Mficha maradhi,kifo humuumbua.Haina haja ya kusubiri watu watumie udhaifu wenu viongozi wa Chadema kukisambaratisha chama.Mmeonesha ukomavu wa kisiasa na mnaendesha siasa za kisasa.Wote mnamchango mkubwa kwenye chama ingawa kila mtu anamapungufu yake.
Ushauri ni kuwa kwa sasa msitoe matamko ambayo yataendelea kukuza taharuki ambayo itakuwa na madhara kwa chama.Kuna vita dhidi ya Chama itokanayo na hasira za wapinzani wenu kutokana na kuwajeruhi katika uchaguzi uliopita.Muda huu ni wa kuwa na mshikamano kikweli kweli,msiruhusu nyufa hata kidogo.Mpaka sasa mnapoint nyingi sana mlizoshinda,mjipange upya kwa mashambulizi mengine bungeni na nje ya bunge katika kushinikiza katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.
Chama kina kanuni na taratibu zake,mkizifuata bila upendeleo siku zote, mtafanikiwa.
Mungu awajalie hekima,na awalinde na naowaangalia kwa jicho la husuda,....AMINA.