Zitto anataka kusaliti CHADEMA?

Status
Not open for further replies.
Zitto je tuko pamoja kwenye kudai katiba mpya na kuisarambatisha nec

Madai ya Katiba mpya nchini sio madai mapya. Toka mfumo wa vyama vingi umeanza kwa nyakati tofauti kumekuwa na madai ya Katiba mpya. Yanaibuka na kupotea. Nimeshiriki katika madai haya toka nikiwa shuleni. Mwaka 1998 nikiwa nimemaliza kidato cha Sita Tosamaganga na kupita Dar es Salaam nikielekea Kigoma nilihudhuria mkutano ulioandaliwa na Busineness times kuhusu Katiba Mpya na kuzungumza. Mwaka 1999 nilishiriki kutoa maoni katika Kamati ya Jaji Kisanga kuhusu Katiba Mpya. Mwaka 2001 nilishiriki maandamano ya vyama vya upinzai kudai Katiba mpya na Tume huru ya Uhaguzi. Mwaka 2005 Februari nikiwa sio Mbunge nilishiriki katika vikao vya kamati ya Bunge ya sheria na Katiba kuhusu madai ya Katiba mpya. Nilipochaguliwa tu niliandika barua kwa Rais kuhusu umuhimu wa kuandika katiba na kubadili mfumo wa uchaguzi. Nina rekodi ya madai ya Katiba hapa nchini.

Ili Tanzania ikue kidemokrasia na kiuchumi ni lazima tujiangalie tunavyojitawala. Mchakato wa kuandika Katiba mpya unapaswa kuanza mara moja. Katiba mpya iweke Tume Huru ya uchaguzi na kutatua tatizo la kero za Muungano na mfumo gani wa Muungano ufuatwe. Ninapenda kuona Tanzania yenye Katiba Mpya wakati wa kusherehekea miaka 50 ya Uhuru wa Taifa letu mwezi Disemba mwaka 2011.
 
Why are you so obsessed with Ms. Mtema? Regina hajawahi kulalamika juu ya Kitila.

Regia Mtema ndiye aliyekuja hapa kumlalamikia Kitila in a rather disgraceful way.

Kitila hakujibu, sasa mtu ninayeshutumu migogoro ya chama, hususan kuanikwa hadharani, nitamlaumu nini hapo Kitila ?

Kama unaongelea kumshutumu Kitila sehemu nyingine, angalia kule kwenye thread ya uteuzi wa wabunge wa viti maalum CHADEMA nimemsema Kitila vizuri tu.

Usitake kujifanya una uwezo wa kusoma threads zote hapa, unataka tuanze kufukua threads hapa?
 
Ndugu Zitto nikupongeze kwa kujitokeza kuelezea msimamo wako pamoja na kutuahidi utiifu wa maamzi ya vikao vya Chama hapo umenena.

Napenda nikueleze tu kuwa ukiona threads nyingi kwenye JF zikiandikwa kinyume chako hapo ujue kuwa umekengeuka au umeenda kinyume na matarajio ya watu waliowengi. Kumbuka kuwa sisi wanaJF wengi wetu nirahia wakawaida(siyo viongozi ndani ya vyama) Hivyo hattatafumbia macho kitendo chochote chenye lengo la kuturudisha nyuma au kuhatarisha umoja ndani ya chama bila kujali kimefanywa na nani? Hata kama ni Mbowe,Lisu,Zitto,Mnyika au hata Rais wetu mtarajiwa Dr wa ukweli Slaa.Tutakemea jambo hilo kwa nguvu zetu zote bila kujali kama limefanywa kwa bahati mbaya au makusudi

Nikishasema hayo napenda kukueleza kuwa mimi ni miongoni mwa Tanzania ambao wanakukubali kwa jinsi unavyojenga hoja na kusimamia haki lakini kitendo cha kushindwa kuungana na akina Lisu,Mnyika Mdee,Mbowe na wabunge wengine wa CDM kususia hotuba ya Rais ulinivunja moyo sana unajua pale ulisababisha mgawanyiko mkubwa sana.

Ladba tu ndugu yangu Zitto nikueleze ukweli kuwa mimi ni miongoni mw Watanzania ambao wanakuamini kama mpigania haki za wanyonge kwa jinsi ulivyo makini katika kujenga hoja na kuzisimamia lakini kitendo cha kukatataa kuungana na wapiganajipya akina Lisu,Munyika,Mdee, Mbowe na wabunge wengine wa Chadema kiliniuma sana na nilianza kuhisi kuwa sasa wewe unamalengo yako tofauti kwakweli mtu mzima lazima ukubali ulipotoka na kama hilo hujalikubali basi sasa tambua kuwa yawezekana umeamua kuchukua
uelekeo wa peke yako na wala siyo wa Chama unajua nalazimika kukueleza hayo kwakuwa kile kitendo chako cha kuchukua msimamo wa peke yako(Shibuda Simsemei Kunaphylosophy nikitaka mzungumzia) kiliwavunja wapenda mabadiriko wengi na athali yake ndoo hizo thread nyingi ambazo ziko negative kwako. Ila maadamu umejitokeza hadharani with objective dirrection sina budi kusema nimekusamehe
 

Dhamira yangu ni nyeupe. Sijanunuliwa maana sina bei. Haya yote baada ya muda yatajulikana ni uwongo, uzushi na siasa za maji taka. Kama Mwanasiasa nina wajibika kwa maamuzi yote nifanyayo, mazuri na mabaya. Kama binaadamu ninijifunza kwa maamuzi mabaya niliyofaya huko nyuma ili nisirudie maamuzi hayo.
 


Haya ndio mambo yanayonifanya nianze kuhisi kumbe Tanzania kila anayejifanya anapigania haki ni muongo, ukweli ni kwamba watu

wanapigania matumbo yao, na ikitokea kasimama kutetea maslahi ya umma basi ujue nyuma ya hiyo ajenda kuna maslahi yake binafsi.

Ubinafsi utatuangamiza mpaka siku ya mwisho wa dunia.
 

Kuna watu wanasema una ego kubwa na katika kujifanya muwazi sana, ukweli ni kwamba una satisfy ego yako tu, na kujipromote at the expense of party cohesion, unasema mengi ambayo hutakiwi kusema, loose lips sinks ships.

Swala la kutounga mkono kumsusia rais bungeni kwa mfano, ilikuwa lazima kuliongelea na kuonyesha tofauti binafsi ndani ya chama wakati chama kilishaamua? Au ulitumwa na chama?

Unasemaje kuhusu hili ?
 
Ungesema hiyo habari imeandikwa na Ansbert Ngurumo kupitia Mwanahalisi,kuliwa na umuhimu gani wa kusema mwandishi ni Press secretary wa Mbowe.

Unaendelea na siasa zako za maji taka kumtaja Antony Komu ni mmiliki wa Mwanahalisi na kuwaacha wamiliki wengine wenye hisa nyingi kama Kubenea kwasababu sio wachaga.
Hii si mara ya kwanza kuihusisha Chadema na ukabila ni wazi unataka wakufukuze ili ukaseme Wachaga wamekufuza.Cha kushangaza mpaka sasa hivi haujui Watanzania wengi wameshaelewa Chadema hakuna ukabila na hakuna atakaye kufukuza.
 

Nikusahihishe kidogo. Mnyika na Halima hawakuwepo kabisa Dodoma siku ya tukio au walikuwepo lakini hawakuja kwenye kikao na kisha Bungei. Mimi nilikuwepo kwenye kikao na kusema wazi mawazo yangu kuwa sioni kama ku walk out ni mkakati mzuri. Kwa kuwa sikuunga mkono maamuzi hayo niliamua kutokwenda kabisa Bungeni. Nimeshalisemea hilo na kulitolea maelezo hapa JF. Sikutaka kuwa mnafiki na kujificha katika pazia la wengine. Sasa kama ni uamuzi wa makos umeshatokea, muhimu ni kusahihisha makosa na kwenda mbele. Nawaomba radhi wale wote niliowaudhi kwa msimamo niliochukua na hivyo mkaumia. Mimi niliona ndio msimamo sahihi (kutokwenda Bungeni kabisa na kama kwenda kuto walk out). Wengi mmeona haukuwa msimamo sahihi. Nimesikia. Tupige mstari na tuendelee na kazi nyingine.
 
Also to Zitto, Mbowe and Chadema please sort out any problems about Chadema behind the scenes no need kuwapa wapinzani ammunition

I love this. Zitto this is important for growth of CDM!!! Please.
 
Nilimtetea huko nyuma, lakini kwa hili inabidi nilisema kama lilivyo. Zitto, jaribu kuwa makini na kile unachozungumza. Kama una tatizo peleka kwenye vikao vya chama na sio hapa JF. Hakuna chama kisicho na matatizo, lakini matatizo ya chama hayatolewi nje au kwenye blogs, yanatatuliwa ndani ya chama. Kuna wakati Kikwete alisema watu ndani ya CCM walikuwa hawaaminiani kiasi cha kushindwa hata kula chakula pamoja, lakini hatukuwahi kusikia mwanachama akiongea kwenye vyombo vya habari mambo yao, ingawaje matatizo yalifahamika ndani ya chama.

Ushauri wangu kwako, sio kila habari inayokuzungumzia wewe lazima uijibu, wewe ni public figure kwa hiyo tegemea kuandikwa; isitoshe hayo magazeti yanafanya biashara na labda wameona habari zako zinauza. Pili, jifunze jinsi ya kuongea, mahali pa kuongea na wakati wa kuongea. Tatu, jifunze kuwaweka maadui wako karibu kuliko marafiki zako. Nne, tambua ya kuwa kwenye huu msuguano unaoendelea one might win the battle, but lose the war (2015). Tano, majibu mengi unayoyatoa hapa yana too much information ambazo nyingine watu wa sio ndani ya chama hawastahili kuzijua.
 
Je hili suala la wewe kugombea uraisi 2015 ni la kweli... sio vibaya kila mtu ana rights za kugombea ila i have heard (am not sure kama ni kweli) kwamba uliwaaga wapiga kura wako kwamba ni mara ya mwisho wewe kwenda kuomba kura zao za ubunge... Je bado una dhamira hiyo ya kugombea 2015
 

samahani kama nimekukosea. Hizo tafsiri za uchaga ni zako. Sio zangu hata kidogo. Niwie radhi lakini. Pole
 

2015 nitakuwa nina umri wa miaka 39. Katiba inasema kuwa Rais lazima awe na miaka 40. Hata hivyo, sio kosa kwa Mtanzania yeyote kusema anataka kuwa Rais ya Jamhuri yetu tukufu.
 
:A S crown-1: Lisemwalo lipo... kama halipo laja.... Kwenye msafara wa mamba hata kenge huwemo.....
 
I think Jamaa amekili kuwa kuna makosa kafanya kama kila binadamu anavyofanya... na amesema tuko bado pamoja, kwahiyo kuliko kupigana wenyewe kwa wenyewe tumpe chance aendelee kutuwakilisha. Na kama alifanya makosa huko nyuma, tuyaache and lets start a new chapter
 

My man Kuhani angeipenda hii.
 
ila kunamengine Zitto ukubali kuwa unakosea kwanini watu wamakujadili wewe sana ndani ya CHADEMA wakati wapo wengi pale? kwanini hasiwe Mdee?
Mkuu, Mh. Zitto kisha sema yeye ni binadamu kama kuna sehemu kakosea atajirekebisha na kama kuna watu wamemzushia yeye atadharau. Nadhani ujumbe hapo kautoa naomba ufike.
 
2015 nitakuwa nina umri wa miaka 39. Katiba inasema kuwa Rais lazima awe na miaka 40. Hata hivyo, sio kosa kwa Mtanzania yeyote kusema anataka kuwa Rais ya Jamhuri yetu tukufu.
Tuko pamoja ushauri wangu ni kuwa just wait your time will come.... Am sure uwezo unao jenga Chama one day your time will come you are still young
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…