Zitto apendekeza Dowans itaifishwe; Serikali yapinga! Mgao waendelea...

Kichwa cha habari kinaweza kubadilishwa lakini na watanzania tuache kuwa "watabiri" kabla mtu hajaongea.

Nimesoma utabiri wa kila mtu hadi nacheka mwenyewe. Ngoja tuone atapoongea kitu tofauti tutarejea kwa style gani hapa... Huenda tukaelekea alikofikia Masatu kwa kumwomba radhi Mhe. Zitto.

Tumpe muda aongee kwanza kisha tukidadavue alichokiongea!

Hii sikutegemea kutoka kwako Kiongozi, mbona umeishahukumu?
 
zitto...zitto...zitto...aliona mbaaali kiza kinavyolinyemelea taifa kwa wachache kuwweka maslahi yao mbele...huenda ikawa moja kati ya ajenda za mkutano.
 
TAMKO LA MBUNGE WA KIGOMA KASKAZINI NA MWENYEKITI WA KAMATI YA BUNGE YA MASHIRIKA YA UMMA, NDUGU ZITTO ZUBERI KABWE KUHUSU MGAWO WA UMEME NCHINI.

COURTYARD HOTEL, DAR ES SALAAM
OKTOBA 15, 2009.


UTANGULIZI

Kwanza niwashukuru ndugu zangu wana habari kwa kukubali kuja kunisikiliza, hatua ambayo kwangu ni fursa ya kuzungumza na umma wa Watanzania hasa katika kipindi hiki ambacho Taifa letu lipo kwenye matatizo mengi, na kwakweli linapita kwenye kipindi kigumu sana kisiasa, kiuchumi na hivyo kijamii. Najua tunakabiliwa na matatizo mengi sana kama Taifa, kiasi kwamba ni vigumu kama kiongozi kuchangia mawazo kuhusu ufumbuzi wa matatizo yote yanayotukabili.

Ni kwa msingi huo, leo nimeona nizungumze nanyi kuhusu hali tete ya mgawo wa umeme unaolikabili Taifa kwa sasa. Mwanzoni mwa mgawo huu sikupenda kusema chochote pamoja na kuulizwa sana na waandishi wa habari na wadau mbalimbali. Sikutaka kusema chochote nikiamini kwamba Shirika la TANESCO, Serikali, na kwa upande wa bunge, Kamati ya masuala ya Nishati na Madini, wangeweza kutoa majibu ya tatizo linatukabili. Badala yake, juhudi nyingi zimetumika kutafuta chanzo cha tatizo na kuchelea kutoa suluhu. Pia kumekuwa na shutma mbalimbali, mojawapo ikidai kuwa baadhi ya watendaji wa TANESCO wanajaribu kuthibitisha madai yao ya kitaalumu ya kununua mitambo ya DOWANS. Shutma kama hizi, ni dhahiri zinauelewa finyu juu ya vyanzo vya mgao wa umeme uliopo sasa, ambao unasababishwa na uhaba wa mashine na upungufu wa maji. Uelewa huu finyu si tu hauna manufaa, bali hautoi ufumbuzi juu ya tatizo lililopo sasa ili kuepuka madhara ya kiuchumi kwa taifa na wananchi wake.

Kwa maendeleo yote duniani, nishati ya umeme ni msingi mmojawapo wa kujenga uchumi. Kwa utambuzi huu nchi mbalimbali duniani, hata zile zinazoweza kutoa huduma ya umeme kwa asilimia 90 kukidhi mahitaji yake, zinajaribu kuimarisha sekta zao za nishati kama msingi wa ujenzi wa maendeleo kwenye viwanda na wananchi wake. Nchi yetu ya Tanzania, huduma ya umeme inauwezo wa kuhudumia asilimia 12 tu na bado kunamgao.

Ni kweli changamoto za kuendeleze sekta ya umeme ni kubwa sana, na mipango ya muda mrefu ipo ingawaji haitekelezwi kwa sababu mbalimbali, lakini si lengo la mazungumzo yangu ya leo. Kwa mazingira tuliyonayo sasa, hasa katika kufuatia kuporomoka kwa uchumi duniani, hatua za haraka hazinabudi kuchukuliwa kuliepusha taifa katika uporomokaji wa uchumi wa kitaifa unauweza kuzuilika. Huu ni wakati ambapo serikali inapaswa kufanya tathimini ya haraka ili kufikia muafaka wa taratibu zipi zichukuliwe kuepuka hasara zitakazoletwa na mgao wa umeme, na hivyo maongezi yeyote yajikite kutafuta suluhu ya kuondoa mgao wa umeme kwa haraka zaidi. Badala ya hali ya sasa ambayo mijadala na hatua mbalimbali zimejikita kutafuta chanzo cha tatizo bila kutoa suluhisho, huku madhara ya mgao yakiendelea kuwaumiza watanzania.

Tumeambiwa na TANESCO kuwa Mgawo wa umeme wa masaa 14 kila siku msingi wake ni upungufu wa 90MW za umeme. Kwa mgawo huu TANESCO wanapoteza mapato ya takribani shilingi 200 milioni kwa siku! Lakini hii ni kwa upande wa TANESCO tu, bado kunamadhara mengi kwa upande wa wananchi na taifa kwa ujumla.

MADHARA YA MGAWO WA UMEME KWA UCHUMI WA TAIFA.

Ndugu zangu, mgawo huu una madhara makubwa sana, kuanzia kwenye uchumi mkubwa wa taifa (macro economy) hadi uchumi mdogo wa makampuni na mtu mmoja mmoja. Madhara ya mgawo wa umeme yana athiri mpaka wasio na umeme;

  • Katika sekta ya Ujenzi, mfano wa viwanda vya Simenti gharama za uzalishaji zimeongezeka sana. Kwa mfano Kampuni ya Twiga Cement hutumia dola za Marekani 10 kama gharama ya kuzalisha umeme iwapo wanatumia umeme wa TANESCO. Gharama hizi huongezeka mara 4 na kufikia dola 40 kwa Tani wakati wa mgawo. Hii maana yake ni kwamba bei ya Saruji itapanda kwa shilingi 1000 zaidi kwa kila mfuko wa Saruji. Watakaoumia hapa ni raia wa kawaida wanaojiwekea akiba ili kujenga nyumba zao.

  • Nimeambiwa sekta ya Mabenki inaathirika sana na mgawo wa umeme kwani gharama za kuwasha umeme katika matawi yao imeongezeka sana. Mfano, Benki ya CRDB sasa itatumia shilingi 400 kwa mwezi kwa gharama za umeme na Benki ya Barclays itatumia zaidi ya shilingi 210 milioni kwa mwezi. Zote hizi zinaongeza gharama za biashara na hivyo kupunguza kodi ya serikali.

  • Katika sekta ya Mawasiliano gharama za kuendesha minara ya simu zimeongezeka kutokana na kampuni za kugharamia mafuta ya kuwasha minara. Takwimu zinaonesha kuwa Kampuni ya Simu ya Zain sasa inatumia shilingi 700 milioni zaidi kwa mwezi kwa sababu ya mgawo. Kampuni ya Vodacom inatumia zaidi ya shilingi 800 milioni zaidi kwa ajili ya kuwasha minara yao. Hii maana yake ni kwamba gharama hizi zitapunguza kodi za makampuni ambazo kampuni zitalipa serikalini. Zaidi ya hapo mgawo husababisha matatizo ya mawasiliano kwa watu kushindwa kutumia simu zao kutokanana ukosefu wa umeme.

  • Madhara ya mgawo wa umeme yanamuathiri kila Mtanzania, Mkulima kwa mfanyakazi, wafanyabiashara wakubwa kwa wafanyabiashara wadogo. Nakumbuka mwanzoni mwa mwaka huu, Kamati yangu ya Mashirika ya Umma tulifanya utafiti mdogo kuangalia madhara ya mgawo wa umeme kwa watu wa kawaida, tulikuta salooni moja wakatwambia wanatumia 8000/= pakiwa hakuna mgawo lakini pakiwa na mgawo wa umeme wanatumia hadi 68000 kwa ajili ya umeme wa jenereta, sawa na gharama ya ziada ya shilingi 60,000/= kwa siku. Hivyo mgawo unawaumiza sana wajasiriamali wadogo wadogo na kuharibu mitaji yao na hivyo kuongeza umasikini.

  • Hivi juzi nilikuwa nazungumza na watu wenye mashine za kusaga nafaka huko Nzega naambiwa , pakiwa hakuna umeme wanatumia mafuta ya diesel na gharama za uendeshaji ni mara tatu ya gharama wanazotumia umeme ukiwepo. Hii maana yake ni kuwa madhara ya mgawo yanamgusa mwananchi wa kawaida kabisa vijijini kwa kuongeza bei za vyakula na hivyo kuongeza mfumuko wa Bei.

  • Nimekwenda Internet café moja hapa Dar es salaam, wanasema bei ya huduma ya internet kwa saa siku za mgawo wa umeme ni shilingi 2000 wakati siku umeme ukiwepo ni sh1000. Hii ni mifano ya maeneo machache tu kuhusu mgawo, ambayo kwa ujumla inaonesha wazi kuwa mgawo wa umeme unapandisha gharama za maisha (cost of living) wakati mapato ya mtanzania yakiwa duni.
Serikali na Taifa linapoteza mabilioni ya fedha kutokana na mgawo huu wa umeme. Naamini baadae Benki kuu itakuja kufafanua hili. Lakini Taifa linapokuwa kwenye mgawo uchumi wa unayumba. Nimewaambia kwamba mgawo wa 2006 peke yakeuliporosha uchumi kwa nukta moja ambayo ni sawa na shilingi billion 250. Na sasa ninawaambia, tukiacha mgawo huu uendelee hata kwa miezi miwili, taifa litatetereka vibaya sana.

  • Mfumuko wa bei utazidi kupanda(cost push inflation),
  • Uwiano wa malipo ya nje utaathirika kwasababu ya kutumia pesa nyingi za kigeni kununua mafuta nje(import),
  • Gharama za uzalishaji viwandani zitapanda sana na kusababisha serikali kupoteza mabilioni ya fedha ambayo ingekusanya kama kodi.
Inaumiza sana kuona kuwa tunaendekeza siasa rahisi tunaposhugulikia masuala mazito ya kitaifa kama Nishati. Inasikitisha zaidi pale tunapoona kuwa serikali inashindwa kuchukua hatua mahususi za kuhami uchumi wa Taifa letu. Serikali na Bunge hazitoi suluhisho la hali hii na ni wazi kuna kutupiana mpira wakati nchi inaumia. Serikali imewekwa madarakani ili ifanye maamuzi na tuihukumu kwa maamuzi hayo. Serikali ni lazima sasa iamue.

3. HATUA NINAZOPENDEKEZA
Nimesema mwanzo kwamba, kuendelea kwa mgawo huu wa umeme ni udhaifu wetu wa uongozi kushindwa kufanya maamuzi magumu lakini ya msingi, na badala yake kujikita katika kutafuta nani mchawi kila tunapokabiliwa na tatizo. Ni bahati mbaya sana hata vyombo vya habari vimejikuta vikiendelea kutoa taarifa za mchawi anatafutwaje badala ya kueleza madhara ya mgawo kama njia ya kushinikiza ufumbuzi wa tatizo.

Wakati Taifa linakabiliwa na upungufu wa 90MW za umeme, na uchumi wa kila mtanzania unaathirika, hapa nchini tuna mitambo ya IPTL yenye uwezo wa kuzalisha 100MW, ambayo imezimwa kwa sababu ‘eti’ ina kesi dhidi ya serikali. Majadiliano kuhusu mgogoro huu bado yanaendelea bila kwisha. Hapa nchini tuna mitambo ya Dowans yenye uwezo wa kuzalisha 125MW, ambayo ni ya kuwasha tu. Lakini kwasababu tu serikali imeshindwa kufikia maamuzi, inaendelea kuwepo nchini huku Taifa linayumba kwa giza.

Kama nilivyoeleza hapo awali, nishati ya umeme ni kichocheo kikubwa sana cha ukuaji wa uchumi na hatimae maendeleo ya kiuchumi. Kwahiyo kama kiongozi sikubaliani kabisa kuona nchi inaendelea kuwa gizani na kugharimu uchumi wa Taifa, kuongeza gharama za maisha ya mwananchi wa kawaida na hata kupunguza mapato ya serikali.

Ninapendekeza;

  • Serikali ihakikishe mitambo ya IPTL inawashwa mara moja wakati mazungumzo yake na IPTL yakiendelea kwa kuharakishwa (fast tracking). Hali ya nchi ni mbaya, ni sawa na vita, haiwezekani serikali yenye mamlaka ishindwe kuhakikisha IPTL inazalisha umeme wakati mazungumzo yakiendelea. Haiwezekani.Labda kama haina uchungu na maisha ya watu wake.
  • Kwa kuwa mapendekezo ya TANESCO ya kununua mitambo ya kampuni ya Dowans yalipingwa na baadhi ya wanasiasa wenzangu na hatimaye kutonunuliwa na hivyo kusababisha mgawo uliopo hivi sasa, na kwa kuwa mitambo ile inaweza kuingiza 125MW katika gridi ndani ya siku moja na kumaliza kabisa mgawo uliopo hivi sasa na kuliokoa Taifa na kuhami uchumi wetu, na kwa kuwa mitambo ya Dowans inahusishwa na mkataba wa kifisadi wa Richmond, ninaishauri serikali itaifishe mara moja kampuni ya Dowans.

4. HITIMISHO

Mgawo huu wa takribani mwezi sasa umeshaligharimu Taifa kwa kiasi kikubwa sana. Mgawo huu ukiendelea kwa wiki tatu zijazo, madhara yake ni makubwa kiasi cha hata maamuzi ya serikali kuhami uchumi (stimulus Package) yaliyotajwa na Rais Kikwete mjini Dodoma mwezi Juni yatakuwa hayana maana kabisa kwani mfumuko wa bei na kudorora kwa shughuli za uchumi kutaporomosha ukuaji wa uchumi uliotarajiwa na mkakati huo.

Mazingira magumu kama haya yanahitaji maamuzi magumu (extra ordinary circumstances require extra ordinary decisions). Ninaamini serikali itazingatia ushauri wangu.

Asante sana.

KABWE ZUBERI ZITTO,MB
Dar es Salaam.
 
Hili la kutaifisha mitambo ya Dowans sijui Serikali inasubiri nini. Kama kampuni iliyoileta hii mitambo ilikuwa hewa, kigugumizi kinatoka wapi cha kuichukua bure kwa manufaa wa watanzania!
 
Duh kazi kweli safari tunayo nayo ni ndefu, jamani Zitto hivi umeona IPTL sijui na DOWANS ndo suluhisho?

Jamani tununue mitambo mipya na tuanze programs za kufikiria njia za kumaliza kabisa tatizo la umeme. Tufikirie vyanzo vingine vya umeme na sio maji tu na majenereta. Jamani kuna Geo-therms, nyukilia sijui na makaa ya mawe jamani wanageologia mko wapi sasa tunahitaji utaalaam na sio porojo hizi za kisiasa
 
zitto...zitto...zitto...aliona mbaaali kiza kinavyolinyemelea taifa kwa wachache kuwweka maslahi yao mbele...huenda ikawa moja kati ya ajenda za mkutano.
zitto kaona mbali nini sasa tunataka suluhisho la longterm na sio hivi vijereta vya umeme
 
waache longolongo, tunataka umeme, tumechoka kufanywa mafala kwenye nchi yetu wenyewe
 
Mwaka jana au juzi kama sikosei, JK alisema hakuna madhara yeyote ya kiuchumi yalitokana na mgao wa umeme kwa kipindi hicho.

What make you think that he will treat this one differently?
 
zitto kaona mbali nini sasa tunataka suluhisho la longterm na sio hivi vijereta vya umeme
Sasa hao akina Mwakyembe waliokwambieni bora mkae gizani lakini mitambo ya Dowans isinunuliwe...hawana wayout, siku nyengine wakikwambieni bora mfe njaa lakini msikubali misada...mtakubali eee?
 
•Serikali ihakikishe mitambo ya IPTL inawashwa mara moja wakati mazungumzo yake na IPTL yakiendelea kwa kuharakishwa (fast tracking). Hali ya nchi ni mbaya, ni sawa na vita, haiwezekani serikali yenye mamlaka ishindwe kuhakikisha IPTL inazalisha umeme wakati mazungumzo yakiendelea. Haiwezekani.Labda kama haina uchungu na maisha ya watu wake.

•Kwa kuwa mapendekezo ya TANESCO ya kununua mitambo ya kampuni ya Dowans yalipingwa na baadhi ya wanasiasa wenzangu na hatimaye kutonunuliwa na hivyo kusababisha mgawo uliopo hivi sasa, na kwa kuwa mitambo ile inaweza kuingiza 125MW katika gridi ndani ya siku moja na kumaliza kabisa mgawo uliopo hivi sasa na kuliokoa Taifa na kuhami uchumi wetu, na kwa kuwa mitambo ya Dowans inahusishwa na mkataba wa kifisadi wa Richmond, ninaishauri serikali itaifishe mara moja kampuni ya Dowans.

KABWE ZUBERI ZITTO,MB
Dar es Salaam.

Very good comments na observation. Bravo Zitto.
Nakubaliana naye 100% kwenye issue ya IPTL kwa kuwa tuko kwenye CRISIS na ukizingatia tunacholose it is better tu-run IPTL at any cost kulinganisha na harasa zinazolikumba taifa kama alivyo comment.

Issue ya kutaifisha dowans iko wazi kabisa, na ilishajadiliwa hapa, nashangaa ni kwa nini serikali haichukui haya maamuzi haraka iwezekanavyo. Sijui wanasubiri nini.
 
Yaani...Zitto bora ungekuwa ww ndo waziri wa nishati...labda...labda...labda tungekuwa tunazungumza lugha ya ki-balbu na si-chemli.
 
Hili la kutaifisha mitambo ya Dowans sijui Serikali inasubiri nini. Kama kampuni iliyoileta hii mitambo ilikuwa hewa, kigugumizi kinatoka wapi cha kuichukua bure kwa manufaa wa watanzania!

Pengine Serikali haina ushahidi wa kutosha kwa hivyo kina Mwanakijiji walisaidie Taifa kwa kutowa ushahidi na hii itathibitisha kuwa madai wanayoyatowa ni ya kweli.
 
du kazi kweli safari tunayo nayo ni ndefu,jamani ZITTTO hivi umeona IPTL sijui na DOWANS ndo suluhisho?jamani tununue mitambo mipya na tuanze programs za kufikiria njia za kumaliza kabisa tatizo la umeme.tufikirie vyanzo vingine vya umeme na sio maji tu na majenereta.Jamani kuna Geotherms,nukilia sijui na makaa ya mawe jamani wanageologia mko wapi sasa tunahitaji utaalaam na sio porojo hizi za kisiasa

Mitambo iliyokwishakuwa tayari inatuchukua hadi mgao hatujapata suluhisho, ama hayo mengine ni sawa sawa na kusema kuwa tukae miaka mitatu na mgao kabla hayajatekelezeka.
 
•Kwa kuwa mapendekezo ya TANESCO ya kununua mitambo ya kampuni ya Dowans yalipingwa na baadhi ya wanasiasa wenzangu na hatimaye kutonunuliwa na hivyo kusababisha mgawo uliopo hivi sasa, na kwa kuwa mitambo ile inaweza kuingiza 125MW katika gridi ndani ya siku moja na kumaliza kabisa mgawo uliopo hivi sasa na kuliokoa Taifa na kuhami uchumi wetu, na kwa kuwa mitambo ya Dowans inahusishwa na mkataba wa kifisadi wa Richmond, ninaishauri serikali itaifishe mara moja kampuni ya Dowans.

Hivi kwa nini mnasema kukataa kununua mitambo ya Dowans ndo kulikosababisha mgawo hivi sasa? This statement is pissing me off. Hivi tuulizane, kwani mgawo wa umeme nchini Tanzania umeanza leo au jana???????????

Hapo kidogo umesema la maana, mitambo ya Dowans itaifishwe. Lakini hii nchi kwa jinsi tunavyoielewa utendaji kazi wake ni wa kujaza matumbo ya viongozi/watendaji wachache, hata ikiamuliwa itaifishwe; ni nani atahakikisha kama kweli imetaifishwa?? Tutakachoambulia hapa ni kuuziana kinyemela bila wananchi kujua.
 
du kazi kweli safari tunayo nayo ni ndefu,jamani ZITTTO hivi umeona IPTL sijui na DOWANS ndo suluhisho?jamani tununue mitambo mipya na tuanze programs za kufikiria njia za kumaliza kabisa tatizo la umeme.tufikirie vyanzo vingine vya umeme na sio maji tu na majenereta.Jamani kuna Geotherms,nukilia sijui na makaa ya mawe jamani wanageologia mko wapi sasa tunahitaji utaalaam na sio porojo hizi za kisiasa

Mkuu heshima mbele,
Hivi wewe unaelewaje haya maneno EMERGENCY or CRISIS?
Hiyo mitambo mipya unayoongelea itakuja baada ya siku moja au wiki moja??? Jamani hivi tunaelewa sasa tuko kwenye hali mbaya sana kutokana na kukosa umeme. Sio wakati wa kusubiri plan ni wakati wa kufanya maamuzi ya haraka na machungu basi.
This is what we call state of emergency...
 
du kazi kweli safari tunayo nayo ni ndefu,jamani ZITTTO hivi umeona IPTL sijui na DOWANS ndo suluhisho?jamani tununue mitambo mipya na tuanze programs za kufikiria njia za kumaliza kabisa tatizo la umeme.tufikirie vyanzo vingine vya umeme na sio maji tu na majenereta.Jamani kuna Geotherms,nukilia sijui na makaa ya mawe jamani wanageologia mko wapi sasa tunahitaji utaalaam na sio porojo hizi za kisiasa

kuna upepo pia ni chanzo cha umeme yani huko tunakoenda Mungu mwenyewe ndo anaeza kujua.nina uchungu sana na hii nchi basi tuu one person's fault so many people are suffering sijui nilie hihihihihihi :(
 
Kuna haja pia kuziangalia Kamati hizi za Bunge ili kujua majukumu kila kamati, mipaka yake ya kazi na ipi isikilizwe kunapotokea mkanganyiko kama huu. Hapa zipo kamati mbili zilizoichanganya Serikali na TANESCO pia. Kuna Kamati ya Kudumu ya Nishati na Madini inayoongozwa na Mzee Shelukindo na Mh Mwakyembe akiwemo na ile ya Mashirika ya Umma inayoongozwa Mh Zitto. Ni ipi kati hizi ina mamlaka na ushawishi kwa TANESCO?
 
Back
Top Bottom