuhani ni kumwambia awape mikate ile wale hata kama ni marufuku kuila wao. Kuhani akawapa ile mikate wakala wakapona njaa na kusonga mbele na safari yao.

IPTL na Dowans ni kama "mikate" ya madhabauni inayokatazwa kuliwa. Lakini watanzania tuna njaa ya umeme vibaya sana. Tumwambie "kuhani" kwamba sasa ni ruksa kuila ile "mikate" ili tupone. Kama asemavyo Kabwe "Desparate situations call for desparate measures". Kudos brother Kabwe.

Wewe ni Mwaimu mzuri sana. Hongera sana Mkuu. Labda the way ulivyoiweka watu wanaweza kuelewa what it means by crisis situation.
 
Mwaka jana au juzi kama sikosei, JK alisema hakuna madhara yeyote ya kiuchumi yalitokana na mgao wa umeme kwa kipindi hicho.

What make you think that he will treat this one differently?

hivi we na akili zako unakaa unamsikiliza kikwete na ngonjera zake..hakuna kitu hapo.mbona vingi tu kasema na hakuna kilichotimia na yeye anaona poa tu
 
Kuna haja pia kuziangalia Kamati hizi za Bunge ili kujua majukumu kila kamati, mipaka yake ya kazi na ipi isikilizwe kunapotokea mkanganyiko kama huu. Hapa zipo kamati mbili zilizoichanganya Serikali na TANESCO pia. Kuna Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini inayoongozwa na Mzee Shelukindo na Mh Mwakyembe akiwemo na ile ya Mashirika ya Umma inayoongozwa Mh Zitto. Ni ipi kati hizi ina mamlaka na ushawishi kwa TANESCO?

Naungana na wewe,

Mh. Zitto angeongea haya tokea mwanzo bila kuvutana nadhani tungeshasonga mbele zaidi ya hapa. Ndo sasa amepata jibu. Kamati ya Madini hivi vyote ilishavitolea maamuzi tokea awali.
 
And this is exactly what they wanted to happen, watu wawe desparate ili wapate urahisi wa ya kununua mitambo hiyo ya Dowans. Kama unakumbukumbu nzuri this was also what produced Ze Richmond Saga. Emergency and Crisis!

Acha siasa, nini kifanyike sasa hivi, kuna watu wanakufa mahospitalini!

Tuingine mtaani,msituni, TUFANYE NINI??

Hivi ubishi huu unasaidia nini eti??

desperate...m nini, nini....sijui....

what is the solution now???
 
And this is exactly what they wanted to happen, watu wawe desparate ili wapate urahisi wa ya kununua mitambo hiyo ya Dowans. Kama unakumbukumbu nzuri this was also what produced Ze Richmond Saga. Emergency and Crisis!

Hapa ndipo Zitto anaposisitiza tuache Malumbano ya kipuuzi. The issue in hand tunapata wapi umeme wa haraka. Haimaanishi turuhusu UFISADI katika harakati hizo, hapo lazima uelewe. All those things zimeshatoke na zinashugulikiwa the way zinavyoshughulikiwa (that is another topic). The issue at hand ni kwamba tunataka umeme wa haraka.... that is the point.
 
Zitto unastahili kuwa Rais, unao uwezo wa kutoa majibu na kufanya maamuzi katika mambo magumu...sasa akina mwakyembe na shelukindo wao kila siku ni kupinga tu, haya ndio mapendekezo tunayotaka kama Taifa...Bravo zitto...hawa jamaa wa Dowans hata wakienda mahakamani wakatushinda, bado hasara yake hailingani na hasara hizi..du!..zitto wewe kiongozi....hizi ndio siasa kweli....sio porojo
 
Zitto ushauri wako umetulia, Serikali haipo serious ktk suala hili. Kuhusu dowans tumefikia point of no return, hatuwezi kurudi nyuma. Serikali iongee na hao mafisadi wadogo IPTL huku ikichukua hatua za kuitaifisha mitambo ya dowans.
 
Suluhisho la sasa ni hilo katoa zitto. tuna upungufu wa 90MW, zitto anasema tutaifeshe Dowans 125MW, tushinikize IPTL iwashe mitambo 100MW...huu ndio msimamo. iwe kosa isiwe kosa kisheria, tunataka hayo yafanyike...mambo mengine mbele kwa mbele, lakini kwanza mgawo umalizike
 
Acha siasa, nini kifanyike sasa hivi, kuna watu wanakufa mahospitalini!

Tuingine mtaani,msituni, TUFANYE NINI??

Hivi ubishi huu unasaidia nini eti??

desperate...m nini, nini....sijui....

what is the solution now???
cha kufanya wanakijua hao tanesco na serikali sio mara yao ya kwanza kununua mitambo, source wanazijua, exmption clause ipo raisi anaweza kuitumia ili wanunue toka kwa reputable manufacturer's na madege ya mizigo yapo , mzigo unatua Dar, yaani leo hii tanesco kupitia waziri husika wakipeleka quotation zao tatu kwenye kikao cha dharura cha baraza la mawaziri kesho turbines hizo zina nunuliwa na next flight mzigo upo bongo.
wakitaka ya rich aka dowans ni kufungulia mashtaka wahusika na kuimaliza kesi kabla hatua zingine hazijafuatwa. iwe kuinunua baada ya kesi au kuitafisha ni baada ya kesi.
 
Acha siasa, nini kifanyike sasa hivi, kuna watu wanakufa mahospitalini!

Tuingine mtaani,msituni, TUFANYE NINI??
?

Si tumesema:

1, Kuitaifisha na si kununua mitambo ya Dowans.

2, Kuagiza mitambo mipya as soon as possible.

3, Waliotufikisha hapa kushtakiwa kama WAHUJUMU WA UCHUMI.
 
Tatizo Kamati ya madini haikuwa inatoa proposal. ilikuwa inapinga tu...mara ya kwanza zitto alikuja na proposal kuwa mitambo inunuliwe....ikapingwa bila kutoa pendekezo mbadala....leo kaja na pendekezo tutaifishe....akina mwakyembe wako wapi?
 
Haya mambo ya kutaifisha kwenye ulimwengu wa sasa wa good governance hayana nafasi. If anything yata tuingiza katika migogoro ya kimahakama na hatimae ni kushindwa kesi na hasara kubwa zaidi ( refer IPTL na City water kesi )

Talk about mikataba ya kifasadi, hivi IPTL leo ni wasafi hivyo? kweli watanzania wepesi kusahau.

Hoja ya msingi ni ya rafiki yangu Waberoya, acha siasa pembeni taifa lipo kwenye kiza tunafanya nini? Hii habari ya mitambo hii ya kifisadi sijui sheria ya manunuzi and all that rubbish tunaangamia jamani we.

Walau sasa wengi tunakubaliana kuwa nchi ipo kwenye crisis inayo fanana na vita. Kama ni hivyo lets act now badala ya kuanza kutafutana mchawi nunua Dowans, nunua IPTL washa umeme halafu tukutane Dodoma tuanze kulumbana nani kala 10% nani kafanya nini lakini viwanda, mahospital, mashule nk yanapata umeme.
 
Back
Top Bottom