Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Status
Not open for further replies.
Nimefarijika na Kumpongeza Zitto Kabwe katika hili!
 
Zitto hakuwa na sababu za msingi kuutangazia umma anagombea nafasi ya KUB kabla ya kujua chama chake kitafuata mfumo upi.Ningeshanga sana kama CHADEMA wangekubali kuyumbishwa kwa jambo dogo kiasi hiki lazima wajue watakutana na mambo makubwa kuliko hili mbele ya safari.
 
mafisadi mbinu mliyoitumia kwa nccr mageuzi 1995 hapa mmenoa tafuteni nyingine mlikolalia chadema ndio wameamkia sie wananchi tutaendelea kuwasapoti na huko bungeni wakiwaburuza tu 2015 hawapati viti hata 40 waone nguvu ya umma
 
Chadema sio ccm. Hawakimbilii vyeo. Kila mtu anapata stahili yake
 
Wamewasahau CUF? Hiyo ya WestMinster wangewaachia wazungu wenyewe!

Kwani hilo Bunge letu si la Westminster? CUF mwanzo walianza wao tu lakini baadaye wakawashirikisha wengine. Hii ni nzuri kwa sababu: 1. Kumzuia Mrema kuharibu move zote za upinzani ndani ya bunge; 2. Bunge letu liko kwenye Umoja wa Madola; 3. Chadema wana urafiki na Conservative Party cha UK; 4. wapinzani wengine wafahamu kwanza mlengo wa Chadema kabla ya kujumuishwa.
 
hata mimi nimefurahishwa sana na natarajia kuwa baada ya kufanya kazi kwa ukaribu kwa miaka mitano watadumisha mshikamano ndani ya chama.
 
Kingekuwa kichekesho kwa kweli. Zitto awe KUB, Anne Makinda awe Spika, Job Ndugai awe NS, Chenge awe Chief Whip wa wabunge wa CCM,....., Bunge la hovyo kabisa tangu uhuru!
 
pongezi za nini wakati zitto alisema wazi kuwa ikiwa westminster system itafuatwa ambapo mwenyekiti wa chama ndiye anakuwa kiongozi wa upinzani basi yeye angekubaliana na uamuzi huo na kumuunga mkono mbowe lakini ikiwa american democracy style ingefuatwa basi angegombea...maana kimarekani huwa ni gombea goli..

mi nadhani Zitto ni mkomavu sana kidemokrasia kuliko wengi wetu hapa jamvini...na ni kwa sababu ya huo ukilaza wetu ndiyo kila mara tunamuona kama msaliti ingawaje ameshasema mara kadhaa...kamwe hatokisaliti chama alichoshiriki kukijenga..Zitto ameingia chadema akiwa sekondari kwao kigoma..si kama wengi wetu humu ambao mpaka juzi hapa 2005 tulimpigia kura kikwete.....ni baada ya slaa kulipua mafisadi pale TMK ndiyo baadhi humu wakaanza kujua alah..kumbe kuna upinzani!!!!

tofauti na wanasiasa wengi wa kiafrika na mashabiki wao...kwao upinzani maana yake ni kutaka kuleta mgawanyiko na ni uadui..hatujui kushindana kwa hoja...ni kwa mantiki hiyo mara nyingi zitto anashindwa kueleweka katika macho ya 'wanaojiita' wapinzani:smile-big:
 
Ila Mbowe atumie sana hekima na busara kwenye kuongea kwani jamaa anaonekana ngumi mkononi!

Tunamtarajia amhenyeshe WM ajaye bila kuangalia makunyanzi ya Anne Makinda na waliomweka pale. Mbowe ni mjengaji wa hoja mzuri tu.
 
Ila Mbowe atumie sana hekima na busara kwenye kuongea kwani jamaa anaonekana ngumi mkononi!
Kwani hii ndiyo mara ya kwanza kwa Mbowe kuingia Bungeni, 1995 mbona hakurusha ngumi. Acha majungu na siasa za majitaka kama Chenge.
 


Ni PM nikuelekeze wapi utazipata
 
Tatizo kubwa la Zitto ni msimamo. Hana tofauti na Spika Mstaafu Sitta. Sisi wengine kwenye siasa za Nchi hii tumo tangu 1975! Hata sijui Zitto alikuwa wapi wakati huo.
 
Zitto amekomaa kisiasa
Nawapongeza CHADEMA kwa hii move.
Tunaitaka nafasi ya uspika sasa.
hata kama tukiikosa lets try it
 
Congratulation Mh. Zitto!!! Hiyo ndiyo Democracy mze najua wabaya kinawauma, CHADEMA mwendo mdundooo!!!! Jamani huyu dogo Zitto upresida unamhusu for the futureeee!!!
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…